Oct 30, 2010

DR JAKAYA ALIPOHUBIRI AMANI NA KUONYA WATANZANIA WANAOHUBIRI NA KUKUMBATIA UDINI!!

Jakaya Kikwete akiongea katika mkutano wake na waandishi usiku wa kuamkia leo ukumbi wa Anatouglou jijini Dar ambapo alihojiwa maswali mbalimbali juu ya mustakabali wa nchi endapo atachaguliwa kuwa rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa awamu nyingine Uchaguzi mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani unafanyika Kesho Oktoba 31 nchini kote. Katika mahojiano hayo RaisDr. Jakaya Kikwete amewatahadhalisha watanzania kufanya maamuzi pasipo kuhubiri wala kuzingatia udini kwani kuzungumzia udini ni hatari na ni jambo litakaloigawa nchi kwa kiwango kikubwa na hakuna wa kutuokoa kwani hatuna pa kukimbilia kwakuwa nchi hii ni yetu hivyo tunatakiwa kuilinda na kuiheshimu ili tuishi kwa amani (Picha na Ankal Issa Michuzi)
Jakaya Kikwete na mgombea mwenza Dr Mohamed Gharib Bilali wakiondoka ukumbi wa Arnautoglou jijini Dar baada ya kuongea na waandishi wa habari usiku wa kuamkia leo.
Wahudhuriaji wakimsikiliza JK kwenye mkutano wake na waandishi wa habari katika ukumbi wa Arnautoglou jijini Dar usiku usiku wa kuamkia leo
Wahudhuriaji wakimsikiliza Jakaya Kikwete kwenye mkutano wake na waandishi wa habari katika ukumbi wa Arnautoglou jijini Dar usiku usiku wa kuamkia leo
Wahudhuriaji wakimsikiliza Jakaya Kikwete kwenye mkutano wake na waandishi wa habari katika ukumbi wa Arnautoglou jijini Dar
Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu Bw. Salva Rweyemamu akimuamkia Dk. Mohamed Ghalib Bilali kabla ya kuanza kwa mkutano wa Jakaya Kikwete na waandishi usiku wa kuamkia leo ukumbi wa Arnautoglou jijini Dar
Jakaya Kikwete akiwashukuru watangazaji wa TV mbalimbali waliokuwa wakimhoji kwenye mkutano na waandishi usiku huo kwenye ukumbi wa Arnautoglou jijini Dar
Jakaya Kikwete akisalimiana na waandishi na wageni waalikwa kwenye mkutano wake na waandishi ukumbi wa Arnautoglou jijini Dar
Hassan Mhelela wa BBC London akimhoji mgombea mwenza wa urais Tanzania bara Dk. Mohamed Gharib Bilal baada ya mkutano wa JK na waandishi usiku wa kuamkia leo ukumbi wa Arnautoglou jijini Dar
Hassan Mhelela wa BBC London akimhoji Makamu Mwenyekiti wa CCM Mh. Pius Msekwa baada ya mkutano wa JK na waandishi wa habari
Fundi mitambo mkuu wa Clouds TV Mehboub al Hadad akiwa kazini ambapo kituo hicho kiliungana na vingine kurusha mkutano wa JK na waandishi live
Baadhi ya wahariri wa vyombo mbalimbali wakimsikiliza JK akijibu maswali usiku wa kuamkia loe katika ukumbi wa Arnautoglou jijini Dar

