Sep 26, 2010

ziara ya mama salma kikwete mkoani lindi

Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya wanawake WAMA Mama Salma Kikwete katika ziara yake ya uhamasishaji wanachama wa UWT Mkoa wa Lindi kujitokeza kwa wingi kupiga kura wakati wa Uchaguzi Mkuu wa rais, wabunge na madiwani oktoba 31 mwaka huu nchini Hapa likuwa akimnadi Mgombea ubunge Lindi mjini kupitia CCM Bw. Mohamed Abdulaziz.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akimnadi mgombea Ubunge jimo la Mchinga Lindi vijjini Sulemani Mtanda
Mzuka unapopanda! mwachama wa UWT Lindi mjini akifurahia hotuba ya Mama Salma Kiwete wakati wa mkutano Lindi mjini
Umeyaona mambo ya vuvuzela! mwenye macho haambiwi tazama. hadi Lindi vijijini yapo pia.
Wanachama Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Lindi mjini wakimsikiliza Mke wa Rais Mama Salma Kikwete wakati alipokuwa akiwahutubia.Picha na Mwanakombo Jumaa

dr. bilal mkoani kagera


Mgombea Mwenza wa Urais Kupitia tiketi ya CCM, Dk. Mohamed Gharib Bilal, akimvisha kofia yake msanii mlemavu, Athuman Yunus, baada ya kufurahishwa na staili zake za uchezaji wa ngoma ya kabila la Kihaya, wakati wa mapokezi yake alipokuwa akiingia Kijiji cha Ruzinga Kanyigo Wilaya ya Misenyi Mkoa wa Kagera kufanya mkutano wa kampeni jana.
Mgombea Mwenza wa Urais Kupitia tiketi ya CCM, Dk. Mohamed Gharib Bilal, akifurahia staili za msanii mlemavu, Athuman Yunus, aliyekuwa akicheza ngoma ya kabila la Kihaya,wakati wa mapokezi yake alipokuwa akiingia Kijiji cha Ruzinga Kanyigo Wilaya ya Misenyi Mkoa wa Kagera kufanya mkutano wa kampeni jana.

Mke wa Mgombea Mwenza wa Urais wa CCM Bi Zakia Bilal, akicheza wimbo wa kabila la Kihaya na Msanii Bahati Ibrahim, aliyekuwa akitoa burudani wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika kwenye Uwanja wa Mashujaa wa Mayunga Mjini Bukoba jana .

Sep 25, 2010

Jk Aifunika musoma uwanja wa Mkendo!!

nMgombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia maelfu ya wananchi wa Musoma Mjini kwenye mkutano mkubwa wa kampeni leo tarehe 25.09.2010
Malefu ya wakazi wa mji wa Musoma wakimkaribisha mjini Musoma mgombea Urais kwa tiketi ya CCM Dr.Jakaya Mrisho Kikwete wakati alipowasili katika viwanja vya Mkendo mjini Musoma na kuwahutubia katika mkutano mkubwa wa kampeni(picha na Freddy Maro)

Maalim Seif aahidi kupunguza kodi zanzibar


Mgombea Urais wa Zanzibar kwa tiketi ya CUF, Maalim Seif Sharif Ahmad


Na Mauwa Mohammed, Zanzibar

MGOMBEA wa urais wa Zanzibar, kwa tiketi ya Chama cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Sharif Hamad, amesema kama akichaguliwa kuwa rais wa Zanzibar, ataangalia upya viwango vya kodi ikiwa ni pamoja na kuvipunguza viwango vya ulipaji kodi ili kuvutia wawekezaji na wafanyabiashara wengi zaidi.

Alisema utozaji kodi kwa kiwango kidogo kutawavutia wawekezaji wa ndani na nje kuwekeza Zanzibar na kwamba uwekezaji huo pia utawanufaisha Wazanzibari wote tufauti na ilivyo hivi sasa ambapo wengine wamekuwa wakikwepa kuilipa.

Ahadi hiyo ameitoa leo hii alipokuwa akizungumza na wajasiriamali kwenye mkutano uliofanyika kwenye ukumbi wa Shule ya Sunni Madrassa Mkunazini Mkoa wa Mjini Magharibi.

Alisema wafanyabiashara wadogo wadogo wanapaswa kusaidiwa na kuongezewa ujuzi ili waweze kuingia katika ushindani wa biashara ambapo Tanzania imeridhia kuingia kwenye soko la pamoja katika Jumuiya ya Afrika Mashariki.

“Nchi yoyote inayoendelea duniani, haiwakomoi wananchi wake katika kodi na badala yake inawawekea viwango vya chini, ili wazidi kuongezeka na mimi nitapunguza viwango vya ulipaji wa kodi kama mkinichagua kuingia ikulu,’’ alisema.

