Mgombea Mwenza wa urais kwa tiketi ya CCM, Dk. Mohamed Gharib Bilal, akiwahutubia wananchi wa Kijiji cha Mndemu Wilaya ya Bahi Mkoa wa Dodoma leo wakati alipofanya mkutano wa kampeni na kumnadi mgombea ubunge wa Jimbo hilo la Bahi, Omar Baduwel.
Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Dk. Mohamed Gharib Bilal akisalimiana na Mkuu wa Wilaya ya Bahi, Betty Mkwasa wakati alipowasili kwenye Kijiji cha Mndemu Wilaya ya Bahi Mkoa wa Dodoma leo mchana kwa ajili ya kufanya mkutano wa kampeni.
Dk. Mohamed Gharib Bilal akivua kofia yake na kumvisha Kijana, James Charles wakati akifurahia ngoma ya asili ya Kikundi cha Vijana cha Chomamoto wakati alipowasili Kijiji cha Mndemu Wilaya ya Bahi Mkoa wa Dodoma leo kufanya mkutano wa kampeni na kumnadi mgombea ubunge wa Jimbo hilo la Bahi, Omar Baduwel.Picha na Muhidin Sufiani
No comments:
Post a Comment