Aug 6, 2012

HAYA NDIO MAGAZETI YA LEO AUG 6, UDAKU MICHEZO NA HARDNEWS.



.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.

HIZI NDIO PICHA ZA MSIBA WA MAMA WA P SQUARE NIGERIA.

Hili ndio gari lililobeba jeneza la mwili wa marehemu.
.
Kwa mbele ya gari waliwekwa hii picha ya Marehemu.
Mabango ya msiba mpaka barabarani.
.
Pater na Paul wakiwa kwenye upande wa kulia na kushoto mwa jeneza la mama yao mzazi.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
Marehemu mama mzazi wa Peter na Paul wa P Square.
Mama mzazi wa waimbaji Peter na Paul Okoye wanaounda kundi la P-Square alifariki dunia july 11 2012 baada ya kuugua kwa muda mrefu, na alipelekwa India miezi michache iliyopita baada ya kuzidiwa.
Mrs Okoye alikua mmoja kati ya watu waliowasaidia sana P Square kufanya vizuri kwenye muziki ikiwemo kuwapa ushauri watoto wake hao ambao sasa hivi wamepanda ngazi na kufanikiwa mpaka kufanya kazi na wakali wa dunia kama Akon pamoja na Rick Ross.(kwa hisani ya www.millardayo.com)

Makala: Linex unastahili kuigwa




Na Emmanuel Msigwa aka DJ Msigwa, Radio journalist, Presenter, Radio DJ & Club DJ

Natumaini jina la Linex si geni miongoni mwa majina makubwa katika tasnia ya muziki hapa nchini. Historia yake si kubwa ukilinganisha na wasanii wengine. Ngoma yake ya Mama Halima ndiyo iliyomfungulia njia. Moyo wa subira ikaja kupigilia msumari pale alipofikia na kuanzia hapo akapewa “mashavu” katika ngoma mbalimbali kuanzia Sina Jiwe, Kankutume na nyinginezo.

Kifupi ni msanii mkali ambaye alikuja kuhit baada ya kuamua kutumia vionjo vya kabila lake la kiha kutoka Kigoma na utaona hata katika ngoma ya Leka Dutigite alipewa yeye kufanya kiitikio “chorus” kwakuwa tu anaoufahamu mkubwa juu ya matumizi ya lugha yao. Naamini hiyo ndiyo silaha ambayo amekuwa akiitumia katika ngoma zake.

Achilia mbali uwezo wake mkubwa katika kuimba, Linex amekuja pia na mtazamo mpya wa utunzi wa mashairi ya nyimbo zake nyingi. Angalia hadithi ya wimbo wa Mama Halima, Ngekewa, Moyo wa Subira na huu wa sasa Aifola. Utakubaliana nami kuwa jamaa ni mbunifu na ujumbe wake umekuwa rahisi kufika kwa walengwa wake…………big up sana.

Lakini tukiachana na ubora wa matoleo ya nyimbo zake bado Linex anaweza kuwa mmoja kati ya wasanii wa kitanzania walau wanaojaribu kuweka uhalisia wa video zake na audio zake kwa maana ya kwamba mashairi yake yake yanawakilisha pia matendo yake katika video.

Aangalia vizuri Ngekewa, njoo katika Moyo wa Subira na angalia wa sasa hivi Aifola. Sio kwamba anafanikiwa kwa 100% yapo makosa madogo madogo ambayo amekuwa akiyafanya katika video zake. Mfano anapokuwa anaimba ishara ( kwa maana anapotumia) lugha ya vitendo katika video nafikiri siyo sahihi kwa kuwa katika video tunahitaji zaidi tuone lugha hizo za ishara kwa kuona matendo halisi.

Makosa mengine ambayo anayafanya Linex yanachangiwa na timu yake ya video. Mfano katika  Aifola, video imefanywa na Adama Juma wa Visual Lab, Next Level.

Huyu ni kati ya waandaji bora wa video hapa nchini lakini kuna makosa anayoyafanya hasa katika  baadhi ya “angleshoot” ni kama vile hamtendei haki. Mfano katika closeup shoot ambapo Linex anaonekana akiwa ametupia suti nzuri sana na imempendeza lakini cha ajabu katika fullclose shoot anaoneka kavaa raba.

Kwa mtazamo wangu wakati wa editing wangeondoa kipande kile au kuna kipande Linex yupo na yule msichana wake wamekaa sijui ni sebuleni, sijui ni wapi, lakini inaonekana zile sofa ni kama zimefunikwa, yaani hazitumiki au ni dukani na hiyo ni baada ya fullclose shoot yake.

