Aug 16, 2012

HAYA NDO MAJEMBE MAPYA YA SIMBA!



Mohamed Nassor (kushoto) akimshuhudia mshambuliaji  wa klabu ya Simba, Daniel Akuffo akisaini mkataba wa kuichezea klabu hiyo. 

 
Mohamed Nassor (kushoto) akimshuhudia beki mpya ,Paschal Ochieng akisaini mkataba wa kuichezea klabu hiyo.
Ochieng kulia na Akuffo kushoto

SIMBA B YAIRARUA AZAM FC NA KUTINGA FAINALI SUPER8 CUP





Timu ya soka ya Simba B imeifunga timu ya Azam katika mchezo wa nusu fainali wa kombe la Super 8 katika uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam.

Magoli ya Simba yalifungwa na wachezaji na wachezaji Rashid Ismial na Haroun Athumani wakati goli la kufutia machozi la Azam lilifungwa na beki wake wa kutumainiwa Saidi Morad.

Kwa ushindi huo Simba itacheza fainali ya Super 8 siku ya Jumamosi dhidi ya wakata miwa wa manungu Mtibwa Sugar ambao mapema leo waliwafunga Jamhuri ya Pemba mabao 5-1.

Simba leo waliwakilishwa na kikosi cha Abuu Hashimu(18), Miraj Adam (19), Omary Salum (11)/William Lucian ‘Gallas’, Hassan Isihaka (5), Hassan Hatibu (15) Said Ndemla (13), Haroun Athumani (7), Abdallah Seseme (17), Rashid Ismail (8), Edward Christopher (9)/Ramadhan Mzee na Frank Sekule (4)Ibrahim Ajibu.
Benchi; Saleh Malande (1), Ramadhan Mzee (2), William Lucian ‘Gallas’(3), Kenny Alex (12), Mohamed Salum (16), Ibrahim Ajibu (20) na Jesse Nyambo (14).
Makocha: Suleiman Matola. Msaidizi; Amri Said.

Azam FC - Wandwi Jackson (18), Ibrahim Shikanda (21), Samir Hajji Nuhu (11), Said Mourad (15), Luckson Kakolaki (5), Abdulhalim Humud (24), Sunday Frank (12), Jabir Aziz (25)/Khamis Mcha, Gaudence Mwaikimba (17)/Zahor Pazi, Abdi Kassim (20) na Kipre Herman Tcheche (27)Hamisi Mcha.

Benchi; Aishi Mfula (1), Omary Mtaki (2), Himid Mao (23), Khamis Mcha (22), Kelvin Friday (28). Abdulghani Gullam (14) na Zahor Pazi (9).
Makocha: Boris Bunjak (Serbia). Msaidizi; Vivek Nagul (India).(kwa hisani ya www.shaffihdauda.com)

PAMOJA NA KUFANYIWA OPERATION YA MOYO - MADAKATARI WAMWAMBIA MUAMBA HAWEZI KUCHEZA SOKA TENA - ATANGAZA KUSTAAFU





Hatimaye mchezaji wa Bolton Fabrice Muamba ametangaza kuachana na soka leo hii kutokana na ushauri wa daktari.

Mchezaji huyo mwenye asili ya Congo, alipata mshtuko wa moyo wakati wa mechi ya FA Cup dhidi ya Tottenham, amesema ana uchungu mkubwa kuachana na kucheza soka lakini hana budi zaidi ya kuweka mbele afya yake.

Muamba ameishukuru sana timu ya madaktari kwa kuokoa maisha yake na ameshukuru kwa maombi na sapoti kubwa aliyoipata kutoka kwa wapenzi wote wa soka duniani.

Moyo wa Muamba ulisimama kwa saa 78 baada ya kudondoka kwenye dimba la White Hart Lane baada ya kupatwa mshtuko wa moyo hali iliyopelekea kufanyiwa matibabu na kuweza kuokoa maisha yake.