Oct 29, 2010

KATIBU MTENDAJI WA BARAZA LA UWEZESHAJI (NEEC)AAGWA RASMI

Mwenyekiti wa Baraza la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC) Bw. Emmanuel Kija Kamba akizungumza katika sherehe ya kumuaga Eliseta Kwayu (katikati)Katibu Mtendaji wa Baraza hilo aliyestaafu na kumkaribisha Katibu Mtendaji mpya Bw Anaclet Kashuliza katika hafla iliyofanyika kwenye Hoteli ya Paradise City jijini Dar es salaam jana jioni (kulia) ni mama Freita Kwayu.
Katibu Mtendaji Mpya wa Baraza la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi Anaclet Kushuliza akizungumza na Bodi ya wakurugenzi wa baraza hilo pamoja na wafanyakazi wakati wa kumuaga katibu mtendaji aliyestaafu Bw Eliseta Kwayu aliyekaa (kushoto) katikati ni mke wa Mzee Eliseta Kwayu mama Freita Kwayu.
Bw. Eliseta Kwayu akiiaga Bodi ya Baraza hilo pamoja na wafanyakazi na katika hafla iliyofanyika kwenye Hoteli ya Paradise City jijini Dar es salaam kulia ni mwenyekiti wa Baraza hilo Bw. Emmanuel Kija Kamba na kushoto ni mama Freita Kwayu.
Wfanyakazi wa baraza hilo walikuwepo katika kumuaga kiongozi wao wa zamani na kumkaribisha kiongozi mpya.
Viongozi waandamizi wa Baraza hilo kutoka kulia ni Mjumbe wa bodi Charles Singili, Ally Laay Mkurugenzi wa Fedha na Utawala na mwisho ni Joyce Chonjo Mkurugenzi Uwezeshaji.
Katibu Mtendaji mpya wa Baraza hilo Anaclet Kashuliza kulia akigonganisha glasi ya mvinyo na Mjumbe wa baraza Bw. Peter Noni kama kutakiana kheri katika hafla hiyo katikati ni katibu Mtendaji wa zamani Eliseta Kwayu.
Wafanyakazi na viongozi wa Baraza hilowakigonganisha glasi kama ishara ya kutakiana kheri
Wafanyakazi wa Baraza la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi NEEC wakimkabidhi zawadi ya (Laptop) Kompyuta ndogo Katibu Mtendaji wa zamani wa baraza hilo Eliseta Kwayu na Mkewe walipomuaga Bw. Eliseta amestaafu utumishi wa umma.
Wafanyakazi wa Baraza la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi NEEC wakimkabidhi zawadi ya Katibu Mtendaji mpya wa baraza hilo Anaclet Kashuliza wakati walipomkaribisha na kumuaga Katibu Mtendaji wa zamani Bw. Eliseta amestaafu utumishi wa umma.
Hapa sasa wafanayakazi hao ilikuwa ni full kucheza tu
Mambo ni burudani tu kwa kwenda mbele si ndiyo eeeeeeeeeeeeeeeeh!

Safari Lager yatangaza kukamilisha mipango yote ya kuipeleka timu ya taifa ya Pool katika mashindano ya dunia,nchini ufaransa


Meneja wa Bia ya Safari lager,Fimbo Buttalah (kati) akizungumza mbele ya vyombo vya habari katika mkutano uliofanyika leo,wakati wa kutangazwa kwa timu ya Taifa ya Pool itakayoshiriki mashindano ya kimataifa huko nchini Ufaransa mapema mwezi ujao.Kushoto ni Mwenyekiti wa Pool Taifa,Isack Togocho na kulia ni Katibu mkuu Pool Taifa,Amos Kafwinga.
Kocha mkuu wa timu ya Taifa ya Pool,Dennis Lungu,akitangaza kikosi chake chenye wachezaji saba ambao wataondoka nchini tarehe 6,Novemba kuelekea nchini Ufaransa kushiriki mashindano ya Kimataifa.wachezaji waliopo katika kikosi hicho ni Godfrey Muhando (nahodha),Omary Akida,Mohamed Iddy,Issa Mkindi,Felix Atanas pamoja na Vaileth Mrema (mshichana pekee katika timu hiyo).katikati ni Mwenyekiti wa Pool Taifa,Isack Togocho na kulia ni Meneja wa bia ya Safari Lager ambao ndio wadhamini wakuu wa timu hii ya Pool,Fimbo Buttalah.
Baadhi wa wachezaji wa timu ya Taifa ya Pool wakiwa katika picha ya pamoja na mdhamini wao pamoja na viongozi wa timu.

