Jul 26, 2010

ZANZIBAR NAO NI FULL KUJIPANGUSA

Hapa Mwandishi Siddy akiwa na Nina na Barnaba.
Msanii kutoka Arusha anayejulikana kwa jina la Angel ametikisa Ngome Kongwe kwa jinsi alivyonyonga kiuno kama pia, kitu kilichowafanya mashabiki kumshangilia kwa nguvu wakati akiimba jukwaani katika tamasha la Fiesta lililofanyika usiku huu mjini Zanzibar na kushirikisha wasanii wengi wa muziki wa kizazi kipya Bongofleva.
Tamasha hilo linafanyika baada ya lile la Tanga lililofanyika jumamosi kwenye uwanja wa Mkwakwani mkoani humo na linadhaminiwa na kampuni ya bia ya Serengeti Breweriers (SBL) ya jijini Dar es Salaam.

Barnaba na Nina wakitafuta muafaka wa SMS!
Binamu Mwana FA akiwarusha mashabiki wake.
Mustafa wa G5 Click akiwa kazini Ngome Kongwe.
Mwasiti naye hakubaki nyuma, alikamua vilivyo na kuwapambanisha mashabiki ambao aliwaita vidume (hawapo pichani), yote ikiwa ni burudani tu.
Amini naye akafanya mambo makubwa katika tamasha hilo kama unavyomuona.

Msanii huyu pia alikuwepo na akavuta hisia za mashabiki kwa staili yake.
Mr. Wise akitoa burudani na mrembo ambaye alivuta hisia za mashabiki wengi usiku huu na kushangiliwa kwa nguvu. (picha kwa hisani ya mzee wa full shangwe)

MASHUJAA WAKUMBUKWA

Rais Jakaya Kikwete pamoja na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama,Jenerali Davis Mwamunyange na viongozi wengine wa jeshi wakitoa heshima zao jana wakati wa maadhimisho ya siku ya kuwakumbuka mashujaa waliopigana vita kuu ya Dunia 1939-1943.maadhimisho hayo yamefanyika leo asubuhi katika viwanja vya Mnazi Mmoja, jijini Dar es Salaam.
Maadhimisho hayo yamehudhuriwa na wageni mbalimbali wakiwemo Mabalozi, Mawaziri, Viongozi wa vyama vya siasa, Marais na Mawaziri wakuu wastaafu . viongozi pamoja na wananchi.
(Picha zote ni za Aron Msigwa na Mwanakombo Jumaa) - MAELEZO.

afu ya viongozi wakuu serikali Mabalozi tasisisi na chama
Mzee Ali Hassani Mwinyi Rais Mstaafu (kushoto) akisalimiana na kanalli mstaafu JWTZ mzee Shadrack Malinzi.
Kanali mstaafu wa JWTZ mzee Shadrack Malinzi (87) akiongea na waandishi wa habari baada ya maadhimisho katika viwanja vya mnazi.
Kiongozi wa mabalozi nchini Balozi Juma Khalfan Mpango akiweka shada la maua jeo jijini mkatka maadhimisho ya mashujaa.
Baadhi ya askari wakiwa kaatika viwanja vya Mnazimmoja jana

Jul 24, 2010

SI MSHAKIONA?


Hii ndio chupa yenyewe ambayo ilikuwa ikisubiriwa kwa hamu sana na watu wengi.

Wanadada mrembo kabisa akiionyesha chupa nyenyewe.
wadau wa tembo kama kawa huwa wanajumuika sana popote liwapo gambe.
sasa hiki ndo kile ambacho ni zaidi ya bora aisee.
Maboss wa Ndovu wakipiga chiazi kwa pamoja kusherehekea mafanikio haya
Kaka choka nae kama kawa huwa hakosi kwenye minuso kama hii.
dadaz ni full kujiachia aisee .


