Sep 22, 2010

Ridhiwani akemea wanaotumia udini katika kampeni!

Na Richard Mwaikenda,Tunduru.
MJUMBE wa Kamati ya Utekelezaji ya Baraza Kuu la Umoja wa Vijana
wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Taifa, Ridhiwani Kikwete, amekemea
tabia ya baadhi waumini wa dini ya kiislamu kudhihaki dini zingine
kwa kuwaita makafiri baadhi ya wagombea katika kampeni za Uchaguzi
Mkuu zinazoendelea nchini.
Ridhiwani,alikemea tabia hiyo katika mkutano wa kampeni juzi mjini
Tunduru, baada ya kupata taarifa kuwa kuna baadhi ya viongozi wa
Chama cha Wananchi (CUF) wanatumia udini katika mikutano yao ya
kampeni kwa kuwaambia wananchi kuwa wasimchague Mgombea ubunge wa
Jimbo la Tunduru Kaskazini kupitia Chama Cha Mapinguzi (CCM),
Injinia Ramo Makani kwa kumuita kafiri, kwa vile yeye ni mkristo.
"Jamani mimi pia ni mwislamu, si vizuri kumwita mwenzio kafiri, si
neno zuri, kwani kila mmoja anayo haki ya kufuata imani ya dini
anayoitaka na isitoshe katika uchaguzi huu hatutafuti Imamu wala
Sheikh wa kutuongoza bali tunatafuta kiongozi imara wa kuleta
maendeleo ya jimbo na nchi kwa ujumla,"alisema Ridhiwani huku
akishangiliwa na umati wa watu katika mkutano uliofanyika Lindi
mjini.
Alisema kuwa hata wakiamua kumchagua Imamu ama Sheikh kuwa mbunge,
kwa hali ya kawaida hatokuwa na muda wa kwenda kuswalisha
msikitini, kwani muda wake mwingi ikiwezekana hata kufikia miezi
sita ataupoteza kwa kuhudhuria vikao vya bunge Dodoma, hivyo kwenda
tofauti na maadili ya kazi hiyo ya kiroho.

No comments:

THE DON HIMSELF

Karibuni sana kwenye blog hii ya kijamii iliyosheheni makila kitu kuanzia siasa uchumi afya na burudani kwa ujumla wake.uingiapo kwenye blog hii ni mengi ambayo utapata nafasi ya kukutana nayo,kumbuka mawazo yako ndo hasa yanayojenga na kunifanya niwe na ufanisi zaidi.kariiiiiiibuuuuuuuuuuuu saaaaaaaaaaaaaaanaaaaaaaaaa.(THE DJ HIMSELF-JIWE)

Followers

BLOG ZA MARAFIKI

Search This Blog

ZILIZOPITA

DUNIA MUZIMA