Oct 27, 2010

JAMANI WANASINGIDA MJINI DEWJI HAJAKODI GARI LANGU, MMILIKI….!!!

Na Hillary Shoo,Singida.

HATIMAE sakata la Mgombea Ubunge wa Jimbo la Singida mjini kupitia chama cha CHADEMA, Josephat Isango kudai kuwa mgombea mwenzake wa CCM, Mohammed Dewji amelikodi gari alilokuwa akitumia mgombea huyo kwenye kampeni,limeingia katika sura mpya baada ya mmiliki wa gari hilo kudai kuwa alimnyang’anya kutokana na usumbufu wa malipo na kwenda kinyume na makubaliano.

Akizungumza na gazeti hili nyumbani kwake jana mmiliki wa gari hilo Saidi Madeira alisema kuwa gari hilo lilikodiwa na ofisi ya CCM mkoa wa singida na wala Dwewji hahusiki na hilo.

"Mimi niwe muwazi kwa kweli Dewji sijawahi kuzungumza nae kuhusu suala la gari langu na wala mtu yoyote kutoka katika ofisi yake, mimi gari nimelikodi kwa Katibu wa CCM Mkoa wa Singida baada ya kuona hawa jamaa wa CHADEMA ni wababaishaji katika suala la malipo.

"Awali tulikubaliana kuwa kila siku gari hilo litalipiwa shilingi 20,000 ikiwa ni pamoja na kuwaziwa mafuta na kumlipa dreva lakini nilikaa karibu wiki nzima sijalipwa fedha zangu na mbaya zaidi gari lilikuwea linakwenda hadi Ikungi sehemu ambayo haikuwa katika makubaliano namia." Alisisitiza Madeira na kuongeza.

"Malipo yalivyokuja na kushauriana na familia yangu tukaona tusiwape tena hili gari hawa jamaa wa Chadema maana linakwenda kinyume na makubaliano ndipo alifika Katibu wa CCM mkoa Naomi Kapambala na kulihitaji gari hilo kwa ajili ya shughuli zao za chama.

Alisema baada ya kuafikiana na katibu juu ya utaratibu mzima wa kazi aliamua kuwapa gari hilo aina ya Suzuki Vitara lenye namba za usajili T 663 ASZ na alilipwa fedha zake zote hadi mwisho wa uchaguzi mkuu kwisha Oktoba 31 mwaka huu.

Aidha Madeira alisema hivi sasa gari hilo liko chini ya ofisi ya CCM mkoa na wala halipo kwenye kampeni za Dewji kama inavyodaiwa na watu.

"Mimi sijawahi kuzungumza na mwandishi wa habari juu ya hili gari zaidi yako leo wewe unayenihoji, nashangaa sana kuasikia kuwa mimi nimezunguza na vyombo vya habari hii sio kweli uhandishi wa namna hii ni wa kunichonganisha mimi pamoja na familia yangu kwa ujumla."Alisisitiza.

Hata hivyo Madeira amesema kuwa anandaa utaratibu wa kisheria ili aweze kmfikisha mwandishi wa habari aliyeandika habari hiyo mahakamani ili aweze kuthibitisha madai hayo, kuwa Dewji alikodi gari hilo.

Kwa upande wake Dewji alisema anasikitishwa sana na taarifa hizo na kwamba hajawahi kukodi gari la mtu yoyote binafsi kwa ajili ya shughuli zake za kampeni.

"Mimi nina magari yangu matatu ambayo ndiyo nayatumia katika kampeni sasa nikodi gari jingine la nini, siwajawahi kufanya hivyo na wala sina haja ya magari mengine haya niliyonayo yananitosheleza kufika kila eneo na kuzungumza na wapiga kura wangu." Alisema Dewji kwa masikitiko makubwa.

Hata hivyo Dewji aliwataka wananchi pamaoja na wanachama wa CCM hivi sasa kuwa watulivu na kuachana na siasa za kuchafuana na badala yake wasubiri siku ya kupiga kura ili wamalize kazi.

Katibu wa CCM mkoa wa singida Naomi Kapambala amesema kuwa gari hilo wamelikodi wao kwa ajli ya shughuli za chama na wala Dewji hahusiki kwa lolote.

"Sisi ndio tumelikodi hili gari, Dewji hahusiki kabisa,yeye ana magari yake anayotumia katika kampeni zake, sasa hili la nini tena kwake alihoji Kapambala."Alisema

No comments:

THE DON HIMSELF

Karibuni sana kwenye blog hii ya kijamii iliyosheheni makila kitu kuanzia siasa uchumi afya na burudani kwa ujumla wake.uingiapo kwenye blog hii ni mengi ambayo utapata nafasi ya kukutana nayo,kumbuka mawazo yako ndo hasa yanayojenga na kunifanya niwe na ufanisi zaidi.kariiiiiiibuuuuuuuuuuuu saaaaaaaaaaaaaaanaaaaaaaaaa.(THE DJ HIMSELF-JIWE)

Followers

BLOG ZA MARAFIKI

Search This Blog

ZILIZOPITA

DUNIA MUZIMA