Otherwise hayo si makosa ya Linex lakini timu yake ilipaswa kuliangalia hilo.
Tuna tatizo kubwa sana katika utoaji wa video zetu ndiyo maana video hizo zimekuwa na makosa ya hapa na pale, wakati Ne-yo anaelezea ubora wa video yake ya So Sick,  alisema mtayarishaji wake Hype Williams, alitumia miezi 6 kuipika video hiyo na ilipotoka kila mmoja alikuja kuikubali.

Timu zetu za video zisiharakishe kazi za wasanii hao ili tuone ubora tunaoutaka na pia kuviendeleza vipaji vya wahusika wa nyimbo hizo. Lakini yote ni yote Linex amekuwa akijaribu kutuonyesha uhalisia katika kazi za video kwa maana ya storyboard yake tunaiona.

Endelea na ubunifu huo muziki unapokuwa mzuri hauitaji kulazimishwa ili uweze kuukubali uzuri huo, wengine waige kutoka kwako Linex.
BIG UP SANA MWANA KIGOMA ALL STARS…………..!

BREAKING NEWS!!!!!!! RAMADHANI CHOMBO LEDONDO ASAINI SIMBA MCHANA HUU


Mchezaji Ramadhani Chombo Ledondo mchana huu amesaini Mkataba wa kuitumikia timu ya Simba baada ya kuwa ametolewa kwa Mkopo msimu uliopita. Habari za kina zitakujia Punde zikiambatana na Picha za Kutiliana Saini kwa Mkataba Huo. Hii ni www.mwanatanga.blogspot.com yenye habari za Uhakikika na Ukweli hapa Hakuna TETESI ni Habari zilizopimwa 

UJENZI BARABARA YA MSATA KIWANGWA BAGAMOYO KIWANGO CHA LAMI KUKAMILIKA PUNDE


Ujenzi wa Barabara ya urefu wa Kilomita sitini na tano (65) kutoka Bagamoyo kupitia Kiwangwa hadi Msata yenye urefu wa kilomita 65 umekamilika kwa asilimia takribani 59.6% baada ya jumla ya kilomita 35 kukamilika kwa kiwango cha lami. Wakala wa Barabara Tanzania TANROADS wanakusudia kutumia barabara hii kwa Magari yote ya Usafiri wa Umma yanayotokea Kanda ya Kaskazini kwa maana ya Mikoa ya Tanga, Kilimanjaro, Manyara na Arusha kutumia barabara hii pindi itakapokamilika ili kupunguza msongamano kwenye barabara ya Morogoro hususan pale Chalinze na Kibaha kwenye Mzani (Weight Bridge).
HUU NDIYO MUONEKANO WA BARABARA YA MSATA-KIWANGWA-BAGAMOYO KWA SASA
 Matarajio ya hivi karibuni ni kujenga kituo cha Mabasi kwa ajili ya Mabasi ya Mikoani eneo la Kunduchi yalipokuwepo Machimbo ya Kunduchi yaliyofungwa ili kuyafanya mabasi yanayotokea Kanda ya Kaskazini kuanzia Safari zake na kuishia kwenye Kituo hicho kipya pindi kitakapokamilika ili kupunguza msongamano katikati ya Jiji.
HAPA NI MJINI KIWANGWA ENEO MAARUFU KWA ULIMAJI WA MANANASI WILAYA YA BAGAMOYO MKOA WA PWANI

Mradi mwingine ni ujenzi wa barabara ya Bagamoyo Saadan Pangani hadi Tanga kwa Kiwango cha lami utakaoyawezesha mabasi yatokayo Tanga na Mombasa kupitia barabara hiyo ili kukuza utalii wa Mbuga pekee Duniani ambayo Wanyama huwa wanakwenda Beach (MBUGA YA SAADAN) ambayo inaambaa na Ukingo wa bahari kutokea Bagamoyo hadi Tanga. Kwa kufanya hivyo Mbuga hii itakuwa kwa kasi na kuwa kivutio kwa Watalii kuja kuona Maajabu hayo ya Dunia ya wanyama wanaoshinda Beach kupunga Upepo. Mradi huu wa Bagamoyo Saadan Pangani umeshaanza kutokea Muheza kwa kiwango cha lami na ujenzi unakwenda kwa Kasi ya kutia moyo.