M-Net's Big Brother All Stars- Nomination Recap


Monday was just the first day of M-Net’s Big Brother All Stars – and already, it was nomination time! The housemates spent some time getting to know each other on Sunday night as dancehall superstar Sean Paul chilled with them in the house. All the housemates know the game inside out - and the mind-games are already in full swing! The housemates were told about how their game of secrets was to work, which only added to the drama. After an entertaining first evening where they shared a few drinks and caught up, the housemates had a late start on Monday morning. Late they may have been, but their awakening was a rude one as Big Brother immediately started summoning them to the Diary Room for nominations. Once everyone had had their say – or in Mwisho’s case, not much to say – it was Lerato and Mwisho who gathered the most nominations. Big Brother, never shy of a twist, didn’t tell the housemates who their nominations

had put in the firing line and instead announced that all housemates were up for eviction this week. During their Nomination Sessions, a few of the housemates had trouble remembering the names of the people they wanted to nominate, while others already seem to have a firm handle on who needs to go!
The Housemate who receives the least number of votes will be evicted. You can vote to keep a nominated housemate in the house in three different ways: 1. Via the website, or the WAPsite on your mobile phone. 2. By sending an SMS 3. Using MXit To vote on the website: Cast your vote by clicking on the housemate who you want to keep in the house.(You can vote once per hour per registered email address.) To vote via SMS: send the word VOTE followed by the housemate's name to the number for your country (displayed below). For example if you are voting from Botswana send Vote Thato to 15626. SMSes are charged per specified network tariffs in the various countries. VAS rates apply. Free minutes do not apply. (You can vote 100 times by SMS per mobile number during each voting period.) Tanzania Vodacom 15726 Tsh 600 Tigo 15726 Tsh 600 Zantel 15726 Tsh 600 Zain 15726 Tsh 600 Sasatel 15726 Tsh 600

TANGA NI FULL KUJIPANGUSA AISEE!!!!!!!!!!


Nao vijana wa kundi maarufu na linalotikisa nchini kwa sasa katika burudani THT lilifanya mambo makubwa jukwaani kutokana na staili mbalimbali za uchezaji wao hivyo kuwafanya mashabiki waliohudhuria kwenye tamasha hilo katika uwanja wa mkwakwani kulipuka kwa shangwe za kujipangusa na Fiesta 2010 kila mara wakati kundi hilo lilipokuwa likicheza jukwaani.

Meneja Mkuu wa Uhusiano, mwasiliano na Jamii wa kampuni ya Bia ya Serengeti Teddy Mapunda wa pili kutoka kushoto akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wenzie Nandi Mwiyombela wa nne na Bahati Singh aliyesimama nyuma ya Teddy na juma Nature mwenye fulana nyeusi mstari wa mbele pamoja na wasanii mbalimbali jana usiku kwenye tamasha la Fiesta Jipanguse 2010 katika Uwanja wa Mkwakwani mkoani Tanga.

Mashabiki mbalimbali walijitokeza kwenye tamasha hilo kama unavyoona kwenye picha.

Chui wa Serengeti walishiriki kikamilifu katika kunogesha tamasha hilo.

Hapa sio kwamba wameamrishwa kunyanyua mikono yao juu hapana, ni burudani ya Fiesta Jipanguse 2010.

Msanii maarufu Juma Nature kutoka kundi la TMK Halisi akilishambulia jukwaa katika tamasha la Fiesta Jipanguse 2010 lililofanyika usiku wa kuamkia leo kwenye uwanja wa Mkwakwani mkoani Tanga na kujumuisha wasanii wengi wa muziki huo.
Tamasha hilo lilivuta hisia za mashabiki wengi na wapenzi wa muziki huo kutoka maeneo mbalimbali ya vitongoji vya mkoa wa Tanga waliokuwa wakiimbishwa kila wakati na kunyanyua mikono yao juu mara kwa mara.
Fiesta Jipanguse 2010 tayari imeshafanyika katika mikoa ya Dodoma, Morogoro, Arusha, Kilimanjaro na Tanga na leo inaendelea tena wakati itakapofanyika katika visiwa vya Zanzibar usiku wa leo, wadhamini wakuu wa tamasha hilo ni kampuni ya bia ya Serengeti Breweriers LTD.
(Picha kwa hisani ya Michuzijunior).