****** ****** ******

Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia bia yake ya Safari Lager leo imetangaza kukamilisha mipango yote ya kuipeleka timu ya taifa ya Pool katika mashindano ya dunia yatakayofanyika katika jiji la Paris, nchini Ufaransa mwezi Novemba.

Akitangaza kukamilika kwa maandalizi ya safari hiyo muhimu kwa timu yetu ya Taifa ya Pool, meneja wa Bia ya Safari Lager, Fimbo Butallah alisema; “timu yetu ya Taifa imekuwa ikionesha mafanikio makubwa na kupanda kwa kiwango cha mchezo mwaka hadi mwaka.

Nafasi hii ya kushiriki mashindano ya Dunia imetokana na matokeo mazuri ambayo timu yetu ilionesha katika mashindano ya Afrika yaliyofanyika mwaka jana nchini Afrika ya Kusini na kuibuka namba tano, hivyo kupata nafasi ya kuwa moja ya nchi zitakazowakilisha bara la Afrika katika mashindano hayo makubwa”

Bia ya Safari Lager inaungana na watanzania wote katika kufurahia matokeo na mafanikio haya mazuri ya timu yetu ya Taifa, na hii ndio sababu kubwa iliyopelekea tuhakikishe kuwa safari hii ya kwenda Paris inafanikiwa. Pia tunaahidi kuendelea kuudhamini mchezo huu wa Pool na kuuendeleza ili tutimize ahadi zetu, ambazo ni kuufanya mchezo huu kuwa ajira ya kutegemewa kwa vijana na pia kulitangaza Taifa letu kote ulimwenguni kupitia ushiriki wa mashindano kama haya ya kimataifa.

Nachukua nafasi hii pia kuipongeza kampuni ya Integrated Communication kwa ufanisi mkubwa wanaouonesha katika kuendesha mashindano yetu ya mchezo wa Pool, kampuni hii imetusaidia sana sisi wadhamini na chama cha pool kuhakikisha tunafikia malengo yetu.

Akizungumzia Safari hiyo, Katibu wa Chama cha Pool Taifa Amos Kafwinga alisema “timu itaondoka tarehe 6 Novemba na kuwasili Paris tarehe 7, itaelekea katika mji wa LIMOGES, ambako mashindano hayo yatafanyika na timu inategemea kurudi tarehe 15. Mashindano haya yanashirikisha jumla ya nchi 32 toka katika mabara matano, na bara la Afrika linawakilishwa na timu tano ikiwemo Tanzania.

Nae Mwenyekiti wa Chama cha Pool Taifa Isaac Togocho alitoa shukrani nyingi kwa Safari Lager kwa jinsi wanavyoendeleza mchezo huu wa Pool hapa nchini, hususani kufanikisha safari hii muhimu zaidi kwa timu yetu na Taifa kwa ujumla, pia alisisitiza suala zima la nidhamu kwa vijana na ujumbe wote unaoelekea Ufaransa ili kulitangaza jina la nchi yetu vizuri na kuleta sifa hapa nyumbani.

Oct 28, 2010

RETURN OF PNC

Anajulikana kama PNC jamaa ambaye ilipata kusumbua sana kwenye gemu ya muziki wa kizazi kipya kabla ya kukaa kimya muda mrefu na sasa anarejea tena kwa nguvu kubwa zaidi akiwa na ngoma yake mpya inayokwenda kwa jina la TUZUNGUMZE.
PNC na mchizi wake SHOW ME LAV wakisikiliza ngoma ya PNC- TUZUNGUMZWE iliyokuwa inatambulishwa via 106.5fm Mlimani Radio na mkali toka pande hizo JIWE4EVER aka MWANAKIJIJI.



Oct 27, 2010

Rais Kikwete avunja rekodi Mkutano wa Kampeni Mwembeyanga,

Mgombea Urais kwa tiketi ya CCM ,Rais Dr. Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia maelfu ya wanachama wa CCM katika viwanja vya Mwembeyanga Temeke jijini Dar es Salaam leo jioni (Picha na FreddyMaro)
Umati wa wanaCCM ukimsikiliza Rais Jakaya Mrisho Kikwete katika viwanja vya Mwembeyanga jijini Dar es salaam.

