Sep 15, 2010

sugu na wakali kibao kudondosha shoo ya ukweli ndani ya mbeya



Mgombea Ubunge jimbo la Mbeya Mjini kwa tiketi ya Chama cha


Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Joseph Mbilinyi ‘Sugu’, Ijumaa hii ataweka kando gwanda maalum ambalo ni sare ya chama chake, na kulipa kisogo jukwaa la siasa, na atashika kipaza sauti ‘MIC’ na kudondosha shoo kali ya Hip Hop kama ilivyokawaida yake. Sugu, anatarajia kutoa shoo kwa kushirikiana na mastaa wengine wa muziki wa kizazi kipya kwenye Ukumbi wa Mtenda Sunset uliopo Mbeya. Wasanii ambao wametajwa kupanda jukwaa moja na Sugu siku hiyo (Septemba 17) ni Suleiman Msindi ‘Afande Sele’, Ferouz Mrisho Rehani, Abbas Hamis Kinzasa ’20 Percent’, Danny Msimamo, Fred Maliki ‘Mkoloni’, Gerald Mwanjoka ‘G Solo’, Mapacha ‘Maujanja’ na Isanga Family’. Akifafanua kuhusu kupanda jukwaani na kuvua kombati ya CHADEMA, Sugu alisema atafanya hivyo kama sehemu ya harambee ya kukusanya fedha za kumaliza kazi ya kulitwaa Jimbo hilo. “Wala siyo utani kaka, Ijumaa navua gwanda, navaa jeans. Nitakuwa na saa nzima ya kutoa shoo ya muziki kwa watu watakaohudhuria onesho hilo. Nataka niwaoneshe watu wangu wa Mbeya kile ambacho huwa nafanya. “Kuna watu wanasikia tu lakini hawajawahi kuona shughuli yangu jukwaani. Nitawaonesha. Wanakuja wakali kama Ferouz, Afande Sele, 20 Percent, Mkoloni, Msimamo, G Solo, Mapacha, Isanga Familiy na wengineo,” alisema Sugu na kuongeza: “Ni shoo maalum ya kuchangia kampeni. Tumegawa kadi maalum ambapo kuna maeneo zinanunuliwa kama njugu. Kila kadi tunauza shilingi 10,000. Tunapiga hatua kubwa na naamini tutafika kwa sababu tunapata sapoti ya kutosha kutoka kwa watu wangu kama ambavyo unaona wanamuziki wanaacha kazi zao wanakuja kushirikiana na mimi kaka yao kukusanya michango ili kuniwezesha.” Kuhusu maendeleo ya kampeni zake, Sugu alisema kuwa tumaini la ushindi linaongezeka kila siku kiasi ambacho haoni wapi ambapo anaweza kukosea na kutoa nafasi kwa mpinzani wake kupenya. Alisema, juzi alifanya mkutano uliohudhuriwa na maelfu ya wakazi wa Mbeya kwenye Uwanja wa Mbembela uliopo Kata ya Nzovwe, Iyunga na kuvunja rekodi ya mahudhuria ya ule wa uzinduzi wake uliochukua nafasi Uwanja wa Ruanda Nzovwe, Kwamama John. Kuhusu afya ya mshirika wake, Mkoloni aliyelishwa sumu, Sugu alisema: “Kwanza namshukuru Mungu anaendelea vizuri, leo (juzi) alikwenda tena hospitali kuangalia macho. Anaendelea vizuri, pengine waliompa sumu walitaka kummaliza ila yote tunayaacha apone kwanza, muhimu ni kwamba Ijumaa tutakuwa naye hapa kufanya shoo.” HABARI KWA HISANI YA (GPL)

Rais Kikwete katika kampeni Same na Mwanga mkoani Kilimanjaro!!

Chipukizi wa CCM akimkaribisha maua mgombea Urais kwa tiketi ya CCM Dr.Jakaya Mrisho Kikwete wakati alipowasili huko Ndungu,wilayani Same jana mchana na kuwahutubia wananchi katika mkutano wa kampeni. (Picha na Freddy Maro)
Mgombea Urais kwa tiketi ya CCM Dr.Jakaya Kikwete akiwahutubia wanachama wa CCM wakati wa mkutano mkubwa wa kampeni uliofanyika katika uwanja wa michezo mjini Mwanga,Mkoani Kilimanjaro jana jioni(picha na Freddy Maro)
Baadhi ya wananchi wa Ndungu Same wakimsikiliza Mgombea wa Urais kwa tiketi ya CCM Dr.Jakaya Mrisho Kikwete waakti alipohutubia mkutano wa Kampeni.
Mgombea urais kwa tiketi ya CCM Dr.Jakaya Mrisho Kikwete akiwasalimia wakazi wa mji wa Same, Mkoani Kilimanjaro jana jioni.

Mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji ya Baraza la Umoja wa Vijana Taifa, Ridhiwani Kikwete, akivishwa skafu na chipukizi Asha Khalifa alipowasili Kata ya Tingi, Jimbo la Uchaguzi la Kilwa Kusini,wilayani Kilwa, Mkoa wa Lindi kuanza ziara ya kuweka mikakati ya ushindi wa kimbunga wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika Uchaguzi Mkuu Oktoba 31, mwaka huu. (PICHA NA RICHARD MWAIKENDA)
Mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji ya Baraza la Umoja wa Vijana Taifa, Ridhiwani Kikwete, akisalimiana na Mwenyekiti wa UVCCM, Kata ya Njinjo, Hemed Kipembekile alipowasili Kata ya Tingi, Jimbo la Uchaguzi la Kilwa Kusini,wilayani Kilwa, Mkoa wa Lindi kuanza ziara ya kuweka mikakati ya ushindi wa kimbunga wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika Uchaguzi Mkuu Oktoba 31, mwaka huu. (PICHA NA RICHARD MWAIKENDA)
Mwenyekiti wa Wenyeviti wa Chama Cha Mapiduzi Tanzania Bara na Visiwani, Profesa wa Siasa Mtopa Ali Mtopa akitoa nasaha zake katika mkutano wa ndani wa viongozi wa UVCCM, Wilaya Kilwa, uliohutubiwa na Mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji ya Baraza la UVCCM Taifa, Ridhiwani Kikwete (katikati), mjini Kilwa Masoko,juzi. Ridhiwani na makada wengine wa UVCCM wameanza ziara ya kuhamasisisha vijana kuhakikisha chama hicho kinapata ushindi mkubwa katika uchaguzi Mkubwa. Kulia ni Mwenyekiti wa UVCCM,Mkoa wa Lindi Hassan Masala.
Mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji ya Baraza la Umoja wa Vijana Taifa, Ridhiwani Kikwete, akihutubia katika mkutano Kata ya Tingi, Jimbo la Uchaguzi la Kilwa Kusini,wilayani Kilwa, Mkoa wa Lindi kuanza ziara ya kuweka mikakati ya ushindi wa kimbunga wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika Uchaguzi Mkuu Oktoba 31, mwaka huu. (PICHA NA RICHARD MWAIKENDA)

Dr. Kikwete anguruma Bumbuli


Mgombea Urais kwa tikiti ya CCM,Dr. Jakaya Kikwete akipokelewa kwa shangwe na umati mkubwa wa watu na wapenzi wa CCM wa jimbo la Bumbuli wilani Lushoto Jumatatu jioni katika uwanja wa mkutano wa Togotwe, Bumbuli.
Mgombea ubunge jimbo la Bumbuli, January Makamba
akimwaga sera baada ya kunadiwa na Mgombea urais kwa tiketi ya CCM,Dr. Jakaya Kikwete kwenye mkutano huo
Wana Bumbuli mkutanoni

Sep 13, 2010

BASATA YAJA JUU UVAAjI NUSU UCHI WA WANENGUAJI


Katibu Mtendaji wa BASATA,Ghonche Materego (kushoto) akisisitiza jambo kuhusu sanaa ya unenguaji nchini.Katikati ni mwasilishaji wa mada,Mama Nsao Shalua na Katibu wa CAJAtz,Hassan Bumbuli.
Mkurugenzi wa Extra Bongo,Ally Choki ‘Mzee wa Farasi’ naye alikuwepo.Hapa akichangia ambapo alisema kwamba, tatizo la wanamuziki wa dansi wana wivu uliokithiri hivyo kushindwa kuwa na unenguaji wenye kubeba utambulisho wetu.
Wadau wa Jukwaa la Sanaa wakiangalia kupitia Projector moja ya picha chafu ya mnenguaji wa bendi.
Sehemu ya umati wa wadau wa Sanaa ukifuatilia kwa makini kauli kuhusu unenguaji zilizokuwa zikitolewa na Katibu Mtendaji wa BASATA,BW.Materego (hayuko pichani).

Na Alistide Kwizela,BASATA

Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) limewataka viongozi wa Bendi kuacha mara moja tabia ya kuwadhalilisha wacheza shoo (wanenguaji) kwa kuwavalisha mavazi ya kutia aibu na yanayodhalilisha utu wao.