BAADHI YA VIZUIZI VYA KUONYESHA TAHADHALI KWA WATUMIAJI WA BARABARA HIYO YA MSATA KIWANGWA BAGAMOYO WAKATI WA UJENZI KUEPUSHA AJALI

Sambamba na Mradi huu pia Wakala wa Barabara Tanzania unaendelea na ukarabati wa barabara ya Chalinze Segera Tanga ambao awamu ya kwanza iliishia eneo la Kitumbi Wilaya ya Handeni chini ya Kampuni ya Wachina na sasa ujenzi huo unaendelea kuanzia Kitumbi hadi Kwamichi Tanga chini ya Kampuni ya Kiisrael iitwayo SBI International. Ukarabati huu sasa unaendelea kwa kasi sana na unatarajiwa kukamilika katikati ya mwaka 1913.
WAJENZI KAZINI BARABARA YA MSATA KIWANGWA BAGAMOYO

Aidha ujenzi wa awamu ya kwanza wa kilomita 76 kuanzia Segera hadi Mkumbara kupitia vijiji na miji ya Segera Mashine, Chang'ombe, Mailikumi, Mandera, Kwakombo, Kwamdulu, Korogwe Mjini, Msambiazi, Mgobe, Nkhalekwa, Magila, Gereza, Kwasunga, Kwasunga Mpirani, Makuyuni, Madumu, Madala, Chepete, Chekelei, Mwisho wa Shamba, Mombo Mjini, Jitengeni, Kasiga, Mazinde, Mheza, , Kwenangu, Magila, Mkumbara, Goha, Manga, Mtindiro, Mkomazi na Bwiko. Mradi huu unajengwa na Kampuni ya STRABAG ambayo pia inajenga Barabara yenye urefu wa kilomita 21.9 ndani ya jiji la Dar es Salaam kwa ajili ya Mradi wa Mabasi Yaendayo Haraka-DART.
VIFAA VYA UJENZI VYA KISASA KWENYE BARABARA YA MSATA KIWANGWA BAGAMOYO

MAMA KARUME AONGOZA JOPO LA YANGA KUWASILISHA KOMBE LA KAGAME MJENGONI LEO


MWENYEKITI WA YANGA AKIWA NA MAMA FATMA KARUME
 Kombe la Kagame limetinga Mjengoni muda mchache uliopita na kulitikisa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Baada ya utambulisho uliofanywa na Mheshimiwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Anna Makinda. Alianza kwa kusema. “Tunao Wageni Mashuhuri walioiletea Sifa Nchi yetu kwa kutwaa Kombe la Afrika ya Mashariki na Kati Maarufu kama Kombe la Kagame mara mbili Mfululizo tena kwa KISHINDO siku chache zilizopita ndani ya Uwanja Mpya wa Taifa Pale Dar es Salaam ambao ni Timu ya YANGA. Timu hii imeongozwa na Mama yetu Mke wa Muasisi wa Muungano Mama yetu Bi. Fatma Karume Mama Karibu sana na nimefurahi kukuona ukiwa bado na afya tele. Pamoja na Mama Karume pia ameandamana na Mjumbe wa Baraza la Wadhamini la Yanga Eng. Francis Mponjoli Kifukwe (Makofi Mengi), Mwenyekiti wa Klabu ya Yanga Ndugu Yusuph Mehboob Manji (Makofi Mengi Sanaaaaaaaaaaaaaaa), Makamu Mwenyekiti Ndugu Clement Sanga (Makofi) pamoja na viongozi wengine waandamizi na Wazee wa Yanga wakiongozwa na Mzee Akilimali. Pia tunao wachezaji wote wa Yanga kama mnavyowaona wakiwa kwenye nguo zao zinazopendeza za Njano wote kwa ujumla simameni…. (Bunge lazizima kwa Ndelemo na Vifijo huku Captain wa timu hiyo Carnavaro ainua Kombe juu). Spika aliendelea najua Mheshimiwa Spika Mstaafu Samwel Sitta amenuna sana lakini hiyo ndiyo hali halisi na hata Simba wakija na kombe nitawatangaza… (Vicheko Bungeni)….. Tunawakaribisha sana na tunawatakia kila la kheri kwenye shughuli zenu za kuijenga klabu yenu ili mtuletee furaha zaidi siku zijazo jambo ambalo tunaimani linawezekana (Makofi mengi sanaaa na Sauti ya Mheshimia Nasari ilisikika kwa mbali ikisema Tano bila Kichekooooo na makofi ya kuipongeza Yanga yaliendelea na kumfanya Spika Acheke na kuwataka Wabunge kuwa watulivu ili shughuli nyingine ziendelee). 
Mama Fatma Karume
Baada ya Spika kukamilisha zoezi la kuikaribisha Yanga Mjengoni Spika alimuita Mheshimiwa Bernard Camilus Membe Waziri wa Mambo ya Nje na Uhusiano wa Kimataifa awasilishe Hotuba yake. Katika utangulizi wake Mheshimiwa Membe alisema “Nimefurahishwa na Ujio wa Yanga humu ndani wakati wa Hotuba yangu kwakuwa name ni mdau mkubwa wa Timu ya Yanga Hongereni kwa ushindi wa Kagame (Makofi mengiii)” Mwisho wa kunukuu.

