Jun 18, 2010

UFARANSA KIMEO CHALI WC



HALI imeendelea kuwa mbaya kwa vigogo wa soka duniani baada ya Ufaransa kupokea kipigo cha mabao 2-0 kutoka kwa Mexico, huku kiungo wa Nigeria, Sani Kaita akiomba msahama kwa mashabiki kwa kitendo chake kilichoighalimu timu yake kufungwa 2-1 na Ugiriki.

Hakuna aliyeamini kilichokuwa kinatokea kwenye Uwanja wa Polokwane ambako kulishudia miamba mabingwa wa Dunia 1998 wakiendeshwa mchamchaka na vijana wa Mexico walionekana kujipanga na kufanya watakalo katika dakika zote tisini.

Mexico iliyotawala mchezo huo iliandika bao lake la kwanza dakika 63, kupitia kwa Javier Hernandez aliyevunja mtego wa kuotea uliowekwa na mabeki wa Ufaransa waliokosa ushirikiano katika muda wote wa mchezo huo.

Beki Erick Abidal alimwangusha Pablo Barrera kwenye eneo la hatari na ambayo mwamuzi kutoka Saudi Arabia aliamuru penalti iliyofungwa na Cuauhtemoc Blanco dakika ya 78 na kumaliza kabisa matumaini ya Ufaransa ya kupata sare kwenye mchezo huo.

Kwa matokeo hayo sasa Ufaransa imeungana na wenyeji Afrika Kusini kujiandaa na safari za kuaga mashindano hayo mapema, kwani watalazimika kuomba Mexico na Uruguay zitoke sare ili zifungwe ili iweze kufuzu.

Kiungo wa Nigeria, Kaita ameomba msamaha kwa watu wote barani Afrika kwa kitendo chake kilichosababisha kupewa kadi nyekundu iliyowasaidia Ugiriki kupata ushindi wa mabao 2-1 kwenye mchezo wa Kundi B uliochezwa Uwanja wa Free State jana.

"Naomba msamaha kwa kila moja. Watu wa Nigeria, viongozi na wachezaji wenzangu," alisema kiungo huyo mwenye miaka 24 mbele ya wanahabari baada ya kutolewa kwa kitendo chake kutaka kumkanyaga mchezaji mwenzake.

Huku Super Eagles wakiwa wanaongoza kwa bao 1-0 lililofungwa kwa mpira wa adhabu ya Kalu Uche walionekana kutawala mchezo hadi pale Kaita alipofanya kitendo cha kipuuzi cha kumkanyaga Vassilis Torosidis dakika ya 33 na kutolewa nje kwa kadi nyekundu.

Kiungo huyo anayecheza soka yake nchini Russia aliondoka uwanjani hapo akiwa amejifunika uso wake kwa jezi, na kufanya mchezo huo kubadilika kabisa na Ugiriki kutawala zaidi.

Dakika 11 baadaye Ugiriki walisawazisha kupitia kwa Dimitris Salpingidis na kuipa nchi yake bao la kwanza katika historia yao ya Kombe la Dunia na walifanikiwa kupata bao la pili zikiwa zimebaki dakika 20 lililofungwa na Torosidis.

"Nakubali na uamuzi wa kupewa kadi nyekundu, nimeuzunika kwa kitendo changu, natumaini Argentina itaweza kutusaidia," aliongeza Kaita ambaye atakosa mechi ya mwisho ya kundi hilo.

Ushindi wa Ugiriki umewafanya kufikisha pointi tatu sawa na Korea Kusini, ambayo imefungwa kwa mabao 4-1 na Argentina mapema jana, huku Nigeria ikishikiria mkia bila ya pointi baada ya mechi mbili.

Nigeria, moja ya nchi zilizotegemewa na Afrika kufanya vizuri kwenye fainali hizo, sasa watalazimika kushindi dhidi Korea Kusini hapo Juni 22 mjini Durban na kuomba Ugiriki ifungwe na Argentina mjini Polokwane ili waweze kufuzu kwa hatua ya pili.

Lakini hali hiyo imeonekana kutomshitua mkongwe Nwankwo Kanu ambaye anaamini bado nchi yake ina nafasi ya kusonga mbele.

"Kama ukiangalia jinsi kundi lilivyo uwezi kuwa na wasiwasi sana, lakini tunachotakiwa kwetu ni kushinda," alisema.

