Nov 5, 2010

JAKAYA ASHINDA KUWA RAIS WA TANZANIA UCHAGUZI MKUU 2010

NA MAGRETH KINABO – MAELEZO

MWENYEKITI wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, ( NEC), Jaji Mstaafu, Lewis Makame leo jioni amemtangaza mshindi wa kiti cha urais wa Tanzania wa mwaka 2010 kuwa ni Ndugu Jakaya Kikwete kutoka Chama cha Mapinduzi(CCM).

Matokeo hayo ya uchaguzi huo, yalitangazwa leo majira ya saa kumi jioni na Mwenyekiti huyo katika viwanja wa Karimjee jijini Dar es Salaam.

Kabla ya kutangazwa kwa matokeo hayo, Jaji Mstaafu , Makame alisema kwa mujibu wa Ibara ya 41(6) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, mwaka 1977 mgombea wa kiti cha urais atatangazwa kuwa amechaguliwa kuwa rais iwapo tu amepata kura nyingi kuliko mgombea mwingine yeyote.

Aidha Makame alisema kwa mujibu wa ibara ya 47(2) ya Katiba hiyo, mgombea wa kiti cha urais akichaguliwa basi na mgombea mwenza wake atakuwa Makamu wa Rais.

“Kwa kuwa Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete wa CCM amepata kura yingi kuliko mgombea yeyote, kwa niaba ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi na kwa mujibu wa vifungu vya 35E, 35F (8) na 81 B vya Sheria ya Taifa ya Uchaguzi Sura 343, ninatangaza rasmi matokeo ya uchaguzi wa urais wa 2010.

“Mheshimiwa Kikwete Jakaya Mrisho amechaguliwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mheshimiwa Bilal Mohammed Gharib amechaguliwa kuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,” alisema Mwenyekiti huyo.

Aliongeza kuwa idadi ya wapigakura waliojiandikisha ni 20,137,303, waliopiga kura ni 8,626,283 sawa na asilimia 42.84 ya wapiga kura wote waliojiandikisha, zilizoharibika ni 227,889 ambazo ni sawa na asilimia 2.64 ya kura zilizopigwa.

Alizitaja idadi ya kura halali kuwa ni 8,398,394 sawa na asilimia 97.36 ya kura zote zilizopigwa, hivyo Kikwete amepata kura 5,276,827 ambazo ni sawa na asilimia 61.17 ya kura zote halali.

Wagombea waliofuatia ni wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA) ambaye ni Slaa Willibrod Peter amepata kuwa 2,271,941 ambazi ni sawa na silimia 26.34 ya kura zote halali, Lipumba Ibrahim Haruna wa chama cha CUF, amepata kura 695,667 sawa na asilimia 8.06 ya kura zote halali, Mziray Kuga Peter wa APPT – Maendeleo amepata kura 96,933 sawa na asilimia 1.12 ya kura zote halali.

Wengine ni Rungwe Hashim Spunda wa NCCR- MAGEUZI amepata kura 26,388 sawa na asilimia 0.31 ya kura zote halali, Mgaywa Muttamwega Bhatt wa TLP amepata kura 17,482 sawa na silimia 0.20 na Dovutwa Yahmi Nassoro Dovutwa wa UPDP amepata kura 13,176 sawa na asilimia 0.15 ya kura zote halali.

Akitoa salamu kwa niaba ya wenzake badala ya Slaa ambaye ahakuwepo uwanjani hapo, Lipumba ambapo alimpongeza Kikwete na Makamu huku akisisitiza suala ya ushiriki wa watu katika kupiga kura liangaliwe na kusema Rais aliyeshinda ni Watanzania wote.

Alisisitiza suala la elimu bora , ajira, ujengaji wa miundombinu na uvumulivu wa kisiasa ni muhimu, hivyo alimshauri Rais Mteule Kikwete kujiwekea malengo katika kipindi cha miaka 5 ijayo, ambayo ni uongozi wa demokrasi, ujenzi wa uchumi ajira kuboresha miunbombinu, utawala na kupamban na rushwa.

