Aug 13, 2010

SHIRIKISHO LA SANAA ZA MAONYESHO WAPATA VIONGOZI


Viongozi waliochaguliwa wakiwa kwenye picha ya pamoja na wajumbe mbalimbali wa mkutano huo pia wasimamizi wa uchaguzi huo.Katikati waliokaa kwenye viti ni Msimamizi Mkuu wa Uchaguzi huo,Dkt.Hebert Makoye.


Picha/Habari na Afisa Habari wa BASATA,Alistide Kwizela.


Mkakati wa kuyawezesha na kuyapa nguvu mashirikisho ya wasanii nchini leo umeendelea tena ambapo shirikisho la Wasanii wa Sanaa za Maonyesho limefanya uchaguzi na kujipatia viongozi wake wa muda watakaoliongoza jahazi kwa mwaka mmoja.

Katika uchaguzi wa leo uliofanyika kwenye Ukumbi wa Baraza la Sanaa,BASATA na kusimamiwa na Mkuu wa Idara ya Sanaa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam,Dkt.Hebert Makoye,Bi.Agnes Lukanga aliibuka kidedea katika kiti cha urais baada ya kuwashinda wapinzani wake ambao ni Alex Mwakabama (6) na Denis Mango (6).

Ushindani mwingine ulikuwa kwenye kiti cha Makamu wa Rais ambapo, Bw.Abraham Bawadhil ambaye ni Mkufunzi katika Taasisi ya Sanaa Bagamoyo TaSUBA aliibuka mshindi baada ya kumuangusha Alex Mwakabama aliyeambulia kura 6 pekee.

Aidha,nafasi ya Katibu Mtendaji ilinyakuliwa na Denis Mango aliyepata kura 15 dhidi ya tatu za Irene Sanga huku nafasi ya mweka hazina ikichukuliwa na Mary Mwangato aliyepata kura 9.Nafasi za ujumbe zilienda kwa Alex Mwakibinga, Nkwama Bhalanga na Mahadia Ally.

Baada ya uchaguzi kumalizika, jopo la usimamizi likiongozwa na Dkt.Makoye lilitoa nasaha kwa viongozi kwa kuwataka kuja na mikakati ya muda mfupi na mrefu ya kulifanya shirikisho hilo kusimama na kuwa na nguvu pia kujenga umoja miongoni mwa wasanii wa sanaa za maonyesho kwa ajili ya utetezi wa haki na maslahi yao.

Katibu Mtendaji wa BASATA,Ghonche Materego aliwaeleza viongozi kwamba, kazi kubwa ya shirikisho hilo ni kufufua nguvu ya sanaa za maonyesho ambazo katika siku za hivi karibuni imefifia kutokana na ujio wa teknolojia mpya.Alisema kwamba, leo hii hakuna sehemu mtu anaweza Kwenda kuangalia ngoma, maigizo, sarakasi nk. na hii ni kutokana na wadau kulala,hivyo shirikisho halina budi kuja na mikakati ya kukuza sanaa hiyo adhimu.

Naye Mlezi wa Mashirikisho ya Wasanii,Mzee Rashid Masimbi ambaye pia ni Mjumbe wa Bodi ya BASATA alisema kwamba, kazi iliyoko mbele ya shirikisho hilo ni kuja na mpango kazi kabambe, kuandaa kanuni za kuliongoza shirikisho, kutafuta ofisi, kuongoza wanachama wapya na kusaka fedha kwa ajili ya kuendesha rasmi shughuli za shirikisho.

Kesho ni zamu ya Shirikisho la Sanaa Jongevu (Filamu) ambapo litapata rasmi viongozi wake na kuanza safari ya kuandika historia mpya katika tasnia ya sanaa nchini.Wadau wote mnakaribishwa sana kushiriki.Matokeo yatatangazwa kwenye vyombo vya habari

No comments:

THE DON HIMSELF

Karibuni sana kwenye blog hii ya kijamii iliyosheheni makila kitu kuanzia siasa uchumi afya na burudani kwa ujumla wake.uingiapo kwenye blog hii ni mengi ambayo utapata nafasi ya kukutana nayo,kumbuka mawazo yako ndo hasa yanayojenga na kunifanya niwe na ufanisi zaidi.kariiiiiiibuuuuuuuuuuuu saaaaaaaaaaaaaaanaaaaaaaaaa.(THE DJ HIMSELF-JIWE)

Followers

BLOG ZA MARAFIKI

Search This Blog

ZILIZOPITA

DUNIA MUZIMA