Sep 23, 2010

WAZIRI MKUU MIZENGO PINDA NA MATUKIO KATIKA PICHA NEW YORK

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisalimiana na Waziri Mkuu, wa Saint Vincent and Grenadines, Dr. Ralph Gonsalves kabla ya mazungumzo yao kwenye ukumbi wa Umoja wa Mataifa, New York Septemba 23, 2010. Wote wanahudhuria mkutano wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na Rais Yoweri Museveni wa Uganda (kulia) na Waziri MKuu wa Saint Vincent and Grenadines, Dr. Ralph Gonsalves katika kikao cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, New York Septemba 23, 2010. (Piocha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

TANZANIA NI NCHI YA KUPIGIWA MFANO KWA UTAWALA BORA NA DEMOKRASIA: OBAMA!

Na Mgaya Kingoba, Mbarali MAREKANI imesema kwamba Tanzania ni moja ya nchi inazozipigia mfano miongoni mwa nchi zinazoendelea, kwa uongozi bora na unaodumisha utawala bora na utawala wa sheria. Kwa mujibu wa Rais Jakaya Kikwete, Rais Barack Obama wa Marekani aliyasema hayo juzi wakati akihutubia mkutano wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa (UN) jijini New York, nchini humo. Rais Kikwete alisema wakati akihutubia mkutano mkubwa wa kampeni kwenye Uwanja wa Barafu mjini Rujewa wilayani hapa katika Mkoa wa Mbeya, kuomba kura kwa wananchi wa wilaya hiyo. Alisema muda mfupi kabla ya kuhutubia maelfu ya wananchi uwanjani hapo, alizungumza na Balozi wa Marekani nchini, Alfonso Leonhadt, na kumuelezea jinsi Rais Obama alivyoimwagia sifa Tanzania katika hotuba yake UN. “Kabla ya kupanda hapa jukwaani kuzungumza nanyi, mliniona nazungumza na simu…alikuwa Balozi wa Marekani, ananiuliza kama nimesikia hotuba ya Rais Obama jana usiku kwenye Umoja wa Mataifa,” alisema Rais Kikwete. “Nikamwambia niko huku nahangaika, nitasikia saa ngapi? Wakati mwingine niko hoi bin taaban hata kusikiliza redio au televisheni huna muda. “Ameniambia kuwa Rais Obama ameeleza misingi ya Marekani kusaidia nchi zinazoendelea, na mfano wake akatoa Tanzania. Akasema nchi yetu inaongoza kwa kujali utawala bora, utawala wa sheria, kuheshimu NGO,s, na tunatawala vizuri,” Rais Kikwete aliwaeleza wananchi. “Kama siyo mimi na akina Mwandosya, nani mwingine anayemsifu,” alisema Rais Kikwete akimtaja Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Profesa Mark Mwandosya, ambaye alikuwapo kwenye mkutano huo akiwa ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM (NEC) kupitia Mkoa wa Mbeya. Alisema kauli hizo za Marekani kuisifu Tanzania, hazitoi yeye, lakini kila anapofanya hivyo, baadhi ya watu huhoji kwani kila mara na Marekani. “Nikisema sifa hizi zinazotolewa na Marekani, watu wanasema, ‘huyu naye na Marekani kila siku.’ Wanasema wenyewe, siyo mimi,” alifafanua Rais Kikwete. Marekani imekuwa mshirika mkubwa wa maendeleo kwa Tanzania tangu Rais Kikwete aingie madarakani miaka mitano iliyopita, ikitoa ufadhili mkubwa katika miradi mbalimbali ya sekta za elimu, afya, miundombinu na nishati. Chini ya Shirika la Milllennium Challenge (MCC), Marekani itafadhili miradi ya umeme katika mikoa sita nchini; itajenga barabara kadhaa ikiwemo ya Tunduma- Laela- Sumbawanga na hivi karibuni ilitoa vitabu 800,000 kwa ajili ya shule za sekondari nchini hasa kwa masomo ya sayansi.

KALUNDE BAND YAENDELEA NA MAANDALIZI YA SAFARI YA MSUMBIJI!!

Mmoja wa wafadhili wa Bendi ya Kalunde Linus Mbanga (VIP) kulia akiteta jambo na rais wa bendi ya Kalunde Deo Mwanambilimbi wakati wa mazungumzo yao yaliyofanyika kwenye Hoteli ya New Africa ikiwa ni mikakati na mipango ya maadalizi ya safari ya bendi hiyo kwa ajili ya safari yao ya kuelekea nchini Msumbiji katika jiji la Maputo kwa ajili ya maonyesho kadhaa nchini humo.

Deo amesema “Tumepata mwaliko wa kwenda kutumbuiza nchini Msumbiji kwenye moja ya tamasha ambalo hufanyika kila mwaka hivyo tunatarajia kwenda kupiga nyimbo zote za Kalunde” alisema Mwanambilimbi.

