Aug 28, 2010

Uzinduzi wa Kampeni za Chadema wafanyika Jangwani.


Mgombea Urais wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dr. Willbrod Slaa akizungumza leo jioni wakati wa uzinduzi wa kampeni na ilani ya chama chao mbele ya maelfu ya watu waliofika kuushuhudia uzinduzi huo katika viwanja vya jangwani.Slaa alisema kuwa akipewa ridhaa ya kuiongoza nchi hii basi atahakikisha ndani ya siku 100 za kwanza,katiba ya jamhuri ya Muungano wa Tanzania inafanyiwa marekebisho makubwa na pia kuhakikisha mfumo wa Elimu hapa nchini unabadilishwa kabisa.
Mgombea Urais wa chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Dr. Willbrod Slaa akimtambulisha rasmi mkewe mbele ya maelfu ya watu waliofika kwenye uzinduzi wa kampeni na ilani ya chama hicho jioni ya leo katika viwanja vya jangwani.
Mwenyeki wa chama cha CHADEMA,Freeman Mbowe akimkabidhi vitabu vya Ilani ya chama hicho kwa mgombea Urais wa chama hicho Mh Willbrod Slaa leo jioni katika viwanja vya Jangwani jijini Dar mara baada ya kuizindua.
Mwenyeki wa chama cha CHADEMA,Freeman Mbowe akionesha vitabu vya Ilani ya chama chao mara baada kuizindua leo jijini Dar ndani ya viwanja vya Jangwani.
Muasisi wa vyama vingi nchini na Mwenyekiti wa kwanza wa Chama cha NCCR-Mageuzi, Mabere Marando, ambaye pia amejiunga na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema),akionesha kitabu cha Ilani ya chama hicho mbele ya Wananchi,Marando aliongeza kwa kusema kuwa siku ya Jumatatu wataweka pingamizi kwa mgombea wa chama cha CCM,Mh DK.Jakaya Kikwete kwa kudaiwa kukiuka baadhi ya sheria za Uchaguzi.
Aliyekuwa Mgombea Ubunge kwa tiketi ya chama cha CCM,na baadae akahamia chama cha CHADEMA hivi karibuni,John Shibuda akizungumza mbele ya wananchi leo jioni wakati chama hicho kilipokuwa kikizindua kampeni na Ilani yake katika viwanja vya Jangwani na kuhudhuriwa na mamia ya watu.
Msanii mkongwe wa muziki wa kizazi kipya na Mgombea Ubunge kwa tiketi ya chama cha CHADEMA jimbo la Mbeya mjini,Joseph Mbilinyi a.k.a Mr II a.k.a Sugu akiimba moja ya wimbo wake uitwao wananiita Sugu ambao ulionekana kuwachangamsha vijana wengi waliofika viwanjani hapo jioni ya leo wakati wa uzinduzi wa kampeni ya chama hicho pamoja na Ilani yake.
Mwanasheria wa chama cha CHADEMA na mgombea Ubunge wa jimbo la Tabora Mjini,Tundu Lisu akiwasalimia wananchi kwa nguvu.
Mwenyeki wa chama cha CHADEMA,Freeman Mbowe akijaribu kuwatuliwa baadhi Wananchi kuwa wawe na utulivu hakuna kitakachoharibika,Mbowe ilibidi awatulize Wananchi mara baada kubaini shirika la utangazaji la TBC1 kukatisha matangazo ya uzinduzi wa kampeni ya chama hicho yaliyokuwa yakirushwa LIVE na hata kuthubutu kutaka kumpiga mmoja wa watangazaji wa kituo hicho, na baadae TBC1 waliamriwa waondoke uwanjani hapo kwa usalama wao.
Mgombea Urais kwa Chama cha CHADEMA,Mh.Willibrod Slaa akiwapungia wananchi mbalimbali waliofika kwenye viwanja vya Jangwani leo jioni mara ya kushuka kwenye gari.
Mtangazaji wa Mahiri wa TBC1 Marin Hassan Marin akisindikizwa na askari wa usalama kujaribu kuzuia lolote baya lisimkute nalo,wakielekea kwenye gari kwa lengo la kuondoka kabisa eneo la tukio,hata hivyo baadhi ya wananchi waliokuwa na jazba ya tukio hilo waliendelea kulalama mpaka Mwenyekiti wa chama cha CHADEMA,Freeman Mbowe aliposimama na kuwasihii wananchi watulie na amani itawale eneo hilo la jangwani,na kweli baadae hali ikawa shwari na uzinduzi wa kampeni ukaendelea.
maelfu ya wanachadema waliofika katika viwanja vya jangwani leo.
Mgombea Ubunge kwa tiketi ya chama cha CHADEMA jimbo la Kawa,Halima Mdee akipitisha bakuri la kuomba msaada kutoka kwa watu mbalimbali waliofika viwanjani hapo,fedha hizo ambazo imeelezwa kuwa zitatumika kwenye mbio za kampeni ambazo wamezindua leo na wanatarajia kuzianza hivi karibuni Tanzania nzima.

wadau wakiwa juu ya mti ili kuweza kupata kila kinachoendelea katika viwanja vya jangwani leo.
Askari Polisi wakituliza ghasia zilizotaka kuletwa na wanachama wa Chadema katika gari la kurushia matangazo la Television ya Taifa TBC.
Gari la matangazo la TBC.
wana Chadema wakiwasikiliza viongozi wao leo.
wakikumbatiana kwa kusabahiana.
walielekea jukwaa kuu.
gari lililommbeba mgombea urais wa Chadema likiwasili katika viwanja vya jangwani leo.
moja ya vioja vilivyokuwepo jangwani leo.
umati wa wanachadema leo.
(kwa msaada wa blog jirani)

Happy Birthday Ankal Michuzi


Leo ni siku kuu ya kuzaliwa Ankal a.k.a Mzee wa Libeneke mkuu Issa Michuzi.hivyo nami nikiwa kama mdau mkuu wa libeneke sina budi kumtakia kila la kheri katika sikukuu yake hii na kumuombea kwa mungu azidi kumjaalia afya njema na maisha marefu.

HAPPY BIRTHDAY ANKAL

Rais Kikwete Awasili Mkoani Kigoma


Rais Jakaya kikwete akipungia mkono baada ya kuwasili kijijini Buhingwe, Kigoma vijijini, kwa helikopta akitokea Ngara na kuelekea Uvinza
Rais Jakaya Kikwete akiwa na watoto wa kijiji cha Buhingwe.
Rais Kikwete akiwapungia wananchi wa kijiji cha Buhingwe kilichopo Kigoma vijijini.
Rais Kikwete akiwahutubia wananchi wa kijiji cha Buhingwe,Kigoma vijijini.
Wananchi wa Uvinza wakimpungia Rais Kikwete wakati akiwahutubia.

Aug 27, 2010

TEGETE,YONDANI,UHURU NJE TIMU YA TAIFA

KOCHA WA TAIFA STARS JAN PAULSEN

Wakongwe watano TAIFA STARS wakosa safari ya Algeria

WACHEZAJI wakongwe WATANO na wachezaji WAWILI wa timu ya taifa, TAIFA STARS wameachwa na kocha JAN PAULSEN katika kikosi kitakachosafiri kwenda nchini ALGERIA mchezo uliopangwa kuchezwa SEPTEMBA TATU.

