Na Emmanuel Msigwa aka DJ Msigwa, Radio journalist,
Presenter, Radio DJ & Club DJ
Natumaini jina la Linex si geni miongoni mwa majina makubwa
katika tasnia ya muziki hapa nchini. Historia yake si kubwa ukilinganisha na
wasanii wengine. Ngoma yake ya Mama Halima ndiyo iliyomfungulia njia. Moyo wa
subira ikaja kupigilia msumari pale alipofikia na kuanzia hapo akapewa
“mashavu” katika ngoma mbalimbali kuanzia Sina Jiwe, Kankutume na nyinginezo.
Kifupi ni msanii mkali ambaye alikuja kuhit baada ya
kuamua kutumia vionjo vya kabila lake la kiha kutoka Kigoma na utaona hata
katika ngoma ya Leka Dutigite alipewa yeye kufanya kiitikio “chorus” kwakuwa tu
anaoufahamu mkubwa juu ya matumizi ya lugha yao. Naamini hiyo ndiyo silaha
ambayo amekuwa akiitumia katika ngoma zake.
Achilia mbali uwezo wake mkubwa katika kuimba, Linex amekuja
pia na mtazamo mpya wa utunzi wa mashairi ya nyimbo zake nyingi. Angalia
hadithi ya wimbo wa Mama Halima, Ngekewa, Moyo wa Subira na huu wa sasa Aifola.
Utakubaliana nami kuwa jamaa ni mbunifu na ujumbe wake umekuwa rahisi kufika
kwa walengwa wake…………big up sana.
Lakini tukiachana na ubora wa matoleo ya nyimbo zake
bado Linex anaweza kuwa mmoja kati ya wasanii wa kitanzania walau wanaojaribu
kuweka uhalisia wa video zake na audio zake kwa maana ya kwamba mashairi yake
yake yanawakilisha pia matendo yake katika video.
Aangalia vizuri Ngekewa, njoo katika Moyo wa Subira na
angalia wa sasa hivi Aifola. Sio kwamba anafanikiwa kwa 100% yapo makosa madogo
madogo ambayo amekuwa akiyafanya katika video zake. Mfano anapokuwa anaimba
ishara ( kwa maana anapotumia) lugha ya vitendo katika video nafikiri siyo
sahihi kwa kuwa katika video tunahitaji zaidi tuone lugha hizo za ishara kwa
kuona matendo halisi.
Makosa mengine ambayo anayafanya Linex yanachangiwa na
timu yake ya video. Mfano katika Aifola,
video imefanywa na Adama Juma wa Visual Lab, Next Level.
Huyu ni kati ya waandaji bora wa video hapa nchini
lakini kuna makosa anayoyafanya hasa katika
baadhi ya “angleshoot” ni kama vile hamtendei haki. Mfano katika closeup
shoot ambapo Linex anaonekana akiwa ametupia suti nzuri sana na imempendeza
lakini cha ajabu katika fullclose shoot anaoneka kavaa raba.
Kwa mtazamo wangu wakati wa editing wangeondoa kipande
kile au kuna kipande Linex yupo na yule msichana wake wamekaa sijui ni sebuleni,
sijui ni wapi, lakini inaonekana zile sofa ni kama zimefunikwa, yaani
hazitumiki au ni dukani na hiyo ni baada ya fullclose shoot yake.
Otherwise hayo si makosa ya Linex lakini timu yake
ilipaswa kuliangalia hilo.
Tuna tatizo kubwa sana katika utoaji wa video zetu ndiyo
maana video hizo zimekuwa na makosa ya hapa na pale, wakati Ne-yo anaelezea
ubora wa video yake ya So Sick, alisema
mtayarishaji wake Hype Williams, alitumia miezi 6 kuipika video hiyo na
ilipotoka kila mmoja alikuja kuikubali.
Timu zetu za video zisiharakishe kazi za wasanii hao ili
tuone ubora tunaoutaka na pia kuviendeleza vipaji vya wahusika wa nyimbo hizo.
Lakini yote ni yote Linex amekuwa akijaribu kutuonyesha uhalisia katika kazi za
video kwa maana ya storyboard yake tunaiona.
Endelea na ubunifu huo muziki unapokuwa mzuri hauitaji
kulazimishwa ili uweze kuukubali uzuri huo, wengine waige kutoka kwako Linex.
BIG UP SANA MWANA KIGOMA ALL STARS…………..!
No comments:
Post a Comment