Alisema mwaliko huo umekuja baada ya baadhi ya mashabiki wa bendi hiyo kuvutiwa na nyimbo wanazopiga.

Kalunde kwa sasa inatamba na nyimbo za ‘Itumbangwewe’, ‘Hilda’, ‘Nataka Kuzaa na Wewe’ , ‘Usiniguse’ ,’Fikiria’ na ‘Kilio Kilio’.

Pia imetoa vibao viwili vipya ambavyo ni ‘Fungua’ na ‘Maiwane’ ambazo tayari zimeanza kutamba katika kumbi za burudani ambazo bendi hiyo inapopiga.

Baadhi ya wanamuziki watakaoondoka na bendi hiyo ni Mwanambilimbi mwenyewe, Shehe Mwakichui, Junior Gringo, Deborah Nyangi, Sarafina Mshindo, Mwapwani Yahya, Othman Majuto na Remmy.

Rais wa Bendi Deo Mwanambilimbi akiimba katika moja ya maonyesho yao yanayofanyika kila alhamisi kwenye Hoteli ya New Africa jijini Dar es salaam.
Debora Nyange mmoja mwa wanamuziki watakaoondoka katika safari hiyo.
Mwanamuziki Junior Gringo akiim ba katika onyesho lao lao jioni kwenye Hoteli ya New Africa.
Edson Alen mpiga solo wa bendi ya Kalunde

Wateja wa Vodacom sasa kuneemeka na punguzo la bei

Ni kupitia programu ya Tuzo Pointi

Dar es Salaam, Kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom Tanzania imezindua programu mpya ya Tuzo Pointi ambayo itawawezesha wateja wake kupata punguzo kubwa la bei wakati wakipata huduma katika sehemu mablimbali kama mahotelini, ofisi za bima na madukani.

Mkuu wa Idara ya Mahusiano ya Wateja, Aika Matiku alisema kwamba huduma hiyo itawawezesha wateja wake kupata punguzo la kati ya asilimia 5 hadi 20 kutoka kwa wauzaji mbalimbali wa bidhaa hapa nchini.

Aliwataja baadhi ya watoaji wa huduma ambao wataanza nao kuwa ni duka la Woolworth, Sunrise Beach Resort na kampuni ya Bima ya Real Insurance. Hoteli za Kunduchi Beach Resort na Zanzibar Beach Resort zitaanza kutoa huduma baada ya kukamilisha taratibu.

Alisema wateja wanaoweza kupata punguzo hilo kubwa ni wale wenye pointi 250 za Tuzo na kuendelea.

“Tumeanzisha huduma hii kwa lengo la kuhakikisha kwamba wateja wetu wanapata huduma bora na kwa bei nafuu,” alisema.

Alisema huduma hiyo ni sehemu ya programu ya Tuzo Pointi ambayo lengo lake ni kuwazawadia wateja wake waaminifu na kuboresha maisha ya wateja wake.

Alisema mteja anapata pointi kwa njia kuu tatu. Moja ni kwa utumiaji ambapo wateja wa malipo ya kabla watakapotumiaSh 100 na wale wa malipo ya baada watakapotumia Sh 500 wote watapata pointi moja ya Tuzo.

Njia ya pili ni kwa kuongea, akifafanua njia hii alisema mteja akipokea simu kutoka mtandao mwingine atapata pointi moja ya Tuzo

Njia ya tatu ni ile ya mteja wa Vodacom atakapoendelea kuwa mteja wa Vodacom kwa wiki moja huku akitumia simu yake kwa kupokea simu, kupiga, kutuma ujumbe wa maneno au kupokea ujumbe wa maneno atapata pointi nyingine moja ya Tuzo

Alisema kwa wateja wa mikoani wataweza kupata huduma wakiwa huko huko kutoka kwa vituo mbalimbali vya huduma na maduka vilivyoko mikoani.

NI JAMBO JEMA KUWASAIDIA WENYE SHIDA!!

Mgombea Urais wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete, akiwa ameketi chini ardhini ili kumsikiliza Mama Sara Mageni wa Wilaya ya Makete, wakati mgombea huyo alipowasili kuhutubia mkutano wa kampeni. Sara alikuwa akitoa shukrani zake kwa Mheshimiwa Kikwete baada ya kumnunulia Bajaj ili kurahisisha shughuli zake, alipotembelea wilaya hiyo mwaka jana

Hifadhi yaTabaka la Hewa ya Ozoni Mwanza!!

Evelyn Mkokoi

Afisa Habari, Ofisi ya Makamu wa Rais

Serikali inakabiliana na changamoto kubwa ya wananchi kutokuelewa suala zima la sayansi ya hifadhi ya tabaka la hewa ya Ozoni.