Maalim Seif, aliongeza kuwa Serikali ya Umoja wa Kitaifa itakayoongozwa na CUF haitaruhusu wawekezaji matapeli wenye lengo la kunufaika kupitia migongo ya wananchi, bali itaruhusu wawekezaji ambao watainufaisha Zanibar na wananchi wake.

Alisema hawezi kuruhusu mtu kunufaika kwa gharama za Wazanzibari, lazima wawekezaji wenye tabia kama hiyo watawajibishwa kwani kuwaadhibu wananchi kwa kuwatetea wageni ni kosa na ni kuwadharau wananchi wazalendo.

“Mimi siamini kuwa kodi kubwa au utitiri ndio msingi wa maendeleo ya nchi, pia siamini kuwakamua wafanyabiashara wadogo wadogo ndiko kujenga nchi, naamini wafanyabiashara hawa wanatakiwa kusaidiwa ili wajiendeleze katika biashara zao,” alisema.

Aliongeza kuwa akiingia madarakani atahakikisha mafunzo kwa wajasiriamali yanatolewa kwa kiwango cha juu ili kuwajenga uwezo wa kufanya biashara zao kwa ufanisi zaidi kwa lengo la kukuza kipato chao.

Alisema wafanyabiashara wengi hususan wadogo wadogo wamekuwa wakifanya kazi zao kwa utundu, lakini wakipatiwa mafunzo watapiga hatua kubwa zaidi na taifa linanufaika.

DK. BILAL AVUNA KADI LUKUKI ZA WAPINZANI BUKOBA


Mgombea Mwenza wa urais kupitia tiketi ya CCM, Dr. Mohamed Gharib Bilal akiwahutubia wananchi wa Kijiji cha Mabila Wilaya mpya ya Kyelwa Mkoa wa Kagera, wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika kijijini hapo jana Sept 24 na kumnadi mgombea wa Ubunge wa Jimbo la Karagwe, Rustas Katagila.
Mgombea Mwenza wa urais kupitia tiketi ya Chama Cha Mapinduxi CCM, Dk. Mohamed Gharib Bilal, akipokea kadi za waliokuwa wanachama wa Vyama vya TLP, CHADEMA na CUF waliotoka katika Kata mpya ya Lukula, ambao walifika katika mkutano wa kampeni uliofanyika Kijiji cha Mabila Wilaya ya Karagwe Mkoa wa Kagera jana Sept 23, ambapo jumla ya wanachama 144 kutoka vyama vya upinzani walitarajia kurejesha kadi zao na 14 kati yao walikabidhi kadi hizo kwa mgombea mwenza.

wanja la dr. kikwete na dr. bilal




Habari zenu Ndugu wapendwa,

Tunayofuraha kubwa kuwafahamisha ya kwamba tovuti maalumu na rasmi ya Mhe. Jakaya M. Kikwete na Dr. M. Gharib Bilal sasa inapatikana kwenye mitandao:


Tembelea tovuti hii maalumu ya Mgombea Uraisi na Mgombea Mwenza kwa tiketi ya CCM mwaka 2010 upate habari mbalimbali kama:

· Wasifu wa Wagombea – Mhe. Jakaya M. Kikwete na Dr. Mohammed Gharib Bilal.

· Mafanikio katika sekta mbalimbali.

· Sera na Malengo 2010 – 2015.

· Ratiba za kampeni.

· Hotuba maalumu.

· Matoleo ya Habari.

· Video na picha.

· Mitandao ya Facebook,Twitter na Youtube.

Kupitia tovuti hii na mitandao yake utaweza kupata taarifa mbalimbali na kutoa maoni yako.

“ PAMOJA TUZIDI KUSONGA MBELE”

Sep 24, 2010

P - FUNCK ATOA UFAFANUZI

P-Funk aka Majani ameizungumzia issue yake na Afande (Live kwenye Powerjamz Show - East Africa Radio) na kusema kuwa ni kweli Afande Sele alikua ana ngoma kwake lakini alikua hajamalizia kuilipia na jana ndio alikuja ghafla tena usiku na kuilipia but Afande alikua anaitaka fasta ili akai-release kwenye radio ila Majani alikua ana ratiba zake nyingine....So alikua hajambonji almost wiki nzima na alikua amekunywa dawa na kupumzika kidogo na ndipo Afande alipotinga na kutaka track yake ili akaiachie kwenye show. ......Kwa mujibu wa P-Funk sababu ya kumpiga "tena kibao tu" Afande ni kuwa alipotoka nje alimkuta Simba Dume akila "Cha Arusha" nje ya geti lake...na Majani ametamka kuwa hana noma wakae pamoja then wayamalize wala si lazima yafike "kwa kova"! KINACHOONEKANA HAPA NI KUWA HAKUNA BEEF,BALI NI LUGHA GONGANA TU BAINA YAO!
Kuna mtafaruku umetokea kati ya Afande Sele na Producer P-Funk wa Bongo Records mida hii ya mchana (Ijumaa) na Afande kupigwa na kwa mida hii amechukua RB kwa ajili ya kumfikisha Majani kwenye kwenye vyombo vya sheria. ......Ishu kwa mujibu wa Afande Sele ni hivi Afande alitoka Moro jana usiku akiwa na Ferooz na kumpatia Majani mkwanja kwa ajili ya kumalizia ngoma na kuambiwa aje leo (Ijumaa) kuchukua ngoma yake na alipofika kuchukua singo kwa mujibu wa Afande,Majani alimwambia yuko bize na kuanza kumpa kipondo!!!!(kwa hisani ya chini ya carpet blogspot.)

