Aliongeza kwakusema , kila mwaka chini ya Huduma ya Jamii kupitia mradi wa “Bayport Change a Life”, Bayport hutoa msaada chini ya huduma hii wa zaidi ya shilingi milioni 50 kwa jamii nchi nzima. Misaada hii imetolewa kwa waathirika wa majanga, watoto yatima, mipango ya vijiji kama vile uchimbaji wa visima vya maji safi na salama, na kuimarisha jamii kielimu kwa kutoa udhamini kwa wanafunzi wa Chuo Kikuu au ukarabati wa shule kama Shule ya Msingi Airport Kigoma.
Ngula Cheyo alisema kampuni hii imetoa shilingi milioni 20 kwa ajili ya ukarabati wa shule, ambayo ni mchango mkubwa wa Huduma za Kijamii kufanywa na taasisi yoyote za kifedha au kampuni yoyote binafsi katika shule moja Nchini Tanzania. Alieleza kuwa ukarabati huu ulikuwa wa ujenzi kamili wa ofisi mbili mpya za Utawala, ambayo moja kwa ajili ya Mwalimu Mkuu na nyingine ikiwa ofisi ya Waalimu, pia utengenezaji wa madawati 160, ambayo ni madawati 40 kwa kila darasa kuanzia darasa la kwanza mpaka la nne na ukarabati wa sakafu zote nje na ndani na upigaji rangi wa shule nzima.
Wakuu wa idara kutoka Bayport Makao Makuu waliohudhuria sherehe hii ni Dk Ken Kwaku Mwenyekiti wa bodi wa kampuni, Ibrahim Kaduma Mkurugenzi wa bodi, Etienne Coetzer Afisa Mtendaji Mkuu, John Mbaga Afisa Mkuu wa Uendeshaji, na Ngula Cheyo Meneja Masoko na Mahusuiano ya Jamii. Bw. Ibrahim Kaduma aliongea kwa niaba ya kampuni katika sherehe hiyo
.
Ngula Cheyo alisema shule hiyo ilitakiwa kuzinduliwa rasmi na Mkuu wa Mkoa Kigoma Kanali Mstaafu Joseph Simbakalia ambaye alikuwa ndio mgeni rasmi, lakini kutokana na shughuli za kimkoa ilishindikana kuhudhuria kwake katika uzinduzi huo na kuwakilishwa na Mkuu wa Wilaya Mhe. John Mongela.
Wakuu wa Idara kutoka Bayport baadaye walialikwa kwenye ofisi ya Mkuu wa Mkoa, ili kupewa shukrani za kipekee kutoka kwa Mkuu wa Mkoa kwa mchango wa shilingi milioni 20 ya ukarabati wa Shule ya Msingi Airport Kigoma.
Bw. Cheyo alisema, Bw. Ibrahim Kaduma ambaye aliongea kwa niaba ya kampuni alisema ahadi yetu kwa Tanzania imeonyeshwa hapa leo, huu mchango wa shilingi milioni 20 kwa ajili ya elimu ni ukweli usio na pingamizi kwamba Bayport ni kampuni imara na ipo hapa kubaki.
Katika miezi ijayo Bayport itafungua tawi jipya wilayani Kasulu katika Mkoa wa Kigoma. Bayport Tanzania imekua katika shughuli hii ya utoaji mikopo nchini kwa zaidi ya miaka minne na nusu. Kampuni inaendelea kukua zaidi Vijijini na Mijini na sasa tuna matawi 40 katika mikoa yote ya Tanzania Bara. Kampuni inaamini kuwa na matawi karibu na makazi ya wateja wetu na wao kupata huduma toka kwa mwakilishi wa Bayport ambaye ni mwanajumuiya na si tuu mteja kuweza kupata mtaji kwa haraka bali inamhakikishia faraja na imani kwamba kampuni yetu iko tayari kusikiliza mahitaji ya mteja hata kwa lugha asilia ikibidi, Alisema Bw. Cheyo
Taasisi ya Kifedha ya Bayport ni kikundi cha Pan-Afrika inayojihusisha na utoaji wa mikopo ambayo haina dhamana au amana kwa wafanyakazi walioajiriwa, ambao kulingana na kipato chao Benki za kibiashara hushindwa kuwapatia mitaji. Taasisi ya Bayport imeanzishwa mwaka 2002, na Makao yake makuu yako Mauritius.
Mafanikio ya shughuli zake za utoaji mikopo zimepanua wigo katika nchi sita, kutoka Ghana katika nchi za Afrika Magharibi, Uganda na Tanzania katika nchi za Afrika Mashariki, kupitia Zambia, Botswana hadi Afrika Kusini. Kundi la Bayport limetoa huduma kwa zaidi ya wateja 300,000 kupitia matawi yake 235 na zaidi ya wafanyakazi 2,500.
No comments:
Post a Comment