Ni globu ya kijamii inayojihusisha na mambo yote ya kijamii,natumaini jamii yangu ya kitanzania itafaidika sana pindi ichukuapo fursa ya kuperuzi kwenye globu hii,dhamira yangu ni kufikisha ujumbe pamoja na kuiburudisha jamii yangu na furaha yangu ni kuona natimiza dhamira yangu kwako.natumaini kuwa wewe utaniunga mkono kwa kile ambacho nataka kukifanya kwa ajili ya jamii yangu ya kitanzania.NASHUKURU KWA KUNIELEWA.
Aug 21, 2012
REKODI ZA MBWANA SAMATTA ZAMPANDISHA THAMANI MARA 3 ZAIDIYA SIMBA WALIYOPEWA NA TP: KTK MECHI 7 AFUNGA MABAO 5, MANNE YA KICHWA.
Mbwana Ally Samatta anazidi kung'ara kwenye soka la anga ya kimataifa akiwa na klabu yake ya TP Mazembe.
Mbwana Samatta ambaye tayari anatimiza mwaka mmoja tangu ajiunge na timu yake hiyo ya Kinshasa Congo akitokea klabu bingwa ya Tanzania bara Simba Sports Club, amekuwa mmoja ya wafungaji bora na tegemeo kabisa kwenye timu hiyo inayomilikiwa na tajiri Moise Katumbi.
Kwa takwimu zilizo sahihi kabisa za Mbwana Samatta katika msimu huu 2011/12 upande wa Ligi ya mabingwa wa Afrika amecheza mechi 7 tu.
Katika mechi hizo saba Samatta "Golden Boy" amefunga mabao 5. Katika magoli hayo matano, kichwa chake kimeweka kambani mabao 4 na moja amefunga kwa guu lake la kulia.
Mabao hayo matano ya Samatta kwenye Africa Champions league amezifunga timu za Power Dynamo akiwa Ugenini, Akafunga bao lingine dhidi ya Al Merreikh aTP wakiwa nyumbani kabla ya kuja kuwafunga tena Wasudan hao nyumbani kwao Khartoum. Alhly wakawa majeruhi wengine wa Mbwana Samatta baada ya kuwaumiza wakiwa kwao Misri. TP Mazembe wakiwa uwanja wao nyumbani Tanzania Golden Boy akatupia bao moja kwenye mechi dhidi ya Berekum Chelsea. Ikafika zamu ya waarabu Zamalek ambaye akawafunga bao moja moja nyumbani na Ugenini na kutimiza mabao matano.
Dakika ambazo Mbwana Samatta anafunga sana magoli ni kuanzia kati ya dakika ya 16-30 ambapo hapo amefunga mabao mawili. kuanzia dk ya 31 mpaka 42 amafunga goli moja tu, huku akionekana kuwa hatari zaidi kwenye dakika ya 75 ya mchezo kwani tayari ameshafunga mabao mawili kwenye dakika hiyo.
Mafanikio hayo ya Samatta kwenye michuano mbalimbali TP Mazembe inayoshiriki yamezidi kumuongezea thamani kwenye soko la usajili duniani, kutoka kuuzwa kwa dola 100,000 na Simba kwenda TP Mazembe mpaka sasa anakadiriwa kuwa na thamani ya £175,000 ambayo ni mara 3 ya zaidi TP waliilipa Simba kumsaini Samatta.(www.shaffihdauda.com)
MVIVU, MCHELEWAJI MAZOEZINI NA UTOVU WA NIDHAMU VYAMUONDOA ALEX SONG ARSENAL - ATAMBULISHWA RASMI BARCA
Aug 17, 2012
NDUGU ZANGU WA ARSENAL, HIKI NDICHO ALICHOSEMA KOCHA WENU KUHUSU KUMSAJILI WA KUZIBA NAFASI YA VAN PERSIE!
Kwanza poleni sana katika
kipindi hiki kigumu cha kuchukuliwa mkali Robin van Persie ambae
ameingia kwenye familia ya Alex Ferguson.
Ninachotaka kuwaambia ni ripoti
ya gazeti la The Sun Uingereza kuandika kwamba kocha Arsene Wenger wa
Arsenal amesisitiza kwamba hatonunua striker mwingine ili kuchukua
nafasi ya Robin Van Persie.
Yani kasema washambuliaji
Olivier Giroud na Lukas Podolski wanatosha kabisa kuziba nafasi ya Van
Persie na muda wote wawili hao walikua wakiandaliwa kuchukua hiyo
nafasi.
Kocha huyo Mfaransa mwenye
miaka 62 toka aletwe duniani, amesema japo inauma kupoteza mchezaji kama
Van Persie kulikua hakuna njia yoyote isipokua kumuuza tu.
Kwenye line nyingine ni kwamba
kocha wa Manchester United amesema anaamini jumatatu Van Persie
atacheza kwenye mechi dhidi ya Everton.
August 15 2012 usiku ndio
ilithibitisha kumchukua Van Persie ambapo Fergie alithibitisha kwamba
mkali huyo alitarajiwa kufika Old Traford August 16 jioni kuonana na
madaktari wa club hiyo na ana imani yote yaliyobakia yatamalizika kabla
ya mechi ya jumatatu.
Kwa kumalizia amefananisha
uwepo wa Wyne Rooney, Van Persie, Chicharito na Danny Welbeck kama
ilivyokua 1999 kwa uwepo wa vichwa vikali kama Yorke, Cole, Sheringham
and Solskjaer — the four best strikers in Europe.(www.millardayo.com)
Subscribe to:
Posts (Atom)
ME MYSELF & I
THE DON HIMSELF
Karibuni sana kwenye blog hii ya kijamii iliyosheheni makila kitu kuanzia siasa uchumi afya na burudani kwa ujumla wake.uingiapo kwenye blog hii ni mengi ambayo utapata nafasi ya kukutana nayo,kumbuka mawazo yako ndo hasa yanayojenga na kunifanya niwe na ufanisi zaidi.kariiiiiiibuuuuuuuuuuuu saaaaaaaaaaaaaaanaaaaaaaaaa.(THE DJ HIMSELF-JIWE)