SERIKALI KUDHIBITI WAGANGA NA WAKUNGA WA TIBA ASILIA WANAKIUKA SHERIA!!

MAGRETH KINABO NA ARON MSIGWA- MAELEZO

SERIKALI imeagiza kuwa kila halimashuri ya wilaya,miji, manispaa na majiji iwe na Mratibu wa Tiba Asili ambaye atakuwa msimamizi wa masuala ya hayo, ikiwa ni hatua ya kuwadhibiti watoa huduma wa tiba hiyo watakaokiuka sheria.

Kauli hiyo ilitolewa jana na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda katika hotuba yake iliyosomwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Blandina Nyoni kwa niaba yake wakati uzinduzi wa usajili wa waganga wa tiba asili nchini.

“Mratibu huyu awe ni mfanyakazi katika idara ya afya aliyechini ya Mganga Mkuu wa Halimashauri husika,” alisema Waziri Mkuu Pinda.

Waziri Mkuu alisema hayo huku akiagiza kuwa waganga wanaofanya matendo yanayohatarisha uhai wa watu yanayohusisha waganga wa tiba asili ambayoni uuaji wa vikongwe, albino, watoto wadogo na uchunaji wa ngozi za binadamu kuwa hawatakuwa sehemu ya wizara hiyo.

“Yeyote atakayebanika kujihusisha na vitendo hivyo, wizara haitamtambua kuwa ni mganga na hivyo hatasajiliwa na kuruhusiwa kutoa huduma ya asili,” alisisitiza huku akisema waganga na wakunga na hasa waganga wa tiba asili nchini wanatakiwa kuzingatia sheria, kanuni na miongozo yakiwemo maelekezo mbalimbali ya wizara hiyo.

Aliongeza kuwa waganga hao wanatakiwa kuanzisha vituo rasmi, kutoa huduma kwa mfumo wa kitaasisi na si mtu mmojammoja , kutayarisha dawa katika mazingira safi kujiendeleza kielimu na kuanzisha vitalu na mashamba ya miti dawa ili kuhifadhi dawa na mazingira ikiwemo kutunza kumbukumbu.

Akizungumzia kuhusu usajili huo, Mganga Mkuu wa Serikali, Dk. Deo Mutasiwa alisema waganga na wakunga wa tiba asili wataruhusiwa kusajiliwa kwa mujibu wa sheria namba 23 ya mwaka 2002 na kanuni zake. Hivyo watakaokiuka wataadhibiwa kwa mujibu wa sheria.

Dk. Mutasiwa aliongeza suala la usalama wa dawa za tiba hizo litasimamiwa na Serikali chini , Mamlaka ya Chakula na Dawa nchini (TFDA), lakini la kuhusu jukumu la dawa na jinsi inavyofanya kazi litakuwa na mwenyewe dawa .

Na Mwakilishi Shirika la Afya Duniani Tanzania (WHO) Dk. Rufaro Chatora, alishauri wanasayansi kufanya utafiti wa dawa za asilia ili kuboresha huduma hiyo. Pia utafiti wa dawa hizo ukishirikisha na ule dawa za kisasa ufanyanyike ili kuimarisha na kuendeleza huduma hizo kwa kisasa.

AFANDE ACHEZEA KICHAPO TOKA KWA MAJANI


Kuna mtafaruku umetokea kati ya Afande Sele na Producer P-Funk wa Bongo Records mida hii ya mchana (Ijumaa) na Afande kupigwa na kwa mida hii amechukua RB kwa ajili ya kumfikisha Majani kwenye kwenye vyombo vya sheria. ......Ishu kwa mujibu wa Afande Sele ni hivi Afande alitoka Moro jana usiku akiwa na Ferooz na kumpatia Majani mkwanja kwa ajili ya kumalizia ngoma na kuambiwa aje leo (Ijumaa) kuchukua ngoma yake na alipofika kuchukua singo kwa mujibu wa Afande,Majani alimwambia yuko bize na kuanza kumpa kipondo!!!!

