Hapa Mwandishi Siddy akiwa na Nina na Barnaba.
Msanii kutoka Arusha anayejulikana kwa jina la Angel ametikisa Ngome Kongwe kwa jinsi alivyonyonga kiuno kama pia, kitu kilichowafanya mashabiki kumshangilia kwa nguvu wakati akiimba jukwaani katika tamasha la Fiesta lililofanyika usiku huu mjini Zanzibar na kushirikisha wasanii wengi wa muziki wa kizazi kipya Bongofleva.
Tamasha hilo linafanyika baada ya lile la Tanga lililofanyika jumamosi kwenye uwanja wa Mkwakwani mkoani humo na linadhaminiwa na kampuni ya bia ya Serengeti Breweriers (SBL) ya jijini Dar es Salaam. Msanii kutoka Arusha anayejulikana kwa jina la Angel ametikisa Ngome Kongwe kwa jinsi alivyonyonga kiuno kama pia, kitu kilichowafanya mashabiki kumshangilia kwa nguvu wakati akiimba jukwaani katika tamasha la Fiesta lililofanyika usiku huu mjini Zanzibar na kushirikisha wasanii wengi wa muziki wa kizazi kipya Bongofleva.
Barnaba na Nina wakitafuta muafaka wa SMS!
Binamu Mwana FA akiwarusha mashabiki wake.
Mustafa wa G5 Click akiwa kazini Ngome Kongwe.
Mwasiti naye hakubaki nyuma, alikamua vilivyo na kuwapambanisha mashabiki ambao aliwaita vidume (hawapo pichani), yote ikiwa ni burudani tu.
Amini naye akafanya mambo makubwa katika tamasha hilo kama unavyomuona.
Msanii huyu pia alikuwepo na akavuta hisia za mashabiki kwa staili yake.
Mr. Wise akitoa burudani na mrembo ambaye alivuta hisia za mashabiki wengi usiku huu na kushangiliwa kwa nguvu. (picha kwa hisani ya mzee wa full shangwe)
No comments:
Post a Comment