Aug 12, 2010

WAZIRI WA KAZI PROF.KAPUYA AZINDUA MWAKA WA VIJANA!!

Mgeni Rasmi Waziri wa Kazi, Ajira na Maendeleo ya Vijana Prof. Athman Jma Kapuya akiongea na vijana wakati wa kongamano la vijana lililoandaliwa na Asasi ya Vijana ya Umoja wa Mataifa YUNA na kufanyika ukumbi wa APEADU kwenye ofisi za Umoja huo mtaa wa Mafinga Kinondoni Jijini Dar es salaam katika kuadhimisha siku ya vijana Duniani.
Katika kongamano hilo vijana wamejadili mambo mbalimbali yanayowahusu kama vile Elimu, Afya, Ajira, Michezo, Haki zao na mambo mengine mengi wanayokumbana nayo katika maisha ya kawaida kama vijana huku wakiazimia kuomba Serikali iwaruhusu kuunda Baraza la Vijana la Taifa litakalosimamia mambo yao yote ili kuwatetea na kuwasimamia katika mipango mbalimbali ya Kisera inayowahusu vijana.
Katika Hotuba yake Waziri Kapuya amewaasa vijana kuunda Baraza litakalokuwa ni la kitaifa zaidi kuliko kuwa Baraza la kiubabaishaji linaloweza kuleta athari kubwa kwa taifa Waziri pia alizindua mwaka wa Vijana unaoanza leo tarehe 12 Agosti 2010 mpaka Agosti 11 , 2011 na utakuwa ukiadhimisha kila mwaka Duniani kote.
Waziri wa Kazi, Ajira na Maendeleo ya Vijana Prof. Athman Juma Kapuya akiingia kwenye ukumbi wa mkutano wa kati wa kongamano la vijana lilioandaliwa na Asasi ya Vijana ya Umoja wa Mataifa YUNA na kufanyika ukumbi wa APEADU kwenye ofisi za umoja huo Mtaa wa Mafinga Kinondoni jijini Dar es salaam nyuma ya Waziri ni Mwakilishi wa UNIDO Nchini Emmanuel Kalenzi.
Vijana kutoka shule na Asasi mbalimbali za vijana waliohudhurika katika kongamano la vijana lililofanyika leo kwenye ofisi za Umoja wa Mataifa katika kuadhimisha siku ya vijana Duniani.

Mikoko ya Vodacom kukuza uchumi kwa washindi!!

Baadhi ya washindi wa magari ya Hyundai i10 yanayotolewa na Kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom Tanzania kupitia promosheni yake ya ‘Shinda Mkoko’ wamesema zawadi hiyo itawasaidia kukuza uchumi wao kwani itarahisisha usafiri katika shughuli zao.
Akizungumza kwa njia ya mahojiano kutokea Dodoma baada ya kuibuka mmoja wa washindi wa promosheni hiyo, Tolino Pechaga ambaye ni fundi umeme wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) alisema anatumaini gari hilo litakamilisha ndoto yake ya kimaisha katika kujiletea maendeleo.
Akifafanua alisema, ingawa alikuwa akitumia magari ya wafanyakazi kutoka Maili mbili anakoishi hadi Udom, ujio wa Hyundai i10 utamaliza muda wa kukimbizana na basi hilo na kumpa nafasi ya kufanya kazi zake binafsi baada ya muda wa kazi kwa mwajiri wake.
“Unajua mimi ni mwajiriwa wa chuo, lakini nafanya pia kazi zangu binafsi. Usafiri ulikuwa kikwazo namba moja kufikia malengo yangu, lakini sasa kila kitu kitaenda sawa kwani tayari nitakuwa na usafiri wangu binafsi utakaorahisisha maendeleo yangu,” alisema Pechaga.
Kwa upande wake Benard Asenga wa Keko Magurumbasi jijini ambaye ni mfanyabiashara wa duka la bidhaa ndogondogo na vyakula alisema alikuwa akitumia muda mwingi na baiskeli kufuata bidhaa sokoni Kariakoo, lakini gari hilo litamuwezesha kuboresha utoaji huduma kwa wateja wake.
Aidha Asenga alifafanua kwamba mara baada ya kukabidhiwa Hundai i10 aliyojishindia atabadilisha mtindo wa biashara anaoufanya na anafikiria kuwa mjasiriamali wa kati (SME’s) na kumiliki duka la bidhaa za jumla na rejareja.
“Sasa sitatumia tena baiskeli kufuata bidhaa mjini, nafikiria kukuza biashara yangu kutoka hatua moja kwenda nyingine jambo litakaloniwezesha kukuza hali yangu kiuchumi,” alisema mfanyabiashara huyo.
Naye Simon Kihuru ambaye ni dereva wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Songea alisema zawadi hiyo iliyotolewa na Vodacom Tanzania itampunguzia gharama za usafiri kwa ajili kuwapeleka na kuwarudisha watoto wake shule kwani wataweza kutumia gari hiyo kwa matumizi ya binafsi.
“Kama nilivyosoma kwenye magazeti mbalimbali kwamba gari hiyo haitumii gharama kubwa kuihudumia, kwa kuwa mimi ni dereva itaniwezesha kutunza fedha zangu baada ya kukwepa huduma za daladala ambazo sio salama sana hususani kwa watoto,” alisema Kihuru.
Akizungumza hivi karibuni kwenye hafla ya uzinduzi wa promosheni ya ‘Shinda Mkoko’ iliyopanga kuwazawadia wateja wake gari moja aina ya Hyundai i10 kila siku Mkurugenzi wa Masoko wa Vodacom Tanzania Ephraim Mafuru alisema shindano hilo litawahusisha wateja wote wa kampuni hiyo nchini na kwamba ndani ya siku 100 kila siku mtu atakuwa anajipatia gari moja

Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii yakabidhi vifaa Tiba Dodoma!!