Pia alimkabidhi Rais Mteule Kikwete Ilani ya chama chake kwa ajali ya kusaidia katika utendaji wake wa kazi.

Kwa Upande wake Rais Mteule Kikwete, alitoa shukura za ushindi alioupata na kusema watazifanyia kazi changamoto zilizibuliwa wakti wa kampeni yakiwemo mawazo ya Lipimba.

Alivishukuru vyombo vya habari kwa tendaji wao wa kazi , lakini aliviomba kufanmya kazi zaidi ya kusaidia kutibu majeraha ya nchi ili kurejesha umoja na amani badala ya kuongeza chumvi.

Naye Dovutwa alisema sasa ni wakti wa kumsaidia Rais Mteule kujenga nchi malumbano yamekisha.

Mziray amesema hajakata tama ananjiandaa kwa baade , huku Muttamwega alisema matokeo yameenda vizuri.

Rais Mteule Jakaya Kikwete akiingia kwenye viwanja vya Karimjee leo mchana wakati Tume ya Uchaguzi ilipotangaza matokeo ya Kura za urais na mgombe huyo kupitia chama cha Mapinduzi kuibuka mshindi matukio zaidi ya picha tutawaletea baadae.
1. KUGA PETER MZIRAY APPT - MAENDELEO: 96, 933 (1.12%) 2. KIKWETE JAKAYA MRISHO/CCM: 5,276,827 (61.17%) 3. SLAA WILLIBROD PETER/CHADEMA: 2,271,941 (26.34%) 4. LIPUMBA IBRAHIM HARUNA/CUF: 695,667 (8.067%) 5. RUNGWE HASHIM SPUNDA/NCCR-MAGEUZI: 26,388 (0.31%) 6. MGAYWA MUTTAMWEGA BHATT/TLP:17,482 (0.20%)
7. DOVUTWA YAHMI NASSORO DOVUTWA/UPDP: 13,176 (0.15%)

----------------------------------------

WALIOJIANDIKISHA KUPIGA KURA: 20, 137, 303

WALIOJITOKEZA KUPIGA KURA: 8, 626 (42.64%)

KULA HALALI ZILIZOPIGWA: 8,398,394

KURA ZILIZOHARIBIKA 227,889 (2.64)

Rais Mteule Jakaya Mrishjo Kikwete kulia akiwa amekaa pamoja na aliyekuwa mgombea wa urais Kupitia chama cha PPT Maendeleo Kuga Peter Mziray leo

Mgombea Urais kwa tiketi ya CCM Dr.Jakaya Mrisho Kikwete akionyesha cheti cha ushindi katika mbio za urais mwaka 2010 muda mfupi baada ya tume ya Uchaguzi kumtangaza kuwa mshindi wa kiti cha urais katika uchaguzi wa mwaka huu 2010.Hafla hiyo ilifanyika katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam leo mchana.
Rais wa awamu ya Tatu Benjamin William Mkapa akimpongeza Rais Dr.Jakaya Mrisho Kikwete muda mfupi baada ya tume ya Uchaguzi kutmangaza Rais Kikwete kuwa mshindi wa kiti cha Urais katika uchaguzi wa mwaka huu 2010 katika hafla iliyofanyika katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es salaam leo mchana(picha na Freddy Maro)

Mgombea urais kwa tiketi ya CUF Profesa Ibrahim Lipumba akimpongeza Mgombea urais kwa tiketi ya CCM Dr.Jakaya Mrisho Kikwete muda mfupi baada ya tume ya Uchaguzi kumtangaza Dr.Jakaya Kikwete kuwa mshindi katika kinyang’anyiro cha Urais katika uchaguzi wa mwaka huu 2010.
Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Jaji Lewis Makame amkikabidhi cheti Mgombea Urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi Dr.Jakaya Mrisho Kikwete muda mfupi baada ya kumtangaza kushinda katika mbio za urais katika uchaguzi wa mwaka huu.Hafla hiyo ilifanyika katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam.

