Aug 16, 2010

VODACOM TANZANIA YAFUTURISHA WATOTO YATIMA JIJINI DAR ES SALAAM!!

Mgeni rasmi Sheikh Mkuu wa Tanzania Sheikh Issa Shaabani Simba akisoma hotuba yake katika viwanja vya Karimjee leo jioni wakati wa Futari iliyoandaliwa na Kampuni ya simu za mkononi Vodacom Tanzania kupitia kitengo chake cha Vodacom Foundation maalum kwa watoto yatima wa vituo mbalimbali vya jijini Dar es salaam katika mfungo huu wa mwezi mtukufu wa (Ramadhan) ambapo waislamu kote duniani hufunga kama utekelezaji wa nguzo muhimu katika kumcha mwenyezi mungu.
Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania Bw. Dietlof Mare akizungumza wakati akikaribisha watoto yatima kutoka vituo mbalimbali vya jijini Dar es salaam na wageni waalikwa wakati wa futari kwenye viwanja vya karimjee leo jioni kushoto ni mkurugenzi wa kitengo cha Teknohama Vodacoma Tanzania Maharage Chande.
Sheikh Mkuu wa Tanzania Sheikh I ssa Shaabani Simba kushoto akipokea ndoo ya mafuta ya kula kutoka kwa Mkurugenzi wa Vodacom Tanzania Dietlof Mare kwa niaba ya watoto hao kama moja ya zawadi ambazo kampuni hiyo imetoa kwa vituo hivyo ili mkusaidia kwa ajili ya futari kulia nia Mkurugenzi Vodacom Foundation Mwamvita Makamba na katikati ni mmoja wa wasaidizi wa Sheikh Mkuu wa Tanzania Sheikh Issa Shaaban Simba.
Wafanyakazi mbalimbali wa vodacom wakiwa katika picha ya pamoja na watoto hao.
Sheikh Mkuu wa Tanzania Sheikh Issa Shaabani Simba kushoto akiwasili kwenye viwanja vya Karimjee kama mgeni rasmi katika futari iliyoandaliwa na Vodacom Tanzania kulia ni Mkurugenzi wa kampuni hiyo Dietlof Mare.
Mkurugenzi wa Vodacom Foundation Mwamvita Makamba akiwaongoza wageni walioonozana na Sheikh Mkuu Issa Shaaban Simba wakati walipowasili kwenye viwanja vya Karimjee.
Mkurugenzi wa Vodacom Foundation akiwa katika picha ya pamoja na watoto kwa ajili ya kupokea zawadi kutoka Vodacom.
Meneja wa Vodacom Foundation Yessaya Mwakifulefule kulia akiwa na wadau wa Vodacom Edwin Temba kati na mdau mwingine Mohamed Kalambo wa Vodacom.
.Afisa Uhusiano wa Vodacom Mwamvua Mlangwa kushoto, Afisa wa Vodacom Foundation Grace Lyon katikati na Meneja Mawasiliano wa Vodacom Tanzania Necta Foya wakijiandaa kupokea wageni mbalimbali katika futari hiyo.
Hapa watoto wakiimba kaswida kabla ya muda wa kufuturu kuwadia.
Hapa watoto wakisuburi kufuturu vituo mbalimbali vya kulelea watoto villialikwa na mkuleta watoto kwa ajili ya kupata futari na wenzao ktoka maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es salaam.

Uchaguzi mkuu wa TASWA wafana

Sehemu ya wanachama wa Taswa wakati wa uchaguzi mkuu huoWagombea wakisubiri matokeo

Wajumbe

Tom Chilala na wajumbe wengine mkutanoniJuma Pinto na Ibrahim Masudi 'Maestro' kabla ya matokeo kutangazwaMwenyekiti mpya wa TASWA na Kamati yake kuu

Vicheko wakati wa kusubiri matokeo

'Takukuru' nao walikuwepo kuangalia mambo....

Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi TASWA akitangaza matokeo

Mwenyekiti mpya wa TASWA Juma Pinto na viongozi wenzie

Wana TASWA mkutanoni

wana TASWA

Wajumbe wa TASWA mkutanoniUongozi wa TASWA uliomaliza muda wake katika picha ya pamoja

Chama cha waandishi wa habari za michezo nchini Tanzania, TASWA, kimefanya uchaguzi wa viongozi wapya baada ya uongozi wa zamani kumaliza muda wake wa miaka mitatu kama katiba inavyoelekeza. Katika uchaguzi huo viongozi wapya waliochaguliwa ni:

MWENYEKITI: JUMA PINTO
MAKAMU MWENYEKITI:
MAULID KITENGE
KATIBU MKUU:
: AMIR MHANDO
KATIBU MSAIDIZI:
GEORGE JOHN
MTUNZA HAZINA:
SULTAN SIKIRO
MSAIDIZI:
MOHAMED MKANGARAKWA
WAJUMBE: ELIUS KAMBIRI, GRACE HOKA, ZENA CHANDE, ALFRED LUCAS, OSMAN KAPINGA, SALUM JABA

Ufafanuzi wa CCM juu ya sakata la kuenguliwa Mwakalebela kugombea Ubunge Iringa mjini

Baada ya jina la Frederick Mwakalebela kuenguliwa katika orodha ya wagombea Ubunge kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi, CCM, baadhi ya watu wamekuwa wakihoji uhalali wa kufanya hivyo il hali wana-CCM wengine wanaogombea viti hivyo katika majimbo mengine nchini wana kesi mahakamani lakini wameruhusiwa kuendelea na kinyang’anyiro hicho. Maswali hayo yaliifikia CCM na hapa ni ufafanuzi wake:

Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Halmashauri Kuu ya CCM (NEC-CCM), Mh. John Chiligati amesema kesi inayomkabili mshindi wa kura za maoni aliyepokwa ‘haki’ ya kuteuliwa kugombea ubunge wa Iringa Mjini kwa tiketi ya chama hicho, Frederick Mwakalebela, haifanani na washindi wengine wa kura za maoni walioteuliwa ambao ni Basil Mramba anayegombea jimbo la Rombo na Andrew Chenge anayegombea jimbo la Bariadi Mashariki licha ya kuwa na kesi mahakamani kama yeye.

Alisema

Mh. Andrew Chenge

Mh. Basil Mramba

Bw. Frederick Mwakalebela

Mwakalebela ameachwa kwa sababu ya kukosa kwake maadili.

“Suala kwa Mwakalebela ni maadili tu, katika mchakato huu, kakamatwa kwa tuhuma za rushwa na TAKUKURU wamesema wanayo sababu ya kumpeleka mahakamani.” “Lakini alikuwa ndio kwanza kaingia katika mchezo wenyewe na katika mchezo huu huu kabla ya dakika 90, akapigiwa filimbi kuwa amecheza faulo,” alisema Chiligati.