Katibu Mkuu wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii bi. Blandina nyoni amekabidhi vifaa mbalimbali vya tiba katika Hospitali ya Mkoa wa Dodoma, makabidhiano hayo yamefanyika juzi mkoani humo na hii ni moja ya mashine ya usingizi iliyokabidhiwa kwa hospitali hiyo
Katibu mkuu Bi Blandina Nyoni akikabidhi moja ya vifaa tiba vinavyotumika kwa ajili ya operesheni ya akina mama wajawazito kwa katibu Tawala wa mkoa wa Dodoma bi. Madenge
Moja ya kitanda kinachotumika kulazia mgonjwa anayehitaji uangalizi wa hali ya juu katika chumba cha watu mahututi(ICU)

BLOOD DIAMONDS - A TRAGEDY OF HISTORIC PROPORTION!!

African and international headlines have been dominated with the trial of former Liberian President, Charles Taylor and his alleged gift of blood diamonds to supermodel Naomi Campbell.
In the 1990s, the African countries of Sierra Leone, Liberia, Angola and the Democratic Republic of Congo disintegrated into civil war. Civilians were raped, murdered and attacked during the decade-long war. Collectively over 4 million civilians died.
What connected each conflict was the currency used to fund them – diamonds. HISTORY™ will provide a detailed look into the harsh reality behind the production of the world’s most valuable gems. Blood Diamonds depicts the brutality of a regime – supposedly backed by Charles Taylor – where millions of people lost their lives due to the conflicts over blood diamonds.
As citizens in four African warzones suffered, diamonds from those countries flowed freely into the world’s diamond market. Diamonds are the world’s most precious gems, but in West and Central Africa, their cost has been greater than anyone could have ever imagined.
Tune in to watch BLOOD DIAMONDS on the History Channel (DStv channel 254) on Saturday August 14 at 21.30.

MWENYEKITI WA (YUNA) HAPA NCHINI AWAPA CHANGAMOTO VIJANA!!

Mwenyekiti wa Asasi ya Vijana ya Umoja wa Mataifa hapa (YUNA) chini Benny Kikove akizungumza na wajumbe waliohudhurika kwenye kongamano la vijana linaloendelea kwenye ofisi za UN katika ukumbi wa APEADU Mtaa wa Mafinga Kinondoni jijini Dar es salaam, kongamano hilo linajadili mambo mbalimbali yanayowahusu vijana pamoja na changamoto wanazokumbana nazo katika ujana wao katikamkuadhimisha siku ya vijana duniani. Wanafunzi wa shule mbalimbali wakiwa katika kongamano hilo wamesema wana matarajio mengi mara baada ya kongamano hilo kwani litawafanya kupeana uzoefu mbalimbali katika kukabili chanagamoto wanazokutana nazo katika maisha ya sasa. Mmoja wa Wajumbe wa mkutano huo na Afisa wa UN hapa nchini Bi Hoyce Temu kushoto akiandika mambo mbalimbali yanaojadiliwa na vijana katika kongamano hilo.

Wajumbe mbalimbali wakimsikiliza mwenyekiti wa Asasi ya Vijana ya Umoja wa Mataifa hapa nchini YUNA Bw. Benny Kikove wakati alipokuwa akiongea na wajumbe wa konamano hilo asubuhi hii.

TAIFA STARS NA HARAMBEE STARS NGUVU SAWA!!

Kiungo mshambuliaji wa Timu ya Harambee Stars ya Kenya, Macdonald Mariga (kushoto) akidhibitiwa na wachezaji wa Taifa Stars, Jerry Tegete (katikati) na Nurdin Bakari, wakati wa mchezo wa Kimataifa wa kirafiki uliochezwa kwenye Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam leo jioni. Timu hizo zimetoka sare ya bao 1-1.
Picha kwa hisani ya www.sufianimafoto.blog

Precision Air yaleta ndege mpya!!