"Hatuwezi kwenda tukiwaza sare, tunachotakiwa ni kushinda na kuomba kwa dua zote Argentina ikiendeleze makali yake kwa kuifunga Ugiriki."

Jun 16, 2010

DIAMOND AZURU SENEGAL AS BALOZI WA MARALIA NCHINI

Msanii Diamond hapa akiwa jijini Senegal alipokwenda kukutana na Youssou N Dou akiwa kama balozi wa Malaria kutokea Tanzania.


Mkurugenzi wa Malaria kutoka USA, Diamond na Dokta mkuu kutoka Senegal


Wadau wa Malaria kutoka nchi mbalimbali wakiwa kwenye hospital kuu ya Senegal


Ruge, Mdau wa Malaria kutoka USA pamoja na Diamond


Mtu mzima akiwa amejipumzisha kabla ya kwenda kwenye show iliyoandaliwa na Youssou N Dou


Diouf akiongea maneno yake machache kabla yakumkaribisha Diamond aje kuimba




Diamond alivyopokelewa kwa shangwe nyingi na wakazi wa Senegal



Diamond akiwa na wadau mbalimbali wakitizama kinachoendelea ukumbini





Mtoto wa Mbagala akipewa nafasi ya kupoteza huwa ni soo aisee utasema ameahidiwa ikulu maana makamuzi yake yanakuwa si ya kitoto arifu.big up sana bro


Buba Dou ni mdogo wa Youssou N Dou, katika ni Diamond pamoja na Youssou mwenyewe


Diamond akifundwa na mkongwe ama nguli la muziki toka hapa afrika Youssou N Dou



Shangwe zilikuwa zikiendelea baada ya Diamond kuimba wimbo wa Nenda kamwambie


Hiyo alama ya X ambayo unaona watu wameweka ni alama yakutokomeza Malaria kwa kule Senegal kama ilivyo huku tunasema ZINDUKA kule wao wanasema XEEX SIBBIRU.

Diamond akicheza na watoto huku akielekea kwenye usafiri alioandaliwa wa kumrudisha kwa hotel aliyofikia huko nchini segal

Diamond akiwa ndani ya gari tayari kwa safari yakumrudisha kwa hotel

Jun 13, 2010

KHALID CLIP

TIMU YA MLIMANI TV KAZINI

kijana wa bongo bullet akijiandaa kugonga show la ukweli linalohusiana na mabongo flava hapa yuko teyari kuaza kurekodiwa baada ya kujipaka mapouda ya kutosha though alikuwa akikimbia kila nilipotaka kumgonga picha alitoka mita mbaaaaaaaaaaya.

standby
action
oya ngoja kwanza mugisha mama watoto ananisumbua bana
poa ngoja na mimi niweke poa mic yangu nisije nikakushuti kibubu
daah hizi kazi mwenyewe maxmillian john ngobe mi nazingua tu.
shost akiwa busy kuandaa makala ya radio inayohusu sanaa na muziki
jiwe nini sasa wakati mi nimejificha we unanifata mpaka kwenye ofisi yangu tena bila taarifa mh?ngoja nakusemea umeiba min div.
hatimaye nikamfuma akitupia mapouda kabla ya kugonga makipindi nami nikaitukia vema simu yangu ya mkononi kuweka mambo sawa.
jamaa anajulikana kama KHALID ALLY aka TOZ aka MUUZA NYAGO aka BROTHERMAN aka MAJINA kibao akila kona baada ya kushitukia kuwa nilikuwa namphotoa aisee.


mita mia nisimpige picha chalii angu.
muuza nyago mwengine wa mlimani tv jamaa anajulikana kama SUFIAN akiwa anajichabo baada ya kujipigilia mapouda ya kutosha teyari kuelekea kwenye kurekodi kipindi cha MUZIKI NA MAISHA maeneo ya ubungo na kwa taarifa ambazo nilizipata jamaa alikuwa anakwenda kupiga pindi na AT





SAJNA'S CLIP


hii ni sehemu ya clip ya mahojiano ya sajna na khalid katika studio za mlimani tv,msikie mtoto alivyojaaliwa vocally aisee.KAZA BUTI MZAZI UITOE MWANZA KWA MARA NYINGINE SI UNAJUA HUKO NDO HOME MH?KOMAA BAAAAAAABU