Kocha PAULSEN amewaacha JUMA KASEJA na ATHUMAIN IDD kutokana na kuwa wagonjwa wakati wachezaji wengine WATANO wakidaiwa kushuka kiwango.

Wachezaji hao ni ABDULHALIM HUMUDU, KELVIN YONDAN, JUMA JABU, UHURU SULEIMAN na JERRISON TEGETE.

Kikosi cha TAIFA STARS kitakachokwenda nchini humo kinajumuisha wachezaji ISHIRINI na kitaondoka AUGOST 31 mwaka huu.

HAPPY B,DAY MWAMBA WA KASKAZINI.

Namshukuru Mwenyezi Mungu na wapenzi wa muziki wangu kuwa pamoja nami..............ts Johmakini's birthday.
cheers.
(kwa msaada wa blog jirani)

MARUFUKU WASANII WASIOSAJILIWA KUSHIRIKI SANAA NCHINI.

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

USHIRIKI WA WASANII WASIOSAJILIWA KWENYE TUNZO NA MATUKIO YA SANAA NCHINI

Baada ya BASATA kusimamia na kuratibu uanzishwaji wa Mashirikisho manne ya Sanaa nchini ambayo ni Shirikisho la Sanaa Jongevu (Filamu), Shirikisho la Muziki Tanzania, Shirikisho la Sanaa za Maonyesho na Shirikisho la Sanaa za Ufundi kwa lengo la kuvipa nguvu vyama vya wasanii na kuvipa umoja kitaifa,Baraza linapeleka nguvu kwenye urasimishaji wa sekta ya sanaa ikiwa ni pamoja na wadau wote wanaojihusisha na sekta hiyo hususan wasanii.

Kwa mujibu wa Sheria na. 23 ya Bunge ya mwaka 1984, Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) limepewa jukumu la kutambua na kusajili wadau wa Sanaa, kumbi zote za burudani Tanzania Bara na wasanii wote ikiwa ni pamoja na kutoa vibali vya kufanya shughuli za Sanaa.

Lengo ni kuzifanya shughuli za sanaa kufanyika katika mazingira rasmi na ya kufuata sheria za nchi pia kuwatambua wasanii wote nchini kwa mujibu wa sheria na taratibu za nchi yetu.Ikumbukwe kwamba, kufanya shughuli za sanaa bila kusajiliwa na kupewa kibali na BASATA ni kuvunja sheria za nchi na hivyo kustahili adhabu.

Faida za kurasimisha sekta ya sanaa hususan kwa wasanii

1. Kuendesha shughuli za sanaa kwa mujibu wa Sheria za nchi ili kuepuka usumbufu.

2. Kutambulika kwa shughuli ya msanii binafsi, kikundi, Chama nk. hivyo kufanya kazi kihalali.

3. BASATA kama shahidi wa Jamhuri hutoa utambulisho/uthibitisho kwa msanii, kikundi au chama halali mahali popote panapohitajika kwa mfano wakati wa kufungua akaunti benki, kupata VISA, pasi ya kusafiria, mikopo kwenye asasi za fedha, msaada au ushahidi mahakamani.

4. Ikihitajika kuweka ulinzi wa kisheria wa kazi za sanaa,kwa mfano wa Hakimiliki na Hakishiriki.

5. Kuingilia kati pale makubaliano/mikataba ya msanii, kikundi, chama nk. inapokiukwa na kuripotiwa katika Baraza.

6. Kushauri na kutoa mafunzo ya sanaa.

7. Kutafutiwa masoko na/au kuunganishwa na masoko, wasanii na fursa mbalimbali zinapojitokeza.

BASATA linawaagiza waandaaji wa matukio ya sanaa nchini (Tunzo za Sanaa/matamasha/maonyesho) kuhakikisha wanafanya kazi na wasanii waliosajiliwa tu na inapotokea kufanya vinginevyo basi muandaaji wa tukio husika na msanii atawajibika moja kwa moja.

BASATA linatoa hadi tarehe 31 Oktoba, 2010 kwa wasanii na wadau wote nchini kujisajili vinginevyo hatua za kisheria zitachukuliwa ikiwa ni pamoja na kuwazuia wasanii pia wadau wasiosajiliwa kushiriki tunzo/matamasha/Matukio ya Sanaa.

Ghonche Materego

KATIBU MTENDAJI, BASATA.

MAMA SALMA KIWETE KATIKA ZIARA MAFIA!!

Mwenyekiti wa Taasisi ya wanawake na Maendeleo (WAMA) ,Mama Salma Kikwete, leo akiongea na wanachama wa UWT Wilaya ya Mafia katika ziara ya siku moja kuwahamasisha wanacham wa umoja wa nawake Tanzania kuwachagua wagombea wa CCM katika uchaguzi ujao. (Picha na Mwanakombo Jumaaa Maelezo Dar es salaam)
Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) Mama Salma Kikwete akimtambulisha jana mgombea ubunge wa Mafia kupitia CCM Abdulkarim Shah.
Wanachama wa UWT Wilayani Mafia Mkoa wa Pwani leo wakimsikiliza Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) Mama Salma Kikwete hayupo pichani katika mkutano wake na wanachama hao kuhusu kuwahamasisha masuala ya Uchaguzi Mkuu ujao hapo Oktoka 31 mwaka huu. picha zote na Mwanakombo Jumaa-MAELEZO
Wanachama wa Chama Cha Mapinduzi ambao ni akina mama wa UWT wakimsikiliza mama Salma Kikwete.

Rais wa Kenya aidhinisha katiba mpya


Mashirika ya haki za binadamu yameilaumu serikali ya Kenya kwa kumruhusu Rais Omar Hassan al-Bashir kuitembelea Kenya ambako atahudhuria sherehe ya nchi hiyo ya kuidhinisha katiba mpya.

Kiongozi huyo anatakiwa na Mahakama ya Kimataifa (ICC) kwa mashtaka 10 ya uhalifu, ikiwemo uhalifu dhidi ya binadamu na mauaji ya kimbari yanayodaiwa kufanyika huko Darfur.

Rais Mwai Kibaki akiapa

Yeye ni kiongozi wa kwanza aliye madarakani kutuhumiwa na mahakama hiyo ya the Hague.

Kenya ni moja ya nchi zilizotia saini mkataba wa mahakama ya ICC ujulikanao kama sheria ya Rome unaoitaka kisheria kumkamata na kumkabidhi kwa mahakama hiyo.

Hata hivyo, uamuzi wa mara mbili uliofanywa na Umoja wa Afrika, uliwaamuru wanachama wake wasimkamate Rais huyo wa Sudan, hata hivyo ulikosea tu kusema kama kuna hatua itakayochukuliwa dhidi ya nchi yoyote itakayokiuka maagizo hayo na kutii amri ya ICC.

Shirika rasmi la habari nchini Sudan (SUNA) limesema katika taarifa fupi kuwa Rais Bashir atasafiri kwenda Nairobi akifuatana na mshauri wake Mustafa Ismail, waziri wa mashauri ya kigeni Ali Karti na mkurugenzi mtendaji wa idara ya ujasusi Muhammad Atta Al-Mawla.

