Oct 13, 2010

MAPACHA WA3 KUZINDUA "JASHO LA MTU" OKTOBA 15 TRAVELTINE.

Kutoka kulia ni Khalid Chuma (Chokoraa) wa Bendi ya African Stars, Josse Mara wa FM Academia na Kalala Hamza (Kalala Junior) kutoka katika kundi lao la (Mpacha Wa3) wakiwa katika picha ya pamoja leo kwenye mgahawa wa Hadees wakati walipozungumza na waandishi wa habari kuhusu uzinduzi wa albam yao ya (Jasho la Mtu) utakaofanyika Oktoba 15 kwenye ukumbi wa Traveltine Magomeni jijini Dar es salaam. Uzinduzi hupo umeandaliwa na kampuni ya Alabama Inc na utasindikizwa na bendi ya African Stars ya jijini Dar es salaam pamoja naye mfalme wa taarab kutoka kundi la taarab la Jahazi Molden Taarab Mzee Yusuf ambaye pia ni mjumbe wa kamati ya utendaji ya klabu ya Yanga. U*zinduzi huo umedhaminiwa na Clouds FM, Clouds TV, Channel Ten, DTV, Magic FM, Mama Ife Intertainment, Gazeti la Risasi, Eventlites, Valley Springs Ltd, Lulu Quality Cosmetics, Amos Collection, Rutiginga Commision Agency na Zizou Fashion.
Mapacha watatu wakiwa katika mkutano wao na waandishi wa habari kwenye mgahawa wa Hadees jijini Dar es salaam leo.

No comments:

THE DON HIMSELF

Karibuni sana kwenye blog hii ya kijamii iliyosheheni makila kitu kuanzia siasa uchumi afya na burudani kwa ujumla wake.uingiapo kwenye blog hii ni mengi ambayo utapata nafasi ya kukutana nayo,kumbuka mawazo yako ndo hasa yanayojenga na kunifanya niwe na ufanisi zaidi.kariiiiiiibuuuuuuuuuuuu saaaaaaaaaaaaaaanaaaaaaaaaa.(THE DJ HIMSELF-JIWE)

Followers

BLOG ZA MARAFIKI

Search This Blog

ZILIZOPITA

DUNIA MUZIMA