SAJNA ATIMBA STUDIO ZA MLIMANI TV

Ilikuwa ni mida ya saa tano asubuhi ya leo ambapo presenter wa kipindi cha BONGO BULLETS cha mlimani tv ''elimu kwanza''alipokuwa akijiandaa kufanya kipindi chake cha jumanne ya wiki ijayo nikiwa na maana siku baada ya kesho.ambapo hii leo aliweza kufanya interview na wakali wa KVC pamoja na mkali ambaye kwa sasa anaisumbua saaaaana tansinia ya muziki huu wa kizazi kipya kwa hapa nyumbani tanzania,hapa namzungumzia jamaa ambaye ngoma yake ya IVETA imekuwa gumzo kila kona ya mtaa ingawa makazi yake ni kule mwanza lakini hata shinyanga,bukoba,mtwara na hata hapa dar es salaam ngoma hiyo inakamata mbaaaaaaaaaaaaaya.sina shaka ushanifahamu namzungumzia SAJNA.
kijana ambaye bado angali shuleni akiendeleza libeneke la elimu huku akijihusisha na muziki kama hobbie na si kazi mpaka pale atakapo maliza elimu yake ndo atautolea macho muziki huu wa kizazi kipya.SAJNA aliweka wazi kuwa kwa sasa anajipanga poa na wapenzi wa muziki wake wakae mkao wa tayari kupokea albam iliyosheheni jumla ya pini kumi za maana .
Gisha banyi na Khalid ally
Sajna akiwa na mtayarishaji wa kipindi cha BONGO BULLETS Khalid ally
sajna&khalid wakiwa kwenye studio za mlimani tv
sajna akifafanua jambo
akiwa teyari kutoa kasong ka IVETA
Mzuka ndo umepanda mbaaaaaaaaaaaaya
oyaaaaa niko tayari kwa hayo mainterview.

Jun 12, 2010

POLE KAKA MKUBWA KWA KUWA GONJWA

Nilipotembelea blog yake asubuhi ya leo ndo nikakutana na maneno haya hapa chini
''Ndugu zangu jana usiku nimeng'oa jino so maumivu nayoyapata nimeamua kutulia tu nyumbani, naomba ki mda kidogo nikiwa sawa nitaliendeleza gurudumu hili ndugu zangu, nawatakia weekend njema.
Samahani kwa usumbufu utakao tokea.
NAWAPENDA SANA.
ONE''

pole sana bro mungu atakupa afya njema soon ili uendeleze libeneke la kuwapa watanzania habari.

NAKAAYA ATOSWA SONY



UNAZIKUMBUKA habari za Nakaaya Sumari na mkataba wake wa kufanya kazi na kampuni ya Sony, kwa mujibu wa mwanamuziki huyu mkataba huu haupo tena na kama zamani ameingia vitani kupambana kivyake.

Nakaaya ameandika kupitia mtandao wake kuwa kutokana na sababu zilizo nje ya uwezo wake hatafanya kazi tena na watu hao isipokuwa yeye mwenyewe na kuahidi kuwa atapenya tu kwenye soko la Afrika.

Waswahili wanasema Hasidi hana Sababu, na hii ndivyo ilivyokuwa kwa mwanamuziki huyu, mtu kwa sababu zake binafsi alimua kumuharibia dili hiyo.

"Nimepitia kipindi kigumu kwani dili hiyo ilikuwa ni faraja kwa nchi yangu, familia yangu na kwangu mwenyewe, lakini imekweihatokea na hakuna anayeweza kubadilia matokeo,

Namshukuru mungu kwa kuwa na marafiki wazuri ambao walikuwa nami siku zote, Valerie Kimani na Dunga ni kati ya marafiki walionipa moyo na kunirudisha kwenye mstari,

Hivi sasa mimi ni 'Warrior' maumivu niliyoyapata yameniamsha na kunirudisha kwenye ari yangu ya zamani" aliandika Nakaaya. Tembelea humu nakaaya.blogspot.com kupata undani zaidi wa sakata hili.

KUELEKEA UCHAGUZI MKUU 2010



WANAHARAKATI wa mashirika yasiyo ya kiserikali wametoa mapendekezo ambayo wanataka yatekelezwe na vyama vya siasa vinavyogombea kuingia madarakani katika Uchaguzi Mkuu ujao wa Oktoba mwaka huu.