MRISHO MPOTO AZALIWA NA WATOTO YATIMA WA CHAKUWAMA

Mwanamuziki wa miondoko ya kizazi kipya MRISHO MPOTO amewataka wadau mbalimbali kuwasaidia watoto yatima kielimu na kiuchumi hatua itakayosaidia watoto hao kufikia malengo yao kimaisha
Mrisho Mpoto amesema hayo wakati akisherekea siku yake ya kuzaliwa na watoto wa kituo cha CHAKUWAMA kilichopo SINZA jijini DSM ambapo pia amekiri mchango wa watoto wadogo katika mafanikio yake kimuziki.
Naye mlezi wa kituo hicho SAIDA HASSAN ameshukuru watu mbalimbali wanaovutwa kujua mahitaji ya watoto yatima na kutoa misaada yao hali iliyomfanya ashindwe kujizuia na kuwaombea Dua kwa mola
kwa msaada wa blog jirani

CCM YALALAMIKIA MATAMSHI YA MGOMBEA WA CHADEMA TEMEKE!!

Mwenyekiti wa Kamati ya Kampeni ya Chama Cha Mapinduzi CCM Bw. Abdurahman Kinana leo ameongea na waandishi wa habari katika ofisi ndogo ya chama hicho Lumumba jijini Dar es salaam na kulaani vikali matamshi ya mgombea ubunge wa jimbo la Temeke kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA Bw. Dickson Ngilly aliyoyatoa kwenye Mkutano wa Kampeni uliofanyika kwenye viwanja vya Mwembeyanga jijini Dar es salaam. Akizungumzia suala hilo Kinana amesema mgombea huyo Dickson Ngilly amezungumza maneno ambayo ni matuzsi kwa mtu yeyote mstaarabu hivyo ,CCM itawaandikia barua Tume ya Uchaguzi ya Taifa na Msajili wa vyamna vya siasa kulalamika kutokana na matamshi ya kashfa ya mgombea huyo aliyoyatoa kuhusu Mgombea wao wa Urais Dr. Jakaya Kikwete, ukizingatia kwamba Mkutano ulikuwa ni wa Mgombea Urais wa CHADEMA na alikuwepo kwenye mkutano huo lakini hakumkanya wala kumzuia kutokana na matamshi yake hayo.
Wakati huohuo Abdurahman Kinana amesema Mgombea wa Urais kupitia CCM Dr. Jakaya Kikwete atakuwa na mahojiano na vyombo mbalimbali vya habari keshokutwa Oktoba 30 kwenye ukumbi wa Anatouglo jijini Dar es salaam ambapo vyombo vya habari vitaalikwa na kumuuliza maswali mbalimbali ya moja kwa moja kutoka katika ukumbi huo. kipindi hicho kitaanza saa mbili usiku mpaka saa nne usiku.

JAMANI WANASINGIDA MJINI DEWJI HAJAKODI GARI LANGU, MMILIKI….!!!

Na Hillary Shoo,Singida.

HATIMAE sakata la Mgombea Ubunge wa Jimbo la Singida mjini kupitia chama cha CHADEMA, Josephat Isango kudai kuwa mgombea mwenzake wa CCM, Mohammed Dewji amelikodi gari alilokuwa akitumia mgombea huyo kwenye kampeni,limeingia katika sura mpya baada ya mmiliki wa gari hilo kudai kuwa alimnyang’anya kutokana na usumbufu wa malipo na kwenda kinyume na makubaliano.

Akizungumza na gazeti hili nyumbani kwake jana mmiliki wa gari hilo Saidi Madeira alisema kuwa gari hilo lilikodiwa na ofisi ya CCM mkoa wa singida na wala Dwewji hahusiki na hilo.

"Mimi niwe muwazi kwa kweli Dewji sijawahi kuzungumza nae kuhusu suala la gari langu na wala mtu yoyote kutoka katika ofisi yake, mimi gari nimelikodi kwa Katibu wa CCM Mkoa wa Singida baada ya kuona hawa jamaa wa CHADEMA ni wababaishaji katika suala la malipo.