Baadhi ya wanachama wa CCM wakishangilia muda mfupi baada ya Tume ya Uchaguzi kumtangaza Rais Dr.Jakaya Mrisho Kikwete kushinda kiti cha Urais katika uchaguzi wa mwaka huu 2010
Baadhi ya wapigapicha na waandishi wakifuatilia kutangazwa kwa matokeo ya urais a,mbapo Dr.Jakaya Mrisho Kikwete aliibuka mshindi

ALI KIBA NA AMANI MARA BAADA YA KUMALIZA KAZI YA KUREKODI!

ALI KIBA NA FALLY IPUPA BAADA YA KUMALIZA KUPIGWA PICHA ZA KUNDI LAO LA ONE8
ALI KIBA AKITENGEZWA ILI APENDEZE ZAIDI KABLA YA UPIGAJI PICHA WA KUNDI LA MUZIKI LA AFRIKA LIJULIKANALO ONE8 HUKO CHICAGO NCHINI MAREKANI
AMANI NA ALI KIBA WAKIWA KATIKA KATIKA PICHA YA PAMOJA MARA BAADA YA KUMALIZA KUREKODI NYIMBO NA KUNDI LA ONE8 JIJINI CHICAGO.

Swahili Fashion Week

PR&media manager-Saphia introducing designers..

From left Mpho Kuaho-Designer from Botswana,Judy Muya- Representative from Southern Sun and other designers..

Some designers of SFW 2010 in group photo..

WASILIANA NA: Saphia Ngalapi, Media & PR Manager
Wabunifu kutoka nchi tofauti wapo tayari kwa shoo kabambe
KWA SIMU NAMBA: +255-712-099834
BARUA PEPE: media@swahilifashionweek.com

Nyumba ya Swahili Fashion Week – Southern Sun Hotel

Gauni bora itashinda zawadi kutoka Southern Sun


Jukwaa la tatu la Swahili fashion Week linaanza leo katika viwanja vya karimjee jijini Dar es salaam na kudumu kwa muda wa siku tatu hadi tarehe 6 ya mwezi wa November 2010.

Katika jukwaa la mwaka huu jumla ya wabunifu 24 kutoka nchi za Afrika hasa zile zinazozungumza lugha ya Kiswahili wamejiandaa vya kutosha katika kuonesha kazi zenye viwango vya kimataifa.

“Tunashukuru kwani mipango yote inakwend kama tulivyopanga na tayari wabunifu wote wamefika kwa ajili ya shoo kabambe ambapo itakuwa na tofauti kubwa kulinganisha na zile zilizopita. Tayari wabunifu wote 24 kutoka Tanzania na nchi za Pan Afrika wapo tayari kwa shoo ya mwaka, inayoandaliwa nyumbani mwa Swahili Fashion Week.” Alisema Mustafa Hassanali muandaaji wa Swahili Fashion Week

“Kwa mara nyingine tena tupo na Swahili Fashion Week 2010, na kusaidia kukuza Sanaa ya ubunifu wa mavazi hapa nchini, pamoja na kuwakaribisha wageni wetu ambao ni wabunifu wa kimataifa. Southern Sun inajivunia kutokana na mchango wake inayotoa kwa Sanaa ya ubunifu wa mavazi Afrika na hii intupa fursa ya kuendelea kwa njia mbalimbali.” Alisema meneja mkuu wa southern sun Hotel Ndugu Adam fuller

Southern Sun hotel imekuwa nyumba ya Swahili Fashion Week toka mwaka 2009.
Swahili Fashion Week inafanyika kwa mwaka watatu sasa na itawashirikisha wabunifu 24 ambapo kwa mujibu wa ratiba, siku ya kwanza shoo itapambwa na Manju Msita (Tanzania),Sonu Sharma (Kenya),Shelina Ebrahim (Tanzania/Canada),United Against Malaria (Tanzania Various),Farha Sultan (Tanzania),Tanzania Mitindo House (Tanzania - Various), KemiKalikawe (Tanzania) na Asia Idarous (Tanzania)