Hayo yameeelezwa leo na Mkurugenzi wa Idara ya Mazingira kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais Dkt Julius Ningu, katika kilele cha maadhimisho ya Siku ya kimataifa ya hifadhi ya tabaka la Hewa ya Ozoni yanayofanyika kitaifa mjini Mwanza yanayoambatana na uzinduzi wa kituo na mafunzo ya kunasa na kusafisha gesi chakavu za majokovu na viyoyozi.

Dkt Ningu ameeleza kuwa changamoto hii ndo imepelekea serikali kusogeza huduma hii kwa karibu zaidi kwa jamii kwa kupitia mafunzo haya kwa walengwa ambao ni wanafunzi wa chuo cha veta, mafundi mchundo, mafundi mekanika na mafundi wa kawaida.

Akisoma hotuba ya ufunguzi, kaimu katibu tawala wa wilaya ya Njamagana Bw.Elias Makori ameeleza kuwa matumizi ya kemikali haribifu kwa tabaka la hewa ya Ozoni yanatumika zaidi katika nchi zinazoendelea kama vile Tanzania na yanaweza kuleta madhara makubwa sana kwa jamii ikiwa ni pamoja na magonjwa ya saratani ya ngozi, na ugonjwa wa mtoto wa jicho.

Bw. Makori ameeleza kuwa kituo cha veta mkoani Mwanza ni miongoni mwa vituo vitano vya kikanda nchini , vinavyolenga katika kutekeleza mpango wa serikali wa kuondosha matumizi kemikali haribifu kwa tabaka la hewa ya Ozoni.

Vituo vingine nchini vitakavyohusishwa na jukumu hili ni pamoja na VETA Dar, Mbeya, Kigoma na Zanzibar. Uhifadhi wa tabaka la hewa ya Ozoni ni utekelezaji wa mkataba wa Vienna na Montrial ambayo Tanzania ni nchi mwanachama.

Ujumbe wa mwaka huu unasema, ‘Hifadhi ya Tabaka la Hewa ya Ozoni “Tuzingatie Wajibu na Majukumu yetu.”

WADAU WA SEKTA YA NISHATI WAKUTANA KUJADILI CHANGAMOTO ZA UZALISHAJI UMEME NCHINI.

Kamishina wa Nishati na Petroli wa Wizara ya Nishati na Madini Injinia Bashir Mrindoko akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari kuhusu mkutanao wa mwaka wa wadau wa sekta ya Nishati unaojadili namna kukabiliana na changamoto zinazokwamisha maendeleo ya sekta nishati nchini leo jijini Dar es salaam.
Picha na Aron Msigwa – MAELEZO.

Wadau wa Sekta ya Nishati nchini wakifuatilia masuala mbalimbali wakati wa mkutano wa mwaka wa kupitia maendeleo ya sekta ya nishati nchini leo jijini Dar es salaam ambapo sekta ya nishati imeguswa kwa kufanyiwa maboresho ya uongezaji wa idadi ya watumiaji wa nishati ya umeme kutoka 14% mpaka kufikia 75% ifikapo mwaka 2033 pamoja na kuongeza idadi ya wateja wapya wanaounganishiwa umeme majumbani kwa mwaka kutoka idadi ya nyumba 60,000 mpaka kufikia 100,000

Wadau wa Sekta ya Nishati nchini wakifuatilia masuala mbalimbali wakati wa mkutano wa mwaka wa kupitia maendeleo ya sekta ya nishati nchini leo jijini Dar es salaam.

WAZIRI MKUU MIZENGO PINDA AKUTANA NA RAIS WA LIBERIA NA WAZIRI MKUU WA DENMARK!!

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza katika kikao cha kujadili maendeleo ya Millenia alichokiandaa kwa pamoja na Waziri Mkuu wa Denmark, L. Lokke Rasmussen (katikati) na Rais wa Liberia, E. Johnson Sirleaf (kushoto) jijini New York , Septemba 22, 2010.(Picha na Ofisi y a Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza katika kikao cha kujadili maendeleo ya Millenia alichokiandaa kwa pamoja na Waziri Mkuu wa Denmark, L. Lokke Rasmussen (kulia ) na Rais wa Liberia, E. Johnson Sirleaf aliyekaa katikatijijini New York , Septemba 22, 2010.(Picha na Ofisi y a Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda na Rais wa Liberia, E. Johnson Sirleaf wakifuatilia mkutano wa kujadili maendeleo ya millennia waliouandaa wakishirikiana na Waziri Mkuu wa Denmark L. Lokke Rasmussen jijini New York, Septemba 22, 2010. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda na Rais wa Liberia, E. Johnson Sirleaf (katikati) wakizungumza na Waziri Mkuu wa Denmark, L. Lokke Rasmusen baada y kikao walichokiandaa cha kujadili maendeleo ya Millenia kilichofanyika jijini New York Septemba 22, 2010. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

MAMA SALMA KIKWETE AKIWA MKOANI KILIMANJARO!!