Aidha,BASATA imewataka wanenguaji hao kuthamini utu wao na kufikiria upya dhana kwamba bila kuvaa nusu uchi basi sanaa ya muziki wa dansi haiwezi kupata soko na kuvutia watazamaji wengi kwenye maonyesho.

Akizungumza kwenye Jukwaa la Sanaa linaloandaliwa kwa pamoja na BASATA na Chama cha Waandishi wa Habari za Sanaa na Utamaduni (CAJAtz) na kufanyika kila Jumatatu,Katibu Mtendaji wa BASATA,Ghonche Materego alisema kwamba, lazima wadau wa muziki wa dansi wafikirie upya na kubadili mara moja tabia ya kuendekeza maonyesho yanayochafua maadili ya mtanzania.

“Wanenguaji lazima wafikie hatua waseme kwamba, udhalili wa nusu uchi basi tena.Wavae mavazi yenye heshima kama wanavyovaa wale wa kiume” alisema.

Aliongeza kuwa dhana kwamba bila wanenguaji kuvaa nusu uchi maonyesho ya muziki wa dansi hayapati watazamaji na biashara haifanyiki ni uongo na inaonesha jinsi wasanii wa dansi walivyokosa ubunifu wa kuvutia watu kwenye maonyesho yao na badala yake kubaki wakiendeshwa na hisia zisizo za kisanaa.

“Ushindani wa kibiashara ambao unaomfanya msanii kuwa dhalili ili kuvuta watu kwenye maonyesho haukubaliki bali unawafanya wasanii kuwa makapuku na wanaopoteza thamani yao” aliongeza.

Alisisitiza kwamba, BASATA limekuwa likikemea na kuchukua hatua za kisheria dhidi ya unenguaji wa nusu uchi lakini mabadiliko yamekuwa ni ya muda na baadaye kurudi kwenye udhalilishaji uleule.

Aliongeza kwamba,Baraza kwa sasa linafanya utafiti kwenye sanaa ya unenguaji na mara utakapokamilika mwongozo kwenye sanaa hii utatolewa na kutakiwa kufuatwa na wadau wote.

Kwa upande wake, mwasilishaji wa mada Mama Nsao Shalua ambaye ni Mkurugenzi wa Idara ya Ukuzaji sanaa, BASATA alisema kwamba, mavazi katika kazi ya sanaa yapo kwa ajili ya kuwakilisha tamaduni za jamii husika hivyo vichupi vinavyoonekana kwenye majukwaa yetu havina utambulisho wala maana yoyote.

‘Maleba (mapambo/mavazi) katika sanaa yoyote yanakuwa na utambulisho wa jamii na kazi husika hivyo vivazi vya nusu uchi vinavyovaliwa havina nafasi” alisema.

Katika Jukwaa hilo la sanaa lililopambwa na maonyesho ya wanenguaji kutoka bendi mbalimbali nchini waliokuwa katika mavazi tofautitofauti wadau wengi walilamika juu ya mavazi ya kutia aibu wanayovaa wanenguaji na kutoa wito wa hali hiyo kukoma mara moja.

Jukwaa la Sanaa litaendelea kama kawaida Jumatatu ya wiki ijayo kwenye Ukumbi wa BASATA ambapo mada itakuwa ni Soko la Ubunifu wa Mavazi Tanzania na Changamoto zinazowakabili itakayowasilishwa na Mbunifu maarufu nchini Mustapha Hassanali.

WAZIRI MKUU MIZENGO PINDA AKIKAGUA MIRADI MIKUMII!!

1Waziri Mkuu, Mizengo Pinda na mkewe Tunu wakikagua jengo la Hoteli ya Mikumi Wiild Life Lodge wilayniKilosa ambalo liliteketea kw amoto 6/8/2006 na hadi leo limebaki kuwa gofu. Alikiwa katika mapumziko ya Idd Septemba 11, 2010. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiongozwa na Mhifadhi Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Mikumi, John Shemkunde kukagua jengo la Hoteli ya Mikumi Wiild Life Lodge wilayniKilosa ambalo liliteketea kw amoto 6/8/2006 na hadi leo limebaki kuwa gofu. Alikiwa katika mapumziko ya Idd Septemba 11, 2010. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akikagua jengo la Hoteli ya Mikumi Wiild Life Lodge wilayniKilosa ambalo liliteketea kw amoto 6/8/2006 na hadi leo limebaki kuwa gofu. Alikiwa katika mapumziko ya Idd Septemba 11, 2010. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Mwenyekiti wa WAMA Mama Salma Kikwete Mkoani Mara!!