"Awali tulikubaliana kuwa kila siku gari hilo litalipiwa shilingi 20,000 ikiwa ni pamoja na kuwaziwa mafuta na kumlipa dreva lakini nilikaa karibu wiki nzima sijalipwa fedha zangu na mbaya zaidi gari lilikuwea linakwenda hadi Ikungi sehemu ambayo haikuwa katika makubaliano namia." Alisisitiza Madeira na kuongeza.

"Malipo yalivyokuja na kushauriana na familia yangu tukaona tusiwape tena hili gari hawa jamaa wa Chadema maana linakwenda kinyume na makubaliano ndipo alifika Katibu wa CCM mkoa Naomi Kapambala na kulihitaji gari hilo kwa ajili ya shughuli zao za chama.

Alisema baada ya kuafikiana na katibu juu ya utaratibu mzima wa kazi aliamua kuwapa gari hilo aina ya Suzuki Vitara lenye namba za usajili T 663 ASZ na alilipwa fedha zake zote hadi mwisho wa uchaguzi mkuu kwisha Oktoba 31 mwaka huu.

Aidha Madeira alisema hivi sasa gari hilo liko chini ya ofisi ya CCM mkoa na wala halipo kwenye kampeni za Dewji kama inavyodaiwa na watu.

"Mimi sijawahi kuzungumza na mwandishi wa habari juu ya hili gari zaidi yako leo wewe unayenihoji, nashangaa sana kuasikia kuwa mimi nimezunguza na vyombo vya habari hii sio kweli uhandishi wa namna hii ni wa kunichonganisha mimi pamoja na familia yangu kwa ujumla."Alisisitiza.

Hata hivyo Madeira amesema kuwa anandaa utaratibu wa kisheria ili aweze kmfikisha mwandishi wa habari aliyeandika habari hiyo mahakamani ili aweze kuthibitisha madai hayo, kuwa Dewji alikodi gari hilo.

Kwa upande wake Dewji alisema anasikitishwa sana na taarifa hizo na kwamba hajawahi kukodi gari la mtu yoyote binafsi kwa ajili ya shughuli zake za kampeni.

"Mimi nina magari yangu matatu ambayo ndiyo nayatumia katika kampeni sasa nikodi gari jingine la nini, siwajawahi kufanya hivyo na wala sina haja ya magari mengine haya niliyonayo yananitosheleza kufika kila eneo na kuzungumza na wapiga kura wangu." Alisema Dewji kwa masikitiko makubwa.

Hata hivyo Dewji aliwataka wananchi pamaoja na wanachama wa CCM hivi sasa kuwa watulivu na kuachana na siasa za kuchafuana na badala yake wasubiri siku ya kupiga kura ili wamalize kazi.

Katibu wa CCM mkoa wa singida Naomi Kapambala amesema kuwa gari hilo wamelikodi wao kwa ajli ya shughuli za chama na wala Dewji hahusiki kwa lolote.

"Sisi ndio tumelikodi hili gari, Dewji hahusiki kabisa,yeye ana magari yake anayotumia katika kampeni zake, sasa hili la nini tena kwake alihoji Kapambala."Alisema

Rais Kikwete afanya mikutano ya kampeni ukonga na Segerea.

Mgombea Urai kwa tiketi ya CCM Dr.Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na baadhi ya wanachama wa CCM kata ya Kiwalani jimbo la ukonga ambapo alifanaya mkutano wa kampeni leo asubuhi. (Picha Freddy Maro na Muhidin Issa Michuzi)
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha mapindizi CCM akiendelea kusalimiana na wananchi wal;iojitokeza kwenye mikutano yake ya kampeni jijini Dar es salaam leo.
Wananchi wa jimbo la Ukonga wakiwa tayari kwa kumsikiliza mgombea wa urais kupitia CCM Dr. Jakaya Kikwete.
Wananchi waliojitokeza kwenye Mkutano wa kapeni huko Segerea leo.
Wananchi wa eneo la Segerea waliohudhuria mkutano wa kampeni wa CCM
auliohutubiwa na mgombea urais wa CCM Dr.Jakaya mrisho Kikwete leo mchana