ARSENAL KUSAJILI WAWILI KWA MPIGO



Arsenal inajitahidi kukamilisha utiaji saini wa makubaliano ya mkataba wa kudumu na mchezaji Santi Cazorla kutoka klabu ya Malaga pamoja na mchezaji kiungo mwenzake Nuri Sahin anayeingia kwa makubalino ya mkopo kutoka klabu ya Real Madrid. Mpango wa kuhama kwa mchezaji wa Timu ya Taifa ya Uhispania Cazorla mwenye umri wa miaka 27 kumekua na utata wa shida ya fedha inayoikumba klabu ya Malaga hata hivyo anatazamiwa kupitia utaratibu wa afya wiki hii. Mchezaji kiungo wa timu ya Taifa ya Uturuki mwenye umri wa miaka 23 Nuri Sahin atajiunga na Arsenal chini ya mpango wa mkopo wa mwaka mmoja na Real Madrid. Lililobaki ni baina ya mchezaji Sahin kukubaliana na klabu ya Arsenal juu ya malipo na marupurupu. Kuna uwezekano mkubwa kwa wachezaji hawa kuhitimisha utaratibu huu kabla ya msimu mpya kuanza.
Bado Sahin hajapangiwa siku ya kufanyiwa majaribio ya afya. Arsenal inaanza msimu mpya kwa pambano la ugenini dhidi ya Sunderland tarehe 18 Agosti 2012. Tayari Gunners imewasajili wachezaji wawili mshambuliaji Lukas Podolski kutoka klabu ya Cologne na mshambuliaji wa Ufaransa Olivier Giroud aliyekuwa akichezea klabu ya Montpellier. Pamoja na hayo yote wingu zito bado limegubika majaliwa ya nahodha Robin van Persie, ambaye ametamka kua hatoongezewa mkataba wake unaomazika mwaka 2013.
Usajili wa wacheza kiungo Cazorla pamoja na Sahin ingawa hakuna uhusiano na mizengwe ya Van Persie lakini umechagizwa na habari kwamba mchezaji kiungo wa Arsenal Jack Wilshere hatoweza kucheza kabla ya mwezi Oktoba kutokana na jeraha la goti.
Cazorla aliyejiunga na Malaga kutoka klabu ya Villarreal mwaka mmoja tu uliopita ana urefu wa futi 5 inchi 6 na ameichezea timu ya Taifa ya Uhispania mwaka 2008 na kwenye mashindano ya Ulaya ya mwaka 2012. Sahin alisajiliwa na Real Madrid kutoka Borussia Dortmund kwa mkataba wa miaka sita mnamo mwezi May 2011 lakini ameshindwa kupata nafasi katika kikosi Mourinho ambapo kocha huyo ameweza kumruhusu aondoke tu ila kwa mkopo.

UJENZI WA BARABARA YA NJIA SITA KUANZIA KIMARA HADI MIKESE MOROGORO KUANZA PUNDE


Mheshimiwa Waziri wa Ujenzi na Mbunge wa Chato akiwa Kbaruani
WAKAZI wa Jiji la Dar es Salaam waishio kandokando ya barabara ya Morogoro wametakiwa kukaa chonjo kwani ujenzi wa barabara hiyo hadi Mkoani Morogoro utaanza hivi punde. Kufuatia upanuzi huo kuna baadhi ya mali zitakozo athirika yakiwemo Majengo mashamba na mali zote zisizohamishika. Bomoabomoa hiyo itapelekea ujenzi huo wa upanuzi (Uborshaji wa barabara kwa jumla ya kilometa 200 kutoka jijini Dar es Salaam nadi Mji unaokua kwa kasi Morogoro (Mji kasoro Bahari).
Waziri wa Ujenzi, Mh. Dk John Pombe Magufuli alisema hayo jana kwenye mahafali ya nne ya Chuo Kikuu cha Mtakatifu Joseph, Kitivo cha Uhandisi na Teknolojia. Bila Kumung’unya au kung’ata maneno Mheshimiwa Magufuli alisema barabara hiyo inatarajiwa kujengwa kwa kiwango cha lami kwa njia sita (Three Lanes each side) kwa umbali wa kilometa 200 kutoka Dar es Salaam hadi Morogoro jambo ambalo limerudiwa kutamkwa na Mheshimiwa Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje Bernard Membe leo 06/08/2012 Bungeni wakati akiwasilisha hotuba ya Wizara yake.
Waziri Magufuli amewatahadharisha waliojenga kwenye hifadhi ya barabara kuanza kuondoka ili kupisha upanuzi huo kabla hawajaondolewa kwa nguvu. Hifadhi ya Barabara ilikuwa ni mita 22.5 kutoka katikati ya barabara kwa pande zote kwa maana ya mita 45 kwa sheria ya zamani wakati kwasasa sheria hiyo ni mita 30 kila upande kwa maana ya mita 60 kwa sheria ya mwaka 2007 iliyopitishwa na Bunge mwaka 2009.
Namnukuu Mheshimiwa Magufuli “Wote waliojenga kwenye hifadhi ya barabara waanze kujiandaa kuondoka kwasababu sheria ni msumeno,” mwisho wa kunukuu.
Pamoja na mambo mengine mheshimiwa Magufuli alimuagiza Mwenyekiti wa Bodi ya Wakandarasi, Profesa Ninatubu Lema kuwapatia usajili wanafunzi wote waliohitimu Chuoni hapo na wale wanaoendelea na masomo ili watakapokuwa wanatafuta kazi wasisumbuliwe. Kwa kauli yake Mheshimiwa Magufuli alisema “Hadi sasa kuna wahandisi 11,400 waliosajiliwa na Makandarasi 9,126” Mwisho wa Kunukuu.
RAI KUTOKA KWA MWANATANGA:
Kwakuwa sheria ni msumeno kama alivyosema Waziri nashauri wale wote waliojenga kandokando ya barabara hiyo kuanza kuchukua tahadhali mapema kwa kuwasiliana na Wataalam kutoka Wakala wa Barabara ili kujua kama wanaathirika na kupata maelezo ya kina kutoka Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi kujua utaratibu wa Stahiki zao ili kuepusha Migogoro isiyo ya Lazima.