Jul 20, 2010

HILI NDO JESHI LA SIMBA SPOTRS CLUB



Klabu ya simba imetangaza kikosi cha wachezaji ishirini na sita .


JUMA KASEJA
ALLY MUSTAFA.
RAMADHAN SHAMTE .
SALUM KANONI
MUSSA MGOSI.
JUMA JABU.
JUMA NYOSO
AMIR MAFTAH.
JOSEPH OWINO.
MOHAMED BANKA.
KEVIN YONDAN.
DAVID NAFTARI.
ABDULLHIM HUMOOD.
JERRY SANTO .
HILALI ECHESA.
AMIR KIEMBA.
SHIJA MKINA.
NICO NYAGAWA.
RASHID GUMBO.
UHURU SULEIMAN.
SALUM AZIZ.
EMANNUEL OKWI.
PATRICK OCHAN.
MBWANA SAMATA.
MOHAMED KIJUSO.
CHARLES HAULE..


KOCHA MKUU.
PATRICK PHILI


MAKOCHA WASAIDIZI .
SAID AMRI.
SULEIMAN MATOLA

Kikwete ametaja sababu kuu za umasikini wa Bara la Afrika












Na Mwandishi Maalum, Madrid, Hispania

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete ametaja sababu kuu za umasikini wa Bara la Afrika, na kupendekeza mambo saba ambayo anasema kuwa yakifanyika yatachangia kuliondoa Bara hilo katika udhalili wa umasikini wa sasa.

Aidha, Rais Kikwete amesisitiza kuwa Bara la Afrika limeboreka sana katika miaka 15 iliyopita, na sasa liko tayari kutoa mchango wake katika jumuia ya kimataifa kama juhudi za pamoja za Bara hilo na Jumuia ya Kimataifa zitaendelezwa kuboresha hali katika Bara hilo.

Rais Kikwete alisema hayo kwenye ufungaji wa Mkutano wa Kimataifa Kuhusu Maendeleo ya Afrika na Nafasi ya Siasa za Maendeleo katika Bara la Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara uliofanyika katika Jumba la Palacio de Congresos de Madrid, mjini Madrid, Hispania.

Rais Kikwete alikuwa miongoni mwa viongozi wa kimaendeleo kutoka Bara la Afrika walioalikwa kuhudhuria Mkutano huo ulioandaliwa kwa pamoja na chama tawala cha Hispania cha Socialist and Workers Party of Spain (PSOE), chama tawala cha Afrika Kusini cha African National Congress (ANC) pamoja na taasisi isiyokuwa ya kiserikali yenye uhusiano wa karibu na PSOE ya Fundacion Idea.

Pamoja na Rais Kikwete kwenye ufungaji wa Mkutano huo walikuwa ni Rais wa Cape Verde, Mheshimiwa Pedro Pires; Waziri Mkuu wa Hispania, Mheshimiwa Jose Luis Rodriguez Zapatero; Waziri Mkuu wa Ethiopia, Mheshimiwa Meles Zenawi; Rais wa zamani wa Serikali ya muda ya Liberia, Mheshimiwa Amos Sawyer; na Rais wa chama tawala cha FPI cha Ivory Coast, Mheshimiwa Pascal Affi N’Guessan.

Wengine walikuwa ni Rais wa chama tawala cha Ghana cha National Democratic Congress, Mheshimiwa Kwabena Adjei na Katibu Mkuu wa Chama cha Kisoshalisti cha Senegal, Mheshimiwa Ousmane Tanor Dieng ambaye pia alikuwa mgombea urais wa nchi hiyo katika uchaguzi mkuu uliopita.

Akizungumza kwenye mkutano huo, Rais Kikwete alitaja sababu kuu na chanzo cha umasikini wa Afrika kuwa ni pamoja na mazingira adui ya kimataifa dhidi ya Bara la Afrika ambayo ni pamoja na ukoloni, mfumo adui kabisa wa kiuchumi duniani ikiwa ni pamoja na nafasi finyu za Afrika kufanya biashara na ukosefu wa masoko ya uhakika ya Afrika kuuza bidhaa zake, tena kwa bei ya haki.

