* Ni ofa ya mwezi mtukufu wa Ramadhan
Katika kuadhimisha mwezi mtukufu wa Ramadhani, kampuni ya Vodacom Tanzania sasa inawawesha awateja wake zaidi ya milioni saba kupigiana simu bure kuanzia saa sita usiku mpaka saa 12 asubuhi kila siku.
Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Vodacom Tanzania, Bi. Mwamvita Makamba, alisema Jijini leo (Jana) kwamba huduma hii ni zawadi kwa wateja wake katika kipindi hiki cha mwezi mtukufu wa Ramadhan.
Alisema huduma hii ni sehemu ya uwajibikaji wa kampuni yake kwa wateja wake na kwamba siku zote Vodacom imedhamiria kutoa huduma zake kwa bei nafuu, zenye kuaminika na ambazo zinakwenda sanjari na mahitaji ya watu wa Tanzania.
“Vodacom ni sehemu ambayo yanapatikana mambo makubwa na murua kwa ajili ya kukata kiu ya mawasilino kwa wateja wetu na pia kwenda nao sanjari wakati wakitimiza ndoto zao za mafanikio ndani ya nchi hii nzuri,” alisema.
Bi. Makamba alifafanua kwamba kampuni yake itaendelea kutoa huduma bora za vifurishi na za mawawsiliano ya simu za mkononi zikiwa kwenye ubora wa hali ya juu huku zikipatikana kwenye mtandao bora wa mawasiliano wenye viwango vya mawasiliano vyenye ubora wa kimataifa vinavyokidhi mahitaji ya mawasiliano kwa watu wa kada mbalimbali katika jamii yetu wakiwamo wajasiriamali, wakulima wafanyakazi na wafanyabiashara wakubwa.
Bi Makamba alitoa wito kwa Watanzania ambao hawajajiunga na Vodacom Tanzania, kujiunga haraka ili waweze kupata manufaa mengi yanayotokana na huduma bora zinazopatikana ndani ya familia kubwa ya Vodacom.
“Kwa wale ambao tayari ni wateja wa Vodacom endeleeni kufaidi huduma zetu ambazo zimebuniwa ili kurahisisha na kuboresha maisha ya Watanzania,” alisema na kuongeza mara zote kampuni yake imekuwa ikiongoza kwa ubunifu wa huduma za bora akiitaja huduma maarufu ya utumaji pesa hapa nchini ya Vodafone M-PESA kuwa ni kielelezo hai.
Alifafanua kwamba kwa kuwa katika kipindi hiki cha mwezi mtukufu wa Ramadhan, watu wengi huchelewa kulala kutokana na kusubiri daku na shughuli nyingine za taratibu za kidini, basi Vodacom Tanzania inawapa fursa wateja wake kuwasiliana bure wakati wakitakiana heri na fanaka ndani ya mwezi huu wa toba.
Katika kipindi hiki cha mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani, Waislam Duniani kote huungana kwa kufunga sanjari na sala, pia hupata fursa ya kuwasaidia wenzi wao waishio kwenye mazingira magumu.
No comments:
Post a Comment