Alikaa mwezi mzima Hosptali lakini aliwashangaza madaktari kwa jinsi alivyopata nafuu kwa haraka huku akisistiza anataka urudi kwenye dimba aendelee kucheza soka.

Kiungo huyo wa Bolton na England alienda mpaka nchini Ubelgiji wiki iliyopita kwa ajili ya kufanyiwa upasuaji mdogo ili kuweza kuwa fiti kwa ajili kurudi uwanjani.


Mchumba wake Shauna ali-tweet kuwaambia mashabiki wa Muamba kwamba operation imeenda vizuri na atarudi kucheza soka kwa nguvu kuliko ilivyokuwa mwanzoni, lakini siku moja baadae madaktari wakampa taarifa mbaya kwamba kurudi kucheza soka kutahatarisha maisha yake kwa kuwa moyo wake hauwezi kuhimili.

Kabla ya kutangaza kustaafu Mumba aliwaambia mashabiki wake waendelee kutabasamu na kila kitu kitakuwa poa.

Historia yake ya soka na kuanza kujulikana ilianzia katika academy ya soka ya Arsenal mwaka 2002 kabla ya kuhamia Birmingham na baadae akaenda Bolton mwaka 2008.

Aug 15, 2012

MAGAZETI YA LEO TRH 15/08/12

.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.

SIKU YA MWISHO YA USAJILI TANZANIA: YANGA YAWASILISHA MAJINA YA WACHEZAJI WAO WALIOWASAJILI MSIMU HUU

Young Africans imewasilisha jumla ya majina ya wachezaji  28 kwa shirikisho la soka nchini TFF, kwa ajili ya msimu mpya wa ligi kuu nchini inayotazamiwa kuanza mapema septemba mosi.

Katibu mkuu wa Young Africans Mwesigwa Selestine amesema wamepeleka majina ya wachezaji wote 28 kwa ajili ya msimu mpya wa ligi kuu, na hii ni kutokana na benchi la ufundi kuridhia kuwatumia wachezaji wote.


Aidha katika usajili huo uliowasilishwa leo, umeambatana na usajili wa wachezaji wa timu ya vijana U-20 ambapo majina ya wachezaji mahiri wa timu ya Taifa Saimon Msuva na Frank Domayo.
Usajili  kamili kwa timu ya wakubwa ni kama ifuatavyo:
Walinda Mlango:
Yaw Berko, Ally Mustafa 'Barthez' na Said Mohamed 
Walinzi wa pemebeni:
Shadrack Nsajigwa, Godfrey Taita, Juma Abdul, Oscar Joshua, David Luhende na Stephano Mwasika
Walinzi wa kati:
Nadir Haroub 'Cannavaro', Kelvin Yondan, Mbuyu Twite, Ibrahim Job na Ladislaus Mbogo
Viungo wa ulinzi:
Athuman Idd 'Chuji', Juma Seif Kijiko na Salum Telela
Viungo wa pembeni:
Nizar Khalfani, Shamte Ally, Idrisa Rashid na Omega Seme 
Viungo washambuliaji:
Haruna Niyonzima, Rashid Gumbo na Nurdin Bakari 
Washambuliaji:
Said Bhanaunzi, Hamis Kiiza 'Diego', Didier Kavambagu na Jeryson Tegete

Majina hayo yanakamilisha jumla ya 28 ya wachezaji kwa timu ya wakubwa.
Kikosi cha U-20 kina jumla ya majina 22 ambao ni:
Walinda Mlango: Geofrey Nyalusi na Yusuf Abdul
Walinzi: Said Manduta, Zuberi Juma, Said Mashaka, Benson Michael, Issa Ngao, Rashid Said
Viungo: Frank Domayo, Omary Nasry, Clever Charles, Mwinyi Bakari, Mpenda Abdallah 
Washambuliaji wa pembeni: Abdulahman Ally, Hussein Moshi, Abdallah Salum, Rehani Kibingu
Washambuliaji: Saimon Msuva, George Banda, Notikely Masasi, Suleiman Ussi, Kassim Jongo 
NB: Frank Domayo & Saimon Msuva usajili wao umepelekwa katika usajili wa U-20 lakini wataitumikia timu ya wakubwa 

