Oct 15, 2010

uzinduzi wa filamu za ulaya wafana sana leo jijini dar


Balozi wa Umoja wa Ulaya nchini Tanzania,Tim Clarke akizungumza katika uzinduzi wa filamu za Ulaya uliofanyika New World Cinema,Mwenge jijini Dar usiku huu.
Mmoja wa watengeneza filamu kutoka nchini Ujerumani,Matthias Luthardt akitoa maelezo ya filamu yake aliyoitengeneza,kwenye uzinduzi wa filamu za Ulaya uliofanyika jioni hii katika ukumbi wa New World Cinema,Mwenge jijini Dar.
wadau pia walikuwepo.
Balozi wa Ufaransa nchini,Jaque Champagne de Labriolle (kushoto) akiwa katika mazungumzo na mmoja wa wageni waliofika katika uzinduzi huo.
Balozi wa Umoja wa Ulaya nchini,Tim Clarke akibadilishana mawazo na baadhi ya wageni waalikwa waliofika katika uzinduzi huo wa filamu uliofanyika jioni hii katika ukumbi wa New World Cinema,Mwenge jijini Dar.
Tayana Tibenda (shoto) kutoka 1 plus,akifanya mahojiano na mmoja wa watengeneza filamu kutoka nchini Ujerumani,Matthias Luthardt katika uzinduzi wa filamu za Ulaya uliofanyika jioni hii katika ukumbi wa New World Cinema,Mwenge jijini Dar.
Mkuu wa Kitengo cha Habari ofisi ya Umoja wa Ulaya Tom Vens (kushoto) akiwa katika mazungumzo na mmoja wa waakilishi wa balozi za umoja wa Ulaya.
wageni waalikwa wakibadilishana mawazo.
kucheza na nyoka
vijawa wa Wanne Star wakicheza na Nyoka katika uzinduzi wa Filamu za Ulaya uliofanyika jioni hii katika ukumbi wa New World Cinema,Mwenge jijini Dar.
maongezi ya hapa na pale yalitawala kwa mabalozi wa jumuiya ya Ulaya waliofika katika uzinduzi huo wa Filamu za Ulaya.
Balozi wa Umoja wa Ulaya,Tim Clarke (katikati) akiwa katika mazungumzo na Mkuu wa Kitengo cha Habari ofisi ya Umoja wa Ulaya Tom Vens (kushoto) na Mkurugenzi wa 1Plus,Fina Mango
Balozi wa Ufaransa nchini,Jaque Champagne de Labriolle akicheza na Nyoka.
Balozi wa Umoja wa Ulaya,Tim Crarke (pili kulia) akimwangalia Ofisa Habari wa Umoja wa Ulaya nchini,Henry Lyimo (kulia).wengine ni mchezea Nyoka hiyo na mmoja wa wageni waalikwa.
wageni mbali mbali walikuwepo.
Balozi wa Umoja wa Ulaya nchini,Tim Clarke akizungumza katika uzinduzi huo.
furaha ilitawala katika uzinduzi huo.

wageni waalikwa wakibadilishana mawazo.

Rais Jakaya Kikwete ahitimisha mbio za mwenge Kigoma.

kiongozi wa mbio za mwenge kitaifa mwaka huu 2010 Dr.Nassoro Ally Matuzya akimkabidhi mwenge wa Uhuru Rais Dr.Jakaya Mrisho Kikwete wakati wa sherehe za kilele cha mbio hizo kilichofanyika katika uwanja wa michezo wa Lake Tanganyika mjini Kigoma leo mchana.
Kiongozi wa mbio za mwenge kitaifa mwaka huu 2010 Dr.Nassoro Ally Matuzya akikabidhi risala za utii kwa Rais Dr.Jakaya Mrisho Kikwete wakati wa cherehe za kilele cha mbio za mwenge zilizofanyika katika uwanja wa michezo wa Lake Tanganyika mjini Kigoma leo mchana.
Rais Dr.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na timu ya viongozi wa mbio za
mwenge wa Uhuru mwaka huu wakati wa sherehe za kilele cha mbio hizo
zilizofanyika katika uwanja wa michezo wa Lake Tanganyika mjini Kigoma leo(Picha na Freddy Maro)

Oct 14, 2010

MWANAMUZIKI SELIF KEITA AWAPAGAWISHA MASHABIKI WA JIJI LA DAR MOVENPICK USIKU HUU!!