NI KAMA WANASEMA “WE WAINGIA! MIE NATOKA KARIBU BARA”

Mgombea Mwenza wa urais wa CCM, Dk. Mohamed Gharib Bilal (kulia) akisalaimiana na Mgombea urais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein, walipokutana uwanja wa Ndege wa Mwalimu Nyerere wa Jijini Dar es Salaam leo mchana wakati Dk. Shein, akiondoka kuelekea Visiwani Zanzibar na Dk. Bilal, akiwasili jijini kutoka Visiwani humo kwa ajili ya kufanya mkutano wa kampeni leo Okt 27. (Picha na Muhidin Sufiani)
Mgombea Mwenza wa urais wa CCM, Dk. Mohamed Gharib Bilal (kulia) akizungumza na Mgombea urais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein, walipokutana uwanja wa Ndege wa Mwalimu Nyerere wa Jijini Dar es Salaam leo mchana wakati Dk. Shein, akiondoka kuelekea Visiwani Zanzibar na Dk. Bilal, akiwasili jijini kutoka Visiwani humo kwa ajili ya kufanya mkutano wa kampeni leo Okt 27. Kushoto ni mke wa Dk. Shein, Tunu Shein, akizungumza na mke wa Dk. Bilal, Zakia Bilal.
Mgombea Mwenza wa urais wa CCM, Dk. Mohamed Gharib Bilal (kulia) akizungumza na Mgombea urais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein, walipokutana uwanja wa Ndege wa Mwalimu Nyerere wa Jijini Dar es Salaam leo mchana wakati Dk. Shein, akiondoka kuelekea Visiwani Zanzibar na Dk. Bilal, akiwasili jijini kutoka Visiwani humo kwa ajili ya kufanya mkutano wa kampeni leo Okt 27. Kushoto ni mke wa Dk. Shein, Mama Mwanamwema Shein, akizungumza na mke wa Dk. Gharib Bilal, Zakia Bilal.
kwa msaada wa blog jirani

UBA Enhances Trade, Payments, Remittances across Africa; Launches AfriCash and AfriTrade

Trade and commerce in Africa has received a major boost with the introduction of two trade related products; AfriCash and Afritrade by United Bank for Africa (UBA) Tanzania Limited. These unique products have been designed by UBA to facilitate trade transactions across the continent.

The two products which were launched in Dar es Salaam on Wednesday October 27, 2010 will leverage on the

growing continental presence of UBA, currently in nineteen African countries.

While launching the products in Dar es Salaam, Managing Director /CEO for United Bank for Africa (UBA) Tanzania Limited, Mr. Ayobola Abiola said that the products were conceived to ease the stress associated with business transactions and payment processes across borders within Africa.

Abiola said the Afritrade product is designed to give customers convenience in payments to third party in any part of the continent. According to him, “Customers of Afritrade are required to apply for trade transaction at any UBA business office with necessary documents while the initiating UBA location advises the benefiting UBA location in the country of the beneficiary and on receipt of transaction message, beneficiary is notified immediately via phone/e-mail and official written notification is sent within 24hours enclosing original copy of the transaction instrument where applicable, and goods are shipped (or services rendered) by beneficiary.

Documents are presented by beneficiary and examined by UBA staff for regulatory compliance. Claim for value of documents is sent to initiating UBA location and documents sent by courier. Payment is made to beneficiary within 24hours of submission of compliant claim.”

He listed benefits of the Afritrade to the customer to include; significant cost savings to the customer as it provides lower charges than normal local tariff for trade transactions, Real-Time trade payments into accounts within East African Community (EAC), Union Economique et Monétaire Ouest Africaine (UEMOA) and Central African Economic and Monetary Community (CEMAC) regions, faster resolution of discrepancies, same Day completion of Intra-African Transactions by leveraging on our business offices across Africa and not international correspondent banks among others.