www.youngafricans.co.tz

WANAJESHI WA STARS WAPIGA TIZI USIKU KUHAKIKISHA WANAWAFUNGA BOTSWANA



Wachezaji wa timu ya soka ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars wakiwa mazoezini katika Viwanja vya benki ya Botswana kujiandaa na mechi dhidi ya The Zebras ya Botswana ambayo inatarajiwa kupigwa leo jioni nje kidogo ya Mji wa Gaborone.(kwa hisani ya www.shaffihdauda.com)

Aug 14, 2012

kampuni ya bia ya serengeti yamkabidhi Mshindi wake wa gari promosheni ya Vumbua Hazina chini ya Kizibo mjini dodoma leo.

Mshindi wa gari wa shindano la Vumbua Hazina chini ya Kizibo  Bw. Amin Joseph Maro ambaye ni   mkazi wa Dodoma ambae ni mtaalamu wa mambo ya bomba,akiwasha mchuma wake tayari kuaondoka nalo huku shamra shamra za hapa na zikiwa zimetawala kutoka kwa ndugu na jamaa waliofika kwenye tukio hilo adhimu kabisa.

Mshindi wa gari wa shindano la Vumbua Hazina chini ya Kizibo  Bw. Amin Joseph Maro  akiingia ndani ya gari yake aina ya Ford Figo baada ya kukabidhiwa na Mkurugenzi wa Masoko wa Serengeti Breweries Bw. Ephraim Mafuru, hafla hiyo imefanyika jioni ya leo kwenye bustani ya Nyerere Square mjini  Dodoma. Wanaoshuhudia katikati yao ni Baba yake Mzee Augustine Tengia, wengine wanaoshuhudia tukio hilo ni Allan Chonjo, meneja wa bia ya Serengeti Premium Lager sambamba na Wanahabari .
Mkurugenzi wa Masoko wa Serengeti Breweries Bw. Ephraim Mafuru  akimkabidhi kadi ya gari mshindi wa gari wa shindano la Vumbua Hazina chini ya Kizibo  Bw. Amin Joseph Maro kwenye hafla fupi iliyofanyika jioni ya leo kwenye bustani ya Nyerere Square mjini  Dodoma. Wanaoshuhudia katikati yao ni Baba yake Mzee Augustine Tengia wakiwemo Wanahabari ndugu jamaa na marafiki.
Mkurugenzi wa Masoko wa Serengeti Breweries Bw. Ephraim Mafuru  akimkabidhi funguo ya gari lake mshindi wa shindano la Vumbua Hazina chini ya Kizibo  Bw. Amin Joseph Maro kwenye hafla fupi iliyofanyika jioni ya leo kwenye bustani ya Nyerere Square mjini  Dodoma. Wanaoshuhudia katikati yao ni Baba yake Mzee Augustine Tengia wakiwemo Wanahabari ndugu jamaa na marafiki.
Meneja wa kinywaji cha Serengeti Premium Lager Bwa. Allan Chonjo akifafanua jambo mbele ya Wanahabari kutoka vyombo mbalimbali na wadau wengine kutoka sehemu mbalimbali waliofika kulishuhudia tukio la kukabidhiwa kwa gari aina ya Ford Figo kwa mshindi wa shindano la Vumbua Hazina chini ya Kizibo  Bw. Amin Joseph Maro kwenye hafla fupi iliyofanyika jioni ya leo ndani ya bustani ya Nyerere Square mjini  Dodoma.
Mshindi wa shindano la Vumbua Hazina chini ya Kizibo  Bw. Amin Joseph Maro akifurahia zawadi hiyo na Mama yake Mzazi ambaye pia alikuwepo kulishuhudia tukio hilo lililofanyika jioni ya leo kwenye bustani ya Nyerere Square mjini  Dodoma.
Mshindi wa shindano la Vumbua Hazina chini ya Kizibo  Bw. Amin Joseph Maro akizungumza mbele ya Wanahabari waliofika kulishuhudia tukio hilo jioni ya leo kwenye bustani ya Nyerere Square mjini  Dodoma,kulia kwake ni Baba yake Mzazi Mzee Augustine Tengia.
Baba yake Mzazi Mzee Augustine Tengia akizungumzia furaha alionayo mbele ya Wanahabari mara baada ya mtoto wake kujishindia gari mpya kabisa aina ya  Ford Figo kupitia promosheni ya Vumbua Hazina chini ya Kizibo iliyokuwa ikiendeshwa na kampuni ya bia ya Serengeti.