Hivi karibuni, Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) kwa kushirikiana na mashirika yanayotetea Haki za Binadamu, Jinsia na Ukombozi wa Wanawake Kimapinduzi (FemAct) ulizindua Ilani ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010.

Ilani hiyo imetathmini utendaji wa serikali iliyoko madarakani kwa kipindi cha miaka mitano na kuweka mapendekezo mengineyo.
Katika tathmini ya Ilani ya mwaka 2005 mambo kadhaa yameainishwa kama kipimo cha utekelezaji uliofanywa na Serikali ya Awamu ya Nne.

Ilani hiyo inadai kuwepo kwa jitihada za kukuza uchumi kwa mtazamo wa haki sawa, kuondoa matabaka yanayojitokeza, kupambana na mifumo kandamizi na ubaguzi hususan ule wa kijinsia na kuwepo kwa mipango madhubuti ya kuhakikisha kwamba wanawake wapiga kura wanashiriki katika kuzalisha mali na maamuzi muhimu ya maendeleo ya taifa lao pamoja na kunufaika na matunda ya jasho lao.

Katika tathmini hiyo wanaharakati wamesifia kukua kwa uchumi, lakini wamelaumu utegemezi wa wahisani uliosababisha kukua huko kutodumu:

“Katika kipindi hiki cha miaka mitano, tulishuhudia kukua kwa uchumi kama ilivyotarajiwa katika Mkukuta. Kwa mfano, kwa kutumia kigezo cha Pato la Taifa (GDP) kulikuwa na ongezeko la Pato la Taifa kutoka asuilimia 6.7 mwaka 2004 hadi kufikia asilimia 7.4 mwaka 2008. Hata hivyo, sura ya matokeo ya mfumo tegemezi wa uchumi wetu na jinsi tulivyomezwa na mfumo wa utandawazi.”

Ilani hiyo pia inamulika umasikini uliokithiri licha ya kukua kwa Pato la Taifa. Kwa mfano, asilimia ya watu walio masikini kupindukia ilipungua kidogo tu, kutoka asilimia 35.7 mwaka 2004 hadi asilimia 33.2 mwaka 2007. Takwimu zinaonyesha kuwa, idadi halisi ya Watanzania walio masikini kupindukia iliongezeka kutoka asilimia 11.4 mwaka 2001 hadi kufikia asilimia 12.9 mwaka 2007.

Kuhusu suala la ajira, Ilani hiyo imeonyesha kuwa idadi ya Watanzania walioajiriwa na kujiajiri imeongezeka. Inasema kuwa takriban asilimia 87 ya Watanzania wenye umri wa miaka 15 na zaidi wameajiriwa na asilimia mbili ya kundi hili haina ajira. Hii ni pamoja na asilimia 90.5 ya wanaume na 88.9 ya wanawake.

Nini basi chanzo cha umasikini wa kupindukia kama Watanzania walio wengi wana ajira? Ilani hiyo inabainisha kuwa asilimia 67.2 ya ajira zote ni zile za kujiajiri wenyewe ama kwenye mashamba madogo au katika sekta isiyo rasmi.

“Wengi walioajiriwa au kujiajiri kwenye mashamba au sekta isiyo rasmi wanaishi maisha magumu yasiyo na kipato cha uhakika na kisichotosha. Wengine hasa wanawake, vijana na watoto hawalipwi mshahara wowote kwa kazi au huduma wanayotoa,” wanasema wanaharakati katika ilani yao.

Kwa upande mwingine ilani hiyo inabainisha kuwa sekta rasmi nchini inaajiri asilimia 10 tu ya Watanzania huku wakilipwa mishahara midogo isiyokidhi mahitaji ya msingi ya wafanyakazi. Hiyo nayo ni sababu nyingine inayotajwa kama chanzo cha umasikini uliopindukia.

Licha ya umasikini, ilani hiyo inabainisha kuwepo kwa ongezeko la matabaka. Utafiti unaonyesha kuwa wanaume wana mishahara mikubwa kuliko wanawake. Kwa mfano, utafiti wa Baraza la Taifa la Takwimu mwaka 2006, unaonyesha kuwa, mshahara wa mwanamume mwenye miaka 15 na kuendelea, ulikuwa ni Sh50,000 kulinganisha na Sh32,000 za mwanamke katika umri huo huo.