In addition, he noted that the previously introduced ‘AfriCash’ has been repositioned to target financial remittances from individuals and groups within Africa which have increased dramatically over the past decade. He emphasized that the UBA AfriCash is available in all the 19 countries where the bank has presence including, Kenya, Ghana, Sierra Leone, Cote d’Ivoire, Liberia, Cameroon, Uganda, Chad, Burkina Faso, Senegal, Benin, Gabon, Guinea, Nigeria, Zambia, Tanzania, Mozambique, Congo Brazzaville, Democratic Republic of Congo and still counting.

The bank’s Chairman – Board of Directors, Gen Robert Mboma in his remark noted that the introduction of the new products is premised on the value proposition by UBA as it consolidates its operations in the continent. “Our continent is full of potentials and intra-country trade within the continent will see the potentials translating into growth and development, and that is exactly what these products bring to African trade and commerce,” said Mboma.

United Bank for Africa Plc is one of Africa’s leading financial institutions offering universal banking services to more than 7.5 million customer accounts from over 850 branches across Africa.

With presence in New York, London, and Paris as well as other major financial hubs, UBA combines strong local knowledge of Africa and global expertise to connect people and businesses across Africa and the world through retail and corporate banking, innovative cross-border payments, trade finance and investment banking making it the bank of choice for Africans and African-related businesses globally.

Mh. Kikwete Aunguruma Geita


Mheshimiwa Jakaya Kikwete akiwasalimia wananchi wa Bugando alipowasili kwenye mkutano wa kampeni Nkome Wilayani Geita leo.
Mheshimiwa Kikwete akisalimiana na maelfu ya wananchi waliojitokeza kwenye mapokezi Nkome leo
Mgombea urais wa Tanzania kupitia CCM, Jakaya Kikwete, akipokea bendera ya CHADEMA, kutoka kwa mwenyekiti wa Wanawake wa chama hicho jimbo la Kwimba, Monika Jimotoli mara baada ya kutangaza kukihama chama hicho kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika jimboni humo. Monika amehama chama hicho na wenzake 18.
Maelfu ya wananchi wa Nkome wakimshangilia mgombea urais Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete alipokuwa anahutubia mkutano mkubwa wa kampeni leo Nkome.

**** **** **** ****

Mgombea urais kwa tiketi ya CCM,Mheshimiwa Jakaya Kikwete amewasihi wananchi wa Sumve leo kuchagua CCM kwani hakuna Chama kama CCM kwa ubora wa sera, utekelezaji wa sera na mipango na jitihada za kuleta maendeleo kwa watanzania.

Japo Tanzania bado ni nchi maskini, alieleza Tanzania ya mwaka 1961 na ya sasa sio sawa. “Lakini cha msingi ni kwamba yale tuliyoyaahidi tutayafanya, tumeyatekeleza” alieleza Mgombea Urais wa CCM, Mheshimiwa Kikwete kwenye mkutano huo wa kampeni.

Kwa upande wa elimu, Mheshimiwa Kikwete alisema serikali ya CCM imekabiliana na changamoto kuu nne zilizojitokeza baada ya upanuzi mkubwa wa elimu nchi nzima.

Changamoto zilizopatiwa ufumbuzi ni ile ya upungufu wa walimu ambapo kila kata kuanzia mwakani itapata walimu wa tano. Changamoto ya nyumba za walimu zitajengwa za kutosha kwa sababu bajeti ya elimu imeongezwa mara tatu zaidi kukabiliana na tatizo hilo.

Na tatu ni changamoto ya vitabu vya sekondari ambapo Mheshimiwa Kikwete alieleza mipango imefanywa kushirikiana na Serikali ya Marekani ambapo wamesaidia kuchapisha vitabu vya sayansi vya sekondari. “Kwa hivyo kuanzia mwakani, watoto wetu wa masomo ya sayansi watakuwa na vitabu vya kutosha kwenye shule zote nchi nzima” alieleza Mheshimiwa Kikwete.