Hii ni ziara yake ya pili katika moja ya nchi wanachama zilizotia saini mkataba wa Rome baada ya kuzuru Chad mwezi uliopita. Licha ya ziara hiyo alipuuza mwaliko wa kuhudhuria mkutano wa kilele wa nchi wanachama wa IGAD mjini Nairobi mwaka huu.

Shirika la Human Rights Watch limesema kuwa ziara yake itaweka doa sherehe za kuidhinisha katiba iliyosubiriwa kwa hamu kwa kumpokea kiongozi huyo. Habari na www.bbcswahili.com

Sasa wateja wa Vodacom kuzungumza bure usiku kucha


* Ni ofa ya mwezi mtukufu wa Ramadhan

Katika kuadhimisha mwezi mtukufu wa Ramadhani, kampuni ya Vodacom Tanzania sasa inawawesha awateja wake zaidi ya milioni saba kupigiana simu bure kuanzia saa sita usiku mpaka saa 12 asubuhi kila siku.

Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Vodacom Tanzania, Bi. Mwamvita Makamba, alisema Jijini leo (Jana) kwamba huduma hii ni zawadi kwa wateja wake katika kipindi hiki cha mwezi mtukufu wa Ramadhan.

Alisema huduma hii ni sehemu ya uwajibikaji wa kampuni yake kwa wateja wake na kwamba siku zote Vodacom imedhamiria kutoa huduma zake kwa bei nafuu, zenye kuaminika na ambazo zinakwenda sanjari na mahitaji ya watu wa Tanzania.

“Vodacom ni sehemu ambayo yanapatikana mambo makubwa na murua kwa ajili ya kukata kiu ya mawasilino kwa wateja wetu na pia kwenda nao sanjari wakati wakitimiza ndoto zao za mafanikio ndani ya nchi hii nzuri,” alisema.

Bi. Makamba alifafanua kwamba kampuni yake itaendelea kutoa huduma bora za vifurishi na za mawawsiliano ya simu za mkononi zikiwa kwenye ubora wa hali ya juu huku zikipatikana kwenye mtandao bora wa mawasiliano wenye viwango vya mawasiliano vyenye ubora wa kimataifa vinavyokidhi mahitaji ya mawasiliano kwa watu wa kada mbalimbali katika jamii yetu wakiwamo wajasiriamali, wakulima wafanyakazi na wafanyabiashara wakubwa.

Bi Makamba alitoa wito kwa Watanzania ambao hawajajiunga na Vodacom Tanzania, kujiunga haraka ili waweze kupata manufaa mengi yanayotokana na huduma bora zinazopatikana ndani ya familia kubwa ya Vodacom.

“Kwa wale ambao tayari ni wateja wa Vodacom endeleeni kufaidi huduma zetu ambazo zimebuniwa ili kurahisisha na kuboresha maisha ya Watanzania,” alisema na kuongeza mara zote kampuni yake imekuwa ikiongoza kwa ubunifu wa huduma za bora akiitaja huduma maarufu ya utumaji pesa hapa nchini ya Vodafone M-PESA kuwa ni kielelezo hai.

Alifafanua kwamba kwa kuwa katika kipindi hiki cha mwezi mtukufu wa Ramadhan, watu wengi huchelewa kulala kutokana na kusubiri daku na shughuli nyingine za taratibu za kidini, basi Vodacom Tanzania inawapa fursa wateja wake kuwasiliana bure wakati wakitakiana heri na fanaka ndani ya mwezi huu wa toba.

Katika kipindi hiki cha mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani, Waislam Duniani kote huungana kwa kufunga sanjari na sala, pia hupata fursa ya kuwasaidia wenzi wao waishio kwenye mazingira magumu.

Swahili Fashion week kuandaa mafunzo kwa wabunifu wa Tanzania



Wabunifu wa Tanzania kufundishwa mbinu za biashara kuelekea katika Soko la Uingeraza.

Wanunuzi wakubwa wa bidhaa za ubunifu kutoka Uingeraza kuonyesha mbinu za uuzaji.

Swahili Fashion Week kwa kushirikiana na Tanzania Cotton Board (TCB) na Textile Sector Development Unit (TSDU) kwa pamoja wameandaa mafunzo kwa wabunifu wa Tanzania yenye lengo la kuboresha taaluma ya ubunifu hapa nchini.

“Tunaamini kwamba baada ya mafunzo haya, wabunifu wa watanzania wataweza kutengeneza bidhaa zenye ubora wa hali ya juu ambazo zitaweza kuuzwa sehemu yoyote. Pia kupitia mafunzo haya tunaamini kwamba wabunifu watapata habari muhimu zitakazowawezesha kuchangia moja kwa moja ukuaji wa sekta ya ubunifu Tanzania”. Alisema Mustafa Hassanali muaandaji wa Swahili Fashion Week.

Mafunzo hayo yataendeshwa na Claire Hamer-Stubbs ambae anatoka katika kampuni ya Ei8ht (www.ei8ht.org), kundi ambalo limekuwa likifanya kazi zake nchini Uingereza.

Warsha hiyo itafanyika katika Hotel ya New Africa kwa muda wa siku nne kuanzia Ijumaa ya tarehe 27 mpaka Jumatau tarehe 30 mwezi huu na kuwahusisha wabunifu 12 wa mavazi hapa nchini.

“TSDU kwa sasa tumeshirikiana na Swahili Fashion Week katika programu ya kuwasaidia wabunifu wa Tanzania kwa kutoa mafunzo ya awali , TSDU inaamini kwamba kwa kutoa fursa ya mafunzo kwa wabunifu ambayo yatawawezesha kutambua mpangilio mzima wa kufanya kazi zao. Tunaamini kwamba kupitia semina hii wabunifu watajipatia uelewa mpana wa kufanya kazi na wanunuzi wa rejareja kutoka Uingereza ambao huenda wakavutiwa na bidhaa zinazozalishwa na wabunifu wa Tanzania. Alieleza Mark Bennet, mtaalamu kutoka viwanda vinavyotengeneza nguo vya hapa Tanzani.

Miongoni mwa maeneo yatakayofundishwa katika warsha hii ni pamoja na:

· Biashara na ubunifu, ambapo zaidi itagusia kufafanua ubunifu, mifano mbalimbali, gharama za uzalishaji.

· Masuala ya uzalishaji kwa ujumla, ambapo zaidi wataangalia vipengele vinavyohusu fedha, ufundi, ubora wa bidhaa na jinsi ya kufanya kazi na viwanda vingine vya uzalishaji.

· Ufundi katika ubunifu kwa mfano katika ufungaji, uwekaji wa lebo, maadili ya uzalishaji sambamba na mazingira ya kazi kwa ujimla.

· Watapata pia fursa ya kukutana na wanunuzi kutoka Uingeraza, na kujua ni bidhaa gani zinazohitajika Uingereza, pamoja na kuangalia changamoto mbalimbali na jinsi ya kufikia matarajio.