Kwa upande wa tarehe tano, siku ya ijumaa mwanamitindo kutoka Tanzania Jamila Vera Swai tfungua pazia akifuatiwa na Marinella Rodriguez (Mozambique),Stella Atal (Uganda),Kooroo (Kenya),Zamda George (Tanzania),Mafi Designs (Ethiopia),Moo Cow (Kenya),Robi Morro (Tanzania),Made by Africa (Tanzania) na Asos Africa (UK)

Tarehe sita November siku ya mwisho ya jukwaa la Swahili Fashion Week, wabunifu wtakoonesha kazi zao ni pamoj na wabunifu wanane wanaochipukia waliofanikiwa kuingia fainali kupitia shindano la wabunifu wanaochipukia, Emerging Designers Competition (Tanzania - Various),Gabriel Mollel (Tanzania),Khadija Mwanamboka (Tanzania),KikoRomeo (Kenya), John Kaveke (Kenya), Chichia London (Tanzania/UK), Ailinda Sawe (Tanzania)

“ Pamoja na kuwakaribisha wageni wetu ambao ni wabinifu wa mavazi , pia Southern itatoa zawadi kwa gauni bora katika Swahili Fashion Week kwa huu , lengo ni kusaidia kukuza Sanaa ya ubunifu wa mavazi” Aliongeza Saphia Ngalapi, Swahili Fashion Week PR manager

Swahili fashion week 2010 imedhaminiwa na home of Swahili Fashion Week - Southern Sun, Origin Africa, USAID Compete, , Malaria Haikubaliki, BASATA (Baraza La Sanaa Tanzania), Ultimate Security, Monier 2000, Colour Print Ltd, Global Outdoor Ltd, Amarula, Vayle Springs Ltd, ZG Films, Darling Hair, Danish make up designs, Nipashe, Bilicanas, Perfect Machinery Ltd, 1&1 Internet Solutions, Sengi Tours, iFashion, 361 Degrees na EATV & East Africa Radio.

Kuhusu SOUTHERN SUN
Southern Sun ni hoteli inayojivuni kuwa Afrika kwa zaidi ya miaka 40 sasa, ikitoa huduma bora kwa wageni wa nje na ndani ya nchi. Imetunukiwa sifa ya kuwa kundi la hoteli inayosifika barani Afrika

Nov 4, 2010

CONGRATULATIONS VIJANA

Halima James Mdee-Mshindi Jimbo la Kawe kwa tiketi ya CHADEMA.

January Makamba-Mshindi Jimbo la Bumbuli kwa tiketi ya CCM

John Mnyika- Mshindi Jimbo la Ubungo kwa tiketi ya CHADEMA

Peter Serukamba-Mshindi Jimbo la Kigoma Mjini kwa tiketi ya CCM

Zitto Zuberi Kabwe-Mshindi Jimbo la Kigoma Kaskazini kwa tiketi ya CHADEMA


JESHI LA POLISI LAKABIDHIWA MAGARI MAPYA!

Katibu Mkuu wa Wizara ya Sheria na Katiba, Oliva Mhaiki akikata utepe ikiwa ni ishara ya kukabidhi magari 15 yenye thamani ya sh. milioni 580 yaliyotolewa na Programu ya Maboresho ya Sekta ya Sheria kw Jeshi la Polisi Dar es Salaam jana. Magari hayo yatasaidia kuboresha mfumo wa upelelezi nchini.Picha kwa hisani ya www.michuzijunior.com
Baadhi ya magari yliyotolewa msaada na LRSP kwa Jeshi la Polisi kitengo cha upelelezi.Picha kwa hisani ya Richard Mwaikenda.

URBAN PULSE wamtambulisha Diamond Ubalozini

Diamond akiwa Bond Street, London, Uingereza
Mkuu wa u utawala Bi Carol Chipeta na Diamond
Mh Balozi Kallaghe, Diamond na Kaimu Balozi Chabaka Uingereza
Frank, Balozi Kallaghe, Diamond, Kaimu Balozi Chabaka, Baraka na Nocha.