Kwa upande wa huduma ya afya, Mheshimiwa Kikwete alieleza mikakati ya serikali ya CCM kupambana na maradhi makubwa kama Malaria, UKIMWI na kansa ya shingo ya kizazi kwa wanawake. Kwa kansa ya shingo ya uzazi, Mheshimiwa Kikwete alieleza kwamba kuanzia mwakani wanawake wote wenye umri wa kupata chanjo hiyo watachanjwa bure ili kukabiliana na gonjwa hilo sugu nchini.

Kwenye mikutano hiyo miwili pia Mheshimiwa Kikwete alieleza kuwa CCM iliahidi kuboresha utoaji huduma ya maji ili kufikia asilimia 60 vijijini na asilimia 90 mijini. Mheshimiwa Kikwete alieleza kwenye wilaya ya Kwimba, utoaji huduma ya maji kwa sasa umefikia asilimia 55.5, na bado jitihada madhubuti zinaendelea kuboresha hali hiyo.

Mheshimiwa Kikwete alieleza kuwa kwa msaada wa marafiki wa Tanzania wa maendeleo, vijiji kumi na mbili vya wilaya ya Kwimba vitapatiwa huduma ya maji kwenye mpango mkubwa wa usambazaji wa maji nchini unaodhaminiwa na benki ya dunia.

Kwa upande wa kilimo, Mheshimiwa Kikwete alielezea mpango mkubwa wa kilimo kwanza ambao unalenga kwenye kuboresha mambo makuu manane ambapo yatamsaidia mkulima kupata faida kwa kilimo chenye tija ikiwemo upatikanaji wa ruzuku na utafutaji masoko kwa ajili ya mazao ya wakulima.

Mheshimiwa Kikwete alieleza wakazi wa wilaya hii pia kwamba ilani ya CCM kwa mwaka 2010 – 2015 inaelekeza kipaumbele kwenye uvuvi wa samaki na kuendeleza sekta hiyo muhimu kwa maendeleo ya wakulima.

Na kwenye mkutano wa kampeni huko Ngudu, aliyekuwa Mwenyekiti wa wanawake Chadema Wilayani Kwimba Mama Monica Jimotolo, amerudisha kadi ya chama hicho na kuingia rasmi CCM.

Mama Jimotolo alieleza sababu kuu iliyomfanya kuingia CCM ni kuchoshwa kwake na siasa za chuki na uchochezi ambazo zinalenga kuvunja amani na mshikamano wa nchi yetu.

Alieleza hadhara hiyo kuwa baada ya kufanya uamuzi huo, wengine kumi na saba wameongozana naye na kusema chama hicho kimekufa wilayani hapo. Wanachama hao walikaribishwa na Mwenyekiti wa CCM taifa na kupewa kadi za Chama Cha Mapinduzi.

Mheshimiwa Kikwete aliwanadi wagombea udiwani na ubunge wa Chama Cha Mapinduzi. Aliwasihi wananchi wa Kwimba kupanga jozi iliyokamilika ya CCM ili kuleta maendeleo. Alitoa mfano wa kilimo cha punda na ng’ombe kwa kueleza kuwa unapoamua kulima utumie jozi ya punda au ya ng’ombe, lakini huwezi kuchanganya kwa kulima na ng’ombe na punda kwani punda atakapopiga mluzi, ng’ombe atasimama.

THE DON HIMSELF

Karibuni sana kwenye blog hii ya kijamii iliyosheheni makila kitu kuanzia siasa uchumi afya na burudani kwa ujumla wake.uingiapo kwenye blog hii ni mengi ambayo utapata nafasi ya kukutana nayo,kumbuka mawazo yako ndo hasa yanayojenga na kunifanya niwe na ufanisi zaidi.kariiiiiiibuuuuuuuuuuuu saaaaaaaaaaaaaaanaaaaaaaaaa.(THE DJ HIMSELF-JIWE)

Followers

BLOG ZA MARAFIKI

Search This Blog

ZILIZOPITA

DUNIA MUZIMA