Na Mwandishi Wetu
SHIRIKA la Ndege la Precision linalotoa huduma bora Tanzania, limetangaza kuleta ndege yake mpya ya sita aina ya ATR42-500 itakayowasili Agosti 26 mwaka huu kutoka Toulouse, Ufaransa, ikiwa ni sehemu ya kutekeleza programu ya kutoa huduma za kisasa zaidi. Mkurugenzi Mkuu na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Precision Air, Alfonse Kioko, aliwaambia waandishi wa habari Dar es Salaam jana kuwa, ndege hiyo mpya itakayopachikwa jina la Bukoba, itafuatiwa na nyingine ya saba itakayoingia Septemba 15 mwaka huu.
Mwaka 2006, Precision na ATR ya Ufaransa walisaini mkataba wa dola za Marekani milioni 129 ili kutoa ndege saba mpya. Ndege ya kwanza kati ya hizo iliwasili Machi 2008. Tangu wakati huo, Precision imepokea ndege tano aina ya ATR 72-500 na kufanya iwe na ndege tano mpya mpaka sasa. Pia ina ndege nyingine tatu za zamani. Kioko alisema baada ya ndege hiyo yenye namba 5H-PWF kuwasili, wataizindua Dar es Salaam Agosti 27.
Alisema ina vifaa vya kisasa vya burudani kwa ajili ya wasafiri kuangalia sinema na kusikiliza muziki wakiwa safarini. Ndege hiyo ina uwezo wa kubeba abiria 70. Mkurugenzi huyo pia alitangaza kwamba tangu kuanza mwaka mpya wa fedha, idadi ya abiria wapya imeongezeka kwa asilimia 12 kulinganisha na mwaka jana. Pia mizigo ya biashara imeongezeka licha ya kudorora kwa uchumi duniani.
Akizungumza katika mkutano huo, Meneja Masoko wa Precision, Emillian Rwejuna alisema kampuni hiyo inatarajia kupata ndege ya Boeing 737, kati ya Oktoba na Novemba mwaka huu. Rwejuna alisema kupatikana kwa ndege hiyo kutapanua wigo wa huduma za safari.
Ndege hiyo ya tatu aina ya Boeing 737 itaboresha safari za Johannesburg, Afrika Kusini, na pia katika miji ya Kinshasa na Lubumbashi, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo. Precision Air hivi sasa inafanya safari katika miji ya Dar es Salaam, Mwanza, Tabora, Musoma, Shinyanga, Kigoma, Kilimanjaro, Zanzibar, Mtwara na Arusha. Pia ina safari za Nairobi na Mombasa, Kenya na Entebbe, Uganda.

WAGOMBEA UBUNGE WA CUF (W) ILALA WAJITAMBULISHA!!

Mgombea Ubunge kupitia Chama Cha Wannanchi CUF Hussein Siyoverwa akizungumza mbele ya wanahabari leo kwenye ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo wakati wagombvea hao kutoka Majimbo ya Ilala, Segerea na Ukonga walipojitambulisha mbele ya wanahabari, wanaofuatia katika picha ni Kimangala Ayubu Mussa na Gulam Nasoro Mkurugenzi wa Uenezi, Mahusiano ya Umma CUF Wilaya ya Ilala.
Wagombea wa ubunge katika majimbo ya Ilala, Segerea na Ukonga kupitia Chama Cha Wananchi CUF wakionyesha fomu zao mbele ya waandishi wa habari kwenye ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo leo mara baada ya kukabidhiwa na Mkurugenzi wa Wialaya ya Ilala leo, kutoka kulia ni Heko Pori Ukonga,Husein Siyoverwa Ilala na Kimangala Ayubu Musa Segerea.

MAOFISA HABARI WAKUTANA LEO JIJINI DAR.

Mkurugenzi wa Idara ya Habari(MAELEZO) Clement Mshana akiongea na Maofisa Habari, Elimu na Mawasiliano wa Wizara,Idara zinazojitegemea na wakala wa serikali leo jijini Dar es salaam.Pamoja na mambo mengine amewatoa wito kwa Maofisa hao kushiriki kikamilifu kutoa habari zinazohusu utendaji wa serikali kwa wananchi.
Maafisa habari wakiwa katika mkutano huo.
Baadhi ya Maofisa habari ,Elimu na Mawasiliano wa Wizara,Idara zinazojitegemea na wakala wa serikali wakifuatilia masuala mbalimbali leo jijini Dar es salaam wakati Mkurugenzi wa Idar ya Habari (MELEZO)Bw. Clement Mshana alipokutana nao. Picha na Aron Msigwa.

Aug 11, 2010

BASATA KUYAPA MENO RASMI MASHIRIKISHO YA SANAA

Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) leo Jumanne Agosti 10, 2010 katika ukumbi wake limeanza mchakato wa kuyapa nguvu mashirikisho ya wasanii nchini ili sasa wasanii waweze kusimama na kutetea haki zao mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuwa na umoja katika kujisimamia.

Mchakato huo utakaodumu kwa siku nne hadi Ijumaa umeanza kwa Shirikisho la Wasanii wa Sanaa za Ufundi kuchagua viongozi wao wa muda ambao watasimamia kikamilifu utayarishaji wa kanuni za kuliongoza shirikisho hilo na baadaye kuitisha uchaguzi utakaowaweka viongozi wa kikatiba.

Katika uchaguzi huo uliosimamiwa na Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Utamaduni Kutoka Wizara ya Habari Utamaduni na Michezo Bi.Angela Ngowi, Bw.Adrian Nyangamale ambaye ni Rais wa Chama cha Wasanii wachoraji alichaguliwa kuwa Rais wa Muda wa Shirikisho hilo baada ya kupata kura 12 kati ya 21 zilizopigwa na kuwabwaga wenzake ambao ni Gwalugano Lyimo na Focus Senya.

Kwa upande wa Makamu wa Rais,Mwanamitindo maarufu nchini,Khadija Mwanamboka aliibuka kidedea baada ya kupata ushindi wa kishindo wa kura 18 kati ya 21.Nafasi ya Katibu ilikwenda kwa Godfrey Ndimbo huku mweka hazina akichaguliwa Rashidi Mbogo.

Wajumbe walioteuliwa kuliongoza jahazi la shirikisho hili ni pamoja na Rashidi Munyana,Basil Nyambele na Gwalugano Ayoub.