P.Funk kapigiwa simu now ikiwa ONLINE East Africa Radio na kusema kuwa amelala wampigie baadae, na nia yakumpigia ni kwamba walitaka kujua upande wa pili wa P.Funk.
(Kwa niaba ya NAY WA MITEGO aliyeshuhudia chezo pale bongo recordz)

NITATEKELEZA ILANI YA CCM KWA KASI ZAIDI, NGUVU ZAIDI NA KUWAPA VIJANA AJIRA,MO DEWJI…!!!

MO akihutubia wananchi wa Kata ya Unyambwa.

*******************

Na Hillary Shoo.

Singida. Mgombea ubunge kwa tiketi ya CCM, Mohamed Gulam Dewji, amesema endapo wananchi watampa ridhaa ya kuendelea kuwawakilisha tena bungeni, atatekeleza Ilani ya CCM kwa kasi zaidi ikiwemo kutafuta ufumbuzi wa namna ya kupunguza upungufu wa ajira kwa vijana.

Dewji alisema katika ilani uchaguzi, CCM imeainisha wazi kwamba inatambua tatizo la ajira na hasa ajira ya vijana wanaomaliza elimu ya msingi, sekondari na vyuo vikuu kila mwaka kuwa, ni kubwa mno.

“Vijana hawa wote ni nguvu kazi ya taifa ambayo inaweza kutumika katika kazi na shughuli halali za ujenzi wa nchi yetu na ikapiga hatua kubwa ya kimaendeleo”,alisema Dewji.

Mgombea huyo,alisema ili kukabiliana na tatizo hilo, CCM ina mpango wa kupanua mafunzo ya VETA yaweze kuchukua vijana wengi zaidi, ili waandaliwe kujiajiri wenyewe.

Aidha, alisema vijana watahamasishwa kuanzisha miradi ya kiuchumi na kujiunga katika vikundi vya ushirika vya kuweka na kukopa (SACCOS) ili waweze kupata mikopo kwa masharti nafuu.

“Katika miaka mitano iliyopita, nimewatafutia kazi vijana kutoka jimboni kwetu kwenye kiwanda changu cha nguo cha Afritex kilichopo mkoani Tanga., Kuajiri vijana hao, nimefanikiwa kwa kiasi fulani kupunguza idadi ya vijana wetu wanaomaliza elimu ya sekondari, kukaa vijiweni”,alisisitiza huku akishangiliwa na mamia ya wananchi.

Dewji aliyasema hayo jana katika mkutano wa Kampeni zake, uliofanyika kwenye viwanja vya shule ya msingi Unyambwa.

Wakati huo huo,Dewji alitumia fursa hiyo kumwombea kura mgombea urais Jakaya Kikwete kwa madai kwamba ameonyesha uwezo mkubwa wa kusimamia utekelezaji wa ilani za uchaguzi. Aidha, alimnadi mgombea wa udiwani wa kata hiyo, ya Unyambwa Salum Satu na kuomba apewe kura za kutosha kumwezesha kushika nafasi hiyo.

MO, akisistiza kuwa Katika kipindi cha miaka saba michezo imeweza kupaa katika mkoa wa Singida ambapio Kindai Shooting Stars, timu ya mkoa ilibeba kombe la kilimanjaro Taifa Cup kwa mara ya kwanza katika historia ya mkoa huo.

MO akizcheza ngoma ya Kinyaturu ya kutikisa mabega, maarufu kwa jina la tikisa mabega tingisha kiuno.

Wanafunzi wa shule ya msingi Unyambwa wakimpokea MO kwenye viwanja vya shule hiyo wakati alipokwenda kweye mkutano wa kampeni wa Kata hiyo.

Wanafunzi wakiwa na mabango yanayomnadi MO huko KatikaKata ya Unyambwa.

Visura 10 kuonesha mavazi yaliyooneshwa na Mustafa Hassanali nchini Cameroon February na Zanzibar Julai 2010.

Mwanzilishi na muandaaji wa jukwaa la wanawake wajasiriamali Tanzania (TWENDE ) na Jukwaa la kukuza vipaji vya wabunifu chipukizi Swahili Fashion Week, ambae pia ni mbunifu maarufu wa mavazi, Mustafa Hassanali amealikwa kuwa mgeni rasmi katika maonyesho ya mavazi yanayofanyika jijini Arusha kwa muda wa siku mbili tarehe 23 na 24 ya mwezi huu katika hoteli ya New Arusha.

Maonyesho hayo yameandaliwa na Maridadi. Maridadi ni kikundi kinachojumisha wanawake watatu kutoka mataifa tofauti ya Tanzania, Austarialia na Uholanzi ambao wanaishi nchini katika jiji la Aruha na kujishughulisha na masuala mbalimbali yanayohusiana na mendeleo ya mwanamke..