TAIFA STARS YAWASILI SALAMA GABORONE TAYARI KUUMANA NA WABOTSWANA





Kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) kikiwa na wachezaji 17 kimewasili leo asubuhi jijini Gaborone tayari kwa mechi ya kirafiki ya kalenda ya Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) dhidi ya wenyeji Botswana 'Zebras' itakayochezwa kesho (Agosti 15 mwaka huu).

Stars ilitua kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Sir Seretse Khama saa 5.45 asubuhi kwa saa za hapa ambapo nyumbani ni 6.45 na kupokewa na viongozi wa Chama cha Mpira wa Miguu Botswana (BFA) na Watanzania wanaoishi hapa Botswana.

Baadhi ya wachezaji walioko kwenye kikosi hicho ni Frank Domayo, Ramadhan Singano na Simon Msuva ambao walijiunga na Stars saa chache baada ya kurejea kutoka Nigeria ambapo walikuwa na timu ya vijana wenye umri chini ya miaka 20 (Ngorongoro Heroes) ambayo Jumapili ilicheza mechi ya mashindano ya Afrika dhidi ya Nigeria (Flying Eagles).

Wachezaji wengine kwenye kikosi kilichoko Botswana ni Aggrey Morris, Amir Maftah, Athuman Idd, Erasto Nyoni, Haruna Moshi, Juma Kaseja, Kelvin Yondani, Mrisho Ngassa, Mwadini Ally, Mwinyi Kazimoto, Ramadhan Chombo, Salum Abubakar, Said Bahanuzi na Shabani Nditi.

Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager imefikia kwenye hoteli ya Oasis ambayo pia ndipo Zebras imepiga kambi kwa ajili ya mechi hiyo. Mechi itaanza kesho saa 1 kamili usiku kwa saa za hapa na itafanyika kwenye Uwanja wa Molepolole Sports Complex. Uwanja wa Taifa wa Botswana hivi sasa uko kwenye matengenezo.

Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Kim Poulsen amesema mechi hiyo ni muhimu kwa vile timu yake bado
inakabiliwa na mechi za Kombe la Dunia Kanda ya Afrika, na michuano ya Kombe la Afrika kwa Wachezaji wa Ndani (CHAN) inayotarajia kuanza baadaye mwaka huu.(kwa hisani ya www.shaffihdauda.com)