THAMANI YA OKWI KUUZWA YAZIDI BAJETI YA SIMBA YA SHILINGI 1.6 KAZI IPO


HABARI HII IMEANDALIWA NA BLOG YA BIN ZUBERY 
MWENYEKITI WA SIMBA NA MBUNGE WA TABORA MJINI MHESHIMIWA ISMAIL ADEN RAGE AKITOA UFAFANUZI WA SUALA LA MCHEZAJI EMMANUEL OKWI WAKATI WA MKUTANO WA MWAKA WA SIMBA ULIOBAINISHA KUWA BAJETI YA SIMBA KWA MWAKA HUU NI SHILINGI BILIONI MOJA PINTI SITA (1.6 BILLION TANZANIAN SHILLINGS)
MAKAMU MWENYEKITI WA SIMBA KABURU NYANGE AKITOA MAELEZO YA USAJILI WA MRISHO NGASSA PAMOJA NA MIKAKATI YA SIMBA MSIMU WA 2012/2013
 KATIKA kile kinachoonekana kuwa ni kutaka kuwakomoa mahasimu wao wa jadi, Yanga, klabu ya Simba imetangaza kuwa tayari kumuuza straika wao Emmanuel Okwi kwa dau kufuru la dola za Marekani milioni 2, ambazo ni sawa na Sh. bilioni 3. Bei hiyo ya Okwi kwa Yanga inazidi mara 13 ya kiasi cha pesa walichokihitaji Simba wakati wakimuuza straika wao Mbwana Samatta kwenda klabu tajiri ya TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, ambayo ilikuwa ni dola za Marekani 150,000 tu, sawa na Sh. milioni 230! Mwenyekiti wa Simba, Ismail Aden Rage, ndiye aliyetangaza dau hilo linaloonekana wazi kuwa na dhamira ya kufuta ndoto za Yanga kumtwaa Okwi wakati akizungumza kwenye mkutano wa klabu hiyo ya Msimbazi uliofanyika kwenye ukumbi wa Bwalo la Mafisa wa Polisi Oysterbay jijini Dar es Salaam.
MAMIA YA WANACHAMA WA SIMBA WAKIWASILIKILIZA VIONGOZI WAO WAKATI WA MKUTANO
 Aidha, dau hilo la Okwi pia linazidi takriban mara mbili ya bajeti ya Simba kwa mwaka ujao wa fedha ambayo ilisomwa jana kwenye mkutano huo na kukadiriwa kuwa haitazidi Sh. bilioni 1.6.
Rage alisema kuwa Okwi bado ni mchezaji halali wa klabu yao na kama Yanga wanamuhitaji kweli, basi watoe fedha taslim kiasi cha dola za Marekani milioni 2 (Sh. bilioni 3).