Akizungumza baada ya Uchaguzi,Msimamizi wa uchaguzi Bi.Ngowi alisema kwamba,huo ni mwanzo wa wasanii kujisimamia na kujipanga kwa ajili ya kutetea maslahi yao na kuhakikisha wanalinda haki ya kazi zao na kutafuta masoko kwa ajili ya kazi zao.

Aliongeza kwamba,viongozi waliochaguliwa lazima wahakikishe wanasimamia kikamilifu katiba na kutafuta fursa na mbinu za kupenya kwenye soko la pamoja la Afrika Mashariki.

Kwa upande wake Katibu Mtendaji wa BASATA,Ghonche Materego alisema kwamba, lengo la Baraza ni kuona wasanii wanakuwa na umoja wa kitaifa na Kutoka kwenye makucha ya utegemezi na kupambana mmojammoja.Aliongeza kwamba, wakati umefika kwa wasanii kuonesha usasa na kuachana na ufanyaji kazi za sanaa wakiwa katika mazingira yasiyo rasmi na ya kulalamika tu bila kuwa watendaji na watekelezaji.

Mlezi wa Wasanii wa Sanaa za Ufundi,Rashid Masimbi ambaye pia ni Mjumbe wa Bodi ya BASATA alisema kwamba, kazi iiyopo mbele ni kwa viongozi waliochaguliwa kuja na mipango ya muda mfupi na mrefu katika kulikuza shirikisho, kutafuta wanachama wapya na kuandaa kanuni za kuliendesha shirikisho hilo.

BASATA liko kwenye mkakati kabambe wa kujenga umoja wa wasanii kupitia mashirikisho ambapo sasa wasanii nchi nzima watakuwa na fursa ya kuwa na sauti moja pia kupanga misimamo yao itakayoheshimika kitaifa na kimataifa.

Mashirikisho ambayo yameundwa na sasa uongozi wake unatafutwa ni yale ya Sanaa za Ufundi,Sanaa za Muziki,Sanaa Jongevu (Filamu) na Sanaa za Maonesho.

Baraza linawataka wasanii wote, kuhakikisha wamejisajili na kujiunga na mashirikisho hayo kwa ajili ya kuanza mkakati wa kutetea maslahi yao.


RATIBA KAMILI YA CHAGUZI KATIKA MASHIRIKISHO

1. Jumatano,Agosti 11, 2010-Shirikisho la Muziki Tanzania,Kwenye Ukumbi wa BASATA kuanzia saa 4.00.Asubuhi.
2. Alhamisi,Agosti 12,2010-Shirikisho la Sanaa za Maonesho,Ukumbi wa BASATA kuanzia Saa 4.00 Kamili.
3. Ijumaa Agosti 13, 2010-Ahirikisho la Sanaa za Jongevu (Filamu) Tanzania, Ukumbi wa BASATA kuanzia saa 4.00.

Matokeo yatatangazwa kwnye vyombo vya habari,

WADAU WOTE MNAKARIBISHWA,

Habari na Alistide Kwizela,Afisa Habari wa BASATA.

Ukweli Kuhusu Haruna Moshi ‘ Boban’ : Alikosa Namba Gavle IF

Na Maggid Mjengwa,Gavle, Sweden
HII ni sehemu tu ya makala inayohusu sakata la Haruna Moshi kukatisha mkataba na klabu ya Gavle IF. Kuna mengi yamesemwa na kuandikwa kuhusu Haruna Moshi kukatisha ghafla mkataba wake na klabu ya Gavle IF ya hapa Sweden. Hata hivyo, wapenzi wa soka wa Tanzania hawakuweza kupata ukweli hasa juu ya sakata la Haruna Moshi ‘ Boban’.
Nikiwa katika mji wa Gavle, mahali ambapo Haruna Moshi aliishi na kucheza kandanda ya kulipwa nimeweza kukusanya taarifa zenye kuonyesha nini kilitokea.
Kwa mujibu wa taarifa hizo, Haruna Moshi alikuwa na uwezo wa kuichezea klabu hiyo. Kilichojitokeza ni kwa Haruna Moshi kuwa majeruhi kwa muda mrefu huku nafasi ya kiungo wa kati anayoichezea ikigombaniwa na wachezaji zaidi ya watatu.Katika muda wote aliokuwa na Gefvle IF, Haruna Moshi amecheza mechi tano tu za Ligi Kuu ya Sweden.
Katika mechi hizo, ni mbili tu amecheza tangu mwanzo na nyingine tatu aliingia akitokea kwenye benchi la wachezaji wa akiba.Kwa mujibu wa maelezo ya Mkuu wa Idara ya Michezo ya klabu ya Gefle IF, Per Olson yeye anaamini, kuwa Haruna ana bahati mbaya.
Kuwa hata walipokwenda kwenye kambi ya mazoezi nje ya nchi, Haruna hakuwepo kutokana na familia yake kutarajia kupata mtoto. Hivyo, alikosa mechi tatu muhimu za kujipima nguvu na ambazo zingemweka Haruna Moshi kwenye nafasi nzuri ya kushindania namba.
Na mchezaji aliyesababisha Haruna Moshi abaki kwenye benchi ni Yussif Chibsah kutoka Ghana. Chibsah anachezea nafasi ya kiungo wa kati kama alivyo Haruna Moshi. Kurejea kwake katika klabu hiyo akitokea Ghana ndiko kulikofuta kabisa matumaini ya Haruna Moshi.
Ni nani huyu Yussif Chibsah? Na je, ilikuwa ni sahihi kwa Haruna Moshi kukatisha mkataba wake? Angeweza kubaki Sweden na kucheza katika klabu nyingine? Itaendelea… Habari hii ni kwa hisani ya
http://www.kwanzajamii.com/?p=2705 kwa habari zaidi bofya hapo.