Kuhusu tofauti ya Mramba, Chenge na Mwakalebela Chiligati alisema, “ kisheria wote ni watuhumiwa na hawakutwa na hatia, lakini kimaadili ni tofauti… Mramba anatuhumiwa kutumia vibaya madaraka, tuliita wanasheria wakasema hiyo kesi haimuondolei sifa ya kuwa mgombea.”

Hata hivyo alikiri kuwa Mramba alipitishwa baada ya kufanyika mjadala kati ya wajumbe hao wa NEC.
“Katika Mkoa wa Shinyanga Jimbo la Bariadi Mashariki aliteuliwa Chenge kutetea nafasi yake, anayo kesi ya trafiki, haimkoseshi haki ya kuwa mgombea,” alisema Chiligati.

credit source: http://www.wavuti.com

Aug 15, 2010

WALIOTEULIWA KUGOMBEA UBUNGE KATIKA BUNGE LA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA KWA KUPITIA CHAMA CHA MAPINDUZI KATIKA UCHAGUZI MKUU 2010

1.MKOA WA KIGOMA
(i) Mjini: Peter Serukamba,
(ii)Kigoma South: Gulam Hussein Shaaban Kifu,
(iii)Kasulu Urban: Neka Raphael Neka,
(iv)Kasulu Rural: Daniel Nsanzugwanko,
(v)Manyovu: Albert F. Ntabaliba,
(vi)Buyungu: Christopher Chiza,
(vii)Muhambwe: Jamal Abdallah Tamimu,
(viii)Kigoma North: Rabinson, F. Lembo.

2.MKOA WA KILIMANJARO
(I) Moshi Mjini:Justin Salakana,
(ii) Moshi Vijijini: Dk. Cyril Agust Chami,
(iii)Rombo: Basil Pesambili Mramba,
(iv)Same Mashariki): Anne Kilango Malecela,
(v)Same Magharibi: Dk. David Mathayo David,
(vi)Hai: Fuya Godwin Kimbita,
(vii) Vunjo: Chrispin Theobald Meela,
(viii) Mwanga: Profesa Jumanne Maghembe,
(ix)Siha, Aggrey D.J. Mwanri.

3.MKOA WA MANYARA:
(i)Babati mjin:Kisyeri Werema Chambiri,
(ii)Babati Vijini: Jitu Vrajil Soni,
(iii)Hanang: Dk. Mary Michael Nagu,
(iv)Kiteto: Benedict Ole Nangoro
(v) Mbulu:Philip Sang’ake Marmo,
(vi)Simanjiro:Christopher Ole Sendeka.

4.MKOA WA MARA
(i) Musoma mjini: Vedasto Manyinyi,
(ii)Musoma vijijini:Nimrod Elirehema Mkono,
(iii)Mwibara: Alphaxard Kangi Lugola,
(iv)Bunda: Stephen Masatu Wasira,
(v)Rorya: Lameck Okambo Airo,
(vi)Tarime, Nyambari Chacha Nyangwine,
(vii)Serengeti: Dk. Stephene Kebwe Kebwe.

5.MKOA WA MBEYA
(i) Mbeya Mjini: Benson Mwailugula Mpesya,
(ii) Mbeya Vijijini: Luckson Ndage Mwanjala,
(iii) Kyela: Dk Harrison George Mwakyembe,
(iv)Mbarali: Dickson Modestus Kilufi,
(v)Lupa: Victor Kilasile Mwambalaswa,
(vi) Songwe:Philipo Augustino Mulugo,
(vii) Rungwe Mashariki: Profesa Mark James Mwandosya,
(viii) Rungwe Magharibi: Profesa David Homeli Mwakyusa,
(ix) Ileje: Aliko Nikusuma Kibona,
(x)Mbozi Mashariki: Godfrey Weston Zambi,
(xi)Mbozi Magharibi: Dk. Luka Jelasa Siame.


6. MKOA WA MOROGORO

(i)Morogoro Mjini:Aziz Mohamed Abood,
(ii)Morogoro Kaskazini: Dk. Lucy Sawera Nkya,
(iii)Morogoro Kusini: Innocent Kalogeris,
(iv)Mvomero: Amos Gabriel Makala
(v) Ulanga Mashariki: Celina Ompeshi Kombani,
(vi)Ulanga Magharibi: Haji Hussein Mponda,
(vii)Gairo: Ahmed Mubukhut Shabiby
(viii)Kilosa, Mustafa Heidi Mkulo,
(ix)Mikumi: Abdulsalaam Suleiman,
(x)Kilombero: Abdul Rajab Mteketa.

7.MKOA WA TABORA
(i)Urambo Mashariki: Samwel John Sitta
(ii)Urambo Magahribi: Juma Athuman Kapuya,
(iii)Tabora Mjini: Ismail Aden Rage,
(iv)Igunga: Rostam Abdulsasu Aziz,
(v)Sikonge: Said Juma Nkumba
(vi) Igagula: Athuman Rashid Mfutakamba
(vii) Tabora: Sumar Shaffin Mamlo,
(viii)Bukene: Seleman Jumanne Zedi
(ix)Nzega:Dr. Hamisi Andrea Kigwangala

8.MKOA WA TANGA
(i)Tanga mjini: Omari Rashid Nundu
(ii)Kilindi: Beatrice Matumbo Shelukind
(iii)Muheza: Herbert James Mntangi
(iv)Mkinga: Danstan Luka Kitandula
(v)Pangani: Salehe Ahmed Pamba
(vi)Lushoto: Henry Daffa Shekifu
(vii)Bumbuli: January Makamba
(viii)Korogwe Mjini:Yusuph Nasri
(ix)Mlalo:Brig. Gen. Hassan Athuman Ngwilizi
(x)Korogwe Vijijini: Stephen Ngonyani
(xi)Handeni: Dr. Abdalah Omari Kigoda

10.MKOA WA DAR ES SALAAM
(i).Kinondoni: Idd Mohamed AZAN
(ii).Ubungo: Hawa Mgonja NG’UMBI
(iii).Kawe: Angella Charles KIZIGHA
(iv).Ilala: Musa Azan ZUNGU
(v).Ukonga: Eugen Elishirima MWAIPOSA
(vi).Segerea:Dr. Milton Makongoro MAHANGA
(vii).Temeke: Abbas Zuber MTEMVU
(viii).Kigamboni:Dr. Faustine NDUGULILE