WANASIMBA WAKIWA MKUTANONI
Hata hivyo, inakumbukwa kwamba ni wiki iliyopita tu, Simba ilisema kuwa inatarajia kumuuza Okwi kwa euro 600,000 (sawa na Sh. bilioni 1.1) kwa mabingwa wa Austria, klabu ya Redbull Salzburg ambayo ilishiriki hivi karibuni ilitoka kushiriki hatua ya awali ya Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya.
Viwango tofauti vya bei ya mchezaji huyo, vinamaanisha kwamba Simba iko tayari kumuuza Okwi kwa bei poa Ulaya kuliko kumuona anajiunga na Yanga; na kwamba thamani ya straika huyo wa kimataifa wa Uganda ni mara 13 ya Mbwana Samatta waliyemuuza kwa TP Mazembe.
Akieleza zaidi kwenye mkutano huo uliohudhuriwa na wanachama zaidi ya 700, Rage alisema kuwa kwa vyovyote vile, Okwi hawezi kukataa ofa ya mshahara wa euro 30,000 (sawa na Sh. milioni 57) kwa mwezi nchini Austria na kujiunga na watani zao, Yanga ambao wanasemekana wako tayari kumlipa mshahara wa Sh. milioni 2.5 kwa mwezi endapo atakubali kujiunga nao.

Aug 5, 2012

ROBIN VAN PERSIE - HAVUTIWI NA CITY, JUVE WANAKATAA TAMAA, NI GHALI SANA KWA MANCHESTER UNITED, VIGUMU KUBAKI ARSENAL. NINI HATMA YAKE?????.


Robin Van Pesie - Niende wapi??????

Ni wapi ambapo RVP atacheza msimu ujao???

Robin Van Persie yupo katika hatari ya kuishiwa machaguo - na huku Arsenal wakiwa wanakaribia kukamilisha rasmi usajili wa Santi Cazorla, hali inazidi kuwa mbaya kwa upande wake.

Van Persie ana klabu tatu ambazo zinamtaka: Juventus, Manchester City na Manchester United.

Juventus wameanza kukata tamaa ya kumsaini, wameshatuma ofa ambayo tayari imeshakataliwa na Arsenal na wapo tayari kumpa RVP mkataba wa miaka 5 na mshahara wa £190,000 kwa wiki baada ya kodi.

Lakini huku mabingwa hao wa Italia wakiwa katika hatihati ya kocha wao kufungiwa kwa kutojkna kuhusishwa na kashfa ya upangaji wa matokeo wa mechi, hivyo suala hili linampa wakati mgumu Van Persie kwenda Turin.

Juventus walianza kwanza kutuma ofa ya kiwango chini ambayo ilikataliwa na na Arsenal, wamerudi tena na ofa nyingine ambayo bado haijafikia kiasi cha fedha ambacho Arsenal wanahitaji.

Manchester United wanaonekana kujiamini wakiwa nyuma ya pazia lakini hisia kwamba hawatoongeza ofa yao pamoja na kwamba ofa yao ya mwanzo inayokadiriwa kufikia £15 millioni kupigwa chini na Arsenal.

United wanaelewa fika kwamba van Persie anatimiza miaka 29 mwezi huu, ana rekodi mbovu ya majeruhi na thamani yake ya kuuzwa tena baada ya kusajiliwa na timu mpya kutoka Arsenal inaweza kukaribia na kutoka patupu. Haya yote yapo kinyume na sera ya uhamisho ya klabu ya akina Glazers.

Labda United wanahisi kwamba Arsenal watalazimika kupunguza bei wakati mwezi huu ukiwa unaishia kwa kuwa wanaweza kuwa radhi kumuuza chini ya £20 millioni kuliko kumpoteza bure msimu ujao wakati mkataba wa Van Persie utakapokuwa unaisha.

Pia inaaminika kwamba van Persie havutiwi na Manchester City  - japokuwa tayari wameshatuma ofa kwa ajili yake. City wanaelewa juu ya klabu yao kutomvutia RVP na ndio maana wanajaribu kuangalia namna ya kuweza kumsaini wabadala kama Gonzalo Higuain.
Gonzalo Higuain - Mbadala wa Van Persie @Etihad Stadium?

Lakini pia City inabidi wauze wachezaji wake wengi ili wasajili. Uongozi wa klabu hiyo unataka kwanza kuwaondoa wachezaji wanne wanaokula mishahara mirefu kama Carlos Tevez, Emmanuel Adebayor, Roque Santa Cruz na Edin Dzeko kabla ya kununua wachezaji wengine.

Hilo linamuacha van Persie njia panda. Baada ya mwanzo kabisa kuonekana kuvutiwa na Juventus, wasiwasi wa kumpoteza manager ambaye aliiongoza timu hiyo kutwaa ubingwa ni habari mbaya. Dalili zote sasa zinamuelekeza Old Trafford, lakini United wapo mbali na fedha wanayoitaka Arsenal ukizingatia mchezaji anakinzana na sera za usajili za klabu hiyo.

Lakini ni jambo lisilofikirika kwa Arsenal kutomuuza kipindi hiki cha kiangazi. Wakati Wenger akionekana kutaka kuendelea kuwa na van Persie, lakini Gunners inabidi wamuuze mdachi huyo. Kingine chochote kitakuwa hakielezeki chini utawala wa sasa mwaka mmoja baadae.