TWIGA STARS RECEIVED BY WASHINGTON GOVERNOR CHRISTINE GREGOIRE!

The Twiga Stars pose with Washington's governor, Christine Gregoire.
Photos and Story By Nisha Ligon http://www.twigastars.com/.
Today the Twiga Stars, Tanzania's national women's football team, visited the Washington State Capitol, where they were received by Governor Christine Gregoire. The Twiga Stars, who were brought to Washington State for a training tour by Rahma Al-Kharoosi, president of RBP Oil and Industrial Technologies, got the chance to learn about state legislative procedure, sing a Tanzanian song for their hosts, and to speak to the Governor herself. She wished them the best of luck and told the Tanzania ladies that she has a special interest in women's football as both of her daughters are footballers. Ms. Al-Kharoosi thanked the Governor for taking the time to speak to them, and added that it was inspiring for the girls to meet such an accomplished woman who has shown "yes we can." A special tradition at the Washington Legislative Building is to make a wish while rubbing the nose of a George Washington bust. The Twiga players each took a rub and wished to make it to the Women's World Cup (to be held in Germany in summer 2011). The Twiga Stars have been training in Washington since August 2, and are preparing for the African Women's Championship to be held in South Africa this October. The top two teams from the African Championship will proceed to the Women's World Cup in Germany. The Twiga Stars have shown they're ready for the competition by posting a number of impressive performances here in Washington, including a 4-0 victory over Dos FC last night. Asha "Mwalala" Rashid scored 2 goals, while Mwanahamis Omary and Fatuma "Kitunini" Mustapha each scored one. Ms. Al-Kharoosi said she's very happy with the teams performance and is confident that they are gaining the experience they need to succeed in the continental championship this
The players pose with George Washington Statue!
Twiga Stars matron Rahma Al-Kharoosi rubs George Washington's Statue and wishes for her girls to make it to the World Cup.
Ms. Al-Kharoosi, who has arranged and paid all expenses for this trip.
Photo op outside of the State Capitol

Aug 10, 2010

KENYA WAJIFUA NA MAZOEZI KATIKA UWANJA WA KARUME KUJIANDAA NA MCHEZO DHIDI YA STARS KESHO KATIKA UWANJA WA UHURU JIJINI DSM

wachezaji wa kenya bize na mazoezi kabla ya mchezo na stars hapo kesho
wachezaji wa kenya wakifanya mazoezi asubuhi katika uwanja wa karume
Katikati ni kocha wa kenya kulia ni kocha wa tanzania wakati wa mkutano na waandishi wa habari kuhusiana mchezo wa kimataifa wa kirafiki dhidi ya taifa stars na harambee stars

Rais Kikwete azindua Ujenzi wa Miundombinu ya Mfumo wa Mabasi yaendayo Haraka Dar es Salaam!!

Rais Jakaya Mrisho Kikwete ,Mwakilishi mkazi wa Benki ya Dunia John Mc Intyre(watatu kulia),Waziri wa Miundombinu Dr.Shukuru Kawambwa(kushoto) na Waziri wa TAMISEMI Mhe.Selina Kombani(kulia) wakifunua kitambaa kuashiria kuzindua rasmi ujenzi wa Miundombinu ya mfumo wa mabasi yaendayo haraka jijini Dar es Salaam wakati wa sherehe za uzinduzi zilkizofanyika Ferry kivukoni jijini Dar es Salaam leo mchana.
(Picha na Freddy Maro)
Mtendaji Mkuu wa Mradi wa Mabasi yaendayo Haraka jjijini Dar es Salaam(Dar Rapid Transit Agency ) Bwana Cosmas Takule akieleza jinsi mradi huo utakavyofanya kazi pindi utakapo kamilika hivi karibuni jijini Dar es Salaam huku Rais Jakaya Mrisho Kikwete na mkuu wa mkoa wa Dar es Salaamm williuma Lukuvi wakisikiliza kwa makini.
Mtendaji Mkuu wa Mradi wa mabasi yaendayo Haraka jijini Dar es Salaam Bwana Cosmas Takule akionyesha mchoro wa ramani ya utekelezaji wa mradi huo jiji Dar es salaam huku Rais Jakaya Mrisho Kikwete,Waziri wa Miundombinu Dr.Shukuru Kawambwa, Waziri wa TAMISEMI Bi.Selina Kombani na Mwakilishi Mkazi wa Benki ya dunia Bwana John Mc Intyre wakisikilza kwa makini wakati wa sherehe za uzinduzi wa ujenzi wa miundombinu ya mradi huo zilizofanyika Ferry Kivukoni, jijini Dar es Salaam leo mchana.

BIG BROTHER ALL STARS MUNYA OR TATIANA – AFRICA MUST DECIDE!