Salam,

Baada ya Kuwasili ndani ya UK jumanne jioni Urban Pulse walimpeleka Msanii Mahiri wa Kizazi Kipya Diamond aka mzee wa Mbagala katika ubalozi wa Tanzania hapa jijini London kumtambulisha na kutoa Salam kwa Mh Balozi, Naibu Balozi na pamoja na staff wake. Diamond ametua kwa ajili ya Kufanya Urban Tour dhidi ya malaria. Show ya kwanza itafanyika jumamosi hii hapo ndani ya mji wa MILTON KEYNES CLUB OPUS ikifuatiwa na THE CLUB CROYDON 12/11.

NYOTE MNAKARIBISHWA,
URBAN PULSE CREATIVE

President Kikwete pays his last respects to Elvis Musiba at Karimjee Hall in Dar es Salaam!

President Dr.Jakaya Mrisho Kikwete signs a condolence for the late Elvis Musiba shorly after he paid his last respects to the fallen business leader and author at Karimjee Hall in Dar es Salaam this evening.
(Photos by Freddy Maro)
President Dr. Jakaya Mrisho Kikwete and the First Lady Mama Salma Kikwete pay their last respects to the renowned business leader and author, Elvis Musiba at Karimjee Hall grounds in Dar es Salaam this evening.Musiba who passed away at his residence in Mikocheni in the city on Sunday, will be buried on Friday in his Musoma native town.
President Dr. Jakaya Mrisho Kikwete introduces TLP presidential contestant Mr.Muttamwega Mgahywa to the First Lady Mama Salma Kikwete at Karimjee hall in Dar es Salaam this evening during the farewell and last respects for the late Elvis Musiba .Mr.Musiba a renowned business leader and author passed away on Sunday in the city

BAADA YA KUTANGAZA BAADHI YA MAJIMBO LEWIS MAKAME AJIBU MASWALI YA WANAHABARI JIONI HII!

Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi akijibu maswali mbalimbali na waandishi wa habari jioni hii mara baada ya kumaliza kutangaza kura za urais katika majimbo 25 kati ya majimbo 92 yaliyokuwa yamesalia kwa maana hiyo hivi sasa majimbo yaliyotangazwa yamefikia 172 huku yakisalia majimbo 67 ili kukamilisha kazi ya kutangaza matokeo hayo, kazi ya kutangaza itaendelea leo saa mbili usiku.
Watangazaji wa Idhaa ya Kiswahili ya Radio France International (RFI)wakiwa kazini katika kituo cha Tume ya Taifa ya Uchaguzi cha kutangazaia matokeo ya uchaguzi kilichopo katika Hoteli ya Paradise City jijini Dar es salaam kuanzia kulia ni Ebby Shaban Abdallah, Edwin David Ndeketela na mwisho ni Emanuel Leonard Mbando wakiwa kazini.

Spika Samwel Sitta achukua fomu kutetea nafasi yake leo

Spika anayemaliza mda wake Mhe. Samuel Sitta leo amechukua fomu ya kugombea nafasi ya Uspika wa Bunge katika Bunge la Kumi kwenye uchaguzi unaotarajiwa kufanyika mapema wiki ijayo mjini Dodoma.

Spika Sitta amechukua fomu hiyo kupitia chama chake cha CCM katika ofisi ndogo za CCM Lumumba, Dar es Salaam na kuijaza kisha kuirudisha leo hii baada ya kukamilisha mahitaji yote ikiwa ni pamoja na kugharamia fomu hiyo kwa kiasi cha Tsh 500,000/= kwa mujibu wa taratibu wa chama hicho.

kwa Mujibu wa ibara ya 84 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, 1977, chama chochote cha siasa kilichosajiliwa kina haki ya kushiriki katika Uchaguzi wa Spika kwa kumpendekeza mwananchama wake mmoja ambaye ni Mbunge au asiye Mbunge mwenye sifa za kuwa Mbunge kuwa Mgombea wa nafasi hiyo.