Ziara ya Mwenyekiti wa Taasisi ya Maendeleo ya Wanawake (WAMA) Mama Salma Kikwete Mkoani Kilimanjaro kwaajili ya kuwahamasisha wanachama wa UWT kuhusu umuhimu wa kujitokeza kwa wingi siku ya kupiga kura katika Uchaguzi Mkuu wa rais, wabunge na madiwani utakaofanyika Oktoba 31-2010 nchini kote.
Hapa akimnadi mgombea kupitia Chama cha Mapinduzi CCM aliyepita bila kupingwa katika jimbo la Siha Mkoani kilimanjaro Agrey Mwanri.
(Picha na Mwanakombo Jumaa Maelezo)
Mwenekiti wa WAMA Mama Salma Kikwete akmnadi Ugombea ubunge jimbo la Vunjo Chrispin Meela.
Mwenyekiti wa WAMA Mama Salma Kikwete akimnadi mgombea ubunge wa jimbo la Hai mkoani Kilimajaro Fuya Kimbita
Mwenyekiti wa WAMA Mama Salma Kikwete akiwanadi wagombea wa udiwani kupitia chama cha Mapinduzi CCM na mgombea Ubunge wa Hai Kilimanjaro.
Wanachama wa UWT jimbo la Vunjo na Moshi Vijijini wakionyesha mshikamano wao kuelekea Uchaguzi Mkuu wa rais, wabunge na madiwani utakaofanyika Oktoba 31,2010

BAN KI MOON AMTEUA MKAPA KUONGOZA JOPO LA KUANGALIA MCHAKATO WA KURA YA MAONI SUDAN KUSINI


Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki Moon

Na Mwandishi Maalum,
New York

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki Moon amemteua Rais Mstaafu wa Tanzania Benjamin William Mkapa ,kuongoza jopo la tume ya watu watatu itakayoangalia mchakato wa kura za maoni Sudan Kusini na Jimbo la Abyei.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Umoja wa Mataifa leo, uteuzi huo unatokana na maombi yaliyotolewa pande mbili zinazounga mkono makubaliano ya amani ya kudumu nchini Sudan.Pande hizo ni Serikali ya Sudan na Kikundi cha People’s Liberation Movement.

Wengine walioteuliwa ni aliyewahi kuwa Waziri wa Mambo ya Nje wa Ureno, Bw. Antonio Moteiro na Bw. Bhojraji Pokharel Mwenyekiti wa zamani wa Tume ya Uchaguzi nchini Nepal.

Akizungumzia uteuzi huo, Ban Ki Moon anasema ana imani kwamba tume aliyoiteua itasaidia kufanyika kwa kura hiyo ya maoni itakayozingatia matakwa ya watu wa Sudan Kusini na Jimbo la Abyei

Jukumu kubwa la tume hiyo pamoja na mambo mengine ni kufanya ziara za mara kwa mara nchini Sudani katika kipindi chote cha mchakato wa kuelekea kura za maoni. Upigaji wa kura za maoni unatarajiwa kufanyia mwezi Januari 2011

Tume hiyo pia inatarajiwa kukutana na kushirikiana na pande zote zinazohusika katika mkataba wa amani, tume inayoratibu kura ya maoni, jumuia za kiraia na makundi ya waangalizi wa kura hiyo.

Pamoja na kutoa taarifa kwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, tume hiyo itafuatilia kwa karibu mchakao mzima wa kura za maoni na pia masuala ya kisiasa na hali ya usalama.

Tume itatakiwa pia kufanya kazi ya kuhakikisha inaimarisha imani ya mchako wa kura za maoni, kuhakikisha na kuzitaka pande husika na viongozi kuchukua hatua za pamoja za kutatua matatizo yoyote au migogoro itakayojitokeza.

Wananchi wa Sudan Kusini watapiga kura yao ya maoni kuamua iwapo wajitenge na Serikali ya Khartoum ,wakati wananchi wa Jimbo la Abyei linalogombaniwa na pande zote mbili ,wao watapiga kura ya kuamua wajiunge na upande upi iwapo Sudan Kusini itajitenga na Kaskazini.

Upigaji wa kura ya maoni ni miongoni wa mabadiliko yaliyofikiwa katika Mkataba wa Amani wa mwaka 2005(CPA), uliomaliza vita vya zaidi ya miongo miwili nchini humo. Aidha kura hiyo ni muhimu sana kwa mstakabali wa nchi yote ya Sudan.