MITANANGE YA KIRAFIKI KESHO

FIFA-logo-300Jumatano Agosti 15 ni Siku ya Kalenda ya FIFA iliyowekwa mahsusi kwa ajili ya Mechi za Kimataifa za Kirafiki na Nchi nyingi Duniani zimeandaa Mechi za kujipima ikiwemo Tanzania ambayo Timu yake, Taifa Stars, itakwenda huko Gaborone kucheza na Wenyeji wao Botswana.
Huko Barani Ulaya, ambako Nchi zake zitaanza Mwezi ujao kinyang’anyiro cha Mechi za Mchujo za kuwania kufuzu kucheza Fainali za Kombe la Dunia za Mwaka 2014 huko Brazil, zipo Mechi nyingi na zinazohusisha Timu kubwa.
Mabingwa wa Dunia na Ulaya, Spain, watarudi tena dimbani kwa mara ya kwanza tangu watwae EURO 2012 hapo Julai 1 kwa kucheza na Puerto Rico Siku ya Jumatano ikiwa ni matayarisho ya Mechi yao ya Kundi I la Kombe la Dunia 2014 dhidi ya Georgia hapo Septemba 11, Kundi ambalo pia wapo France, Belarus na Finland.
Italy wao watacheza Kirafiki na England hapo Jumatano huko Berne, Uswisi huku Timu zote hizi pia zikikabiliwa na Mechi za Makundi yao Kombe la Dunia Mwezi Septemba ambapo Italy watacheza na Bulgaria na England watakipiga na Moldova hapo Septemba 7.
France, wakiwa chini ya Kocha mpya Didier Deschamps, watacheza Mechi ya Kirafiki na Uruguay huku wakiwa na Kikosi chenye mabadiliko ambacho hakina Wachezaji maarufu kina Hatem Ben Arfa, Philippe Mexès, Adil Rami, Yohan Cabaye, Alou Diarra, Florent Malouda na Yann M'Vila ambao wote wametemwa.
Na Russia nao watacheza na Ivory Coast wakiwa chini ya Kocha wao mpya Fabio Capello.
Mechi ya Kirafiki ya kusisimua itakuwa ni ile kati ya Netherlands na Belgium ambayo ina Wachezaji wakubwa wanaotamba hivi sasa kina Vincent Kompany, Jan Vertonghen, Thomas Vermaelen, Eden Hazard, Axel Witsel, Moussa Dembélé na Marouane Fellaini.
Vigogo wa Soka Duniani, Brazil, wao watacheza kirafiki na Sweden.
RATIBA BAADHI YA MECHI
Jumatano, Agosti15
Mechi za Kimataifa za Kirafiki
Botswana v Tanzania
Costa Rica v Peru
Ecuador v Chile
El Salvador v Jamaica
Mexico v USA [Saa 9 usiku]
Albania v Moldova [Saa 7 mchana]
Japan v Venezuela [Saa 7 na nusu mchana]
South Korea v Zambia [Saa 8 mchana]
China PR v Ghana [Saa 8 Dak 35 mchana]
Puerto Rico v Spain [Saa 12 jioni]
Russia v Ivory Coast Saa 12 jioni]
Armenia v Belarus [Saa 1 usiku]
Azerbaijan v Bahrain [Saa 1 usiku]
Croatia v Switzerland [Saa 2 na robo usiku]
Bulgaria v Cyprus [Saa 3 usiku]
Luxembourg v Georgia [Saa 3 usiku]
Norway v Greece [Saa 3 usiku]
Sweden v Brazil [Saa 3 usiku]
Ukraine v Czech Republic [Saa 3 usiku]
Denmark v Slovakia [Saa 3 na robo usiku]
Austria v Turkey  [Saa 3 na nusu usiku]
Hungary v Israel [Saa 3 na nusu usiku]
Montenegro v Latvia [Saa 3 na nusu usiku]
Belgium v Netherlands, 19:45
Estonia v Poland [Saa 3 Dak 45 usiku]
Germany v Argentina [Saa 3 Dak 45 usiku]
Macedonia v Lithuania  [Saa 3 Dak 45 usiku]
Northern Ireland v Finland  [Saa 3 Dak 45 usiku]
Serbia v Rep of Ireland [Saa 3 Dak 45 usiku]
Slovenia v Romania [Saa 3 Dak 45 usiku]
Wales v Bosnia-Hercegovina [Saa 3 Dak 45 usiku]
England v Italy [Saa 5 usiku]
France v Uruguay [Saa 5 usiku]
Scotland v Australia [Saa 5 usiku]
Iceland v Faroe Islands [Saa 5 Dak 45 usiku]
Portugal v Panama [Saa 6 Usiku]
Paraguay v Guatemala [Saa 6 usiku]
Alhamisi, Agosti 16
Canada v Trinidad and Tobago [Saa 9 usiku]
Costa Rica v Peru [Saa 9 usiku]
Ecuador v Chile [Saa 9 usiku]
El Salvador v Jamaica [Saa 9 usiku]