“Wabunifu wa Tanzania waitumie nafasi hii ipasavyo katika kujipatia mbinu tofauti za kutengeneza bidhaa zao, pamoja na kujipatia mbinu mpya za masoko kwa bidhaa wanazozalisha. Nafasi hii haitoi fursa kwa mtu mmoja mmoja bali kwa sekta nzima ya ubunifu hapa nchini.” Alimazia Mustafa Hassanali.

KUHUSU SWAHILI FASHION WEEK

Swahili Fashion Week ni jukwaa pekee linalowaleta pamoja wabunifu wa mavazi na watengenezaji wa bidhaa za mapambo kutoka nchi zote zinazozungumza lugha ya Kiswahili, ili kuonyesha ubunifu wao, kuuza bidhaa wanazozalisha, kubuni ajira, sambamba na kutengeneza mtandao kwa wabunifu kutoka maoneo hayo wanayoongea lugha ya Kiswahili, sambamba na kuhimiza dhana nzima ya kuthamini bidhaa zinazotengenezwa Afrika Mshariki.

“Swahili fashion week in tukio ambalo linawajumuisha wabunifu wakongwe na wale wanaochipukia kuonyesha kazi zao, pia kutoa nafasi kwa wapenzi wote wa sanaa ya mavazi kujumuika pamoja na kufurahia bunifu wa watanzani na kutoka nchi za jirani”. Alifafanua Mustafa Hassanali.

Msisitizo zaidi umewekwa katika kuhakikisha kwamba sekta ya ubunifu inakuwa kikanda. Swahili Fashion Week inalenga kukuza sanaa ya ubunifu na kuwa jukwaa bora la kibiashara kimataifa kwa nchi za Afrika Mahariki.

“Kwa mara ya kwanza watu mbalimbali watapata fursa kuuza na kununua bidhaa mbalimbali za Kiswahili kutoka nchi zinazozungumza Kiswahili kama vile vyakula, viatu, nguo na vitu mbalimbali kutoka mwambao wa Kiswahili kupitia Swahili Shopping Festival”. Alimalizia Mustafa.

Kwa mara ya tatu sasa Swahili Fashion Week imekuwa ikifanyika, ambapo kwa mwaka huu itafanyika kuanzia tarehe 4 mpaka 6 November 2010, Dar Es Salaam, Tanzania.

KUHUSU NA UKUAJI WA VIWANDA (TSDU)

The Tanzania Cotton Board’s (TCB) na Textile Sector Development Unit’s (TSDU) zimekua zikisaidia kukuza seka ya viwanda Tanzania. Lengo kuu ni kubuni hali bora na kuhakikisha kukua viwanda vinavyozalisha nguo Tanzania, sambamba na kuhakikisha thamani ya Pamba Tanzania inakua, hali itakayochangia kupatikana kwa nafasi za ajira na kuwepo kwa hali bora kwa nchi ya Tanzania.

KUHUSU TANZANIA GATSBY TRUST (TGT)

The Tanzania Gatsby Trust (TGT - www.gatsby.or.tz) imeanzisha program maalumu ya kusaidia serikali ya Tanzania katika kuhakikisha maendeleo ya viwanda vinavozalisha nguo . miongoni mwa program zake nyingi pia ni kusaidia kukuza hali ya wabunifu wa Tanzania. TGT inaamini kuwa kuimarika kwa sekta ya ubunifu kutachangia kuongezeka kwa ajira Tanzania. Kwa kushirikian ana VETA TGT imeanzisha mafunzo ya wabunifu wa mavazi katika vituo vyake vya mafunzo vilivyopo Dar es salaam. Pia TGT imeamua kufanya kazi na Swahili Fashion Week kwa lengo kukuza hali ya ubunifu Tanzania.

BARAZA LA EWURA CCC LATAKA WATUMISHI WA TANESCO NA WAJUMBE WA BODI WANUNUE UMEME SAWA NA WENGINE


BARAZA la Ushauri la Watumiaji Huduma zinazothibitiwa na Mamlaka ya Udhibiti Huduma za Nishati na Maji (EWURA CCC) limelishauri Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) liondoe bei za viwango maalum vya umeme kwa wafanyakazi wake na wajumbe wa bodi ya shirika hilo kutoka T6 hadi T1 kama ilivyo kwa watumiaji wegine.

Hayo yalisemwa jana na Makamu Mwenyekiti wa EWURA CCC, Said Abeid wakati akitoa maoni juu ya ombi la TANESCO kuongeza bei ya umeme kwa awamu ambapo limeomba ongezeko la asilimia 34.6 kuanzia Januari 2011, asilimia 13.8 mwaka 2012 na asilimia 13.9 mwaka 2013 kwenye mkutano uliofanyika jijini Dar es Salaam.

Alifafanua kuwa viwango hivyo sh. 4.50 kwa uniti zisizozidi 750 kwa mwezi na viwango vya T1 kwa matumizi yanayozidi uniti hizo.

“Kama wafanyakazi wote 5,538 watatumia uniti zote, jumla ya matumizi hayo kwa mwezi yatafikia uniti 4.154 milioni kwa mwezi au uniti 49,842 milioni kwa mwaka. Haya ni matumizi makubwa yanayokaribia kulingana na matumizi ya mkoa mzima wa Kagera kwa mwaka 2010.

Akinukuu maelezo ya mtaalamu mwelekezi wa aliyeteuliwa na TANESCO kuchambua gharama na kuandaa bei ya huduma, ambaye ripoti inadokeza kuwa si sahihi kwa matumizi ya kundi kubwa la watumiaji wa huduma kufidiwa na makundi mengine.

Abeid aliongeza kampuni mbili za kigeni zizoteuliwa na TANESCO kwa ajili ya kutoa ushauri elekezi kuhusu gharama na maombi ya kuongeza bei yawe huru na si yakuajiriwa na shirika hilo ili kuepuka kuipendelea.

Hata hivyo Abeid aliongeza kwamba kuna tozo nyingi ambazo watumiaji wa umeme wanatozwa mfano gharama za kisheria kama 18% VAT , 3% REA na 1% ya EWURA, wasiwasi wa baraza hilo ikiwa bei zitapanda kama TANESCO inavyotaka huenda watu wengi wakashindwa kumudu huduma hiyo na idadi ya watumaji kupungua, hali itakayochangia bei ya nishati hiyo kuzidi kupanda.

Awali akitoa maelezo kuhusu ombi hilo, Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, William Mhando alisema shirika linapata hasara ya sh.41 kwa kila uniti inayouza kulingana na ripoti ya ukaguzi ya mwaka 2008, hivyo kwa mwaka huo ilipata hasara y a sh. bilioni 21.6 kwa sababu makusanyo hayatoshelezi gharama za uendeshaji.

Alisema wastani wa gharama za kuuzia umeme ni sh.111 kwa uniti wakati za kumfikishia mteja ni sh. 152 kwa uniti.

Baadhi ya wadau wengine ambao, ni Janeth Muro na Ramadhani Shebe ambao walipinga hoja hiyo, waliitaka shirika hilo lidhibti tatizo la upotevu wa umeme linalodaiwa kufanywa na baadhi ya watumishi wakishirikiana na wateja ambao si waaminifu.