Mwanamuziki Nguli kutoka nchini Mali Afrika ya Magharibi akipagawisha mashabiki wake katika katika onesho lakezito lililofanyika kwenye hoteli ya Movenpick usiku huu watu ni wengi wanapiga mayowe ya furaha kwa jinsi mwanamuziki huyo Albino alivyowakamata mashabiki wake ni onesho linalosisimua kweli kweli hao wanaocheza ni waimbaji wake kushoto ni mwanadada Bah Koyaute na katikati ni mwanadada mwingine Aminata Doute. Mwanamuziki Selif Keita anadhihirisha uwezo wake wa kuimba na mpangilio wa vyombo vya muziki ukichagizwa na waimbaji wake mahiri ambao wnaonekana kulitawala jukwaa katika kiwango cha hali ya juu.
Mwanamuziki Selif Keita kutoka nchini Mali akipagawaisha mashabiki wake huku akiwa na watoto Ahmed kulia na Abdurahim kushoto ambao ni walemavu wa ngozi kama yeye.
Mpiga gitaa la basi wa kundi hilo akionekana kupiga kwa hisia huku waimbaji wakicheza kwa staili ya aina yake.
Harouna akipiga kifaa cha kiasili kinachoitwa ngoni Ngoni, Mwnamuziki Selif anachanganya vifaa mbalimbali katika kuunda muziki wake ikiwa ni pamoja na vifaa vya muziki vya kisasa kutoka nchi za magharibi na vifaa vya muziki vya asili ya Afrika na muziki unatoka ukiwa na ala yenye ladha ya aina yake.
Mashabiki wa mwanamuziki huyo wakifuatilia kwa karibu onesho la mwanamuziki huyo.
Mwanamziki Keisha kushoto akiimba pamoja na Amina kabla ya Nguli wa muziki kutoka nchini Mali Selif Keita kiupanda jukwaani, mwanamuziki huyo mkali anatarajiwa kipanda muda mfupi kuanzia sasa na tutawaletea matukio ya shughulia yake akiwa jukwaan Live kutoka hapa katika Hoteli ya Movenpick ambapo tumeshaseti mitambo tayari kwa kukuletea tukio zima kama litakavyojiri usiku huu.
Jimmy Kabwe ambaye ndiye MC katika onesho hilo wa pili kutoka kushoto akiwa na waimbaji wa mwanamuziki Selif Keita kabla ya kupanda jukwaani tayari kwa kufanya mambo makubwa mkutoka Afrika Magharibi kushoto ni Aminata Doute, Bah Kouyate na Harouna,
Aliyekuwa mbunge wa viti maalum mama Shaymar Kwegir kushoto akiwa na wageni wengine walioalikwa katika onesho mhilo.
Wabunifu wa mavazi Ally Remtullah na Vida wakiwa katika picha ya pamoja nao wamejitokeza ili kushuhudia onesho hilo usiku huu.
Mratibu wa onesho hilo Bw. Cleitus wa pili kutoka kushoto akitoa maelekezo kwa MC wa onesho hilo Jimmy Kabwe kulia huku Mwanamuziki Keisha akisikiliza mwisho kushoto ni Bw. Fuad.
Hawa wao wanabadilishana mawzo na kupata vinywaji huku wakisubiri burudani kutoka kwa gwiji huyo Selif Keita.
Mashaniki wametulia tulii kwenye viti vyao wakisubiri burudani ya mwanamuziki huyo mkonhwe kutoka Mali Afrika Mgharibi.
Mashabiki mbalimbali wa mwanamuziki Selif Keita kutoka Mali wakiwa tayari kwa kumsikiliza katika onesho lake linalotarajiwa kuanza sio muda mrefu kuanzia sasa kwenye hoteli ya Movenpick jijini Dar es salaam.

kumbukumbu ya miaka 11 ya kufariki kwa Baba wa Taifa Mwalimu J.K Nyerere


Mwalimu akiwa amebebwa juu juu baada ya kupata uhuru
Mwalimu Julias K.Nyerere na Mzee Abeid A.Karume wakipita mitaa ya Dar es Salaam kusherehekea na wananchi siku ya kwanza ya Muungano
Mwalimu akichanganya udongo kwa kuashiria muungano wa Tanganyika na Zanzibar
enzi hizo: Baba wa Taifa,Mwalimu Julius Nyerere akiwa na aliekuwa Rais wa Msumbiji miaka hiyo,Hayati Samora Machel pamoja na wake zao.mama Maria Nyerere (kulia) na mama Graca Machel
Mwalimu Nyerere akiwa na Rais Mstaafu wa awamu ya tatu,Mh. Benjamin Mkapa
Mwalimu akiwa na Fidel Castro wa Cuba.
Mwalimu akifurahi jambo na Shujaa Nyirenda
siku mwili wa Baba wa Taifa ulipowasili nchini toka nchini Uingereza.