Aidha matabaka pia yanajitokeza kwenye suala la elimu. Wasio na elimu wanalipwa mishahara midogo. Ilani hiyo imetoa mfano wa pato la mfanyakazi mwenye elimu ya sekondari na zaidi kuwa ni Sh207,433 kulinganisha na Sh40,134 kwa wale ambao hawakwenda shule. Kwa wale waliojiajiri pato lao ni Sh129,494 kwa wenye elimu ya sekondari huku wasio na elimu wakiambulia Sh 48,920.

Katika sera ya uwekezaji, ilani hiyo inaonyesha jinsi serikali ilivyojikita katika kugawa rasilimali za Taifa kwa wageni bila kujali wazawa... “Katika kipindi cha miaka 10, sehemu kubwa ya ardhi ya nchi yetu imechukuliwa na wawekezaji, wengi wao ni makampuni makubwa ya nje. Si ardhi tu, bali pia maji, madini, misitu, wanyama pori na samaki."

“Wananchi walio wengi wamehamishwa kutoka makao yao kwa nguvu, wanakosa nafasi kwa uzalishaji katika kilimo, ufugaji na uvuvi na wengine wanapambana na maradhi yanayotokana na uchumi za makampuni.”

Ilani mpya
Katika kutoa madai mapya, Ilani ya mwaka 2010 imekuja na madai mapya ikiyaweka katika makundi tofauti yaani serikali, vyama vya siasa, wagombea na asasi za kiraia.

Kwa upande wa serikali, Ilani hiyo imeitaka kusimamia kwa uadilifu matumizi ya rasilimali za taifa letu, ili zitumike kwa manufaa ya Watanzania wote. Vilevile, serikali inapaswa kusimamia utawala bora na uwajibikaji kwa mtazamo wa kijinsia.

Katika masuala ya uchaguzi, serikali imetakiwa kudhibiti matumizi ya mabaya ya fedha za uchaguzi na kuhakikisha fedha zote za umma zitakazotumika katika uchaguzi zinawafikia wanawake kama wapiga kura na wagombea nafasi mbalimbali za uongozi.

Ilani hiyo pia imeitaka serikali kutenga kipindi maalumu kwa wagombea wote kwenye vyombo vya habari vinavyomilikiwa na serikali kwa ajili ya kampeni. Serikali pia imetakiwa kusimamia taratibu za kupiga kura ili kuhakikisha kuwa taratibu hizo haziathiri makundi maalumu.

“Ukomo wa wanasiasa kukaa madarakani uwe ni awamu mbili tu. Isitoshe, wanasiasa wasiwe na vyeo zaidi ya kimoja. Kwa mfano, mkuu wa mkoa, waziri, mbunge na wengineo ili kuepusha mgongano wa kimaslahi katika utekelezaji wa majukumu yao.”

Kwa upande wa vyama vya siasa, ilani hiyo imebainisha kuwa ni mhimili mkuu wa demokrasia shirikishi na ya ushindani inasema ni lango kuu la kuingia katika kinyang’anyiro cha uchaguzi na hatimaye katika nafasi muhimu za uongozi wa taifa.

Hata hivyo, wanaharakati katika Ilani hiyo wanasikitishwa na jinsi mfumo dume unavyotumika katika vyama vya siasa... “Vyama vimewatumia wanawake na baadhi ya vijana kama wapiga debe, wahamasishaji na wasindikizaji katika mchakato wa uchaguzi. Wanawake wengi wanaposimama kama wagombea vyama vinawatupa na kuwaweka pembezoni.”

Ilani hiyo inavilaumu vyama vingi kwa kushindwa kuleta usawa wa kijinsia badala yake vimezidi kuimarisha utamaduni wa ubaguzi dhidi ya wanawake.

“Tunadai vyama vya siasa viache kuwarubuni wanawake kwa kutumia ‘Viti maalumu’ ambavyo hatima yake ni kuwapa wachache waliovipigia debe fursa ya kuchaguzliwa na kuingia katika vyombo vya uwakilishi wa maamuzi katika ngazi duni.”

Kwa upande wa wagombea, wanaharakati wanawataka kutotumia nguvu ya fedha kununua kura bali watumie busara na nguvu ya hoja kushawishi wapiga kura.