11.MKOA WA LINDI
(i)Lindi Mjini:Ndugu Mohamed ABDULAZIZ
(ii)Mtama:Ndugu Bernard Kamillius MEMBE
(iii)Mchinga:Ndugu Said M. MTANDA
(iv)Nachingwea:Ndugu Mathias Meinrad CHIKAWE
(v)Ruangwa:Ndugu Kassim MAJALIWA
(vi)Kilwa kaskazini:Ndugu Murtaza Ali MANGUNGU
(vii)Kilwa Kusini:Ndugu Ramadhan Rashid MADABIDA
(viii)Liwale:Ndugu Faith Mohamed MITAMBO

12.MKOA WA PWANI
(i)Bagamoyo: Dr. Shukuru J. Kawambwa
(ii)Chalinze: Saidi Athuman Bwanamdogo
(iii)Kisarawe: Seleman Saidi Jafo
(iv)Kibiti: Abdul J. Marombwa
(v)Kibaha Vijijini: Mahamud Abuu Jumaa
(vi)Kibaha Mjini: Silvestery F. Koka
(vii)Mkuranga: Adam Kighoma Malima
(viii)Rufiji: Dr. Seif Seleman Rashid
(ix)Mafia: Abdulkarim E. Shaha

13.MKOA WA RUKWA
(i)Kwela: Malocha Aloyce Ignace
(ii)Kalambo: Kandege Sinkamba Josephat
(iii)Nkasi Kaskazini: Ally Mohamed Kessy
(iv)Nkasi Kusini:Deusderius Mipata
(v)Mlele: Mizengo Kayanza Peter Pinda
(vi)Mpanda Kati (mjini): Sebastian Simon Kapufi
(vii)Sumbawanga Mjini: Aeshi Khalfan Hilaly
(viii)Mpanda Vijijini: Moshi S. Kakoso

14.MKOA WA SHINYANGA
(i)Shinyanga Mjini: Steven Julius Masele
(ii)Kishapu: Nchambi Seleman Masoud
(iii)Kahama: James Daud Lembeli
(iv)Msalala: Maige Ezekiel Magolyo
(v)Solwa: AhmeD Ally Salum
(vi)Bukombe: Emanuel Jumanne Luhahula
(vii)Mbogwe: Masele Agustino Manyanda
(viii)Bariadi Mashariki: Makondo Martine Kaunda
(ix)Bariadi Magharibi: Chenge Andrew John
(x)Maswa Mashariki: Bunyongoli Peter Edward
(xi)Maswa Magharibi: Kisena Robert Simon
(xii)Meatu:Salum Khamis Salum
(xiii)Kisesa: Joelson Luhaga Mpina.

15.MKOA WA SINGINDA
(i)Singida Mjini:Mohamed Gulam Dewji
(ii) Manyoni Mashariki:Capt.(mstaafu) John Chiligati
(iii)Manyoni Magharibi: John Paul Lwanji
(v)Iramba Magharibi: Mwigulu Lameck Nchemba Matelu
(vi)Iramba Mashariki:Salome David Mwambu
(vii)Singida Kaskazini:Lazaro Samwel Nyalandu
(viii)Singida Magharibi:Alhaj Mohamed Misanga
(ix)Singida Mashariki:Jonathan Andrew Njau

16.MKOA WA ARUSHA
(i)Arusha:Dr. Batilda BURIANI
(ii)Arumeru Mashariki: Jeremiah Solomon SUMARI
(iii)Arumeru Magharibi: Goodluck Joseph Ole MEDEYE
(iv)Karatu: Dr. Wilbald Slaa LORRI
(v)Longido: Michael Lekule LAIZER
(vi)Monduli: Edward Ngoyai LOWASSA
(vii)Ngorongoro: Saning’o Kaika Ole TELELE

17.MKOA WA IRINGA
(i)Iringa Mjini: Monica Ngenzi MBEGA
(ii)Isimani: William Vangimembe LUKUVI
(iii)Kalenga: William Augustino MGIMWA
(iv)Kilolo:Prof. Peter Mahamudu MSOLLA
(v)Ludewa: Deo Haule FILIKUNJOMBE
(vi)Makete:Dr. Binilith Satano MAHENGE
(vii)Mufindi Kaskazini: Mohamed Hassan MGIMWA
(viii)Mufindi Kusini: Menrad Lutengano KIGOLA
(ix)Njombe Kaskazini:Deo Kasenyenda SANGA (Jah People)
(x)Njombe Kusini: Anne Semamba MAKINDA
(xi)Njombe Magharibi: Gerson Hosea LWENGE

18.MKOA WA KAGERA
(i)Nkenge: Assumpter Nshunju MSHAMA
(ii)Bukoba Mjini: Khamis S. KAGASHEKI
(iii)Bukoba Vijijini:Ndugu Jasson S. RWEIKIZA
(iv)Muleba Kaskazini: Charles J. MWIJAGE
(v)Muleba Kusini: Anna K. TIBAIJUKA
(vi)Chato: John Pombe MAGUFULI
(vii)Kyerwa: Eustace O. KATAGIRA
(viii)Karagwe: Gosbert B. BLANDES
(ix)Biharamulo: Oscar R. MUKASA
(x)Ngara: Deogratias Aloys NTUKAMAZINA

Aug 14, 2010

Rais Kikwete aongoza Kikao Cha halmshauri Kuu ya CCm TaIFA MJINI Dodoma jana aagana na Balozi wapya wa Tanzania Ufaransa na Marekani!!

Mwenyekiti wa CCM Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Waziri Mkuu Mizengo Pinda muda mfupi kabla ya kuanza kwa kikao cha Halmshauri Kuu ya CCM Taifa mjini Dodoma leo asubuhi.Katikati ni Katibu mkuu wa CCM Yusuf Makamba. Baadhi ya wajumbe wa Halmashauri kuu ya CCM Taifa wakiwa katika kikao leo mjini Dodoma. Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiagana na Balozi mpya wa Tanzania nchini Ufaransa Mhe. Begum Taj wakati balozi huyo na mwenzake Balozi Mwanaidi Maajar(kulia) walipokwenda kumuaga ikulu ndogo mjini Dodoma leo asubuhi.Balozi Mwanaidi Maajar aliyekuwa balozi wa Tanzania nchini Uingereza anakuwa balozi wa Tanzania nchini Marekani na kituo chake cha kazi kitakuwa Washington. Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongoza kikao cha halmashauri kuu ya CCm Taifa mjini Dodoma leo asubuhi.Wengine katika picha kutoka kushoto ni Rais Mstaafu awamu ya Tatu Benjamin William Mkapa, Rais Mstaafu awamu ya pili Mzee Ali Hassan Mwinyi,Makamu wa CCM Bara Pius Msekwa na kulia nia katibu mkuu wa CCM Yusuf Makamba.