Akielezea lengo la kuandaa maonyesho hayo, mmoja wa wanawake hao, Lilian Bulengo

amesema kuwa “dhumuni kuu la kuandaa tukio hili linalojulikana kwa jina la “Maridadi Women Show” ni kuwakutanisha pamoja wanawake kutoka maeneo tofauti ya Arusha na Moshi katika Fashion Show, maonyesho ya biashara pamoja na kupata fursa ya kuzungumza mambo mbalimbali yanayowakabili wanawake katika maisha ya kila siku hapaTanzania ikiwemo suala la unyanyasaji wa kijinsia na ubakaji, wanawake na kuondokana na utegemezi na masuala ya uchumi na biashara kwa ujumla”.

Mustafa Hassanali, pamoja na kuwa mgeni rasmi, pia ataonyesha mavazi ambayo kwa mara ya kwanza alionyesha nchini Cameroon mezi wa 2 mwaka huu katika show iliyojulikana kama PARFUM D’AMOUR, na mavazi yanayojulikana kwa jina la Karafuu collection aliyoyaonyesha julai 2010 Zanzibar.

Jumla ya visura 10, kati yao nane kutoka Dar es salaam na wawili kutoka Arusha watapita jukwaani na kuonyesha mavazi hayo ya Mustafa Hassanali, ambayo yanawavutia wengi kutoka na ubunifu wa hali ya juu.

“Nimefurahi sana kupata fursa ya kuwa mgeni rasmi katika tukio hili, pia kuonyesha nguo zangu ambazo zilipendwa sana Cameroon, naamini pia wakaazi wa Arusha watafurahia kazi yangu” . Alisema Hassanali.

Katika maonyesho haya Mustafa ataonyesha na wabunifu wengine kutoka Arusha ambao ni Shwari Collectables,Hanifa Hash na Woolworth.

Mbali na maonyesha hayo pia siku ya jumamosi kutakuwa na manyesho ya kibiashara yatakayojumuisha kazi mbalimbali za sanaa za mikono. Benki nazo zitapata fursa ya kuonyesha na kuelezea shughuli zao mbalimbali wanazozifanya hasa katika kuchangia maendeleo ya wanawake Tanzania.

Sep 23, 2010

WAZIRI MKUU MIZENGO PINDA NA MATUKIO KATIKA PICHA NEW YORK

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisalimiana na Waziri Mkuu, wa Saint Vincent and Grenadines, Dr. Ralph Gonsalves kabla ya mazungumzo yao kwenye ukumbi wa Umoja wa Mataifa, New York Septemba 23, 2010. Wote wanahudhuria mkutano wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na Rais Yoweri Museveni wa Uganda (kulia) na Waziri MKuu wa Saint Vincent and Grenadines, Dr. Ralph Gonsalves katika kikao cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, New York Septemba 23, 2010. (Piocha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

TANZANIA NI NCHI YA KUPIGIWA MFANO KWA UTAWALA BORA NA DEMOKRASIA: OBAMA!

Na Mgaya Kingoba, Mbarali MAREKANI imesema kwamba Tanzania ni moja ya nchi inazozipigia mfano miongoni mwa nchi zinazoendelea, kwa uongozi bora na unaodumisha utawala bora na utawala wa sheria. Kwa mujibu wa Rais Jakaya Kikwete, Rais Barack Obama wa Marekani aliyasema hayo juzi wakati akihutubia mkutano wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa (UN) jijini New York, nchini humo. Rais Kikwete alisema wakati akihutubia mkutano mkubwa wa kampeni kwenye Uwanja wa Barafu mjini Rujewa wilayani hapa katika Mkoa wa Mbeya, kuomba kura kwa wananchi wa wilaya hiyo. Alisema muda mfupi kabla ya kuhutubia maelfu ya wananchi uwanjani hapo, alizungumza na Balozi wa Marekani nchini, Alfonso Leonhadt, na kumuelezea jinsi Rais Obama alivyoimwagia sifa Tanzania katika hotuba yake UN. “Kabla ya kupanda hapa jukwaani kuzungumza nanyi, mliniona nazungumza na simu…alikuwa Balozi wa Marekani, ananiuliza kama nimesikia hotuba ya Rais Obama jana usiku kwenye Umoja wa Mataifa,” alisema Rais Kikwete. “Nikamwambia niko huku nahangaika, nitasikia saa ngapi? Wakati mwingine niko hoi bin taaban hata kusikiliza redio au televisheni huna muda. “Ameniambia kuwa Rais Obama ameeleza misingi ya Marekani kusaidia nchi zinazoendelea, na mfano wake akatoa Tanzania. Akasema nchi yetu inaongoza kwa kujali utawala bora, utawala wa sheria, kuheshimu NGO,s, na tunatawala vizuri,” Rais Kikwete aliwaeleza wananchi. “Kama siyo mimi na akina Mwandosya, nani mwingine anayemsifu,” alisema Rais Kikwete akimtaja Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Profesa Mark Mwandosya, ambaye alikuwapo kwenye mkutano huo akiwa ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM (NEC) kupitia Mkoa wa Mbeya. Alisema kauli hizo za Marekani kuisifu Tanzania, hazitoi yeye, lakini kila anapofanya hivyo, baadhi ya watu huhoji kwani kila mara na Marekani. “Nikisema sifa hizi zinazotolewa na Marekani, watu wanasema, ‘huyu naye na Marekani kila siku.’ Wanasema wenyewe, siyo mimi,” alifafanua Rais Kikwete. Marekani imekuwa mshirika mkubwa wa maendeleo kwa Tanzania tangu Rais Kikwete aingie madarakani miaka mitano iliyopita, ikitoa ufadhili mkubwa katika miradi mbalimbali ya sekta za elimu, afya, miundombinu na nishati. Chini ya Shirika la Milllennium Challenge (MCC), Marekani itafadhili miradi ya umeme katika mikoa sita nchini; itajenga barabara kadhaa ikiwemo ya Tunduma- Laela- Sumbawanga na hivi karibuni ilitoa vitabu 800,000 kwa ajili ya shule za sekondari nchini hasa kwa masomo ya sayansi.