Wagombea pia wasitumie lugha za matusi au ubabe wa kudhalilisha wanawake na wasirubuni wananchi kwa kuwaahidi ahadi zisizotekelezeka... “Kiongozi kama huyo ni sumu kwa taifa letu, ni sumu kwa demokrasia na ni sumu kwa makundi ya wanawake na wanaume yanayotaabika kutokana na rasilimali za taifa kutowafikia.”

Kwa upande wa asasi za kiraia, Ilani hiyo inazitaka asasi hizo kuwatetea wanawake kwa kuwahamasisha kugombea nafasi za uongozi na kukataa kuburuzwa kama wapiga debe au kurubuniwa kwa kupewa ‘nafasi za upendeleo’.

PATASHIKA LA KOMBE LA DUNIA LAANZA RASMI NA KUSHUHUDIA DROO MBILI


Baada ya miaka,miezi,wiki na siku hatimaye yamebaki masaa machache tu kabla filimbi ya kwanza kupulizwa kuashiria kuanza kwa kivumbi cha kuwania ubingwa wa dunia wa soka.Ni wakati wa World Cup 2010.Kwa mara ya kwanza kabisa kindumbwendubwe hicho kipo barani mwetu,Afrika.

Wataalamu na watabiri mbalimbali wa soka wameshaanza kazi zao.Wacheza kamari nao hawapo nyuma.Kuna kulia na kucheka.Mfalme wa soka ulimwenguni,Pele,ametoa utabiri wake.Anasema anaziona Brazil na Spain zikiumana katika fainali.Lakini anasema pia angependa sana kuona timu ya Afrika ikifika fainali.

Mchezo wa fungua dimba hapo baadaye ni kati ya wenyeji Afrika Kusini na Mexico(South Africa Vs Mexico).Historia inaonyesha kwamba hakuna timu wenyeji iliyowahi kupoteza au kufungwa katika mchezo wa fungua dimba.Je South Africa wataendeleza historia hiyo?

Mchezo wa kesho unafanyikia katika uwanja ujulikanao kama Soccer City(pichani) uliopo jijini Johannesburg.Ulianza kujengwa mwaka 1986 na kufunguliwa rasmi mwaka 1987 na una uwezo wa kuchukua watu 94,000 ukitoa watu wa habari na VIP.Uwanja huo upo maeneo ya Soweto(chanzo cha jina ni South West Town.Ni uwanja wenye historia kemkem.Hapo ndipo utakapofanyika pia mchezo wa fainali tarehe 11 Julai.

Wakati homa ya Kombe la Dunia ikiwa ndio inazidi kupaa,ulimwengu unasubiri kwa hamu kitu kimoja.Je,Rais mstaafu wa nchi hiyo,Nelson Mandela “Madiba”,ataweza kuhudhuria japo mchezo huu wa ufunguzi?Mimi binafsi ningefurahi sana kumuona Mzee huyo akihudhuria japo mchezo huo wa ufunguzi kwani mchango wake katika kuzileta fainali hizo barani Afrika ni mkubwa sana.Bila shaka utakumbuka kwamba,alipotoka jela mwaka 1990,hapo hapo katika uwanja wa Soccer City ndipo alipowahutubia watu wake kwa mara ya kwanza baada ya miaka 27.

Baadhi ya wageni wengine maarufu na viongozi wanaotarajiwa kuhudhuria ufunguzi wa fainali hizo ni pamoja na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa,Ban-Ki-Moon, Rais wa Mexico,Felipe Calderon,Makamu wa Rais wa Marekani,Joe Biden, na Mwenyeji wao,Jacob Zuma.Lakini waliotia fora zaidi ni majirani zetu Kenya ambao watawakilishwa na viongozi wao wote wa juu kabisa Rais Mwai Kibaki na Waziri Mkuu Raila Odinga(sijui nchi wamemuachia nani).

Kivutio kingine kinatarajiwa kuwa mwimbaji maarufu wa muziki wa R&B kutoka nchini Marekani,R.Kelly,ambaye anatarajiwa kuimba wimbo wake wa “Sign of Victory” ambao ni anthem maalumu kwa ajili ya ufunguzi wa Kombe la Dunia.Ataimba kwa kushirikiana na Soweto Spiritual Singers. Wasanii wengine wanaotarajiwa kushiriki ufunguzi huo ni pamoja na Hugh Masekela, Femi Kuti na bendi ya Osibisa kutoka nchini Ghana.