Lakini hilo linamuacha Van Pesie - ambaye ameshasema hatosaini mkataba mpya   - katika hali isiyoeleweka.

Je aende City na kupingana na matakwa ya nafsi yake?

Aombe United warudi na ofa nzuri zaidi - japo hilo ni kinyume na sera za usajili za klabu hiyo?

Au aende Juventus, klabu ambayo ipo katikati ya kimbunga?

Juventus siku zote ilionekana itabidi wamshawishi sana Persie ili kuweza kumpeleka Italy. Imekuwa vigumu zaidi sasa.

Huku pia kunaonekana hakuna namna nzuri ya kurudi Arsenal - mashabiki wanaweza kumkataa na kutompa sapoti.
LUKAS PODOLSKI

Arsenal tayari wameshaanza kujipanga kwa maisha bila Van Persie. Lukas Podolski bado hajapewa namba ya jezi lakini kwa hakika yupo njiani kuichukua namba ya jezi ya Van Persie - namba 10.

Klabu hiyo tayari imeshamnunua Olivier Giroud. Podolski anaweza kucheza kushoto, nyuma ya mshambuliaji au katikati  na Giroud na mfungaji mzuri.

Wenger pia atakuwa na machaguo mengine huku Theo Walcott akiwa kulia, Gervinho yupo pembeni bado, huku Andre Santos akiwa anachezeshwa winga ya kulia kwenye mechi za pre-season

Na sasa Arsenal wamebakiza kutangaza tu rasmi kuhusu usajili wa Santi Cazorla. Akiwa na miaka 27 tayari ni mchezaji wa daraja la dunia, akiwa ameshaichezea mechi 45 Spain na kushinda Euro na World Cup, na pia anatajwa kuwa mmoja ya wachezaji wenye uwezo mkubwa kama ilivyo kwa akina Cesc Fabregas.
Cazorla na Alonso

Inaaminika tayari Cazorla ameshaini mkataba wa miaka mitano na kupima vipimo vya afya, Wenger anaweza kumtumia Cazorla kama playmaker akipangwa namba 10 katika msimu ujao unaoanza siku chache zijazo.

Pia kuna uwezekano wakampata kwa mkopo kingo wa Real Madrid Nuri Sahin.

Kwa hakika Arsenal wanajenga upya timu yao, maisha bila Van Persie - hata kabla hajaondoka.
Mdachi huyo amekuwa na msimu bora katika maisha yake miezi 12 iliyopita, akifunga mabao mazuri kwa wingi lakini sasa upepo unaweza ukawa umemgeukia.

Nini hatma ya Robin Van Persie - kwa hakika tutafahamu siku chache zijazo..

Nawasilisha - Aidan Seif Charlie
kwa hisani ya (www.shaffihdauda.com)

BAADA YA AARON RAMSEY KUFUNGA BAO JANA - MTU MWINGINE MAARUFU AFARIKI DUNIA


Aaron Ramsey akifunga bao jana dhidi ya Korea ya kusini.

Jamani huu ni mkosi au ni bahati mbaya tu inatokea?
Kila mchezaji wa Arsenal Aaron Ramsey anapofunga bao basi masaa kadhaa  baadae kuna kifo cha mtu maarufu kinatokea. Hii ilianza wakati alipofunga bao dhidi ya Sunderland na masaa 24 baadae mwanamuziki Whitney Houstona akafariki dunia, na pale alipofunga goli la ushindi ya Manchester United - majeshi ya Marekani yakamuua Osama Bin Laden, Ramsey alipowatungua Tottenhm, mbunifu, mmiliki na aliyekuwa CEO wa kampuni inayotengeneza bidhaa za Apple ya Marekani akafariki dunia, na tena alipowafunga Marseille kwenye Champions league - Colonel Maamar Gaddafi akauwawa na majeshi ya waasi nchini kwake Libya.

Marehemu  - Kirk Urso
Ikiwa imepita miezi kadhaa wakiwa hajafunga bao, jana akiwa anaiwakilisha timu ya taifa ya Uingereza kwenye michuano ya Olympic katika hatua ya robo fainali Ramsey akafunga bao, na kama ilivyo ada asubuhi ya leo klabu ya Columbus Crew ya Marekani imetangaza kwamba mchezaji wake Kirk Urso amefariki akiwa na miaka 22.


By Aidan Seif Charlie(www.shaffihdauda.com)

TENGA KUFUNGUA KOZI YA UONGOZI YA FIFA


Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) Bw. Leodiger Tenga anatarajia kufungua Kozi ya Uongozi na Utawala ya Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) inayoanza kesho (Agosti 6 mwaka huu) Msimbazi Center jijini Dar es Salaam.
 