KALUNDE BAND YAENDELEA NA MAANDALIZI YA SAFARI YA MSUMBIJI!!

Mmoja wa wafadhili wa Bendi ya Kalunde Linus Mbanga (VIP) kulia akiteta jambo na rais wa bendi ya Kalunde Deo Mwanambilimbi wakati wa mazungumzo yao yaliyofanyika kwenye Hoteli ya New Africa ikiwa ni mikakati na mipango ya maadalizi ya safari ya bendi hiyo kwa ajili ya safari yao ya kuelekea nchini Msumbiji katika jiji la Maputo kwa ajili ya maonyesho kadhaa nchini humo.

Deo amesema “Tumepata mwaliko wa kwenda kutumbuiza nchini Msumbiji kwenye moja ya tamasha ambalo hufanyika kila mwaka hivyo tunatarajia kwenda kupiga nyimbo zote za Kalunde” alisema Mwanambilimbi.

Alisema mwaliko huo umekuja baada ya baadhi ya mashabiki wa bendi hiyo kuvutiwa na nyimbo wanazopiga.

Kalunde kwa sasa inatamba na nyimbo za ‘Itumbangwewe’, ‘Hilda’, ‘Nataka Kuzaa na Wewe’ , ‘Usiniguse’ ,’Fikiria’ na ‘Kilio Kilio’.

Pia imetoa vibao viwili vipya ambavyo ni ‘Fungua’ na ‘Maiwane’ ambazo tayari zimeanza kutamba katika kumbi za burudani ambazo bendi hiyo inapopiga.

Baadhi ya wanamuziki watakaoondoka na bendi hiyo ni Mwanambilimbi mwenyewe, Shehe Mwakichui, Junior Gringo, Deborah Nyangi, Sarafina Mshindo, Mwapwani Yahya, Othman Majuto na Remmy.

Rais wa Bendi Deo Mwanambilimbi akiimba katika moja ya maonyesho yao yanayofanyika kila alhamisi kwenye Hoteli ya New Africa jijini Dar es salaam.
Debora Nyange mmoja mwa wanamuziki watakaoondoka katika safari hiyo.
Mwanamuziki Junior Gringo akiim ba katika onyesho lao lao jioni kwenye Hoteli ya New Africa.
Edson Alen mpiga solo wa bendi ya Kalunde

Wateja wa Vodacom sasa kuneemeka na punguzo la bei

Ni kupitia programu ya Tuzo Pointi

Dar es Salaam, Kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom Tanzania imezindua programu mpya ya Tuzo Pointi ambayo itawawezesha wateja wake kupata punguzo kubwa la bei wakati wakipata huduma katika sehemu mablimbali kama mahotelini, ofisi za bima na madukani.

Mkuu wa Idara ya Mahusiano ya Wateja, Aika Matiku alisema kwamba huduma hiyo itawawezesha wateja wake kupata punguzo la kati ya asilimia 5 hadi 20 kutoka kwa wauzaji mbalimbali wa bidhaa hapa nchini.

Aliwataja baadhi ya watoaji wa huduma ambao wataanza nao kuwa ni duka la Woolworth, Sunrise Beach Resort na kampuni ya Bima ya Real Insurance. Hoteli za Kunduchi Beach Resort na Zanzibar Beach Resort zitaanza kutoa huduma baada ya kukamilisha taratibu.