Mwenyekiti wa Taasisi ya Maendeleo ya Wanawake (WAMA) Mama Salma Kikwete akifurahia ngoma ya asili alipowasili katika Uwanja wa ndege wa Musoma Sept.12,2010 katika ziara yake ya kuhamasisha wana UWT Mkoani Mara kuhusu Umuhimu wa Uchaguzi Mkuu ujao. Picha na Mwanakombo Jumaa.
Katibu wa UWT Mkoa wa Mara Helena Chacha (aliesima shoto) akimkaribisha Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) Mama Salma Kikwete (hayupo pichani)alipowasili mkoani Mara Sept.12,2010 kwaajili ya kufanya mikutano ya ndani na kuzungumza na wanachama wa UWT kuhusu umuhimu wa kupiga kura katika Uchaguzi Mkuu mwaka huu. Picha na mwanakombo Jumaa.
Mwenyekiti wa Taasisi ya Maendeleo ya Wanawake (WAMA) Mama Salma Kikwete akisalimiana na Wanachama wa UWT Mkoa wa Mara Sept.12,2010 alipowasili kwenye uwanja wa ndege wa Musoma . Mama Salma Kikwete yupo mkoani hapo kwaajili ya kukutana na wanachama wa UWT katika mikutano ya ndani kuhusu kuwahamasisha umuhimu wa kupiga kura katika Uchaguzi Mkuu Ujao mwaka huu.(kulia) Mwenyekiti wa UWT mkoa Mara Nancy Sessani. (Picha na Mwanakombo Jumaa)
Kikundi cha wakianamama Musoma Mjini wakimshangiria mama salma kikwete alipowasili leo katika uwanaja wa ndege wa Musoma

wadau walihudhuria kwenye inshu nzima na pia zawadi zilimwagwa kwa washiriki wa miss tz

MKurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Utalii Nchini TTB Dr. Aloyce Nzuki akimkabidhi taji balozi wa Utalii nchini Salma Mwakalukwa mara baada ya kutangazwa kwenye shindano la Vodacom Miss Tanzania lililofanyika kwenye ukumbi wa Mlimani City usiku wa kuamkia leo numa ni Mmoja wa Maafisa wa Wizara ya Maliasili na Utalii Bw. Ernest Mwamwaja. Mrembo huyu atafanya kazi kubwa ya kuutangaza utalii wa ndani na kuhamasisha jamii kujua na kupenda au kuwa na utamaduni wa kutembelea vivutio vilivyopo nchini akiacha watalii wanaotoka nje ya nchi ambao ndiyo wamekuwa wakitembelea kwa wingi vivutio hivyo.
Makamanda kutoka vyomnbo mbalimbali wakiwa kazini hebu wacheki wanavyowajibika mdau.
Mkurugenzi Mtendaji wa Shiriki la Nyumba NHC Nehemia Kyando Mchechu kushoto na Mkurugenzi wa Masoko wa Vodacom Tanzania Ephraim Mafuru wakifuatilia kwa makini shindano hilo.
Wadau kutoka vyombo mbalimbali vya habari walikuwepo ili kujua kilichojiri katika shindano hilo na kuipasha habari jamii.
Mdau Lusako Owen kulia akiwa na Mkurugenzi wa Masoko wa benki ya CRDB Tuli Mwambapa kulia.
Mkurugenzi wa Sahara Media Group Samwel Nyalla kulia akiongea na Mkurugenzi wa CM. Co. Limited Charles Mtawali.
Mkurugenzi wa kampuni ya Prime Time Juhayna Kusaga kushoto na Mdogo wake Garina hawakutaka kusimuliwa juu ya shindano hilo.
Katibu Mhutasi wa kampuni ya Prime Time Godliver kushoto na rafiki yake nao walipita kwenye Red Carpert.
Mboni Masimba kushoto Mwanamama Shamimu Mwasha ambaye ni Blogger wa www.8020fashion.blogspot.com akiwa kulia pamoja na rafiki yao. nao hawakukosa kushuhudia shindano hilo.
Mwanamuziki AY wa pili kutoka kushoto akiwa na mwanamuziki E.Sniper kushoto, Castro na promota kutoka Uganda ambaye ni Mkurugenzi wa kampuni ya House Of Talent ya Uganda Bw. Eddie DouglasOkila kulia mwisho.
Vijana wa TMK Family Chege kushoto na Mh Temba wakihojiwa na mtangazaji wa kituo cha Televisheni cha Mlimani TV.
Mkurugenzi wa Masoko wa Vodacom Ephraim Mafuru akiongea na Mkurugenzi wa Kamati ya Miss Tanzania kabla ya kuanza kwa shindano hilo Vodacom ndiyo wadhamini wakuu wa shindano la Vodacom Miss Tanzania.
Wadau kutoka MUZASHA TUORS wakiwajibika vilivyo katika shindano hilo.
Ilikuwa si Mchezo kwenye Red Carpet mdau
Mkurugenzi wa Masoko Vodacom Tanzania Ephraim Mafuru wa pili kutoka kulia George Rwehumbiza Mkuu wa Udhamini Vodacom Tanzania wa kwanza kulia Elihuruma Ngowi Afisa Bidhaa wa kwanza kulia na Matina Nkurlu Afisa Habari wakipozi kwa picha mara baada ya kuhakikisha kila kitu kiko sawa katika shindano hilo.
Wadau kutoka Star TV kutoka kushoto ni Saida Mwilima, James Range, Neema na Christina Mbezi nao walikuwepo.
Vodacom Miss Tanzania Geneviva Emmanuel akipokea mfano wa cheki yenye thamani ya shilingi milioni 10 kutoka kwa Mkurugenzi wa Masoko wa Vodacom Tanzania Ephraim Mafuru katika hafla ya kukabidhi zawadi iliyofanyika jana jioni kwenye hoteli ya Giraffe Ocean View Kunduchi Geneviva Emmanuel aliibuka mshindi na kuwapiku wenzake 29 katika shindano lililofanyika jumamosi mwishoni mwa wiki kwenye ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es salaam na anatarajiwa kuwakilisha nchi kwenye shindano la dunia (Miss World 2010) litakalofanyika mwishoni mwa mwaka huu.
Mkurugenzi wa Masoko wa Vodacom Tanzania Ephraim Mafuru katikati akiwa katika picha ya pamoja na warembo kushoto wa kwanza ni Consolata Lukosi, Groly Mwanga na kulia wa kwanza ni Beatrice Premsingh, na Vodacom Miss Tanzania Geneviva Emmanuel.
Mkurugenzi wa masoko wa Vodacom Tanzania Ephraim Mafuru kushoto akikabidhi cheti cha Ushiriki wa shindano la Vodacom Miss Tanzania mrembo Groly Mwanga ambaye ni mshindi wa pili katika shindano hilo
Meneja Uhusiano wa Scangroup Tawi la Tanzania Bw. Barnabas Lugwisha kulia akipokea cheti kwa niaba ya kampuni hiyo ikiwa ni kutambua mchango wa kampuni hiyo katika kufanikisha shindano la Vodacom Miss Tanzania.
Warembo pamoja na waalikwa mbalimbali wakijimwaga ukumbini kwa burudani ya muziki.
Burudani pia hazikkukosa jana katika hafla ya kukabidhi zawadi kwa warembo wa Vodacom Miss Tanzania iliyofanyika kwenye Hoteli ya Giraffe Ocean View Kunduchi.
Mkurugenzi wa Masoko wa Vodacom Tanzania Ephraim Mafuru katikati akiwa pamoja na Mkuu wa Udhamini wa kampuni hiyo Geprge Rwehumbiza kulia pamoja na Ayubu Ryoba aliyekuwa mmoja wa majaji wa shindano hilo.
Wadau wakijadiliana jambo na mmoja wa warembo walioshiriki katika shindano la Vodacom Miss Tanzania lililomalizika hivi karibuni.
Hashim Lundenga Mkurugenzi wa Kamati ya Miss Tanzania katikati akiwa na Mshauri wa Kamati ya Miss Tanzania wa pili kutoka kulia na wadau wengine wakiwa katika hafla hiyo.
Kutoka kushoto ni Loveness, Benny Kisaka, Jeseline na rafiki yake kushoto.

THE DON HIMSELF

Karibuni sana kwenye blog hii ya kijamii iliyosheheni makila kitu kuanzia siasa uchumi afya na burudani kwa ujumla wake.uingiapo kwenye blog hii ni mengi ambayo utapata nafasi ya kukutana nayo,kumbuka mawazo yako ndo hasa yanayojenga na kunifanya niwe na ufanisi zaidi.kariiiiiiibuuuuuuuuuuuu saaaaaaaaaaaaaaanaaaaaaaaaa.(THE DJ HIMSELF-JIWE)

Followers

BLOG ZA MARAFIKI

Search This Blog

ZILIZOPITA

DUNIA MUZIMA