Sep 22, 2010

tigo wazindua kituo cha huduma kwa wateja temeke


Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Chiku Gallawa akikata utepe kuzindua rasmi kituo cha huduma kwa wateja cha Tigo, Temeke eneo la Mtoni kwa Aziz Ali jijini Dar es Salaam jana. Kushoto ni Ofisa Uhusiano wa Tigo, Jackson Mmbando na wanne kushoto ni Meneja Matawi ya Tigo,Innocent Mayawa.
Mkuu wa Wilaya ya Temeke,Chiku Gallawa (kushoto) akijisajili na huduma ya Tigo Pesa muda mfupi baada ya kuzindua Kituo cha Huduma kwa Wateja cha Tigo, Temeke, Dar es Salaam jana. Kulia ni Ofisa Huduma kwa Wateja wa kituo hicho, Josephine Reuben wa pili kushoto ni Ofisa Uhusiano wa kampuni hiyo, Jackson Mmbando na katikati ni Meneja Matawi wa Tigo, Innocent Mayawa.
Ofisa Huduma kwa Wateja wa Tigo, David Kagusa (kulia) akikabidhi zawadi kwa Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Chiku Gallawa mara baada ya mkuu huyo kuzindua kituo cha Huduma kwa Wateja cha Tigo, Temeke, Dar es Salaam jana.

KCB BANK YAKABIDHI MSAADA WA VITABU SHULE YA SEKONDARI KINONDONI MUSLIM!!

Mkurugenzi Mtendaji wa KCB Tanzania Joram Kiarie akimkabidhi Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Kinondoni Muslim, Rajabu Mruma msaada wa vitabu vya masomo na samani za ofisini kwa ajili ya walimu vyenye thamani ya Milioni 4/- ili kusaidia kupunguza uhaba wa vifaa unaoikabili pamoja na kuinua kiwango cha elimu. Kushoto ni Kaimu mkuu wa shule hiyo, Mohammed Songo.
Mkurugenzi Mtendaji wa KCB Tanzania Joram Kiarie akiwaeleza jambo wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Kinondoni Muslim Tiba Kalufya na Mayasa Hemed mara baada ya kuikabidhi shule hiyo msaada wa vitabu vya masomo na samani za ofisini kwa ajili ya walimu vyenye thamani ya Milioni 4/- ili kusaidia kupunguza uhaba wa vifaa unaoikabili pamoja na kuinua kiwango cha elimu. Kulia ni mkuu wa idara ya masoko na mahusiano wa benki hiyo Christina Manyenye.
Mkurugenzi Mtendaji wa KCB Tanzania Joram Kiarie akizungumza na baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Kinondoni Muslim, mara baada ya hafla ya kukabidhi msaada wa vitabu vya masomo na samani za ofisini kwa ajili ya walimu vyenye thamani ya Milioni 4/- ili kusaidia kupunguza uhaba wa vifaa unaoikabili pamoja na kuinua kiwango cha elimu iliyofanyika shuleni hapo. (Na Mpigapicha Wetu).
Wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Kinondoni Muslim wakijisomea vitabu vilivyotolewa na benki ya KCB Tanzania mara baada ya hafla ya makabidhiano ya msaada wa vitabu vya masomo na samani za ofisini kwa ajili ya walimu vyenye thamani ya Milioni 4/- ili kusaidia kupunguza uhaba wa vifaa unaoikabili pamoja na kuinua kiwango cha elimu iliyofanyika jana (leo) jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa KCB Tanzania Joram Kiarie akiwapa vitabu wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Kinondoni Muslim, mara baada ya hafla ya kukabidhi msaada wa vitabu vya masomo na samani za ofisini kwa ajili ya walimu vyenye thamani ya Milioni 4/- ili kusaidia kupunguza uhaba wa vifaa unaoikabili pamoja na kuinua kiwango cha elimu.

RASCOM, is an intergovernmental, commercial satellite organization in Africa!!

RASCOM, is an intergovernmental, commercial satellite organization and the expression of the strong willingness of the African Governments to pool their efforts in a view to providing the African continent with telecommunications infrastructure based on space technology.

It is intended not only to give African national networks (countries) the opportunity to interconnect directly

without third party networks, but also to

supplement their existing telecom infrastructure by allowing them to provide services in isolated areas where there is no existing infrastructure, and complement the other technologies in order to provide a total solution to our users.

Besides the above objectives, the Mission of RASCOM is also to provide telecommunications services at affordable costs and supporting the creation of access to remote and underserved areas making universal service a reality in Africa.

RASCOM has a membership of 45 African countries including Tanzania. The headquarters are in Abidjan/Ivory Coast. We are here today for the meeting of Board of Directors of RASCOM following an invitation from TTCL which is one of the members of the Board of RASCOM.

To achieve its mission, RASCOM has established strategic partners in RascomStar-QAF Company, which has, under an Agreement, the responsibility to implement the RASCOM telecommunications satellite system dedicated to the African continent.

Our operating company, RascomStar-QAF is entrusted, among other responsibilities, with the task of the operation, maintenance and marketing of the services offered by the RASCOM satellites.

The first Pan African satellite was launched in December 2007 from Kourou/ French Guyana in South America and commercial operations started in 2008. Due to some technical problems it encountered after the launch which reduced its life time, it became necessary to quickly manufacture and launch a replacement satellite.

The current satellite is still in orbit providing services. We are already providing Band Lease Services (BLS) with the current satellite with a continental connectivity to more than 30 African countries to support the Pan African e-network for e-health and e-learning which is a project promoted by the African Union and the Indian Government.