Alisema wateja wanaoweza kupata punguzo hilo kubwa ni wale wenye pointi 250 za Tuzo na kuendelea.

“Tumeanzisha huduma hii kwa lengo la kuhakikisha kwamba wateja wetu wanapata huduma bora na kwa bei nafuu,” alisema.

Alisema huduma hiyo ni sehemu ya programu ya Tuzo Pointi ambayo lengo lake ni kuwazawadia wateja wake waaminifu na kuboresha maisha ya wateja wake.

Alisema mteja anapata pointi kwa njia kuu tatu. Moja ni kwa utumiaji ambapo wateja wa malipo ya kabla watakapotumiaSh 100 na wale wa malipo ya baada watakapotumia Sh 500 wote watapata pointi moja ya Tuzo.

Njia ya pili ni kwa kuongea, akifafanua njia hii alisema mteja akipokea simu kutoka mtandao mwingine atapata pointi moja ya Tuzo

Njia ya tatu ni ile ya mteja wa Vodacom atakapoendelea kuwa mteja wa Vodacom kwa wiki moja huku akitumia simu yake kwa kupokea simu, kupiga, kutuma ujumbe wa maneno au kupokea ujumbe wa maneno atapata pointi nyingine moja ya Tuzo

Alisema kwa wateja wa mikoani wataweza kupata huduma wakiwa huko huko kutoka kwa vituo mbalimbali vya huduma na maduka vilivyoko mikoani.

NI JAMBO JEMA KUWASAIDIA WENYE SHIDA!!

Mgombea Urais wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete, akiwa ameketi chini ardhini ili kumsikiliza Mama Sara Mageni wa Wilaya ya Makete, wakati mgombea huyo alipowasili kuhutubia mkutano wa kampeni. Sara alikuwa akitoa shukrani zake kwa Mheshimiwa Kikwete baada ya kumnunulia Bajaj ili kurahisisha shughuli zake, alipotembelea wilaya hiyo mwaka jana

Hifadhi yaTabaka la Hewa ya Ozoni Mwanza!!

Evelyn Mkokoi

Afisa Habari, Ofisi ya Makamu wa Rais

Serikali inakabiliana na changamoto kubwa ya wananchi kutokuelewa suala zima la sayansi ya hifadhi ya tabaka la hewa ya Ozoni.

Hayo yameeelezwa leo na Mkurugenzi wa Idara ya Mazingira kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais Dkt Julius Ningu, katika kilele cha maadhimisho ya Siku ya kimataifa ya hifadhi ya tabaka la Hewa ya Ozoni yanayofanyika kitaifa mjini Mwanza yanayoambatana na uzinduzi wa kituo na mafunzo ya kunasa na kusafisha gesi chakavu za majokovu na viyoyozi.

Dkt Ningu ameeleza kuwa changamoto hii ndo imepelekea serikali kusogeza huduma hii kwa karibu zaidi kwa jamii kwa kupitia mafunzo haya kwa walengwa ambao ni wanafunzi wa chuo cha veta, mafundi mchundo, mafundi mekanika na mafundi wa kawaida.

Akisoma hotuba ya ufunguzi, kaimu katibu tawala wa wilaya ya Njamagana Bw.Elias Makori ameeleza kuwa matumizi ya kemikali haribifu kwa tabaka la hewa ya Ozoni yanatumika zaidi katika nchi zinazoendelea kama vile Tanzania na yanaweza kuleta madhara makubwa sana kwa jamii ikiwa ni pamoja na magonjwa ya saratani ya ngozi, na ugonjwa wa mtoto wa jicho.

Bw. Makori ameeleza kuwa kituo cha veta mkoani Mwanza ni miongoni mwa vituo vitano vya kikanda nchini , vinavyolenga katika kutekeleza mpango wa serikali wa kuondosha matumizi kemikali haribifu kwa tabaka la hewa ya Ozoni.

Vituo vingine nchini vitakavyohusishwa na jukumu hili ni pamoja na VETA Dar, Mbeya, Kigoma na Zanzibar. Uhifadhi wa tabaka la hewa ya Ozoni ni utekelezaji wa mkataba wa Vienna na Montrial ambayo Tanzania ni nchi mwanachama.

Ujumbe wa mwaka huu unasema, ‘Hifadhi ya Tabaka la Hewa ya Ozoni “Tuzingatie Wajibu na Majukumu yetu.”

WADAU WA SEKTA YA NISHATI WAKUTANA KUJADILI CHANGAMOTO ZA UZALISHAJI UMEME NCHINI.