Rais Kikwete amesema kuwa sababu nyingine za umasikini wa Afrika ni siasa za nchi za Afrika zenyewe ambazo huko nyuma hazikuzaa matunda yaliyokusudiwa na zilizolazimishwa kwa nchi za Afrika na taasisi za kimataifa za Bretton Woods – yaani Benki ya Dunia na Shirika la Kimataifa la Fedha Duniani (IMF).

“Lakini makosa mengine yalikuwa ya kwetu wenyewe, ikiwa ni pamoja na sera ambazo hazikuzaa matunda na mgawo mkubwa mno wa ukosefu wa utulivu wa kisiasa, mapigano, upinduaji wa Serikali,” amesema Rais Kikwete na kuongeza huku akishangiliwa na mamia ya washiriki wa mkutano huo:

“ Tulikuwa hakuna nafasi ya kufikiria jinsi ya kuondoa umasikini na kuendeleza watu wetu kwa sababu tulikuwa na kazi na shughuli za kupigana, kugombea madaraka na kuuawa.”

Hata hivyo, Rais Kikwete amesema kuwa hali ya Afrika imebadilika sana katika miaka 15 iliyopita. “Hili siyo tena Bara la ovyo, siyo Bara ombaomba tena. Tuna utulivu mkubwa zaidi wa kisiasa, ukiondoa Somalia, Bara la Afrika halina mgogoro wa kisiasa ambao kwa sasa hauna majibu yake. Demokrasia inapaa, kuna hali bora zaidi ya utawala bora, tunapambana kweli kweli na rushwa, tunajali haki za binadamu. Tunafanya vizuri, lakini tunahitaji kufanya vizuri zaidi kwa kuwekeza katika hali na maisha ya watu wetu.”

“Sasa tufanye nini?” Rais Kikwete alijiuliza mwenyewe na kuanza kutoa majibu ya kuongeza kasi ya kulitoa Bara la Afrika na watu wake katika umasikini akisisitiza:

“La kwanza ambalo lazima tufanye ni kudumisha na kulinda mafanikio ambayo tumeyapata mpaka sasa. La pili ni kuwekeza zaidi katika watu wetu. Tunahitaji kuboresha zaidi elimu, kuwapa watu wetu maji safi na salama, tunahitaji kujenga miundombinu bora zaidi kwa maana ya barabara, njia za umeme, kuboresha mifumo ya reli na bandari zetu.”

Rais Kikwete amesema kuwa jambo la tatu linalostahili kufanyika ni kufanya mageuzi ya kuboresha kilimo cha Afrika.

“Asilimia 70 ya watu wetu wanaishi katika sehemu za mashamba na shughuli yako kubwa ni kilimo. Hii ndiyo njia rahisi ya kuwatoa watu wetu katika umasikini. Afrika ina asilimoa 10 tu ya wakazi wote wa dunia, lakini Bara letu lina asilimia 30 ya watu wote masikini zaidi duniani.”

Rais Kikwete amezitaja njia nyingine za kulitoa Bara la Afrika katika umasikini haraka zaidi kuwa ni pamoja na kuanza mageuzi ya ujenzi wa viwanda hasa vile za kuongeza thamani ya mazao ya kilimo.

“Hatuwezi kuendelea kuuza mazao ghafi kwenye masoko ambayo yanabadilisha thamani ya mazao hayo na kutuuzia mazao yetu wenyewe tena kwa gharama kubwa zaidi.”

Ameongeza kuwa njia nyingine za kulitoa Bara la Afrika katika umasikini ni kuongezeka kwa uingiaji wa mitaji katika Bara hilo. Kwa sasa Bara la Afrika linapata asilimia mbili tu ya mitaji yote ya uwekezaji duniani.