Oct 13, 2010

MAPACHA WA3 KUZINDUA "JASHO LA MTU" OKTOBA 15 TRAVELTINE.

Kutoka kulia ni Khalid Chuma (Chokoraa) wa Bendi ya African Stars, Josse Mara wa FM Academia na Kalala Hamza (Kalala Junior) kutoka katika kundi lao la (Mpacha Wa3) wakiwa katika picha ya pamoja leo kwenye mgahawa wa Hadees wakati walipozungumza na waandishi wa habari kuhusu uzinduzi wa albam yao ya (Jasho la Mtu) utakaofanyika Oktoba 15 kwenye ukumbi wa Traveltine Magomeni jijini Dar es salaam. Uzinduzi hupo umeandaliwa na kampuni ya Alabama Inc na utasindikizwa na bendi ya African Stars ya jijini Dar es salaam pamoja naye mfalme wa taarab kutoka kundi la taarab la Jahazi Molden Taarab Mzee Yusuf ambaye pia ni mjumbe wa kamati ya utendaji ya klabu ya Yanga. U*zinduzi huo umedhaminiwa na Clouds FM, Clouds TV, Channel Ten, DTV, Magic FM, Mama Ife Intertainment, Gazeti la Risasi, Eventlites, Valley Springs Ltd, Lulu Quality Cosmetics, Amos Collection, Rutiginga Commision Agency na Zizou Fashion.
Mapacha watatu wakiwa katika mkutano wao na waandishi wa habari kwenye mgahawa wa Hadees jijini Dar es salaam leo.

Rais Khama wa Botswana amtembelea Rais Kikwete Mtwara

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimkaribisha mgeni wake Rais wa Botswana Luteni Jenerali Seretse Khama Ian Khama ikulu ndogo ya Mtwara leo mchana.Baadaye viongozi hao walifanya mazungumzo ya faragha.
Rais Jakaya Kikwete akiwa na mgeni wake Rais wa Botswana Luteni Generali Seretse Khama Ian Khama ikulu ndogo mjini Mtwara leo mchana(picha na Freddy Maro)