MCHEZAJI BORA ULAYA: Wagombea ni Iniesta, Messi & Ronaldo

INIESTA

Mshindi wa Tuzo ya UEFA ya Mchezaji Bora Ulaya kwa Msimu wa 2011/12 atajulikana hapo Agosti 30 baada ya leo Listi ya Wachezaji 32 kuchujwa na kubakizwa watatu ambao wametangazwa na UEFA kuwa ni Lionel Messi na Iniesta wa Barcelona, na Ronaldo wa Real Madrid.
Tuzo hii ilifufuliwa upya na Rais wa UEFA, Michel Platini, na kwa mara ya kwanza alitunukiwa Lionel Messi Mwezi Agosti Mwaka jana.
Mshindi wa Tuzo hii atapewa Tuzo yake hapo Agosti 30 huko Monaco.
Kama ilivyokuwa Mwaka jana, Jopo la Wanahabari toka kila Nchi Wanachama wa UEFA, Nchi 53, ndilo lilichagua hao watatu kwa kura kutoka Listi ya Wachezaji hao 32 wa mwanzoni.
Wachezaji hawa watatu waliobakishwa watapigiwa kura ‘laivu’ Agosti 30 na Wanahabari hao hao toka Nchi 53 Wanachama wa UEFA.
LISTI AWALI YA WACHEZAJI 32:
Sergio Agüero (ARG) – Manchester City FC
Xabi Alonso (ESP) – Real Madrid CF
Mario Balotelli (ITA) – Manchester City FC
Jakub Błaszczykowski (POL) – Borussia Dortmund
Gianluigi Buffon (ITA) – Juventus
Iker Casillas (ESP) – Real Madrid CF
Petr Čech (CZE) – Chelsea FC
Fábio Coentrão (POR) – Real Madrid CF
Leslie Davies (WAL) – Bangor City FC
Didier Drogba (CIV) – Chelsea FC (Amehamia Shanghai Shenhua FC)
Cesc Fàbregas (ESP) – FC Barcelona
Falcao (COL) – Club Atlético de Madrid
Joe Hart (ENG) – Manchester City FC
Zlatan Ibrahimović (SWE) – AC Milan
Andrés Iniesta (ESP) – FC Barcelona
Shinji Kagawa (JPN) – Borussia Dortmund (Amehamia Manchester United FC)
Vincent Kompany (BEL) – Manchester City FC
Frank Lampard (ENG) – Chelsea FC
Lionel Messi (ARG) – FC Barcelona
Luka Modrić (CRO) – Tottenham Hotspur FC
Mesut Özil (GER) – Real Madrid CF
Pepe (POR) – Real Madrid CF
Andrea Pirlo (ITA) – Juventus
Sergio Ramos (ESP) – Real Madrid CF
Raúl González (ESP) – FC Schalke 04 (Amehamia Al-Sadd Sports Club)
Cristiano Ronaldo (POR) – Real Madrid CF
Wayne Rooney (ENG) – Manchester United FC
David Silva (ESP) – Manchester City FC
Fernando Torres (ESP) – Chelsea FC
Yaya Touré (CIV) – Manchester City FC
Robin van Persie (NED) – Arsenal FC
Xavi Hernández (ESP) – FC Barcelona