Katika picha juu Spika anayemaliza muda wake Mhe. Samuel Sitta akisaini kitabu cha watu waliochukua fomu ya kugombea nafasi ya Uspika kwenye Ofisi za CCM Lumumba

Mkurugenzi wa Uchaguzi wa CCM Ndg. Mattison Chiza akimkabidhi fomu ya kuwania Uspika katika ofisi ndogo za CCm Lumumba, jijini Dar es Salaam leo
Spika anayemaliza mda wake Mhe. Samuel Sitta akiwasili katika ofisi ndogo za CCm Lumumba, Dar es Salaam kuchukua fomu ya kutetea nafasi yake hiyo nakupokelewa na baadhi ya wananchama wa CCM

LAZARO NYALANDU SINGIDA KASKAZINI AVUNJA REKODI YA USHINDI!.

Nyarandu akipongezwa na meneja kampeni wake hadija lesso,baada ya kutangazwa kuwa mshindi.
.(Picha na Michael Matemanga)

MBUNGE wa Singida Kaskazini, Lazaro Nyalandu ameweza tena kurejea madarakani baada ya kuibuka na jumla ya kura 46,869 ikiwa ni asilimia 91 ya kura zote.

Nyalandu ambaye amekuwa mgombea ubunge wakwanza nchini kutumia helkopta katika kampeni aliwabwaga wapinzani wake Msaghaa Kimia kwa tiketi ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) alipata kura 3,544 wakati Sizimwe Kanyota wa Chama cha Wananchi (CUF) aliyepata kura 550.

Akitangaza matokeo hayo jana usiku, Msimamizi wa uchaguzi katika jimbo hilo, Iliminata Mwenda alisema jumla ya wapigakura waliojiandikisha walikuwa 90,045 wakati waliopiga kura ni 46,869 katika jimbo hilo.

Akizungumza baada ya kutangazwa kwa matokeo hayo, Nyalandu alisema kuwa wananchi wa Singida Kaskazini wamempa heshima kubwa kwa kuonyesha kumwamini na kuwa yuko tayari kuendeleza mambo aliyoyafanya kipindi kilichopita na kutimiza ahadi zake alizotoa wakati wa kampeni.

Dr. Shein aapishwa kuwa rais Zanzibar, Dr.Jakaya Kikwete ahudhuria sherehe na kuwapongeza!

Rais wa Zanzibar Dr. Ali Mohamed Shein akila kiapo cha urais mbele ya jaji mkuu wa Zanzibar Hamid Mahamoud(kushoto) wakati wa sherehe za kumuapisha zilizofanyika katika uwanja wa michezo wa Amaan Stadium mjini Zanzibar leo asubuhi.Katikati anayeshuhudia ni rais wa Zanzibar aliyemaliza muda wake Amani Abeid Karume. (Picha na Freddy Maro wa Ikulu)
Rais Wa Zanzibar aliyemaliza muda wake Amani Abeid Karume akimpongeza na kumkabidhi miongozo ya kazi Rais Mpya wa Zanzibar Dr.Ali Mohamed Shein wakati wa sherehe za kuapishwa zilizofanyika katika uwanja wa michezo wa Amaan mjini Zanzibar leo asubuhi.
Rais Dr.Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na mshindi wa pili katikA KINYANG’ANYIRO cha urais wa Zanzibar Maalim Seif Shariff Hamad wakati wa sherehe za kumuapisha Rais mpya wa Zanzibar Dr.Ali Mohamed Shein mjini Zanzibar leo asubuhi.
Rais Dr.Jakaya Mrisho Kikwete akisalimaina na mgombea Mwenza Dr.Mohamed Gharib Bilal katika uwanja wa michezo wa Amaan mjini Zanzibar wakati wa sherehe za kumuapisha Rais mpya wa Zanzibar Dr. Ali Mohamed Shein leo asubuhi.Katikati ni Mshindi wa pili katika mbio za urais wa Zanzibar kwa tiketi ya CUF Maalim Seif Shariff Hamad.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr.Jakaya Mrisho Kikwete akimpongeza Rais mpya wa Zanzibar Dr.Ali Mohamed Shein muda mfupi baada ya Dr.Shein kuapishwa mjini Zanzibar leo asubuhi.
Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein akimpongeza mumewe Dr.Ali Mohamed Shein muda mfuoi baada ya Dr.Shein kuapishwa kuwa Rais Mpya wa Zanzibar leo asubuhi(picha na Freddy Maro)

MAJIMBO 147 TAYARI, BADO 92 KURA ZA URAIS!!

Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Lewis Makame akiondoka mara baada ya kutangaza matokeo ya kura katika majimbo 34 leo, Mkurugenzi wa Tume hiyo Bw. Rajab Kiravu amesema matokeo katika majimbo mengine yataendelea kutolewa kuanzia saa kumi leo jioni. Mpaka sasa Tume ya Uchaguzi imeshatangaza matokeo ya uchaguzi ya rais katika majimbo 147 na majimbo ambayo bado hayajatangazwa ni 92 kazi ambayo itaenelea leo jioni hiyo saa kumi.
Mwenyekiti wa Tume ya taifa ya Uchaguzi NEC Jaji Lewis Makame akitangaza matokeo ya kura za urais katika kituo cha kutangazia matokeo kilichopo Paradise City jijini Dar es salaam.
Waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali vya habari wakirekodi matokeo ya uchaguzi mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani uliofanyika jumapili iliyopita nchini kote wakati mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi NEC alipokuwa makitangaza matokeo ya majimbo 34 leo kwenye kitu cha kutangazia matokeo kilichopo Paradise City Hoteli Posta jijini Dar es salaam kutoka kulia ni Ashura wa redio Tumaini, Maulid Ahmed Daily News, Khadija na Asha Ban

TIMU 12 ZATHIBITISHA KUSHIRIKI TUSKER CHALLENGE CUP 2010.

Katibu Mkuu wa Shirikisho la Vyama vya Mpira wa Miguu Afrika Mashariki na Kati SECAFA Bw. Nicolas Musonye akizungumza mbele ya waandishi wa habari leo kwenye Hoteli ya New Africa jijini Dar es salaam wakatim alipozungumzia maandalizi ya mashindano ya Tusker Challenge Cup 2010 yanayotarajiwa kuanza Novemba 27 hadi Disemba 11 mwaka huu. Akizungumza katika mkutano huo katibu mkuu huyo wa SECAFA Bw. Nicolas Musonye amesema timu 12 zimethibitisha kushiriki katika mashindano hayo ambazo ni Wenyeji Tanzania,Kenya, Burundi, Uganda, Somalia, Zanzibar, Ethiopia, Sudan, na ytimu zilizoalikwa ni Ivory Coast, Zambia na Malawi.
Mtendaji Mkuu wa SBL Bw. Richard Wells amesema SBL itahakikisha timu zote zinapewa huduma zote muhimu wakati zitakapokuwa hapa nchini kwa ajili ya mashindano ikiwa ni pamoja na Chakul, Mlazi na Usafiri wa ndege na itatoza zwadi kjwa washindi zinazofikia dola za Kimarekani elfu 60.000 ikiwa ni sehemu ya udhamini ambao ni dola za kimarekani laki 450.000 ambapo mshindi wa kwanza atajipatia dola 30.000, mshindi wa pili dola 20.000 huku mshindi wa tatu akijinyakulia dola 10.000. Kampuni ya Serengeti Breweriers ndiyo mdhamini mkuu wa mashindano ya Tusker Chalengfe Cup 2010 kwa mwaka huu.
Anna McCartiney afisa na Mshauri kutoka Mradi wa Malaria No More Tanzania akizungumza katika mkutano huo uliofanyika leo kwenye Hoteli ya New Africa jijini Dar es salaam katika picha wanaofuatia ni Kaimu katibu Mkuu TFF Sunday Kayuni, Nicolas Musonye katibu Mkuu SECAFA, Rais wa TFF Rodger Tenga, Mkurugenzi wa SBL Richard Wells, Mkurugenzi wa Mawasiliano SBL Teddy Mapunda na Mkurugenzi wa Masoko SBL Caroline Ndungu.
Mkurugenzi wa Masoko wa kampuni ya SBL Caroline Ndugu akizungumza mbele ya waandishi wa habari leo wakati Shirikisho la vyama vya mpira wa Miguu Afrika Mashariki na kati lilipozungumzia mashindano ya Tusker Challenge Cup yanayotarajiwa kufanyika hapa nchini hivi karibuni kushoto ni Mkurugenzi wa Mawasiliano wa SBL Teddy Mapunda, kutoka kulia ni Katibu Mkuu wa SECAFA Nicolas Musonye, Rais wa TFF Rodger Tenga na Mkurugenzi wa SBL Richard Wells.
Kaimu katibu Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Nchini TFF Sunday Kayuni akijadiliana jambo na wajumbe wa kamati ya Utendaji ya TFF wakati wa mkutano wa waandishi wa habari kwenye Hoteli ya New Africa leo.