TAARIFA YA MAHAKAMA YA TANZANIA KWA UMMA

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA MAHAKAMA YA TANZANIA TAARIFA KWA UMMA
Taarifa hii ya uongozi wa Mahakama ya Tanzania ni kutokana na yaliyojitokeza leo siku ya tarehe 13 Oktoba 2010 nje ya jengo la Mahakama Kuu mara baada ya kesi Na. 95 ya Mwaka 2003 kuahirishwa. Uamuzi huo wa Mahakama ulipokelewa kwa hisia tofauti.Taarifa hii inakusudia kutoa ufafanuzi sahihi wa suala zima ili kuepuka tafsiri potofu inayoweza kujitokeza. Ieleweke kuwa shauri la msingi lilikwisha Mahakamani kwa kutolewa hukumu ambayo ilitoa ushindi kwa Wazee wa iliyokuwa Jumuiya ya Afrika Mashariki ambao ni Karata Ernest na Wenzake dhidi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali. Kwa mujibu wa sheria, ukazaji wa hukumu dhidi ya Serikali una matakwa yanayotakiwa kukidhiwa, ikiwa ni pamoja na kuwasilisha maombi Mahakamani kwa ajili ya kuomba Hati (Certificate). Hati hiyo huwasilishwa kwa Mlipaji Mkuu wa Serikali (Paymaster General) kwa ajili ya taratibu za malipo (Kifungu cha 16 cha Government Proceedings Act Sura ya 5 ya Sheria kama zilivyorejewa mwaka 2002). Washindi, pamoja na mambo mengine wamekuwa na mitazamo miwili tofauti kuhusiana na tuzo, idadi ya wanaodai na idadi ya wanaostahili kulipwa. Hii ni sababu kuu iliyochelewesha suala hili kufikia tamati. Hili ndio lililopelekea Mahakama kutoa amri tarehe 27 Julai 2010. Tarehe 27 Julai 2010, Mahakama ilitoa amri kwa washindi kuwasilisha maombi ya pamoja baada ya kubaini kuwepo makundi hayo mawili yanayopingana miongoni mwao. Zaidi, tarehe hiyo Mahakama ilipanga kusikiliza maombi haya tarehe 27 mwezi Septemba 2010 baada ya kupokea nyaraka zote muhimu. Kwa bahati mbaya, tarehe hiyo iliyopangwa maombi hayo hayakuweza kusikilizwa sababu Mh. Jaji N. M. Mwaikugile alikuwa katika likizo fupi. Lakini hata kama angekuwepo bado yasingeweza kusikilizwa sababu hakukuwa na Kiapo cha pamoja kwa Washindi (Joint Affidavit by the Decree Holders). Hii ni kutokana na mawakili wanaowakilisha makundi haya mawili walihitaji muda zaidi wa kuhakiki orodha ndefu ya Wadai ili kuandaa kiapo hicho cha pamoja. Mawakili walikuwa na ombi la kuomba kuongezewa muda ili waweze kuwasilisha kiapo hicho. Hii ilipelekea shauri hili kupangwa tarehe ya leo (13 Oktoba 2010) ambapo wangewasilisha maombi yao mbele ya Mh. Jaji anaesikiliza shauri hili. Tarehe ya leo Mh. Jaji, ameamua kujitoa kuendelea na shauri hili ili haki itendeke na kuonekana imetendeka kwa mujibu wa taratibu na kanuni za kimaadili zinavyoelekeza. Jalada liliwasilishwa mbele ya Mh. Jaji Kiongozi ambae alimpangia Mh. Jaji Utamwa. Leo hii, mawakili wa makundi yote mawili pamoja na Wakili wa Serikali wamewasilisha hoja zao mbele ya Mh. Jaji J.H.K. Utamwa kuomba kuongezewa muda wa kuwasilisha nyaraka muhimu. Mh Jaji amelikubali ombi hilo kwa kuwataka wahusika wawasilishe nyaraka hizo kabla au siku ya tarehe 15 Oktoba 2010 saa tano asubuhi. Shauri limepangwa kutajwa tarehe hiyo hiyo kwa ajili ya amri stahili. Huu ndio ukweli wa suala hili na si vinginevyo. Ieleweke pia kuwa kama isingekuwa kutoelewana kwa washindi, suala hili lingekuwa limeshafikia tamati siku nyingi. F.S.K. MUTUNGI MSAJILI MAHAKAMA YA RUFAA 13 Oktoba 2010

dr. bilal ahutubia mkutano wa kampeni wilayani bahi leo



Mgombea Mwenza wa urais kwa tiketi ya CCM, Dk. Mohamed Gharib Bilal, akiwahutubia wananchi wa Kijiji cha Mndemu Wilaya ya Bahi Mkoa wa Dodoma leo wakati alipofanya mkutano wa kampeni na kumnadi mgombea ubunge wa Jimbo hilo la Bahi, Omar Baduwel.
Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Dk. Mohamed Gharib Bilal akisalimiana na Mkuu wa Wilaya ya Bahi, Betty Mkwasa wakati alipowasili kwenye Kijiji cha Mndemu Wilaya ya Bahi Mkoa wa Dodoma leo mchana kwa ajili ya kufanya mkutano wa kampeni.
Dk. Mohamed Gharib Bilal akivua kofia yake na kumvisha Kijana, James Charles wakati akifurahia ngoma ya asili ya Kikundi cha Vijana cha Chomamoto wakati alipowasili Kijiji cha Mndemu Wilaya ya Bahi Mkoa wa Dodoma leo kufanya mkutano wa kampeni na kumnadi mgombea ubunge wa Jimbo hilo la Bahi, Omar Baduwel.Picha na Muhidin Sufiani

THE DON HIMSELF

Karibuni sana kwenye blog hii ya kijamii iliyosheheni makila kitu kuanzia siasa uchumi afya na burudani kwa ujumla wake.uingiapo kwenye blog hii ni mengi ambayo utapata nafasi ya kukutana nayo,kumbuka mawazo yako ndo hasa yanayojenga na kunifanya niwe na ufanisi zaidi.kariiiiiiibuuuuuuuuuuuu saaaaaaaaaaaaaaanaaaaaaaaaa.(THE DJ HIMSELF-JIWE)

Followers

BLOG ZA MARAFIKI

Search This Blog

ZILIZOPITA

DUNIA MUZIMA