Kamishina wa Nishati na Petroli wa Wizara ya Nishati na Madini Injinia Bashir Mrindoko akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari kuhusu mkutanao wa mwaka wa wadau wa sekta ya Nishati unaojadili namna kukabiliana na changamoto zinazokwamisha maendeleo ya sekta nishati nchini leo jijini Dar es salaam.
Picha na Aron Msigwa – MAELEZO.

Wadau wa Sekta ya Nishati nchini wakifuatilia masuala mbalimbali wakati wa mkutano wa mwaka wa kupitia maendeleo ya sekta ya nishati nchini leo jijini Dar es salaam ambapo sekta ya nishati imeguswa kwa kufanyiwa maboresho ya uongezaji wa idadi ya watumiaji wa nishati ya umeme kutoka 14% mpaka kufikia 75% ifikapo mwaka 2033 pamoja na kuongeza idadi ya wateja wapya wanaounganishiwa umeme majumbani kwa mwaka kutoka idadi ya nyumba 60,000 mpaka kufikia 100,000

Wadau wa Sekta ya Nishati nchini wakifuatilia masuala mbalimbali wakati wa mkutano wa mwaka wa kupitia maendeleo ya sekta ya nishati nchini leo jijini Dar es salaam.

WAZIRI MKUU MIZENGO PINDA AKUTANA NA RAIS WA LIBERIA NA WAZIRI MKUU WA DENMARK!!

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza katika kikao cha kujadili maendeleo ya Millenia alichokiandaa kwa pamoja na Waziri Mkuu wa Denmark, L. Lokke Rasmussen (katikati) na Rais wa Liberia, E. Johnson Sirleaf (kushoto) jijini New York , Septemba 22, 2010.(Picha na Ofisi y a Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza katika kikao cha kujadili maendeleo ya Millenia alichokiandaa kwa pamoja na Waziri Mkuu wa Denmark, L. Lokke Rasmussen (kulia ) na Rais wa Liberia, E. Johnson Sirleaf aliyekaa katikatijijini New York , Septemba 22, 2010.(Picha na Ofisi y a Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda na Rais wa Liberia, E. Johnson Sirleaf wakifuatilia mkutano wa kujadili maendeleo ya millennia waliouandaa wakishirikiana na Waziri Mkuu wa Denmark L. Lokke Rasmussen jijini New York, Septemba 22, 2010. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda na Rais wa Liberia, E. Johnson Sirleaf (katikati) wakizungumza na Waziri Mkuu wa Denmark, L. Lokke Rasmusen baada y kikao walichokiandaa cha kujadili maendeleo ya Millenia kilichofanyika jijini New York Septemba 22, 2010. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

MAMA SALMA KIKWETE AKIWA MKOANI KILIMANJARO!!

Ziara ya Mwenyekiti wa Taasisi ya Maendeleo ya Wanawake (WAMA) Mama Salma Kikwete Mkoani Kilimanjaro kwaajili ya kuwahamasisha wanachama wa UWT kuhusu umuhimu wa kujitokeza kwa wingi siku ya kupiga kura katika Uchaguzi Mkuu wa rais, wabunge na madiwani utakaofanyika Oktoba 31-2010 nchini kote.
Hapa akimnadi mgombea kupitia Chama cha Mapinduzi CCM aliyepita bila kupingwa katika jimbo la Siha Mkoani kilimanjaro Agrey Mwanri.
(Picha na Mwanakombo Jumaa Maelezo)
Mwenekiti wa WAMA Mama Salma Kikwete akmnadi Ugombea ubunge jimbo la Vunjo Chrispin Meela.
Mwenyekiti wa WAMA Mama Salma Kikwete akimnadi mgombea ubunge wa jimbo la Hai mkoani Kilimajaro Fuya Kimbita
Mwenyekiti wa WAMA Mama Salma Kikwete akiwanadi wagombea wa udiwani kupitia chama cha Mapinduzi CCM na mgombea Ubunge wa Hai Kilimanjaro.
Wanachama wa UWT jimbo la Vunjo na Moshi Vijijini wakionyesha mshikamano wao kuelekea Uchaguzi Mkuu wa rais, wabunge na madiwani utakaofanyika Oktoba 31,2010

THE DON HIMSELF

Karibuni sana kwenye blog hii ya kijamii iliyosheheni makila kitu kuanzia siasa uchumi afya na burudani kwa ujumla wake.uingiapo kwenye blog hii ni mengi ambayo utapata nafasi ya kukutana nayo,kumbuka mawazo yako ndo hasa yanayojenga na kunifanya niwe na ufanisi zaidi.kariiiiiiibuuuuuuuuuuuu saaaaaaaaaaaaaaanaaaaaaaaaa.(THE DJ HIMSELF-JIWE)

Followers

BLOG ZA MARAFIKI

Search This Blog

ZILIZOPITA

DUNIA MUZIMA