Naye Kamishna Msaidizi wa Baraza la Ushauri la Serikali(GCC), Theophilo Bwakea alishauri kuwa TANESCO ielekeze nguvu za udhibiti wa upotevu wa umeme hasa kwa wateja wakubwa kuboresha huduma na kuongeza idadi ya wateja kutoka 100,000 mwaka mwaka kwa kuwa ni kidogo.

Maoni mengine TANESCO ichukue hatua za haraka za kupunguza matumizi yake yasiyo ya lazima kama vile gharama za utawala ambazo zinazidi kuongezeka mwaka hadi mwaka kwa kasi bila ya kuongeza tija ndani ya Shirika.

Pia tathimini ya mapato na matumizi ya Shirika kwa miaka ya nyuma na na mtiririko wake kipindi kifupi cha mbele inabainisha matumizi yanazidi mapato.

Baraza linashauri Shirika liongeze wigo wa wateja wakubwa, wa kati na wadogo ili liweze kusanya mapato mengi na kupunguza gharama za uendeshaji kwa kila mteja. Kuimarisha ufanisi katika ngazi zote za utendaji hakuepukiki ikiwa Shirika linataka kubaki kama mshindani wa kweli katika soko la biashara ya umeme nchini na katika nchi za Kikanda.

Akijibu hoja hizo Mhando alisema watazifanyia kazi changamoto hizo ili kuboresha huduma na ikiwemo kudhibiti upotevu wa umeme ambapo wameshaanza kuchuaka hatua kwa baadhi ya wahusika.

Mkurugenzi wa EWURA, Haruna Masebu alisema kuwa bado wadau wana nafasi ya kutoa mapendekezo kwa maandishi hadi Septemba 10 saa kumi na moja jioni.

Vodacom Miss Tanzania Watembelea Ofisi za Vodacom Arusha,watoa msaada kituo cha waishio na virusi vya ukimwi


Vodacom Miss Tanzania 2009, Miriam Gerald akimkabidhi msaada wa vyakula na fedha Katibu Mkuu wa Kituo cha watu wanaoishi na virusi vya Ukimwi cha Tumaini Kilichopo Arusha, Richard Laizer ikiwa ni maadhimisho yake ya siku ya kuzaliwa aliyofanyika jana. Kwa niaba ya watoto wanaosoma katika kituo hicho ni mtoto Sweetmercy Emmanuel aliyepokea kwan iaba ya wenzake.
Mkurugenzi wa Vodacom wa Kanda ya Kaskazini, Nguvu Kamando akifafanua jambo kwa warembo wa Vodacom Miss tanzania 2010 juu ya huduma ya mawasiliano kwa kutumia Video inavyofanya kazi wakati warembo hao walipotembelea ofisi za Vodacom Kada ya Kaskazini mjini Arusha jana.
Mkurugenzi wa Vodacom wa Kanda ya Kaskazini, Nguvu Kamando (wapili kulia) na Mtaalam wa Habari wa Vodacom Tanzania, Matina Nkurlu (kulia) pamoja na warembo wa Vodacom Miss tanzania 2010 wakiangalia namna teknolojia ya mawasiliano kwa kutumia Video inavyofanya kazi wakati warembo hao walipotembelea ofisi za Vodacom kada ya Kaskazini mjini Arusha jana.

Timu ya Taifa ya Pool Yaendelea Kujifua Kujiandaa na Mashindano Ya Dunia


Kocha wa timu ya Taifa ya Pool,Denis Lungu akiwaelekeza wachezaji wa timu hiyo namna ya kushika fimbo na kupiga mpira wakati wa mazoezi yao yanayoendelea kufanyika katika klabu ya Break Point,kijitonyama.
Kocha Denis Lungu akiwapa maelekezo wachezaji wa timu ya Taifa ya Pool wanaojiandaa na mashindano ya Dunia yanayotarajiwa kufanyika Novemba,8 2010 huko nchini Ufaransa.timu hii ina wachezaji nane (8) ambani ni Felix Atanas,Abuu Shaban,Godfrey Sway,Mohamed Iddy,Omar Akida,Godfrey Muhando,Aliakber Akberal na Arjuan Lavinja.ikiwa chini ya udamini mkubwa wa bia ya Safari Lager.

NHIF YAWATAKA VIONGOZI TALGWU KUTHIBITISHA MADAI

Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya afya akitoa ufafanuzi kuhusu madai yaliyowasilishwa kwenye vyombo vya habari na viongozi wa Talgwu kuwa wanadai serikali na Mfuko wakati alipokutana na waandishi wa vyombo mbalimbali kwenye ukumbi wa mikutano wa mfuko huo kurasini bendera tatu kushoto kwake ni wakurugenzi wa mfuko.

Na.Paul Marenga NHIF
MFUKO wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) umekitaka Chama cha Wafanyakazi wa Serikali za Mitaa (TALGWU) kutokwepa kueleza ukweli kuhusiana na madai ya makato yaliyokatwa kimakosa kwa wanachama wao wakati wa uanzishaji wa Mfuko huo mwaka 2001.

Kauli hiyo imetolewa na Mkurugenzi Mkuu wa NHIF, Emmanuel Humba wakati akizungumza na waandishi wa habari makao makuu ya Mfuko huo Bendera Tatu, Dar es salaam leo.

“Sisi katika Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya hatutaki malumbano, bali tunapenda kupitia kwenu umma wa Watanzania na wanachama wetu waelewe ukweli kuhusu suala hili ambalo kwanza siyo suala geni,” alisema Humba.

Mfuko huo uliamua kutoa ufafanuzi baada ya baadhi ya vyombo vya habari juzi na jana kutangaza na kuandika kwamba Talgwu itaifikisha mahakamani NHIF kwa kushindwa kulipa wafanyakazi 58,000 wa Tamisemi zaidi ya sh bilioni 3.6 ambazo zilikatwa kinyume cha sheria.

Alisema pamoja na ukweli kwamba madai haya yamekuwa yakitolewa au kuibuka kunapokuwa na uchaguzi ndani ya TALGWU au uchaguzi mkuu wa Serikali, viongozi wa TALGWU wamekuwa hawawaambii wanachama wao maagizo ya serikali kuhusiana na madai yao hayo.

Yapo maagizo ya Serikali katika suala hili, alisema Humba na kuongeza kuwa TALGWU ilipaswa kueleza wazi imefanya nini ili kulimaliza kabisa suala hili ambalo Mfuko tayari ulishatekeleza kwa upande wake, kulingana na maagizo na miongozi ya Serikali.

Kwa mujibu wa Humba, Serikali na NHIF baada ya kubaini kuwa kulikuwa na Watumishi 12,894 waliokatwa kimakosa iliwarejeshea kiasi cha Shilingi 269,563,469.54 watumishi hao.

Alisema kazi ya kuwakabidhi fedha hizo ilifanywa kwa pamoja kati ya Mfuko na Chama cha TALGWU makao makuu na matawi yake mikoani.

Akifafanua zaidi alisema pamoja na hatua hiyo ya kuwalipa watumishi hao, TALGWU ilikuja na madai mapya wakisema bado kuna watumishi 53, 000 ambao hawajalipwa na wanadai kiasi cha Shilingi bilioni 1.8 na sasa wanadai shilingi Bilioni 3.6 kwa watumishi 58,000.