Those who like sports will no doubt remember the under 17 football world cup which took place in Nigeria. These matches were transmitted live using our satellite.

On 4th August, 2010 the second Pan African satellite was launched from the same launch site. Those who are using the first satellite will have a seamless transfer to the replacement satellite.

All of this has been possible thanks to the partnership with other investors: Libyan African Investment Portfolio (LAIP) and Thales Alenia Space (TAS) of France.

We also had financing from some development banks in Africa which are Libyan Foreign Bank (LFB), African Development Bank (AfDB), West African Development Bank (BOAD) and Central African Development Bank (BDEAC) which participated in this project in a form of loan.

The following services will be provided by the satellite:

Broadband Connectivity Services (BCS) which will make it possible to create direct connectivity among all African countries. We will also have Telephony Services (TES) which will extend access to remote and underserved areas in Africa using a special designed terminal supporting voice, data (internet) and radio/TV reception. Band Lease Services (BLS) will also be available. The satellite will also support the transmission of both radio and television broadcasting services.

The RASCOM satellite will be a possible partner for the NEPAD e-school project whose objective is to see internet connectivity in more than 600,000 schools in Africa. We are also working together with Pan African Postal Union (PAPU) and African Telecommunications Union (ATU) in the e-Post project which plans to use ICT in bringing new services within the postal network in Africa.

RASCOM is following with a lot of interests the developments taking place in Africa with the deployment of optical fiber around Africa and across regional networks. This is a great initiative which should be encouraged and the participation of Governments is testimony that the development of the ICT infrastructure is now being given the deserved attention and importance. But I am also convinced that deploying a number of different technologies like fiber and satellite will only complement each other. No technology can singly meet the demands of ICT.

It is a general agreement that Africa needs huge capacities to support development of ICT and to create affordability levels as volumes increase. We also agree that the focus for broadband development should not only be in major towns but should be extended into rural Africa to support a number of e-services. This is why all developments aimed at expanding infrastructure in the continent are most welcome.

We are very thankful to the Leaders of Africa who have continuously been very supportive of the RASCOM project through the African Union.

This is just the beginning

Already we are in the advanced stages in terms of the planning and design for the next generation satellites with very large bandwidths which will respond to the needs of Africa in terms of services, broadband requirement and cost to the users.

The launch event of the second Pan African satellite served to assure the African Continent of RASCOM’s long term commitment to its mission of creating capacities to support Connectivity in Africa and access to information and communication to underserved and remote areas in Africa. For more information on RASCOM, please visit the RASCOM Website

UTURUKI YAANDAA MAONYESHO YA BIDHAA ZAKE JIJINI DAR ES SALAAM!!

NA ZAHRA MAJID- MAELEZO

22/0/2010.

UBALOZI wa Uturuki nchini Tanzania unatarajia umeandaa maonyesho ya pili ya bidhaa za nchi hiyo yatakayoanza Septemba 30 , mwaka huu hadi Oktoba3, mwaka huu kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar-es-salaam.

Hayo yalisemwa jana na balozi wa Uturuki nchini, Tanzania Dk. Sander Gurbuz katika mkutano wake na waandishi wa habari wa ambapo alisema Tanzania na Uturuki zina uhusiano mzuri hivyo , maonyesho hayo kwani yatasaidia kudumisha ushirikiano baina ya nchi hizo.

Alizitaja baadhi ya bidhaa zitakazoonyeshwa ni za nguo, vyakula ujenzi na zana za kilimo.

Dr. Gurbuz pia alibainisha kuwa Uturuki imewekeza katika sekta mbalimbali nchini kama vile kilimo, afya,madini, elimu , nguo na utalii.

“Tumewekeza nchini Tanzania ili tuweze kuzalidha bidhaa mbalimbali kwa ajili ya kuuza ndani ya nchi na nje ya nchi ,” alisema Balozi Gurbuz.

Balozi huyo alisema pia wameandaa mdahalo wa wa wafanyabiashara utakaohusisha nchi za Afrika Mashariki ukaohudhuriwa wajumbe 300 ambao unaotarajiwa kufanyika Ferbuari mwakani mara baada ya uchaguzi mkuu kumalizika. Mdahalo huo unatarajiwa kufanyika jijini Dar es Salaam.

Alielezea pia katika sekta ya elimu wana utaratibu wa kutoa ufadhili wa masomo ya juu huchukua wanafunzi 35 mpaka 45 kwa mwaka.

Aliongeza kuwa wamekuwa wakiwaleta madaktari wenye utaalamu mbalimbali kuja kufanya tiba nchini bure wapatao kati ya 25 hadi 35 jijini Dar es Salaam na wana mpango wa wa kuwaleta wengine ambao watatoa tiba hiyo hadi nje ya mkoa huo.

Balozi huyo alisema pia wana mpango wa kuandaa ziara ya waandishi wa habari kutembela nchi hiyo

Washindi watano wa Shindano la Chemsha Bongo kuzuru China!!

