Ujenzi wa Barabara ya urefu wa Kilomita sitini na tano (65) kutoka
Bagamoyo kupitia Kiwangwa hadi Msata yenye urefu wa kilomita 65
umekamilika kwa asilimia takribani 59.6% baada ya jumla ya kilomita 35
kukamilika kwa kiwango cha lami. Wakala wa Barabara Tanzania TANROADS
wanakusudia kutumia barabara hii kwa Magari yote ya Usafiri wa Umma
yanayotokea Kanda ya Kaskazini kwa maana ya Mikoa ya Tanga, Kilimanjaro,
Manyara na Arusha kutumia barabara hii pindi itakapokamilika ili
kupunguza msongamano kwenye barabara ya Morogoro hususan pale Chalinze
na Kibaha kwenye Mzani (Weight Bridge).
|
HUU NDIYO MUONEKANO WA BARABARA YA MSATA-KIWANGWA-BAGAMOYO KWA SASA |
Matarajio ya hivi karibuni ni kujenga kituo cha Mabasi kwa ajili ya
Mabasi ya Mikoani eneo la Kunduchi yalipokuwepo Machimbo ya Kunduchi
yaliyofungwa ili kuyafanya mabasi yanayotokea Kanda ya Kaskazini kuanzia
Safari zake na kuishia kwenye Kituo hicho kipya pindi kitakapokamilika
ili kupunguza msongamano katikati ya Jiji.
|
HAPA NI MJINI KIWANGWA ENEO MAARUFU KWA ULIMAJI WA MANANASI WILAYA YA BAGAMOYO MKOA WA PWANI |
Mradi mwingine ni ujenzi wa barabara ya Bagamoyo Saadan Pangani hadi
Tanga kwa Kiwango cha lami utakaoyawezesha mabasi yatokayo Tanga na
Mombasa kupitia barabara hiyo ili kukuza utalii wa Mbuga pekee Duniani
ambayo Wanyama huwa wanakwenda Beach (MBUGA YA SAADAN) ambayo inaambaa
na Ukingo wa bahari kutokea Bagamoyo hadi Tanga. Kwa kufanya hivyo Mbuga
hii itakuwa kwa kasi na kuwa kivutio kwa Watalii kuja kuona Maajabu
hayo ya Dunia ya wanyama wanaoshinda Beach kupunga Upepo. Mradi huu wa
Bagamoyo Saadan Pangani umeshaanza kutokea Muheza kwa kiwango cha lami
na ujenzi unakwenda kwa Kasi ya kutia moyo.
|
BAADHI YA
VIZUIZI VYA KUONYESHA TAHADHALI KWA WATUMIAJI WA BARABARA HIYO YA MSATA
KIWANGWA BAGAMOYO WAKATI WA UJENZI KUEPUSHA AJALI |
Sambamba na Mradi huu pia Wakala wa Barabara Tanzania unaendelea na
ukarabati wa barabara ya Chalinze Segera Tanga ambao awamu ya kwanza
iliishia eneo la Kitumbi Wilaya ya Handeni chini ya Kampuni ya Wachina
na sasa ujenzi huo unaendelea kuanzia Kitumbi hadi Kwamichi Tanga chini
ya Kampuni ya Kiisrael iitwayo SBI International. Ukarabati huu sasa
unaendelea kwa kasi sana na unatarajiwa kukamilika katikati ya mwaka
1913.
|
WAJENZI KAZINI BARABARA YA MSATA KIWANGWA BAGAMOYO |
Aidha ujenzi wa awamu ya kwanza wa kilomita 76 kuanzia Segera hadi
Mkumbara kupitia vijiji na miji ya Segera Mashine, Chang'ombe,
Mailikumi, Mandera, Kwakombo, Kwamdulu, Korogwe Mjini, Msambiazi,
Mgobe,
Nkhalekwa,
Magila, Gereza, Kwasunga, Kwasunga Mpirani, Makuyuni, Madumu, Madala,
Chepete, Chekelei, Mwisho wa Shamba, Mombo Mjini, Jitengeni, Kasiga,
Mazinde, Mheza, , Kwenangu, Magila, Mkumbara, Goha, Manga, Mtindiro,
Mkomazi na
Bwiko. Mradi huu unajengwa na Kampuni ya STRABAG ambayo pia inajenga
Barabara yenye urefu wa kilomita 21.9 ndani ya jiji la Dar es Salaam kwa
ajili ya Mradi wa Mabasi Yaendayo Haraka-DART.
|
VIFAA VYA UJENZI VYA KISASA KWENYE BARABARA YA MSATA KIWANGWA BAGAMOYO |
No comments:
Post a Comment