“Kwa taasisi yoyote inayofuata misingi ya fedha taratibu lazima ziwepo na hawa kama wanaona kwamba malipo ya mwanzo hayatoshi basi wafuate maagizo yanayostahili.

“Hakuna wakati wowote ambapo Mfuko huu umekaidi kutekeleza maelezo yoyote halali, kama TALGWU wanavyodai katika taarifa yao iliyotolewa kwa Vyombo vya Habari jana,” alisema.

Mwongozo wa pili wa makato ya wafanyakazi kwenda NHIF kutoka Utumishi uliotolewa Mei 2002, ulifafanua kuwa wanaokatwa ni wale wanaolipwa na Serikali kuu ingawa walikuwa katika Serikali za Mitaa na kubainisha kuwa watumishi ambao hawahusiki na makato ni wale walioajiriwa na Serikali za mitaa na kulipwa kwa kutumia vyanzo vya mapato vya Serikali za Mitaa.

Hata hivyo Serikali, Mwezi Novemba, 2002 illifanyia mapitio Sheria ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya ili kuwajumuisha Watumishi wote walioko kwenye Serikali za Mitaa.

Humba alisema chimbuko la madai ya TALGWU ni kuwa wao hawaikubali tafsiri iliyotolewa na Serikali kuhusu ni nani waliotakiwa kuchangia na vilevile haikubali miongozo ya makato iliyotolewa na Serikali, jambo ambalo liko nje ya uwezo wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya.

“Tunauomba uongozi wa TALGWU kama kuna madai yoyote halali basi wafuate maelekezo waliyopewa ya kuwasilisha orodha ya majina ya watumishi wanaodai kwenye Ofisi ya Waziri Mkuu TAMISEMI na yakishahakikiwa na kuletwa kwetu, sisi tutawalipa mara moja,” Alisema Humba.

Alisema Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya wakati wote unafanya kazi zake kwa kuzingatia Sheria ya kuundwa kwake na kusimamia majukumu yake kwa mujibu wa Sheria. “Fedha hizi ambazo tunazisimamia ni fedha za umma (Public Funds) ambazo zinasimamiwa na kukaguliwa na Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG). Ndiyo maana hata malipo ya awali tuliyalipa kwa kuzingatia taratibu za fedha na idhini kutoka Serikalini.” Alisema.

wanaume kuitambulisha albam yao pamoja na website yao octoba 25


kundi la Wanaume (lililojiengua kutoka kwa kundi la Wanaume Halisi) linatarajia kuitambulisha albamu yake mpya itakayokwenda sambamba na uzinduzi wa Logo pamoja na tovuti yao kwa watu maalumu ndani ya kiota cha maraha kilichopo kati kati ya jiji,Savanah Lodge mnamo Octoba 25.

Akizungumza na blog jirani jijini Dar jioni hii kiongozi wa kundi hilo Rich One amesema kuwa baada kuikamilisha albamu yao yenye jumla ya nyimbo kumi,kwa sasa wanajipanga vyema kuitambulisha albamu hiyo itakayojulikana kwa jana la POA TUA, vile vile utakwenda sambamba na uzinduzi wa Logo na tovuti itakayokuwa na habari zao mbalimbali zikiwemo na kazi zao kama vile vyimbo na video zao.

"Tumeamua kuja na mambo mapya baada ya kimya kidoogo kwa wapenzi wetu,kama nilivyosema hapo awali albamu ina jumla ya nyimbo kumi,ambazo baadhi yake ni Poa Tu, Mapenzi Matamu, Apple, Moyo Wangu, Zaga Zaga na nyingine nyingi," alisema Rich One na kuongeza kuwa albamu hiyo imesheheni mahadhi tofauti tofauti kama vile Zouk, R&B pamoja na Hip Hop.

Rich One amesema kuwa ndani ya albamu hiyo amewashirikisha wasanii kadhaa mahiri katika anga ya muziki wa kizazi kipa,kama vile Chidi Benz,Kitokororo wa FM Academia,Hard Mad,Chiku Keto,Mh Themba na wengineo.

Kundi hilo linaloundwa na wakali akiwemo Athuman Yahya (A.Man), Juma Mbelwa (Juma Jazz), Karim Kaiman (Kakaman), Abdul Ally (Mzimu), Richard Shauri (Rich One) pamoja na David Mpangile (Daz-p).

DR. BILAL AWAASA WASOMI NCHINI

Mgombea mwenza wa nafasi ya urais kupitia tiketi ya Chama cha Mapinduzi, Dk. Mohamed Gharib Bilal, akimnadi mgombea ubunge wa Jimbo la Nachingwea, Mathias Chikawe, baada ya kuingia Wilayani Nachingwea jana jioni Wananchi wa Nachingwa wakimsikiliza Mgombea Mwenza wa nafasi ya urais Dk. Mohamed Gharib Bilal, alipokuwa akiwahutubia wananci wa Wilaya ya Nachingwea katika uwanja wa Sokoine leo mchana kina mama wakiimba.
Mgombea Mwenza Dk. Gharib Bilal, akiongozana na Mgobea Ubunge wa Jimbo la Nachingwea, Mathias Chikawe, baada ya kupokelewa mpakani mwa Wilaya ya Liwale na Nachingwea jana Agost 26, wakati wa zaiara ya mgombea mwenza ya kunadi ilani ya Chama cha Mapinduzi katika kampeni za kukiombea kura Chama hicho katika uchaguzi mkuu ujao unaotarajia kufanyika Oktoba 31 mwaka huu.
Mohamed Gharib Bilal, akipokelewa na Diwani wa Viti maalum, Asina Lutumbo na Mwenyekiti mstaafu wa UWT, Anna Abdalah, baada ya kuwasili kwenye uwanja wa Sokoine wilayani Nachingwea alipofika kufanya mkutano wa kampeni leo
Wananchi wa Kijiji cha Miembeni Wilaya ya Nachingwea wakimzunguka Mgombea Mwenza Dk. Gharib Bilal, baada ya kutanda barabarani na kuwaomba viongozi wa msafara kumruhusu kushuka ili kumuona na kusaliana naye, wakati msafara huo ulipofika mpakanai mwa wilaya ya Nanchingwea ukitokea Wilayani Liwale jana



*Dk Bilal awaasa wasomi nchini

*Awataka kujenga makazi bora na sio kukimbilia magari

*Msafara wake wapata ajali ya gari wilayani Ruangwa


Na mwandishi wetu,lindi

MGOMBEA mwenza wa Chama cha Mapinduzi (CCM),Dk.Mohamed Bilal amewashauri wasomi kote nchini kuanzisha utamaduni wa kujenga makazi yaliyobora ili taifa liweze kupiga hatua katika sekta ya makazi.

Kauli hiyo ya Dk Bilal aliitoa wakati akihutubia mamia ya wakazi wa Manisapaa ya Lindi ambapo pia alitumia nafasi hiyo kumnadi mgombea ubunge kupitia CCM, Mohamed Abdulaziz.

