Mwanamuziki Nguli kutoka nchini Mali Afrika ya Magharibi akipagawisha mashabiki wake katika katika onesho lakezito lililofanyika kwenye hoteli ya Movenpick usiku huu watu ni wengi wanapiga mayowe ya furaha kwa jinsi mwanamuziki huyo Albino alivyowakamata mashabiki wake ni onesho linalosisimua kweli kweli hao wanaocheza ni waimbaji wake kushoto ni mwanadada Bah Koyaute na katikati ni mwanadada mwingine Aminata Doute. Mwanamuziki Selif Keita anadhihirisha uwezo wake wa kuimba na mpangilio wa vyombo vya muziki ukichagizwa na waimbaji wake mahiri ambao wnaonekana kulitawala jukwaa katika kiwango cha hali ya juu.
Mwanamuziki Selif Keita kutoka nchini Mali akipagawaisha mashabiki wake huku akiwa na watoto Ahmed kulia na Abdurahim kushoto ambao ni walemavu wa ngozi kama yeye.
Mpiga gitaa la basi wa kundi hilo akionekana kupiga kwa hisia huku waimbaji wakicheza kwa staili ya aina yake.
Harouna akipiga kifaa cha kiasili kinachoitwa ngoni Ngoni, Mwnamuziki Selif anachanganya vifaa mbalimbali katika kuunda muziki wake ikiwa ni pamoja na vifaa vya muziki vya kisasa kutoka nchi za magharibi na vifaa vya muziki vya asili ya Afrika na muziki unatoka ukiwa na ala yenye ladha ya aina yake.
Mwanamziki Keisha kushoto akiimba pamoja na Amina kabla ya Nguli wa muziki kutoka nchini Mali Selif Keita kiupanda jukwaani, mwanamuziki huyo mkali anatarajiwa kipanda muda mfupi kuanzia sasa na tutawaletea matukio ya shughulia yake akiwa jukwaan Live kutoka hapa katika Hoteli ya Movenpick ambapo tumeshaseti mitambo tayari kwa kukuletea tukio zima kama litakavyojiri usiku huu.
Jimmy Kabwe ambaye ndiye MC katika onesho hilo wa pili kutoka kushoto akiwa na waimbaji wa mwanamuziki Selif Keita kabla ya kupanda jukwaani tayari kwa kufanya mambo makubwa mkutoka Afrika Magharibi kushoto ni Aminata Doute, Bah Kouyate na Harouna,
Aliyekuwa mbunge wa viti maalum mama Shaymar Kwegir kushoto akiwa na wageni wengine walioalikwa katika onesho mhilo.
Wabunifu wa mavazi Ally Remtullah na Vida wakiwa katika picha ya pamoja nao wamejitokeza ili kushuhudia onesho hilo usiku huu.
Mratibu wa onesho hilo Bw. Cleitus wa pili kutoka kushoto akitoa maelekezo kwa MC wa onesho hilo Jimmy Kabwe kulia huku Mwanamuziki Keisha akisikiliza mwisho kushoto ni Bw. Fuad.
Hawa wao wanabadilishana mawzo na kupata vinywaji huku wakisubiri burudani kutoka kwa gwiji huyo Selif Keita.
No comments:
Post a Comment