Aug 13, 2010

BAADA YA 'MACHO KODO' DR LEADER SASA KUJA NA 'KAGOMA KWENDA'

MSANII wa muziki wa kizazi kipya nchini Lucas Silas "Dr.Leader" amewataka mashabiki wake wakae tayari kwa ajili ya ujio wake mpya na wimbo wake mwengine ambao unakwenda kwa jina la "Kagoma Kwenda" anayotarajia kuiachia hivi karibuni.

Msanii huyo ambaye kwa sasa anatamba na wimbo wake Macho Kodokodo ambao unafanya vizuri katika vituo mbalimbali vya redio hapa nchini,na Kueleza kuwa na wimbo huo ambao anatarajia kuuachia utakuwa mzuri zaidi.

Akizungumza na blog hii Dr.Leader alisema kuwa kwa sasa anacho angalia ni kitu gani ambacho mashabiki wake wanakuwa wanakiitaji ili kuweza kuwaridhisha pia kuweza kutambilika kimataifa kupitia mziki huo.

Dr.Leader alisema kuwa wasanii ambao ni chipukizi hawapaswi kukata tamaa hivyo waendeleee kufanya kazi zao vizuri na kwa kuzingatia maadili ya kazi zao pamoja na kujituma ili waweze kutambulika na kupata mafaniko.

Msanii huyo pia alielezea kuwa changamoto zinazowakabili wasanii wa mikoani ni kutokuwa na watu ambao wanakuwa wakiwasapoti katika kazi zao hivyo kuufanya mziki huo kuwa mgumu kwa kwa wasanii wa mikoani.

MAMLAKA YA BANDARI TANZANIA YATAKIWA KUWALIPA FIDIA WAKAZI WA NDUMI TANGA!

WAZIRI wa miundombinu Dkt Shukuru Kawamba ameitaka mamlaka ya Bandari kuharakisha malipo ya wananchi waliochukuliwa maeneo yao kwa ujenzi wa Bandari mpya wa eneo la Ndumi ambapo hekta 82 zinahitaji kufidiwa ili kuepusha migogoro.

Dkt Kawambwa alikuwa jijini Tanga kwa ajli ya uzinduzi wa sera ya Taifa ya usalama barabarani na wiki ya nenda kwa usalama iliyofanyika kitaifa mkoani Tanga,alisema ili kuondoa dhana ya ujenzi bandari ya Tanga ni hadithi wananchi wanapaswa kufidiwa.

Pamoja na agizo hilo kwa mamlaka ya bandari,Waziri Kawambwa alisema yeye na wizara yake itahakikisha kwamba inalisimamia suala hilo ili kuweza kuharakisha ulipwaji wa wananchi sambamba na mchakato wa ujenzi wa bandari hiyo ya Ndumi.

"Mimi kama waziri mwenye dhamana nitahakikisha utekelezaji unakuwepo zoezi la ujenzi wa bandari hii mpya,pia nitahakikisha ujenzi wa miundombinu mingine kama ya reli ya Tanga Arusha na Arusha Musoma unatekelezwa"alisema Waziri Kawambwa.

Hata hivyo waziri Kawambwa alisema kwamba utekelezwaji wa miradi hiyo ni mpango wa serikali katika kutekeleza ilani ya chama cha mapinduzi CCM katika sehemu ya ahadi zake ilizowaahidi wananchi ambapo wamedhamiria kwa dhati kukamilisha suala hilo.

Pia aliwataka wananchi kuwa na subira kuhusiana na ujenzi wa bandari mpya kuhusiana na upitikanaji wa michakato mbalimbali ili kuweza kuwa na umakini wa suala zima la jenzi wa Bandari ya Ndumi sambamba na uimarishaji wa miundombinu ya reli nchini.

Kaimu mkurugenzi mkuu wa mamlaka ya bandari nchini,Julius Mfuko alisema mchakato wa ulipaji umeshaandaliwa na miezi mitatu kuanzia sasa utaanza kulipwa na miezi mitatu kuanzia sasa wananchi wataanza kulipwa na Bil 1.7 zimetengwa kwa ajili ya malipo.

Alisisitiza kuwa mamlaka ya bandari tayari imeandaa upembuzi yakinifu ambapo dola mil 695.5 zimetengwa ili kufanikisha ujezi wa bandari mpya na mil 500 ndizo zilizofanya upembuzi yakinifu ambapo yanasubiriwa maelekezo ya wizara ya miundombinu.

Mfuko alibainisha kuwa kwa upande wa mamlaka ya bandari mchakato unaendelea vizuri ambapo wanasubiri serikali kupitia wizara yake ya miundombinu kuwapatia maelekezo ili ujenzi huo wa bandari uweze kufanyika haraka na kwa ufanisi na tija
(kwa msaada wa blog jirani)

SHIRIKISHO LA SANAA ZA MAONYESHO WAPATA VIONGOZI


Viongozi waliochaguliwa wakiwa kwenye picha ya pamoja na wajumbe mbalimbali wa mkutano huo pia wasimamizi wa uchaguzi huo.Katikati waliokaa kwenye viti ni Msimamizi Mkuu wa Uchaguzi huo,Dkt.Hebert Makoye.


Picha/Habari na Afisa Habari wa BASATA,Alistide Kwizela.


Mkakati wa kuyawezesha na kuyapa nguvu mashirikisho ya wasanii nchini leo umeendelea tena ambapo shirikisho la Wasanii wa Sanaa za Maonyesho limefanya uchaguzi na kujipatia viongozi wake wa muda watakaoliongoza jahazi kwa mwaka mmoja.

Katika uchaguzi wa leo uliofanyika kwenye Ukumbi wa Baraza la Sanaa,BASATA na kusimamiwa na Mkuu wa Idara ya Sanaa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam,Dkt.Hebert Makoye,Bi.Agnes Lukanga aliibuka kidedea katika kiti cha urais baada ya kuwashinda wapinzani wake ambao ni Alex Mwakabama (6) na Denis Mango (6).

Ushindani mwingine ulikuwa kwenye kiti cha Makamu wa Rais ambapo, Bw.Abraham Bawadhil ambaye ni Mkufunzi katika Taasisi ya Sanaa Bagamoyo TaSUBA aliibuka mshindi baada ya kumuangusha Alex Mwakabama aliyeambulia kura 6 pekee.

Aidha,nafasi ya Katibu Mtendaji ilinyakuliwa na Denis Mango aliyepata kura 15 dhidi ya tatu za Irene Sanga huku nafasi ya mweka hazina ikichukuliwa na Mary Mwangato aliyepata kura 9.Nafasi za ujumbe zilienda kwa Alex Mwakibinga, Nkwama Bhalanga na Mahadia Ally.