“Zamani tukisoma chuo kikuu na kuhitimu hatukumudu hata kununua simu. Siku hizi kila mwananchi anayo fursa ya kupata simu. Vijana wetu siku hizi wanahitimu vyiuo vikuu na baada ya mwaka mmoja wanaweza kununua magari. Nadhani sasa ni wakati muafaka kwa wao kuanza mkakati wa kujenga makazi bora,” alisema na kuongeza;


“Tunao mpango madhubuti wa kuhakikisha kuwa kila mwananchi anapata makazi bora. Mpango huu upo katika ilani yetu na ni imani yangu kuwa wananchi wakimchagua Rais Kikwete katika uchaguzi ujao, basi itakuwa kazi rahisi kwetu kufanikisha azma hii muhimu katika maendeleo ya wananchi wetu.”

Dk Bilal bado anaendelea na kampeni katika mkoa wa Lindi ambapo jana alifanikiwa kufanya kampeni katika wilaya za Ruangwa, Liwale na Nachingwea. Katika kapmeni hizo, Dk Bilal alisisitiza umuhimu wa wananchi kutambua kuwa serikali ya CCM imejipanga vema na kwamba ina kila sababu za kutaka kuwapa maendeleo zaidi ya hapo wali[po.

Msomi huyu wa masuala ya Nyuklia alifafanua pia kuwa, serikali ya CCM inatambua kero za barabara zinazoikabili mikoa ya Kusini na kwamba hatua za kukabiliana na hali hiyo zinaonekana kwa kuwa barabara nyingi zinafanyiwa kazi kwa sasa.


Pia alisisitiza umuhimu wa wananchi kuchangamkia fursa za Kilimo Kwanza kwa kuhakikisha kuwa wanawatumia wataalam wachache waliopo sambamba na fursa kama mbegu na mbolea zinazohamasishwa na wananchi kutolewa. Tena alifafanua kuwa, anayo taarifa ya kero kuhusu zao la Korosho na akawaeleza wananchi kwamba tiba ya kero hiyo ipo na rais Kikwete ameshafanya kila awezalo kuhakikisha vyama vya ushirika vinaimarishwa sambamba na kuwapa bei bora wakulima wa Korosho.

Mgombea Mweza, Dk Bilal alifafanua pia umuhimu wa wazazi kuwajali watoto wao na kuhakikisha wanawapeleka katika shule za awali kwa kuwa ilani ya CCM inatamka wazi kuwa, ifikapo mwaka 2015, kila shule ya Msingi itatakiwa kuwa na shule hizo, hivyo wazazi wachangamkie fursa hiyo iliyopo mbele yao.

Sambamba na hilo, gari mmoja lilokuwa ndani ya msafara wa mgombea huyo liliacha njia na kupinduka katika kijiji cha Nangumbo wilaya ya Ruangwa mkoani majira ya saa nne, asubuhi, wakati magari hayo yakiwa katika njia ya kwenda makao makuu ya wilaya ya Ruangwa kwa ajili ya mkutano wa kampeni.

Shuhuda wetu aliyekuwepo katika tukio hilo alieleza kuwa, gari hilo lilipata ajari kufuatia vumbi kali liliolosababisha dereva wa gari kutoona mbele huku akitakiwa kupita katika eneo lililo[kuwa na tuta kubwa.

Gari hilo lilikuwa na abiria wane, lakini wote walisalimika na baada ya jitihada za kuwatioa katika gari hilo kukamilika, msafara uliendelea kama kawaida.

Aug 26, 2010

KAMPENI ZA KIKWETE NGARA


Mkutano wa kampeni kwa mgombea wa CCM uliokuwa ufanyike mjini Ngara jana jioni ulilazimika kuahirishwa baada ya helkopta aliyokuwa akitumia kushindwa kumpeleka mjini humo kutokana na hali mbaya ya hewa.
Hata hivyo ilimlazimu Rais Kikwete kutumia barabara ambapo aliwasiri mjini humo usiku jkwajili ya kuongea na wananchi, hivyo mkutano huo umeahirishwa hadi leo mapema asubuhi.
Wananchi waliofurika katika viwanja vya posta ya zamani kwa ajili yasikiliza hotuba hiyo, waliambiwana Mwenyekiti wa CCM Hellen Adrian, baadae jana saa 11 jioni kuwa mkutano huo usingekuwepo hadi leo.
Baadae usiku Rais aliwasiri kwas njia ya barabara na kuandaliwa futari na kinamama wa wilayani humo kama inavyoonekana alipopokelewa kwa jili ya masafa zaidi kwajili ya kampeni

HILI NDILO BANGO LA DR.SLAA

Haya wakati kampeni za Chadema zinakaribia bango hili limeandaliw akumnadi mgombea!

MTV & BHARTI AIRTEL SIGN PARTNERSHIP TO BRING MTV AFRICA MUSIC AWARDS TO LAGOS IN DECEMBER 2010.


25 August 2010: MTV Networks Africa (MTVNA) and Bharti Airtel have confirmed that they will be holding the 2010 MTV Africa Music Awards (MAMA) in Lagos, Nigeria.
MTVNA’s jubilant celebration of contemporary African music and creativity will be held at the EKO EXPO Hall, Lagos on 11 December 2010, focusing the spotlight on Africa’s most outstanding musicians, from the heart of one of the continent’s most vibrant cities.
The 2010 MTV Africa Music Awards with Airtel will take the form of a stunning live music event and global television spectacular, featuring performances from contemporary African and international music giants and hosted by a major music celebrity. Artists from around the continent will battle to win a coveted MAMA trophy in one of twelve award categories including: Best Male, Best Female, Best Video, Best Group, Artist of the Year, Best Lusophone Act, Best Anglophone Act, Best Francophone Act, Song of the Year, Brand: New Act, Best International Act and MAMA Legend.

Telecommunications giant Airtel comes on board as the headline sponsor of the MTV Africa Music Awards 2010, signalling the telco’s profound commitment to African music and youth culture following its purchase of Zain Africa’s business operations earlier this year. The sponsorship was announced by Andre Beyers, Chief Marketing Officer, Airtel Africa and Alex Okosi, Senior Vice President & Managing Director, MTV Networks Africa.

Sponsorship of the MAMA will provide Airtel with unique brand exposure across multiple platforms including live event activations across the continent. A key component of the partnership will be the development of exclusive mobile and data content for the Airtel subscribers in sub-Saharan Africa including wallpapers and various downloads. The campaign will also be fully activated in the digital space with a bespoke mobi-site (mtvmama.mobi) and a dynamic website (www.mama.mtvbase.com). Multiple SMS voting and interactive mechanics will be integrated into the campaign, to provide Airtel customers with unique access to the MAMA initiative.