Zimbabwe’s Munya and Angola’s Tatiana are up for eviction this week after Monday night’s (9 August) nominations on M-Net’s Big Brother All Stars. Munya finds himself up for eviction for the second week in a row after Sheila saved herself and put him up for eviction in her place.
Head of House Sheila found herself up for eviction after receiving the bulk of nominations from her housemates, based on the fact that she could save herself. · Code nominated Yacob, because as he says "I can't trust him and I can't place him yet". His second nomination went to Sheila. ·
Jennifer nominated Uti and Meryl because she feels they have formed an alliance, which concerns her.
· Kaone nominated Sheila and Meryl – the former because she could save herself. · Meryl nominated Kaone because he "gets on my last nerve” and also because she feels he is judgmental. She also nominated Tatiana because she considers her to be strong competition but pointed out that "it has nothing to do with Lerato, I just don't want her around for too long".
· Munya kept his nominations going along the same lines he has stuck to every week – “strictly business”. He nominated Uti and Yacob, explaining "I'm starting from the top of Africa and moving down”. ·
Paloma nominated Sheila because she could save herself and Uti because she felt his jokes had gone overboard and he is hurting people “and this is getting out of hand”.
· Mwisho nominated Tatiana because he thought everyone would be thinking along the same lines after both her Head of House decisions had seen the people she replaced herself, with evicted from the house. He also named Kaone because "the game has shifted” - he feels he needs to pick a side and take a gamble and Kaone is not on the side he has picked.

O’NEILL AIMUA KUSEPA ASTON VILLA……!!!!

Martin O’Neill.

Kocha huyo amechukua hatua hiyo baada ya kuwa na sintoelewana kati yake na mmiliki wa klabu hiyo ajulikanae kwa jina la Randy Lerner na kikubwa ni kutokana na kuzwa kwa kiungo James Milner kwa Man city na kama angeweza kutumia kitita cha mauzo hayo kununua wachezaji wengine.

Lakini yaonekana kocha huyo alivumilia sana uzwaji wa wachezaji wake tegemeo kama Gareth Barry nae kwenda Man city.

Timu hiyo imemteuwa Kevin Macdonald kuwa mrithi wa mda mfupi nae akikabiliwa na kibarua kigumu cha mechi kati yao na West ham utd siku ya jumamosi

TUIGE MFANO KAMA WA AKINA USHER RAYMOND…!!!

Usher,Bill Clinton & Ciara on the stage.

Usher brought out some of his celebrity friends, including Justin Bieber, former president Bill Clinton, Ciara and Young Money rapper Lil Twist to help him take part in his New Look Foundation’s first annual World Leadership Awards, held Friday night (Aug 6) in Atlanta, GA at the Cobb Energy Performing Arts Center.

Ciara later joined Usher on-stage to perform a duet to John Lennon’s “Imagine,” while Usher’s young protege Justin Bieber hit the stage solo for his own performance set. Usher himself even treated the crowd to a few performances, including his #1 hit single “OMG.”

Ciara na Justin Bieber

Bill Clinton na Usher Raymond wakiwa Back stage.

Usher and His New Look Foundation Host First Annual World Leadership Awards in Atlanta.

Blog team: Wote tunakubali ya kuwa wanamuziki na wacheza filamu wanachukuliwa kama kioo cha jamii hapa nchini kupitia kazi zao wanazo zifanya. kutokana na hadhi hiyo wanayo nafasi kubwa ya kufanya mambo ya muhimu yanayo lenga kuisaidia jamii inayo wazunguka si tu kwa kuingia katika siasa bali kuanzisha taasisi zinazo gusa nyanja mbalimbali za jamii na hata katika kuleta ufanisi wa kazi wa sekta mbalimbali za kiserikali. Na hii si kwa wao tu hata watangazaji wa redio na televisheni ambao wamekuwa wakionekana na kusikika nchi nzima.

NDIVYO ILIVYOKUWA KWENYE USAILI WA BBS

Washiriki wa BONGO STAR SEARCH 2010 wakiandikisha majina yao kwa ajili ya Usaili wa Kushiriki kinyang’anyiro hicho.

Baunsa akiwapanga Vijana waliojitokeza kwa ajili ya Kushiriki kwenye Audition za BSS 2010 zilizoanza leo asubuhi katika Ufukwe wa COCO BEACH.

Askari wa Kampuni ya ULTIMATE Security akiwatuliza washiriki waliokuwa wakileta fujo kuogmbania namba kwa ajili ya kuingia kwenye usaili.

Kikundi cha Vijana wanaoishi Keko walikutwa na Camera ya THE DJwakifanya mazoezi ya kuimba nje ya Ukumbi wa Coco beach kabla ya kufanyiwa usaili.

Washiriki wakiwa kwenye foleni kwa ajili ya kuandikisha namba zao.

Pichani ni mshiriki Angela Batazari (22) mkazi wa mtoni Kijichi akitoa maoni yake mbele ya Camera ya THE DJ juu ya mchakato mzima wa BSS 2010 alisema kwamba kutakuwa na ushindani mkubwa tofauti na mwaka jana kwa sababu watu wamejitambua kuwa wana vipaji vya kuimba ili waweze kupata ajiri kutokana na Tasnia ya Muziki hasa wa Bongo Flava

JAJI MKUU AWAPANDISHA VYEO MAHAKIMU SINGIDA,DODOMA..!!!

Jaji Ramadhan akimwapisha hakimu Aziza Mbadjo (aliyenyanyua Quruan) kuwa hakimu katika mahakama ya hakimu mkazi mjini hapa jana.

Jaji Ramadhan (wa pili kutoka kushoto) akiwa kwenye picha ya pamoja na mahakimu wa mahakama ya hakimu mkazi mjini hapa na viongozi waliofuatana na jaji huyo.Picha zote na Hillary Shoo,

Na Hillary Shoo,

Singida.