HATIMAYE SIMBA WAMALIZANA NA AZAM FC

Redondo

YAMEKWISHA. Naam, sasa Simba SC na Azam FC ni amani tupu. Azam imekubali kupokea Sh. Milioni 15 kutoka Simba SC ili kumuuza kiungo wake, Ramadhan Chombo ‘Redondo’ kwa Wekundu hao wa Msimbazi.
Habari za ndani ambazo Chanzo imezipata, zimesema kwamba hiyo inafuatia viongozi wa Simba SC kuwaangukia Azam kwa kitendo chao cha kumsajili kiungo huyo bila kuwasiliana nao, wakati bado alikuwa ana mkataba na Wana Lamba Lamba.
Awali, Azam walikerwa na kitendo hicho hadi wakataka kusitisha dili la kumtoa kwa mkopo kwa Mrisho Khalfan Ngassa Simba SC.
Azam walimtoa kwa mkopo Ngassa, baada ya kukerwa na kitendo cha mchezaji huyo kubusu jezi ya timu yake ya zamani, Yanga, katika Nusu Fainali ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame, dhidi ya AS Vita ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) mwezi uliopita.
Alifanya hivyo, baada ya kufunga bao la ushindi akitokea benchi na kuiwezesha Azam kutinga fainali ya michuano hiyo, ambako walifungwa na Yanga 2-0, naye kwa mara nyingine akitokea benchi na kushindwa kufunga, hivyo kutuhumiwa kucheza kinazi.
Ilielezwa kwamba Simba walitoa Sh. Milioni 25 kumnunua kwa mkopo mchezaji huyo, ingawa baadaye Simba wakasema waliununua mkataba wa mwaka mmoja aliobakiza mchezaji huyo Azam FC, nao wakamuongezea wa mwaka mmoja kwa kumsainisha kwa Sh. Milioni 30, kati ya hizo Milioni 12 akipewa taslimu na 18 akipewa gari.
Inavyoonekana, Redondo aliwadanganya Simba kwamba amemaliza mkataba na Azam, wakaingia mkenge na kumpa Sh. Milioni 30 wakimsainisha mkataba wa miaka miwili, wakati mkataba wake na Azam unamalizika Juni mwakani.
Hili ni kosa sawa na ambalo Simba walilifanya katika usajili mwingine wa mchezaji wa Azam, Ibrahim Rajab ‘Jeba’, miezi mitatu iliyopita ambaye alikuwa kwa mkopo Villa Squad wao wakaenda kumsajili bila kuwasiliana na klabu yake kujua kuhusu mkataba wake, matokeo yake baadaye mchezaji huyo akarejea Azam.
Simba nao wana lalamiko kama hilo, dhidi ya watani wao wa jadi, Yanga wanaowatuhumu kumsajili beki Kevin Yondan, wakati bado ana makataba na Wekundu hao wa Msimbazi, ingawa TFF iliweka sawa kwa kusema Yondan hakuwa na mkataba na Simba SC.
Baadaye Simba ilitoa ufafanuzi, kwamba ilimuongezea mkataba Yondan baada ya ule wa awali kumalizika na ikawa inasubiri muda wa usajili ufike wauwasilishe TFF. Lakini katika kesi ya awali, Simba walipoupeleka mkataba wao mpya na Yondan, ulionyesha mchezaji huyo anatakiwa kuanza kuutumikia mkataba huo, Desemba mwaka huu, hivyo TFF ikasema kwa wakati ambao yuko huru, aichezee Yanga.
Sakata la Yondan litarudi Desemba, wakati ambao atatakiwa kuanza kuutumikia mkataba wake na Simba, wakati yupo ndani ya mkataba wa miaka miwili na Yanga.

THE DON HIMSELF

Karibuni sana kwenye blog hii ya kijamii iliyosheheni makila kitu kuanzia siasa uchumi afya na burudani kwa ujumla wake.uingiapo kwenye blog hii ni mengi ambayo utapata nafasi ya kukutana nayo,kumbuka mawazo yako ndo hasa yanayojenga na kunifanya niwe na ufanisi zaidi.kariiiiiiibuuuuuuuuuuuu saaaaaaaaaaaaaaanaaaaaaaaaa.(THE DJ HIMSELF-JIWE)

Followers

BLOG ZA MARAFIKI

Search This Blog

ZILIZOPITA

DUNIA MUZIMA