Kozi hiyo itakayokuwa na washiriki zaidi ya 30 itamalizika Agosti 11 mwaka huu na itaendeshwa na Wakufunzi kutoka FIFA na itafunguliwa saa 3 asubuhi. Wakufunzi hao ni Barry Rukoro anayetoka Namibia, Henry Tandau (Tanzania) na Senka Kanyenvu (Botswana).
 
Baadhi ya washiriki wa kozi hiyo ni Makamu wa Kwanza wa Rais wa TFF, Athuman Nyamlani, Rais wa ZFA Amani Makungu, wajumbe wa Kamati ya Utendaji ya TFF; Ahmed Mgoyi, Blassy Kiondo, Stanley Lugenge, Khalid Abdallah, Hussein Mwamba na Eliud Mvella.
 
Wengine ni Katibu Mkuu wa ZFA, Kassim Salum, Katibu Msaidizi wa ZFA, Masoud Attai, wenyeviti wa vyama vya mpira wa miguu vya mikoa ya Kagera (Jamal Malinzi), Dodoma (Nassoro Kipenzi) na Pascal Kihanga (Morogoro).
 
Makatibu wa vyama vya mpira wa miguu vya mikoa ya Mara (Mugisha Galibona), Mtwara (Vincent Majiri), Morogoro (Hamisi Semka), Kagera (Salum Chama), Tanga (Beatrice Mgaya) na Dodoma (Stuart Masima). Pia yumo Mwenyekiti wa Coastal Union, Ahmed Hilal na Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Clement Sanga.
 
Washiriki wengine ni Katibu Mkuu wa TFF, Angetile Osiah, Mkurugenzi wa Ufundi, Sunday Kayuni, Ofisa Habari, Boniface Wambura, Mkurugenzi wa Masoko na Matukio, Jimmy Kabwe na Mkurugenzi wa Mashindano, Saad Kawemba.
 
Wengine ni Ofisa Sheria wa TFF, Neema Lucumay, Ofisa wa Mpira wa Miguu wa Wanawake, Grace Buretha, Amina Karuma (Mpira wa miguu wa wanawake) na nahodha wa zamani wa Taifa Stars, Shadrack Nsajigwa.

JANUARI MAKAMBA AONGOZA MKUTANO WA WANABUMBULI JIJINI DAR ES SALAAM LEO

Mbunge wa jimbo la Bumbuli Mhe. January Makamba akiongea na wakazi kutoka wilaya ya  Lushoto jimbo la Bumbuli katika ukumbi wa Karimjee jijini Dar es salaam leo mkutano huo ulikuwa  unajadili maendeleo ya jimbo la  Bumbuli na kutambulisha shirika la maendeleo la  Bumbuli, January Makamba amesema katika kipindi cha mwaka 2011-2012 kiwango cha elimu ya wilaya hiyo imekuwa chini na kusababisha vijana wengi katika mkoa wa Tanga kuwa na sifa ya kuuza chipsi na kubeba mizigo badala ya kufanya kazi kwenye makampuni.
Mkurugenzi wa shirika la Bumbuli Bw. Najim Msenga (kushoto), mwenyekiti mteule wilaya ya Bumbuli Bw. Amiri Sheiza (kulia)katibu wa CCM wilaya ya Lushoto Bw. Loth Ole Lemeirut (katikati)wakijadiliana jambo mara baada ya kumalizika kwa mkutano huo leo
Wakazi kutoka jimbo la bumbuli wakiwa katika mkutano huo wa kujadili maendeleo ya wilaya ya Bumbuli
Kikundi cha ngoma kijulikanacho Mount  Usambara Voice kikitoa burudani katika mkutano huo
Katibu wa CCM wilaya ya Lushoto Bw. Loth Ole Lemeirut (kushoto)na mwanakamati wa shirika la Bumbuli Bw. Naaman Shauri wakifuatilia kwa umakini mada iliokuwa ikendelea katika mkutato huo leo

THE DON HIMSELF

Karibuni sana kwenye blog hii ya kijamii iliyosheheni makila kitu kuanzia siasa uchumi afya na burudani kwa ujumla wake.uingiapo kwenye blog hii ni mengi ambayo utapata nafasi ya kukutana nayo,kumbuka mawazo yako ndo hasa yanayojenga na kunifanya niwe na ufanisi zaidi.kariiiiiiibuuuuuuuuuuuu saaaaaaaaaaaaaaanaaaaaaaaaa.(THE DJ HIMSELF-JIWE)

Followers

BLOG ZA MARAFIKI

Search This Blog

ZILIZOPITA

DUNIA MUZIMA