Commented Alex Okosi, Senior Vice President & Managing Director, MTV Networks Africa, “We are thrilled to be partnering with Airtel to bring the MTV Africa Music Awards with Airtel to Lagos for the first time and look forward to delivering the most exciting MAMA yet on 11 December.”
Said Mr. Beyers, “Airtel is proud to be at the forefront in nurturing talent in Africa and connecting the passions of millions of youth across the continent through music. Our support for the MAMA awards is founded on our commitment to empower the youth through initiatives that will help Africa to identify and celebrate talent.”
Conceived in 2008 as the ultimate celebration of African contemporary music talent, the MTV Africa Music Awards with Airtel provides a major promotional platform for the African music industry, championing, supporting and empowering African talent by broadcasting their music around the world via MTV’s global multimedia network.
The awards celebrate contemporary African and international genres loved by the youth and young adults across sub-Saharan Africa including Hip Hop, Hip Life, R&B, Afro Pop, Afro House, Kwaito, Boomba, Bongo Flava, Coupé Décalé, Dancehall, Soul and Rock.
The inaugural MAMA was held at the Velodrome, Abuja in 2008, while October 2009 saw the awards move to Nairobi, Kenya, with performances from 2Face (Nigeria), Amani (Kenya), A.Y. (Tanzania), Blu3 (Uganda), Brickz (South Africa), Da LES (South Africa), D’Banj (Nigeria), Fally Ipupa (DRC), HHP (South Africa), Lizha James (Mozambique), M.I. (Nigeria), Mo’ Hits Allstars (Nigeria), Nameless (Kenya), Pype (Nigeria), Samini (Ghana), STL (Kenya), Lira (South Africa), Wahu (Kenya) and Zebra & Giraffe (South Africa), alongside international stars Wyclef Jean and Akon.
Past winners have included 2-FACE (Nigeria), Nameless (Kenya), Samini (Ghana), Wahu (Kenya), HHP (South Africa), D’Banj (Nigeria) and Patricke-Stevie Moungondo (Congo Brazzaville).
-ENDS-

Notes to Editors
The MTV Africa Music Awards with Airtel is open to all soloists or groups who have received airplay on MTV base or MTV during the qualifying period (30 June 2009 to 31 August 2010) including artists from: Angola, Benin, Botswana, Burkina Faso, Burundi, Cameroon, Cape Verde, Central Africa Republic, Chad, Comores, Congo, Cote d’Ivoire, Djibouti, DRC, Equatorial Guinea, Eritrea, Ethiopia, Gabon, Gambia, Ghana, Guinea, Guinea Bissau, Kenya, Liberia, Madagascar, Malawi, Mali, Mauritania, Mauritius, Mozambique, Namibia, Niger, Nigeria, Rwanda, Sao Tome & Principe, Senegal, Seychelles, Sierra Leone, South Africa, St Helena, Sudan, Swaziland, Tanzania, Togo, Uganda, Zambia and Zimbabwe.

WAZIRI MKUU MIZENGO PINDA KUSHUHUDIA SHEREHE ZA KUMUAPISHA RAIS NKURUNZINZA BUJUMBURA LEO

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiwapungia wananchi wa Burundi waliofika kwenye uwanja wa ndege Bujumbura Augosti 25, 2010 jana ambako leo atamwakilisha Rais Jaky Kikwete katika sherehe za kumwapisha Rais wa Burundi, Pierre Nkurnzinza. Kulia ni Spika wa Bunge la Nchi hiyoPie Ntavyohanyuma na wapili kushoto ni mkewe Tunu. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisalimiana na watanzania waishio Burundi baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Bujumbura Augost 25 jana Waziri mkuu leo atamwakilisha Rais Jakaya Kikwete katika sherehe za kuapishwa kwa rais wa chi hiyo, Pierre Nkurunzinza
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda kiongozwa na Spika wa Bunge la Burundi baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Bujumbura Augosti 25 ambako leo atamwakilisha Rais Jakaya Kikwete katika sherehe za kumwapisha Rais wa Nchi hiyo, Pierre Nkurunzinza. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

warembo wa vodacom miss tanzania 2010 wakiwa mkoani manyara


Baadhi ya warembo wa Vodacom Miss Tanzania 2010 wakiwa wameshikilia vyandarua kabla ya kugawa vyandarua kwa baadhi ya wakazi wa mto wa Mbu mkoani Manyara jana. Warembo hao wapo Kanda ya Kaskazini kutembelea vivutuio vya Utalii na kuhamasisha Utalii wa ndani ya nchini.
Mshiriki wa Shindano la Vodacom Miss Tanzania 2010,Geneviver Emmanuel akigawa chandarua kwa mmoja wa wakazi wa Mto wa Mbu Mkoani Manyara jana katika utekelezaji wa Kapeni ya malaria. Warembo hao wapo Kanda ya Kaskazini kutembelea vivutuio vya Utalii na kuhamasisha Utalii wa NMdani Nchini.
Paulina Lowasa dada wa Mbunge wa Monduli na Waziri Mkuu wa Zamani, Edward Lowasa, akiwapa mkono wa kuwatakia heri Warembo wa Vodacom Miss Tanzania alipokutana nao Wilayani Monduli mkoni Arusha jana na kuwapa zawadi ya vikoi vya kimaasai warembo wote 30. Warembo hao wanatembelea Kanda ya Kaskazini kuangalia vivutio vya Utalii nchini.
Baadhi ya Warembo wa Vodacom Miss Tanzania wakiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi wa Shule ya Sekondari Wasichana Maasai iliyopo Monduli Mkoani Arusha wakati wa rembo hao walipotembelea shule hiyo jana wakiwa katika ziara yao ya kutembelea vivutio vya utalii na kuhamasisha utalii wa ndani nchini.
Washiriki wa Shindano la Vodacom Miss Tanzania 2010 wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Viongozi wa UWT Wilayani Monduli pamoja na Viongozi wa Kamati ya Miss Tanzania baada ya akina mama hao kuwapa zawadi ya vikoi vya kimasai na kuwatakia kila la heri katika mashindano hayo yatakayo fikia Kilele Septemba 11 mwaka huu jijini Dar es Salaam.

Wateja wa Zain sasa Kupeta Kinamna hii..!

FREE CALLS, FREE SMS, FREE INTERNET

Zain Tanzania the most respected company, today has announced a Customer rewarding promotion, with free calls during the holy month of Ramadan.

The offer adds-up on the company’s championship in rewarding their customers and today it continues to re enforce its commitment by providing unmatched offer to their customers.

Speaking on the promotion, the company’s Managing Director, Sam Elangalloor said “we are happy to announce this promotion for the holy month of Ramadan to reward our customers”.
“We wish our customers Ramadhan Karim and hope they will communicate with their families, friends and loved ones more. Our aim is to continue making all communications services in Tanzania more affordable and make your Zain phone a must have”, he said.

He further added that the promotion will give our customers free calls, free sms and free internet access. “We are confident Tanzania will see more affordability in the months to come guaranteed by the widest coverage and quality network from Zain”.

This promotion will enable Zain customers to have free calls after the first minute, 100 free sms and 200mb/s free Internet Access all from midnight to 6 in the morning and hence continues to enjoy the only true 1 Tshs tariff.

The offer will be for Zain prepaid customers only and will not require any registration

THE DON HIMSELF

Karibuni sana kwenye blog hii ya kijamii iliyosheheni makila kitu kuanzia siasa uchumi afya na burudani kwa ujumla wake.uingiapo kwenye blog hii ni mengi ambayo utapata nafasi ya kukutana nayo,kumbuka mawazo yako ndo hasa yanayojenga na kunifanya niwe na ufanisi zaidi.kariiiiiiibuuuuuuuuuuuu saaaaaaaaaaaaaaanaaaaaaaaaa.(THE DJ HIMSELF-JIWE)

Followers

BLOG ZA MARAFIKI

Search This Blog

ZILIZOPITA

DUNIA MUZIMA