JAJI mkuu wa mahakama ya Tanzania,Augustino Ramadhan, amewaagiza wafanyakazi wa mahakama nchini,kuhakikisha wanajiendeleza kielimu ili kujijengea mazingira mazuri ya kuweza kumudu vema majukumu yao ya kila siku.

Jaji Ramadhan ametoa wito huo jana (9/8/2010) muda mfupi baada ya kuwaapisha mahakimu watatu kuwa mahakimu wa mahakama ya hakimu mkazi.Hafla hiyo ilifanyika kwenye ofisi ya hakimu wa mahakama ya hakimu mkazi mjini hapa.

Alisema katika dunia ya sasa mambo mengi yanabadilika kwa kasi yakiwemo ya kisheria,kanuni na taratibu na hivyo,ili hakimu au mfanyakazi wa mahakama aweze kumudu kutekeleza wajibu wake vizuri, hana budi kujiendeleza kielimu.

Aidha, aliwataka kujiwekea mikakati ya kujiendeleza wenyewe au kutafuta misaada mbalimbali kwa madai kwamba wakisubiri mafungu ya fedha za serikali,wanaweza kuchelewa kujiendeleza kielimu. ”Binafsi nawapongeza sana ninyi kwa juhudi zenu binafsi za kujiendeleza kielimu,ninyi ni mfano mzuri wa kuigwa na wafanyakazi wengine wa mahakama nchini na hata sekta zingine”alisema.

Katika hatua nyingine, Jaji Ramadhan aliwaagiza mahakimu hao kwenda kutekeleza wajibu wao kwa kuzingatia sheria,kanuni na taratibu zilizowekwa na si vinginevyo. ”Nendeni mkafanye kazi kwa uadilifu mkubwa,msiige mambo yasiyofaa.Sheria,kanuni na taratibu ndio ziwaongoze katika kutekeleza majukumu yenu.Serikali inawalipa mishahara mizuri kwa lengo la kuwaokoa msijiingize kwenye matatizo”alifafanua.

Mahakimu walioapishwa jana, ni Fedinard Vugingi ambaye alikuwa hakimu wa mahakama ya mwanzo Kondoa mkoani Dodoma na sasa anakuwa hakimu mfawidhi wa mahakama ya wilaya ya Kondoa. Aziza Hassan Mbadjo aliyekuwa karani katika mahakama kuu ya ardhi Dar-es-salaam,sasa amekuwa hakimu katika mahakama ya hakimu mkazi mjini hapa.

Naye Terrysophia Cornelio Tesha aliyekuwa hakimu wa mahakama ya mwanzo Ipembe,sasa anakuwa hakimu katika mahakama ya hakimu mkazi Singida mjini.

Mahakimu wote hao watatu, wamejiendeleza kwa nguvu zao wenyewe. Jaji Ramadhan na msafara wake wameondoka Singida mjini leo (jana) asubuhi kuelekea mkoani Shinyanga.

HASEEM THABEET ATUA DAR KUTOA SOMO KWA VIJANA WANAOPENDA MPIRA WA KIKAPU

HASHEEM THABEET
HASHEEM THABEET akiwa katika ukumbi wa (MAELEZO)

THABEET ambaye anacheza mpira wa kikapu nchini marekani ametua jijini kwa lengo la kutoa mafunzo kwa wachezaji vijana ili kuendeleza mchezo wa kikapu hapa nchini hasa kwa vijana.

Akizungumza Jijini DSM THABEET amesema yuko likizo kwa muda ndani ya siku ambazo atakuwa hapa atatoa mafunzo kwa vijana kama alivyofanya katika nchi mbalimbali kabla ya kufanya hapa nchini.

Mafunzo hayo yanatarajia kufanyika katika ukumbi wa DONBOSCO UPANGA Jijini DSM kuanzai alhamisi wiki hii

HARAMBEE STARS NA TANZANIA STARS KUKIPIGA UWANJA WA UHURU JUMATANO WIKI HII

MSEMAJI WA TFF FLORIAN KAIJAGE.


Mchezo wa kirafiki wa kimataifa baina ya timu ya Taifa ya TANZANIA,TAIFA STARS na timu ya Taifa ya KENYA,HARAMBE STARS utachezwa kwenye dimba la UHURU na sio kwenye dimba la TAIFA kama ilivyokawaida ya michezo mingine ya TAIFA STARS.

Msemaji wa shirikisho la soka hapa nchini FLORIAN KAIJAGE amesema hakuna tatizo lolote lilofanya mchezo huo ukafanyike kwenye dimba la UHURU bali ni mpangilio tu wa TFF kama wasimamizi wakuu wa mchezo huo.

Mchezo huo utachezwa siku ya jumatano AUGUST 11 ambayo ni siku ya michezo ya kimataifa kama ilivyo kwenye karenda ya FIFA ambapo TAIFA STARS itaingia dimbani ikiwa na kocha mpya JAN PAULSEN toka DENMARK alieanza kuinoa timu hiyo toka wiki iliyopita.

Katika hatua nyingine wachezaji watatu wa TANZANIA wanaocheza soka la kulipwa nje ya nchi wanatarajiwa kuwasili jumanne wiki hii kwaajili ya mchezo huo.