Benjamin Sawe na Vicent Tiganya

Maelezo -Dar es Salaam

Imeelezwa kuwa Serikali ya China na Tanzania zimekuwa na ushirikiano wa muda mrefu katika sekta ya habari ambapo shirika la habari la China (Xinhua News Agency) limekuwepo

nchini kwa miaka mingi likiandika habari za maendeleo.

Hayo yamesemwa jana jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi wa Idara ya Habari,Utamaduni na Michezo Bwana Clement Mshana katika sherehe za kutuoa tuzo kwa washindi wa Chemsha Bongo kuhusu miaka 45 ya uhusiano wa kibalozi kati ya serikali ya China na Tanzania.

Bwana Mshana alisema licha ya kuwa na kukabiliana na propaganda za nchi za magharibi shirika la habari la China (Xinhua News Agency) limekuawa likiandika habari za maendeleo na kuongeza sauti ya nchi zinazoendelea.

Alisema vipindi vinavyotangazwa na shirika hilo kwa lugha ya Kiswahili vimesaidia kuimarisha ushirikiano na udugu uliopo kati ya Tanzania na Serikali ya China.

“Ni jambo la kufurahisha kuona kuwa kutokana na mawasiliano kati ya China na Tanzania katika sekta mbalimbali ,Watanzania wengi wamekuwa na hamu kubwa ya kuelewa mambo ya China hivyo kupelekea watu wengi kujifunza lugha ya Kichina.”.Alisema Mkurugenzi Mshana.

Alisema shindano la Tuzo kwa waandishi wa Chemsha Bongo lililoendeshwa kwa mara ya kwanza kwa mara ya kwanza kwa ushirikiano kati ya vyombo vya Habari vya China na Tanzania limeutangaza,limeelimisha na kudumisha uhusiano kati ya Tanzania na China.

Katika hatua nyingine Balozi wa China nchini Tanzania Liu Xinsheng mashindano ya Chemsha Bongo yalilenga kufuata moyo wa ushirikiano na mawasiliano kati ya China na Afrika katika mambo ya Utamaduni

Alisema katika kuadhimisha miaka 45 ya uhusiano kati ya China na Tanzania Radio za China na Tanzania zimefanikiwa kufanya kufanya ushirikiano katika matangazo ya Chemsha Bongo hiyo zilitangaza vipindi mbalimbali vya utangazaji vya Kiswahili vya kukumbusha mchakato wa kukua kwa urafiki kati ya nchi ya China na Tanzania.

Balozi Xinsheng alifafanua kuwa Chemsha Bongo hiyo imeweka daraja la kuongeza urafiki,maelewano na mawasiliano kati ya wachina na watanzania na kusukuma mbele maendeleo ya uhusiano wa wenzi wa mikakati kati ya China na Tanzania.

Katika mashindano ya ya Chemsha Bongo Radio ya China ya kimataifa (CRI), TBC na Sauti ya Tanzania Zanzibar zilifanya ushirikiano katika kurusha matangazo ya shindano la Chemsha Bongo ambapo wasikilizaji walitakiwa kutoa mapendekezo kwa ajili ya kuendeleza zaidi kati ya China na Tanzania

Aidha mashindano hayo yalishirikisha zaidi ya wasikilizaji 1600 kutoka mikoa 20 ya Tanzania ambapo washindi watano maalum watakwenda kutembelea nchi ya China kwa siku kumi na washindi wa pili walipata zawadi ya Vereheni ambapo washindi wa tatu walipata zawadi ya Luninga za rangi.

FM ACADEMIA KUTOA ZAWADI KWA WAKAZI WA MBAGALA KUU!!

WAANDAJI wa Onesho la Bendi ya FM
Academia wazee wa Ngwasuma wametangaza zawadi kwa
washindi watakaibuka katika shindano
maalum la kucheza mitindo ya bendi hiyo,
kwenye utambulisho wa bendi hiyo
utaofanyika kesho kwenye Ukumbi wa Nawina Mbagala Kuu jijini Dare es laam salaam.
Mratibu wa Onesho hilo Zahor Said, alisema kuwa usiku huo
maalum wa Ngwasuma utakuwa na burudani mbalimbali ambazo
zitausindikiza utambulisho huo.
Said alisema watafanya utambulisho huo kwa kusindikizwa na
vikundi vya unenguaji vya kiduku.
Alisema utambulisho huo wa albamu ya Vuta nikuvute utakuwa
chini ya Rais wa bendi hiyo Nyoshi El Saadat watapiga nyimbo zote 11
zilizopo kwenye Albamu hiyo ikiwa ni pamoja na nyimbo za
zamani.
Alizitaja nyimbo zilizobeba albamu hiyo kuwa ni Heshima kwa
Wanawake ambayo ilipata tunzo mwaka jana,Mwili wangu,
Usiku wa juma tano na Jasmini.
Nyimbo zingine ni Angalia shida yangu,Mgeni,Heiken
Ngwasuma,Moses Katumbi,Fadhila kwa mama Intro Ngwasuma
Mathematics na vuta ni kuvute ambayo imebeba jina la albam.
Usiku huo umedhaminiwa na Henkein Bear, Kampuni ya Inoch,
Blog za JaneJohn5, Mamapipiro na Full Shangwe.

