Mwenyekiti wa Kamati ya Kampeni ya Chama Cha Mapinduzi CCM Bw. Abdurahman Kinana leo ameongea na waandishi wa habari katika ofisi ndogo ya chama hicho Lumumba jijini Dar es salaam na kulaani vikali matamshi ya mgombea ubunge wa jimbo la Temeke kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA Bw. Dickson Ngilly aliyoyatoa kwenye Mkutano wa Kampeni uliofanyika kwenye viwanja vya Mwembeyanga jijini Dar es salaam. Akizungumzia suala hilo Kinana amesema mgombea huyo Dickson Ngilly amezungumza maneno ambayo ni matuzsi kwa mtu yeyote mstaarabu hivyo ,CCM itawaandikia barua Tume ya Uchaguzi ya Taifa na Msajili wa vyamna vya siasa kulalamika kutokana na matamshi ya kashfa ya mgombea huyo aliyoyatoa kuhusu Mgombea wao wa Urais Dr. Jakaya Kikwete, ukizingatia kwamba Mkutano ulikuwa ni wa Mgombea Urais wa CHADEMA na alikuwepo kwenye mkutano huo lakini hakumkanya wala kumzuia kutokana na matamshi yake hayo.
Wakati huohuo Abdurahman Kinana amesema Mgombea wa Urais kupitia CCM Dr. Jakaya Kikwete atakuwa na mahojiano na vyombo mbalimbali vya habari keshokutwa Oktoba 30 kwenye ukumbi wa Anatouglo jijini Dar es salaam ambapo vyombo vya habari vitaalikwa na kumuuliza maswali mbalimbali ya moja kwa moja kutoka katika ukumbi huo. kipindi hicho kitaanza saa mbili usiku mpaka saa nne usiku.
No comments:
Post a Comment