Baada ya uchaguzi kumalizika, jopo la usimamizi likiongozwa na Dkt.Makoye lilitoa nasaha kwa viongozi kwa kuwataka kuja na mikakati ya muda mfupi na mrefu ya kulifanya shirikisho hilo kusimama na kuwa na nguvu pia kujenga umoja miongoni mwa wasanii wa sanaa za maonyesho kwa ajili ya utetezi wa haki na maslahi yao.

Katibu Mtendaji wa BASATA,Ghonche Materego aliwaeleza viongozi kwamba, kazi kubwa ya shirikisho hilo ni kufufua nguvu ya sanaa za maonyesho ambazo katika siku za hivi karibuni imefifia kutokana na ujio wa teknolojia mpya.Alisema kwamba, leo hii hakuna sehemu mtu anaweza Kwenda kuangalia ngoma, maigizo, sarakasi nk. na hii ni kutokana na wadau kulala,hivyo shirikisho halina budi kuja na mikakati ya kukuza sanaa hiyo adhimu.

Naye Mlezi wa Mashirikisho ya Wasanii,Mzee Rashid Masimbi ambaye pia ni Mjumbe wa Bodi ya BASATA alisema kwamba, kazi iliyoko mbele ya shirikisho hilo ni kuja na mpango kazi kabambe, kuandaa kanuni za kuliongoza shirikisho, kutafuta ofisi, kuongoza wanachama wapya na kusaka fedha kwa ajili ya kuendesha rasmi shughuli za shirikisho.

Kesho ni zamu ya Shirikisho la Sanaa Jongevu (Filamu) ambapo litapata rasmi viongozi wake na kuanza safari ya kuandika historia mpya katika tasnia ya sanaa nchini.Wadau wote mnakaribishwa sana kushiriki.Matokeo yatatangazwa kwenye vyombo vya habari

Matukio ya Kikao cha Kamati Kuu ya CCM Ddodoma Jana


Baadhi ya Wajmbe wa Kamati Kuu ya CCM wakikusanya makabrasha ya agenda za Kikao
cha Kamati Kuu ya CCM,mara baada ya kuahirishwa leo huko Dodoma Makao Makuu ya
Chama hicho.


Wajumbe wa wakimsikiliza katibu Mkuu wa CCM Rajab Yussuf Makamba akitoa taarifa
ya kuahirishwa kikao cha kamati kuu ya CCM leo Dodoma.picha kwa hisani ya Ramadhan Othman Abdalla.


Wajumbe wa Kamati Kuu ya CCM wakijadili jambo,wakiwa nje ya Ukumbi wa Mkutano
wa Mako Makuu ya CCM Dodoma leo.

HALI TETE CCM, CC YAAHIRISHWA


Sadick Mtulya, Dodoma

UKIUKWAJI mkubwa wa taratibu wakati wa kura za maoni, tuhuma za rushwa na wanachama kupinga maamuzi ya baadhi ya kamati za siasa za mikoa kugeuza matokeo, ni mambo ambayo yanaendelea kuisumbua CCM kiasi cha kamati kuu kulazimika kuahirisha kikao ambacho kilitakiwa kufanyika jana.

Ratiba ya awali ilionyesha kuwa kamati hiyo ingefanya kikao chake jana na leo kujadili ajenda za halmashauri kuu baada ya kamati ya maadili kumaliza kuzipitia ajenda hizo.

Lakini, taarifa zilizolifikia gazeti hili jana zilieleza kuwa kamati ya maadili ilishindwa kumaliza kazi ya kupitia ajenda hizo kutokana na wingi wa malalamiko yaliyowasilishwa na wagombea na baadhi ya wanachama kupinga matokeo ya kura ya maoni na maamuzi ya kamati za siasa.

Katibu mkuu wa CCM, Yusuf Makamba aliwaambia wajumbe wa kamati kuu jana akisema: “... kikao chetu cha leo cha CC kimepata udhuru kidogo, hivyo tumekiahirisha hadi kesho saa 3:00 asubuhi.

“Sababu kuu ni kamati ya maadili ya chama hadi sasa (saa 9:26 alasiri) bado haijamaliza kazi yake.”

Kikao cha kamati ya maadili kilianza jana majira ya 5:00 asubuhi mara baada ya sekretarieti ya CCM kumaliza kikao cha kuandaa ajenda za kamati kuu. Sekretarieti ilikuwa na kikao chake kuanzia juzi.

Hata hivyo, vyanzo vyetu vilisema uzito wa malalamiko yaliwayosilishwa kuhusu mchakato mzima wa kura ya maoni ya kuchagua wagombea ubunge na udiwani ulivyofanyika Agosti mosi, hasa vitendo vya rushwa, ndio sababu kubwa ya kamati ya maadili kushindwa kumaliza kikao chake kwa wakati.

“Kwa asilimia kubwa karibu wagombea wote waliojitokeza kwa ajili ya kuchaguliwa katika kura za maoni ya CCM, walivunja maadili ya chama, hasa kwa kujihusisha na vitendo vya rushwa," alisema mmoja wa watu walio karibu na kamati kuu.

“Suala hili ndilo limesababisha kamati kushindwa kumaliza kikao chake kulingana na ratiba.”

Baada ya kauli ya Makamba, baadhi ya wajumbe wa kamati ya maadili, akiwamo rais mstaafu wa serikali ya awamu ya pili, Alhaji Ali Hassan Mwinyi na wa awamu ya tatu, Benjamin Mkapa walitoka katika kikao cha ndani cha kamati hiyo na kuchukua nyaraka zao zilizokuwepo katika meza kuu ya ukumbi wa White House na kurudi nazo ndani, kuashiria kuendelea na kikao cha kamati ya maadili.

Kampeni na kura za maoni za CCM zilitawaliwa na vitendo vya rushwa na kusababisha wagombea wengi na viongozi wa matawi na kata wa chama hicho kukamatwa na kuhojiwa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru). Hadfi sasa ni wagombea watatu tu ambao wameshafikishwa mahakamani.

Mbali na vitendo vya rushwa, upigaji kura za maoni ulitawaliwa na ukiukwaji mkubwa wa taratibu uliosababisha vurugu kwenye baadhi ya vituo na hivyo kusababisha wagombea wengi kukata rufaa baada ya matokeo kutangazwa wakidai kuwa kulikuwa na rafu nyingi.

