Mmoja wa wafadhili wa Bendi ya Kalunde Linus Mbanga (VIP) kulia akiteta jambo na rais wa bendi ya Kalunde Deo Mwanambilimbi wakati wa mazungumzo yao yaliyofanyika kwenye Hoteli ya New Africa ikiwa ni mikakati na mipango ya maadalizi ya safari ya bendi hiyo kwa ajili ya safari yao ya kuelekea nchini Msumbiji katika jiji la Maputo kwa ajili ya maonyesho kadhaa nchini humo. Deo amesema “Tumepata mwaliko wa kwenda kutumbuiza nchini Msumbiji kwenye moja ya tamasha ambalo hufanyika kila mwaka hivyo tunatarajia kwenda kupiga nyimbo zote za Kalunde” alisema Mwanambilimbi.
Alisema mwaliko huo umekuja baada ya baadhi ya mashabiki wa bendi hiyo kuvutiwa na nyimbo wanazopiga.
Kalunde kwa sasa inatamba na nyimbo za ‘Itumbangwewe’, ‘Hilda’, ‘Nataka Kuzaa na Wewe’ , ‘Usiniguse’ ,’Fikiria’ na ‘Kilio Kilio’.
Pia imetoa vibao viwili vipya ambavyo ni ‘Fungua’ na ‘Maiwane’ ambazo tayari zimeanza kutamba katika kumbi za burudani ambazo bendi hiyo inapopiga.
Baadhi ya wanamuziki watakaoondoka na bendi hiyo ni Mwanambilimbi mwenyewe, Shehe Mwakichui, Junior Gringo, Deborah Nyangi, Sarafina Mshindo, Mwapwani Yahya, Othman Majuto na Remmy.




No comments:
Post a Comment