Rais Kikwete ametaja ongezeko kubwa zaidi la biashara kama njia nyingine ya kupunguza umasikini wa Afrika. Kwa sasa Afrika inachangia asilimia mbili tu katika biashara duniani. Pia ametaja umuhimu wa kuongeza kasi ya ushirikiano wa kikanda miongoni mwa nchi za Afrika na umuhimu wa kumalizika kwa mazungumzo ya kuleta mfumo mpya wa kibiashara duniani chini ya majadiliano ya Doha.

Akizungumza baada ya hotuba ya Rais Kikwete, Waziri Mkuu Zapatero alikubaliana na mapendekezo mengi ya Rais Kikwete na kuahidi kuwa Hispania imeamua kuwa sehemu na kuchangia ya maendeleo ya Afrika. “Napenda kutangaza kuwa kuanzia leo hii Hispania iko ndani ya Afrika, na Afrika iko ndani ya Hispania.”



SOMETHING NEW IS COMMIN,WHAT DAT?WAIT N YOU WILL SEE.





Kunako huu mnara uliopo kando ya bara bara ya moroko kama unavyoonekana umefichwa ila kilichofichwa hakijulikani na mimi na wewe bado hatujakijua ingawa kwa upande wangu nilifanikiwa kuchungulia ila wewe unapaswa kusubiri na kuona baada ya hizo 4 dayz.


MTOTO WA NYOKA NI NYOKA-JANUARY MAKAMBA NAYE AJITOSA BUMBULI


Januari Makamba akimsalimia mtoto aliyekuwa akipiga ngoma wakati wa shamrashamra za kuchuka fomu jimboni Bumbuli mkoani Tanga.

Januari Makamba akilakiwa kwa shangwe na wana Bumbuli mkoani Tanga jana wakati alipochukua fomu za kuwania ubunge kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi jimboni humo mamia ya wana CCM jana walijitokeza kuchuyka fomu zakugombea ubunge na udiwani katika uchaguzi mkuu ujao unaotarajiwa kufanyika Oktoba mwaka huu.

Wana CCM wakimsindikiza Bw. Januari Mkamba kwenda kuchukua fomu zake za kuwania ubunge wa jimbo la Bumbuli.

Jul 18, 2010

FULL MAKEKE MJENGONI AISEE


Wakati washiriki wakiingia ndani hapa Tatiana alikuwa akibadilishana mawazo na Mwisho Mwampamba. Kuna kitu kilikuwa kikiendelea ndani ya house kila mshiriki alitakiwa kusema SECRET yake ni nini, ilifika zamu ya mtu mzima Mwisho kusema Siri yake na alisema kwamba
"My secret is, i have lost ma two chicks, one is sing like Celion Dion and another one is sing Hip Hop"
Sasa kithungu nilichokitumia hapa nimekipatia au?

Sean Paul alivyoingia ndani ya House kusalimiana na washiriki wanaogombania $200,000 alikaribishwa na Tatiana na kuonyeshwa kulivyo ndani ya jumba hilo




Watu wazima mda ulivyofika ikatakiwa kusepa ndani ya jumba hilo

Sean Paulllllllllllllllllllllllll ndio sauti aliyokuwa akiitoa huku akimuaga kwa kumiss

Akaona haitoshi mwanadafada alimfuata hadi mlango na kumukumbatia mwisho mwisho, ha hah i like dat
(kwa msaada wa blog jirani-dj choka)

THE DON HIMSELF

Karibuni sana kwenye blog hii ya kijamii iliyosheheni makila kitu kuanzia siasa uchumi afya na burudani kwa ujumla wake.uingiapo kwenye blog hii ni mengi ambayo utapata nafasi ya kukutana nayo,kumbuka mawazo yako ndo hasa yanayojenga na kunifanya niwe na ufanisi zaidi.kariiiiiiibuuuuuuuuuuuu saaaaaaaaaaaaaaanaaaaaaaaaa.(THE DJ HIMSELF-JIWE)

Followers

BLOG ZA MARAFIKI

Search This Blog

ZILIZOPITA

DUNIA MUZIMA