Vikao vya kamati za siasa za mkoa ambazo hutoa alama kwa wagombea navyo viliamsha tatizo jingine kutokana na wanachama karibu katika kila mkoa kufanya maandamano kwenda kwenye ofisi za chama hicho kupinga taarifa zilizokuwa zimezagaa kuwa washindi kwenye kura hizo wamepewa alama za chini zinazomaanisha kuwa hawastahili kupitishwa na chama kugombea.

Kamati ya maadili inaongozwa na Rais Jakaya Kikwete ambaye pia ni mwenyekiti CCM, na wajumbe wengine ni pamoja na makamu mwenyekiti wa CCM Bara, Pius Msekwa, na makamu mwenyekiti wa CCM Zanzibar, Amani Abeid Karume ambaye pia ni rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Wengine ni Makamba, marais wastaafu, Mwinyi na Mkapa.

Katika hatua nyingine, wajumbe wote wa kamati kuu jana walihudhuria kikao isipokuwa mwanasiasa mkongwe, John Samuel Malecela pamoja na waziri mkuu wa zamani, Edward Lowassa.

Haikuweza kufahamika sababu ya wajumbe hao kukosekana katika kikao hicho muhimu cha chama.

Baadhi ya wajumbe waliohudhuria ni spika wa Bunge anayemaliza muda wake, Samuel Sitta, na naibu wake, Anne Makinda, spika wa Baraza la Wawakilishi, Pandu Amir Kificho, mgombea mwenza wa urais kwa tiketi ya CCM, Dk Ghalib Bilal pamoja na Abdallah Kinana.

Katika hatua nyingine, wanachama 40 wa CCM Kata ya makulu jana walikamatwa wakati walipokuwa wakiandamana kwenye kundi la wanachama 100 kupinga kubadilishwa kwa jina la Ally Bilingi aliyeshinda katika kura za maoni za udiwani katika kata hiyo.

Mwenyekiti wa Kitongoji cha Bilingi, Steven Ngogo aliliambia Mwananchi kuwa waliamua kwenda ofisi ya CCM ya Wilaya ya Dodoma Mjini kuhakikisha kama kweli ushindi wa Bilingi ulibatilishwa.

“Tulikuwa zaidi ya 90, lakini wenzetu zaidi ya 40 wamekamatwa na Polisi majira ya saa 6:00 mchana wakati tulipokuwa tunakuja huku kama kweli jina la Bilingi ambaye alishinda kwa kura 190, limeondolewa,’’ alisema Ngogo.

Ngogo alifafanua kwamba taarifa ya kubadilishwa kwa ushindi wa Bilingi ziliwafikia mapema na kwamba ilisemekana uamuzi huo ulitokana na kamati ya siasa ya kata kumpa alama ya D.

Hata hivyo, mwenyekiti wa wilaya hiyo, Denis Bendera aliwahakikisha wanachasma hao kuwa hakuna matokeo yeyote yaliyobatilishwa.
“Hakuna matokeo yeyote ya kata na viti maalum hadi sasa yaliobatilishwa. Lakini Agosti 15, ndio majibu yatatolewa rasmi na mtapewa siku tatu za kupinga,’’ alisema Bendera.

Kamanda wa polisi wa Dodoma, Steven Zelothe alisema: "Kwa sasa siwezi kuzungumzia kukamatwa kwa hao watu... wewe si unajua kwamba kwa sasa Dodoma ina ugeni mkubwa wa rais, makamu, mawaziri,” alisema Zelothe.

CHANZO: MWANANCHI

UTAFUTAJI WA WABUNIFU UMEANZA SASA


Ubunifu wa Vera Swao katika Swahili Fashion week 2009
Modo akiwa katika vazi la Kemi Kalikawe Swahili Fashion week 2009

Modo wa kiume katika vazi la Manju Msita Swahili Fashion Week 2009


Kwa mara nyingine tena sekta ya ubunifu Tanzania inatoa fursa kwa wabunifu wote wenye ndoto za kuwa wabunifu bora kushikiri katika shindano la kuibua vipaji vya wabunifu hapa Tanzania . Shindano hili la mwaka limekua likifanyika chini ya mwanvuli wa jukwaa kuu la Africa Mashariki Swahili Fashion Week.

“Tunaangalia wabunifu ambao wana malengo ya kuwa wabunifu bora wa mavazi hapa Tanzania ” Alisema Mustafa Hassanali, mbunifu maaruvfu wa mitindo ambaye ndiye mwandaaji wa shughuli hiyo .

"Shindano hili linafanyika kwa mwaka wa tatu sasa, halina kikwazo cha umri, na linatoa fursa kwa watu wote wanaoamini kwamba wana kipaji cha ubunifu, na wanataka kuwa wabunifu. “Swahili Fashion Week ni jukwaa bora kwa wabunifu kuonyesha uwezo wao wa ubunifu na kuibua sindano la wabunifu wapya, ni jukwaa linalowawezesha watu kufikia malengo yao ”, aliongeza Mustafa Hassanali, ambaye pia ndiye mwasisi wa Swahili Fashion Week.

Shindano hili linatoa fursa kwa wabunifu kutoka pande zote za Tanzania . Mwisho wa kujisajili ni tarehe 30th ya mwezi wa August 2010. “Mwaka 2008 Edwin Musiba alishinda, na mwaka 2009 alishinda 2jenge Afrika Matalay, najiuliza nani atashinda mwaka huu?”, alimalizia Hassanali.

Kwa maelezo zaidi kuhusiana na shindano la ubunifu, tafadhali wasilina na Mratibu wa Swahili Fashion Week bwana
Washington Benbella,
simu namba
0717 547792

au
kupitia barua pepe ,

designers@swahilifashionweek.com

Rais Jakaya atambua mchango wa wakulima!!