Ridhiwani akemea wanaotumia udini katika kampeni!

Na Richard Mwaikenda,Tunduru.
MJUMBE wa Kamati ya Utekelezaji ya Baraza Kuu la Umoja wa Vijana
wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Taifa, Ridhiwani Kikwete, amekemea
tabia ya baadhi waumini wa dini ya kiislamu kudhihaki dini zingine
kwa kuwaita makafiri baadhi ya wagombea katika kampeni za Uchaguzi
Mkuu zinazoendelea nchini.
Ridhiwani,alikemea tabia hiyo katika mkutano wa kampeni juzi mjini
Tunduru, baada ya kupata taarifa kuwa kuna baadhi ya viongozi wa
Chama cha Wananchi (CUF) wanatumia udini katika mikutano yao ya
kampeni kwa kuwaambia wananchi kuwa wasimchague Mgombea ubunge wa
Jimbo la Tunduru Kaskazini kupitia Chama Cha Mapinguzi (CCM),
Injinia Ramo Makani kwa kumuita kafiri, kwa vile yeye ni mkristo.
"Jamani mimi pia ni mwislamu, si vizuri kumwita mwenzio kafiri, si
neno zuri, kwani kila mmoja anayo haki ya kufuata imani ya dini
anayoitaka na isitoshe katika uchaguzi huu hatutafuti Imamu wala
Sheikh wa kutuongoza bali tunatafuta kiongozi imara wa kuleta
maendeleo ya jimbo na nchi kwa ujumla,"alisema Ridhiwani huku
akishangiliwa na umati wa watu katika mkutano uliofanyika Lindi
mjini.
Alisema kuwa hata wakiamua kumchagua Imamu ama Sheikh kuwa mbunge,
kwa hali ya kawaida hatokuwa na muda wa kwenda kuswalisha
msikitini, kwani muda wake mwingi ikiwezekana hata kufikia miezi
sita ataupoteza kwa kuhudhuria vikao vya bunge Dodoma, hivyo kwenda
tofauti na maadili ya kazi hiyo ya kiroho.

KALUNDE BAND KUTIKISA JIJI LA MAPUTO OKTOBA 2, 2010!!

BENDI ya muziki wa dansi ya Kalunde imepata mwaliko wa kwenda kutumbuiza Jijini Maputo nchini Msumbiji.

Akizungumza Jijini Dar es Salaam jana Rais wa bendi hiyo Deo Mwanambilimbi alisema itatumbuiza Oktoba 2 mwaka huu.

Aidha aliongeza kwa kusema kuwa bendi hiyo inatarajia kuondoka nchini Oktoba Mosi na wanamuziki wake wote.

“Tumepata mwaliko wa kwenda kutumbuiza kwenye moja ya tamasha ambalo hufanyika kila mwaka hivyo tunatarajia kwenda kupiga nyimbo zote za Kalunde” alisema Mwanambilimbi.

Alisema mwaliko huo umekuja baada ya baadhi ya mashabiki wa bendi hiyo kuvutiwa na nyimbo wanazopiga.

Kalunde kwa sasa inatamba na nyimbo za ‘Itumbangwewe’, ‘Hilda’, ‘Nataka Kuzaa na Wewe’ , ‘Usiniguse’ ,’Fikiria’ na ‘Kilio Kilio’.

Pia imetoa vibao viwili vipya ambavyo ni ‘Fungua’ na ‘Maiwane’ ambazo tayari zimeanza kutamba katika kumbi za burudani ambazo bendi hiyo inapopiga.

Baadhi ya wanamuziki watakaoondoka na bendi hiyo ni Mwanambilimbi mwenyewe, Shehe Mwakichui, Junior Gringo, Deborah Nyangi, Sarafina Mshindo, Mwapwani Yahya, Othman Majuto na Remmy.

THE DON HIMSELF

Karibuni sana kwenye blog hii ya kijamii iliyosheheni makila kitu kuanzia siasa uchumi afya na burudani kwa ujumla wake.uingiapo kwenye blog hii ni mengi ambayo utapata nafasi ya kukutana nayo,kumbuka mawazo yako ndo hasa yanayojenga na kunifanya niwe na ufanisi zaidi.kariiiiiiibuuuuuuuuuuuu saaaaaaaaaaaaaaanaaaaaaaaaa.(THE DJ HIMSELF-JIWE)

Followers

BLOG ZA MARAFIKI

Search This Blog

ZILIZOPITA

DUNIA MUZIMA