Wachezaji hao ni NIZAR KHALFAN anacheza soka nchini CANADA,DANY MRWANDA anaecheza soka nchini VIETENAM na HENRY JOSEPHA anaecheza soka nchini NORWAY wakati mlinzi IDRISA RAJABU anaecheza soka nchini KENYA yeye alishawasili toka jumapili.

SHINDANO LA MISS TANZANIA SEPTEMBER 11 WAREMBO 31 KAMBINI AUGASTI 16

HASHIM LUNDENGA MWAANDAAJI WA MISS TANZANIA.

Mashindano ya urembo ya VODACOM miss TANZANIA 2010 yatafanyika Septemba 11 mwaka huu Jijini DSM huku warembo thelathini na moja waliochaguliwa katika kanda zote zilizoandaa mashindano hayo wanatarajia kuingia kambini .

Akizungumza Jijini DSM mkurugenzi wa miss TANZANIA HASHIM LUNDENGA amesema kuwa shindano la mwaka huu litakuwa la aina yake na litaandaliwa tafauti na miaka ya nyuma

LUNDENGA amesema kuwa mwaka huu kumekuwa na ushindani mzuri katika ngazi mbali mbali za mashindano hayo hivyo wanatarajia katika fainali atapatikanana mrembo ambaye ataweza kuwakilisha nchi vyema katika mashindano ya dunia.

Amesema licha ya kuingia kambini katika kipindi cha mfungo wa ramadhani lakini warembo hao wataweza kuendeela na ibada zao kama kawaida

KIPA NAMBA MOJA WA SIMBA JUMA KASEJA HATIHATI KUCHEZA MECHI YA NGAO YA HISANI


Mchezaji wa timu ya simba juma kaseja ambaye pia ni mchezaji wa timu ya taifa ambaye ameitwa baada ya kocha mpya jan kuanza kazi hivi karibu,huenda asicheze katika mechi ya ngao ya hisani na wahasimu wao yanga baada ya kuumia mkono katika mazoezi ya timu ya taifa.

Kaseja atajiona mtu mwenye bahati mbaya kutokana na kuchaguliwa kwa mwaka huu katika timu ya taifa lakini ndani ya siku chache kaseja ameumia mkono

Msajili John Tendwa aliasa Baraza la Vyama vya Siasa!!

Benjamin Sawe Maelezo Dar es Salaam.
Msajili wa Vyama vya Siasa John Tendwa ameliasa Baraza la Vyama vya Siasa kuhakikisha uchaguzi wa mwaka huu unakuwa wa Kidemokrasia na wa amani.
Bwana Tendwa alisema hayo jana (leo) jijini Dar es Salaam wakati akifungua mkutano wa kwanza wa Baraza la vyama vya siasa ambapo alilitaka Baraza lililoundwa kisheria kuishauri serikali na jamii hasa katika kipindi cha uchaguzi.
Aidha alisema Baraza hilo si la kujitolea bali limeundwa kwa mujibu wa sheria na linawajibika kwa serikali na ni mshairi mkuu wa serikali katika shughuli za kisiasa. Alisema ni wajibu kwa baraza hilo kuhakikisha uchaguzi unafanyika kwa amani na utulivu na alilitaka baraza hilo kutoa tamko kulaani vitendo vinavyovunja amani na sheria ikiwa ni pamoja na kukemea vyama vya siasa vilivyoanza kampeni kabla ya tarehe ya kampeni.
Pia alivionya vyama vya siasa kuachana na siasa za kutumia lugha ya matusi wakati wa kampeni na ni wajibu wa Baraza hilo kutoa miongozo mbalimbali ambayo itafuatwa na vyama vya siasa.. Bwana Tendwa alilitaka Baraza hilo kuitisha mikutano ya mara kwa mara ambapo itatoa miongozo ambayo italiweka taifa katika mahala pazuri ili kufanikisha uchaguzi kwa amani na utulivu.
Alisema baadhi ya vyama vya siasa vimeanza kapeni kabla ya uchaguzi na vinajua kufanya hivyo ni kukiuka sheria za uchaguzi na moja ya athari za kuanza kampeni kabla ya uchaguzi ni kuwekeana pingamizi na kama likikubalika chama kitakuwa hakina mgombea hivyo amevitaka vyama kufuata taratibu na sheria za uchaguzi.
Akitoa shukrani kwa niaba ya Baraza hilo Mwenyekiti wa Baraza hilo Dr.Emanuel Makaidi amesema hawatamuogopa mwanasiasa au chama chochote cha siasa kitakachokiuka maadili kwani Baraza hilo limeundwa kwa mujibu wa kanuni na sheria. Dr. Makaidi alisema Baraza hilo litakuwa mshauri mzuri wa Serikali katika mambo ya kisiasa hasa katika kipindi cha uchaguzi.

THE DON HIMSELF

Karibuni sana kwenye blog hii ya kijamii iliyosheheni makila kitu kuanzia siasa uchumi afya na burudani kwa ujumla wake.uingiapo kwenye blog hii ni mengi ambayo utapata nafasi ya kukutana nayo,kumbuka mawazo yako ndo hasa yanayojenga na kunifanya niwe na ufanisi zaidi.kariiiiiiibuuuuuuuuuuuu saaaaaaaaaaaaaaanaaaaaaaaaa.(THE DJ HIMSELF-JIWE)

Followers

BLOG ZA MARAFIKI

Search This Blog

ZILIZOPITA

DUNIA MUZIMA