Na Stella Chipanha –Bunge - Dodoma
1: Benki ya kilimo kuanzishwa
2:Wakulima wapatiwa tumaini jipya
3:Umwagiliaji wapanuka
4:Jakaya aunda wizara mpya ;Mifugo na uvuvi
5:Aahidi ari zaidi kasi zaidi
Akiahidi ari zaidi na kasi zaidi Rais Jakaya ametoa uhakika zaidi kwa wakulima katika Maswala ya pembejeo, mbegu na kuimarisha masoko kwa mazao ya kilimo, akieleza hayo katika kilele cha nanenane mjini Dodoma Rais kikwete alisema tuna mikakati endelevu ya kuimarisha juhudi katika masoko kwa mkulima na mfugaji
Wakati wa hotuba yake Rais Jakaya Kikwete alisema wanamikakati maalum kuunda vyama vya ushirika kwa wafugaji alisema lazima tuunde vyama vyetu ambavyo vitasimamia shuguli za wafugaji ili ufugaji huo uwe wenye mafanikio na tija, alisisitiza kuwa kiwepo kitengo cha ukaguzi wa vyama vya ushirika waaminifu na si wababaishaji
Katika hotuba yake aliwataka sekta binafsi kuwa na mashamba makubwa zaidi nakuwataka wauze kwa bei nzuri inayo wezekana kwa kila mwananchi mwenye kipato cha chini (affordable price) Wakati huo huo Rais Jk alisema serikali yake inamikakati zaidi kuanzisha viwanda vya kusindika na kutengeneza bidhaa mbalimbali nchini na si kuendelea kutegemea nje.
Rais Jakaya alisema Serikali imeongeza million kumi na moja kwenye benki ya wakulima itakayosaidia kuongeza viwanda katika kukamilisha sera ya mapinduzi ya kijani, kilimo, ufugaji, uvuvi kupewa kipao mbele, kwa maarifa zaidi ili kusukuma maendeleo kwa kasi kubwa zaidi nchini
Alimaliza kwakusema bidhaa nyingi zinaonekana tu siku ya maonyesho ya nanenane nakupotea,” msije kwa ajili ya maonesho bali mtumie teknolojia inayowezekana kuifanya bidhaa hiyo hai zaidi popote nchini inapohitajika”

ANDREW CHALE ASEMA VIJANA TUSIWE MITAJI YA WAGOMBEA!!

VIJANA wameaswa kuepuka kurubuniwa na vitu vidogo kwa kipindi hiki cha kuelekea uchaguazi mkuu na baadala yake wajihadhari ili kuepuka kutumiwa vibaya sambamba na kugeuzwa mitaji ya watu wenye uchu wa madaraka.
Hayo yalisema jana jijini Dar es Salaam, na mwenyekiti wa muda wa Kata ya Magomeni kwa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Andrew Chale wakati wa kupitisha maadhimio,kuziba nafasi zilizokua wazi pamoja na mikakati ya kampeni kwa ngazi ya udiwani wa Kata hiyo zinazotalajia kuanza Agost 20 mwaka huu Chale ambaye ni mwandishi wa habari wa gazeti la Taznzania Daima na mwanaharakati wa kutetea haki za vijana na watoto waishio katika mazingira magumu, aliwaomba vijana kuacha kutumiwa na wenye uchu wa madaraka wanaowafuata kipindi hiki na kuwaahidi kuwasaidia wakati zaidi ya miaka mitano awajaonekana katika majimbo yao.
“Jamani vijana wenzangu wa magomeni na wa Tanzania huu sasa ni wakati wa kusema basi tusiwe jalala la wanasiasa,wakiwapa pesa kuleni siri yenu ipo CHADEMA kipe kura yako ilikuweza kuleta mabadiliko ya kweli’ alisema Chale.
Aidha, aliwataka vijana kutokubaliana na sera za viongozi juu ya kuwapatia ajira kwani kila miaka wanasema hayo na hakuna kipya; Nawaomba vijana wenzangu kwa muda mwingi viongozi tunaowachagua wanatumia migongo yetu kujinufaisha huku wahusika tukiwa hatuna thamani tukatae kugeuzwa mitaji’ Katika mkutano huo uliodhuriwa na wajumbe mbalimbali wa chadema kata hiyo ambapo Chale alichaguliwa kushika nafasi hiyo kwa muda wa siku 72 muda ambao utafanyika uchaguzi wa viongozi ndani ya Kata hiyo, Awali nafasi hiyo ya mwenyekiti ilikua ikishikiliwa na Said Omary Said ‘Afsa’ ambaye kwa sasa anawania udiwani katika Kata hiyo.
Kwa upande wake Mwenyeki wa Vijana wa Kata hiyo, Abdalah Mtundu aliwataka vijana kuchagua chama makini na kukipa kura ilikuweza kuendeleza demokrasia nchini. “Umefika wakati wa kila kijana kujitambua ilikujiongezea upeo na maalifa,ni kwa kuichagua chama makini

Vodacom Tanzania yamwaga Vifaa kwa Vilabu Ligi Kuu!!

Dar es Salaam 13, August 2010. Vodacom Tanzania leo imekabidhi vifaa mbalimbali vyenye thamani ya shilingi milioni 290 kwa timu zinazoshiriki Ligi Kuu ya Vodacom msimu wa mwaka 2010/11.
Akizungumza na Waandishi wa Habari wakati wa hafla fupi ya kukabidhi vifaa hivyo kwa wawakilishi wa vilabu vinavyoshiriki ligi hiyo, Mkuu wa Udhamini wa Vodacom Tanzania George Rwehumbiza alisema ni matumaini ya kampuni yake kwamba vifaa hivyo vitakuwa ni kichocheo cha kuinua kiwango cha soka hapa nchini.
Alisema huu ni msimu wa tisa tangu Vodacom ianze kudhamini Ligi hiyo na kwamba Vodacom inafarijika kuona kiwango cha soka kikipanda.
Mbali na kukabidhi zawadi hizo, alivishauri vilabu kutafuta njia nyingine za kuongeza mapato ikiwamo kutafuta wadhamini wengine ili kukabiliana na kupanda mara kwa mara kwa gharama za uendeshaji wa vilabu.
Alisema msimu huu Vodacom imetenga zaidi ya shilingi bilioni moja kudhamini ligi hiyo.
Alisema kati ya hizo shilingi milioni 667 zimetengwa kwa shughuli za uendeshaji wa Ligi ikiwemo nauli za timu pamoja na gharama nyingine kama posho za marefa.
Rwehumbiza alisema msimu huu vifaa vimeboreshwa zaidi na kuvitaka vilabu kuvitumia vifaa hivyo kuboresha Ligi.
Alivipongeza Vilabu vya Simba na Yanga kwa kufanya vizuri msimu uliopita na kuvitakia kila lakheri msimu huu.
Aidha Mkuu wa Udhamini huyo alitoa rai kwa vilabu kuvitumia vifaa hivyo kama changamoto ya kufanya vizuri katika Ligi ya Vodacom msimu wa mwaka 2010/11na hivyo kutupatia mwakilishi bora wa katika mashindano mbalimbali ya kimataifa.

Rais Kikwete afungua mkutano mkuu wa Tanganyika Law Society Dodoma!!