Mpira utakaotumika ni Jabulani.Ingawa umelalamikiwa na makipa kadhaa(akiwemo Muharami Mohammed wa Taifa Stars) kwamba haufai na unawapa shida,FIFA wamesisitiza kwamba ndio utakaotumika.Jabulani ni neno la kiZulu linalomaanisha “kuleta furaha kwa kila mtu”.

Ratiba kamili ya Fainali hizi unaweza kuipata kupitia mtandao wa FIFA kwa kubonyeza hapa.Pia jamaa wa SoccerNet.com wana ratiba nzuri zikiwa na masaa ya hapo ulipo(local time).Kama hukufanikiwa kuliona tamasha la ufunguzi (2010 FIFA Official World Cup Kick Off Concert) bonyeza hapa.Jamaa wa Vevo bado wanalionyesha kwa kulirudia kila mara.It is Time For Africa.Viva Africa!!

Baada ya mchezo wa fungua dimba, Ufaransa(mabingwa wa dunia mwaka 1998) watakipiga na Uruguay.

Jun 11, 2010

NAS B AKIWA KWENYE HARAKATI ZA KUGONGA MAWE,KABLA YA KUNITIMBIA KWENYE STUDIO ZA RADIO MLIMANI KUPIGA PINDI.

hapa ndo pa kuingizia vocal aisee.
Si unacheki jamaa ndo kaanza kuproduce full kakiza ndo kama kanaingia mzazi


full busy na kugonga beat ya mkali SERIAL NUMBER aka JIWE4EVER


jamaa akiwa studio akigonga pini balaa

Mkali NAS B aka NAS PRODUCER akiwa ndani ya studio za radio mlimani,jamaa ni mkali wa kugonga mabeat toka enzi OM RECORDS pale kwa OMARY MKALI kisha akasonga pande za LAP RECORDS kabla ua kula shavu pande za PAMOJA RECORDS ambako aliminya kimtindo na kusepa baada ya vifaa vyake vya productio kuibiwa na kwa sasa jamaa yuko pande za IBAM RECORDS masaki ikiendeleza libeneke la kuachia mabeat ya hatari.

(NAS B )
Jana nilipata nafasi ya kuzuru kwenye studio za jamaa pale maeneo ya masaki karibu na hotel ya wachina na hapa nilimkuta akinyonga beat za hatari kiasi akaweza kunizawadia vitu viwili ambavyo mimi binafsi niliridhika navyo ile saaaaaaaaaaaana.unajua alinizawadia gani mh?
jamaa alinizawadia BEAT moja la hip hop pia akanizawadia aka mpya inayokwenda kwa jina la SERIAL NUMBER.So from dis tyme u can call me DJ JIWE4EVER aka SERIAL NUMBER.













Jun 10, 2010

PICO NDANI YA STUDIO ZA MLIMANI RADIO

Anajulikana kama Pico aka Mzee wa Kikongwe ambaye hakika alisumbua sana alipotambulishwa kwa mara ya kwanza kwenye ulimwengu wa muziki wa kizazi kipya na kukonga sana nyoyo za mashabiki wa muziki huo na kiasi ambacho hakika aliweza kuwa juu.

jamaa alipotea tena kwenye gemu la muziki wa kizazi kipya kabla ya hivi karibuni kurejea tena na ngoma kali iliyojaa UDAKU wa kila namna inayojulikana kama GAZETI.Na kwa taarifa nilizozipata toka kwa meneja wake GURU RAMADHANI ni kwamba jamaa atakuwa chini ya yake.

KAKA FEDE NA KATUNI YA LEO


THE DON HIMSELF

Karibuni sana kwenye blog hii ya kijamii iliyosheheni makila kitu kuanzia siasa uchumi afya na burudani kwa ujumla wake.uingiapo kwenye blog hii ni mengi ambayo utapata nafasi ya kukutana nayo,kumbuka mawazo yako ndo hasa yanayojenga na kunifanya niwe na ufanisi zaidi.kariiiiiiibuuuuuuuuuuuu saaaaaaaaaaaaaaanaaaaaaaaaa.(THE DJ HIMSELF-JIWE)

Followers

BLOG ZA MARAFIKI

Search This Blog

ZILIZOPITA

DUNIA MUZIMA