Waziri wa Katiba na Sheria Mathias Chikawe akimkaribisha Rais Jakaya Mrisho Kikwete kufungua mkutano mkuu wa Tanganyika Law Society uliofanyika katika ukumbi wa Chimwaga uliopo chuo Kikuu cha Dodoma leo asubuhi.
(Picha na Freddy Maro)
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwahutubia wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Tanganyika Law Society katika ukumbi wa Chimwaga uliopo Chuo Kikuu cha Dodoma leo asubuhi.
Baadhi ya wajumbe wa mkutano mkuu wa Tanganyika Law society(TLS) wakimsikiliza Rais Jakaya Kikwete akitoa hotuba yake ya ufunguzi wa mkutano mkuu wa TLS uliofanyika katika ukumbi wa Chimwaga mjini Dodoma leo asubuhi.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete(watatu kulia) akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe waliohudhuria Mkutano mkuu wa Tanganyika Law society mjini Dodoma leo

Aug 12, 2010

SHIRIKISHO LA MUZIKI NALO LAPATA VIONGOZI WAO!!!

Mwanamuziki mkongwe wa dansi nchini ambaye pia ni mwenyekiti wa Chama cha Muziki wa Dansi (CHAMUDATA),Kassim Mapili akijinadi mbele ya wanachama kwa ajili ya kuomba nafasi ya Makamu wa Rais wa shirikisho.Mkongwe wa Muziki wa Reggae,Ras Inno Nganywangwa ambaye aliwakilisha chama cha Tanzania Urban Music Association (TUMA) akimwaga sera zake wakati akiomba nafasi ya Katibu Mkuu wa shirikisho.
Katibu Mtendaji wa BASATA,Ghonche Materego akitaja majina ya viongozi waliochaguliwa kuliongoza shirikisho kwa muda wa mpito wa mwaka mmoja.
Viongozi wote waliochaguliwa wakiwa kwenye picha ya pamoja na msimamizi wa uchaguzi Bw.Yustus Mkinga (mwenye mwenye suti).

Na Alistide Kwizela.

Hatimaye Shirikisho la Wanamuziki Tanzania leo (Jumatano) limepata viongozi wake wa muda katika uchaguzi uliofanyika kwenye Ukumbi wa BASATA na kusimamiwa na Afisa Mtendaji Mkuu wa COSOTA,Bw.Yunus Mkinga.

Katika uchaguzi huo uliokuwa wa vuta ni kuvuta,Bw.Ibra Washokera aliweza kuibuka kidedea kwenye nafasi ya urais baada ya kupata kura 12 na kumbwaga Mkongwe wa muziki wa dansi,Hamza Kalala ‘Komandoo’ aliyeambulia kura 2 tu.

Kwa upande wa nafasi ya Makamu wa Rais,Mwanamuziki wa muziki wa asili,Che Mundugwao aliibuka kidedea kwa kupata kura 9 na kuwaacha mbali wapinzani wake ambao ni Mkongwe Kassim Mapili na Gwalugano Ayoub walioambulia kura 3 kila mmoja.

Nafasi ya Katibu ilichukuliwa na Salum Mwinyi huku nafasi ya Mkurugenzi wa Fedha na Mipango ikikamatiwa na Samwel Semkuto.Aidha, wajumbe waliochaguliwa ni Samatha Rajab, Said Mukandara na George Mbata.

Wakiongea kwa kwa nyakati tofauti baada ya uchaguzi, Katibu Mtendaji wa BASATA,Ghonche Materego,Bw.Yustus Mkinga na Mlezi wa Mashirikisho ya wasanii,Mzee Rashid Masimbi walisema kwamba, kazi iliyopo mbele ni kwa viongozi hao kupanga mikakati ya muda mfupi na muda mrefu ya kuwaendeleza wasanii na kupigania maslahi yao.

Aidha, walisisitiza kwamba, kwa sasa wasanii wa muziki wanatakiwa kusimama imara chini ya shirikisho lao na kuwa na msimamo thabiti katika masuala mbalimbali yanayowahusu.

Kesho itakuwa ni zamu ya uchaguzi wa Shirikisho la Sanaa za Ufundi na keshokutwa ni shirikisho la Sanaa Jongevu (Filamu),Wadau wote mnakaribishwa kwenye chaguzi hizo ambazo ni maendeleo makubwa kwa wasanii na sekta ya sanaa kwa ujumla.

Miss Universe 2010 kwisha kwiva mjini Vegas!


While we all waiting "kwa hamu kubwa" the gorgeous Miss Tanzania 2010 Hellen Dausen gets ready for this BIG day to come, had her make up done by Kryolan Make-Up Artist Sanah Hassan as she starts the registration and fitting process in preparation for the Miss Universe 2010 Competition at Mandalay Bay Hotel and Casino in Las Vegas, Nevada on Sunday August 8th 2010.

The Miss Universe 2010 competition that will air live on the NBC Television Network at 9 PM ET, August 23, 2010.

RAMADHAN KAREEM


May Allah grant you the strength and yaqeen to complete this blessed month of Ramadhan

And may you take full advantage of these powerful days, Insha-Allah.

May I take this opportunity to wish you, your family, friends and loved
ones, A Blessed Month of Ramadhan...

May Allah's mercy and blessings be with you throughout the Holy month of
sacrifice and throughout the year, Insha-Allah.

May all your good deeds & du'as be accepted, your wishes fulfilled and all your sins forgiven.

May Allah grant us the strength to help those less fortunate in Allah's
name, Insha-Allah!

Have a splendid Ramadhan!

Remember me & my family in your Du'as

*WANACHAMA WA CCM DAR WAANDAMANA KUMPINGA MGOMBEA ALIYEPITISHWA NA KUACHWA WALIYEMCHAGUA

Wanachama hao wakiingia na mabango kwenye Lango Kuu la Ofisi za CCM Makao Makuu Lumumba leo mchana.

Wanachama wa CCM wakiandamana na mabango kuingia kwenye Ofisi za makao makuu ya CCM Lumumba Jijini Dar es Salaam leo mchana kwa kile wanachopinga kupitishwa jina la mgombea ambaye hawakumchagua katika kura za maoni kwenye Kata zao

Katibu Mwenezi wa Siasa, akijaribu kuwatuliza wanachama hao bila mafanikio baada ya kuingia kwenye ofisi hiyo.

THE DON HIMSELF

Karibuni sana kwenye blog hii ya kijamii iliyosheheni makila kitu kuanzia siasa uchumi afya na burudani kwa ujumla wake.uingiapo kwenye blog hii ni mengi ambayo utapata nafasi ya kukutana nayo,kumbuka mawazo yako ndo hasa yanayojenga na kunifanya niwe na ufanisi zaidi.kariiiiiiibuuuuuuuuuuuu saaaaaaaaaaaaaaanaaaaaaaaaa.(THE DJ HIMSELF-JIWE)

Followers

BLOG ZA MARAFIKI

Search This Blog

ZILIZOPITA

DUNIA MUZIMA