Nov 3, 2010

Balozi wa Marekani apongeza ushindi wa Dr. Shein, Zanzibar


Balozi wa Marekani nchini Tanzania,Alfonso E. Lenhardt

Marekani inampongeza Dk. Ali Mohamed Shein kwa kuchaguliwa kwake kuwa Rais wa Zanzibar. Uchaguzi huu wa kihistoria na ambao umeripotiwa kuwa uchaguzi wa amani na uliosimamiwa vyema zaidi katika historia ya Zanzibar, utawezesha kuundwa kwa serikali ya kwanza ya umoja wa kitaifa visiwani humo.

Watu wa Zanzibar walijitokeza kwa wingi kutekeleza wajibu wao wa kupiga kura, wakitambua kuwa serikali yao mpya itawawakilisha Wazanzibari wote.

Viongozi wote wawili, Dk. Shein na Maalim Seif Sharif Hamad, ambao hivi sasa wanageuka kutoka kuwa wapinzani wakuu na kuwa wabia katika kuiongoza nchi yao, wanastahili pongezi kwa kuendesha kampeni za kuwaandaa wanachama na wafuasi wao kwa aina mpya ya serikali.

Ni imani kwamba Dk. Shein and Maalim Seif wataweza kufanyakazi pamoja kama wabia na kuweka malengo ya pamoja kwa maslahi ya Wazanzibari wote.

Watu wameshatoa kauli yao, hivi sasa ni wakati wa kujenga imani katika taasisi za serikali na kujenga Zanzibar mpya yenye msingi imara kwa ustawi na maendeleo ya kijamii. Kwa kujenga utamaduni mpya wa kisiasa, viongozi wa Zanzibar wataweza kuchochea ubunifu wa watu wa Zanzibar.

Serikali mpya itawajengea wapiga kura imani kwa kuhakikisha kuwa manufaa ya fursa za maendeleo ya kijamii na kiuchumi yanafika katika mikoa yote ya Zanzibar.

Urafiki kati ya Marekani na Zanzibar ni wa kina na wa kihistoria. Ninapenda kuwahakikishia Wazanzibari kwamba Marekani itaendelea kuwa rafiki wa kweli wa Zanzibar.

Tutadumisha kiwango cha juu cha misaada yetu katika maeneo muhimu na yanayowagusa watu wote, ambayo ni pamoja na elimu, afya, nishati na miundombinu. Mradi wa umeme wa Megawati 100 kwenda Unguja unaendelea.

Mradi wa ujenzi wa barabara huko Pemba unaendelea. Jitihada zetu katika kuzuia na kutokomeza maradhi nazo zitaendelea.

Tukishirikiana na wadau wengine duniani katika nyanja ya teknolojia, tunaongeza jitihada zetu za kupeleka kompyuta katika kila shule ya msingi visiwani Zanzibar. Ni matarajio yangu kuwa nitashirikiana na uongozi mpya wa Zanzibar katika kutekeleza mambo yote haya muhimu.

Ni vyema tuwe wakweli kuhusu changamoto zilizo mbele yetu. Serikali ya umoja wa kitaifa itakuwa na masuala mengi magumu ya kutatua. Pamoja na hayo, ni matumaini yangu ya dhati kwamba uchaguzi huu ni hatua muhimu sana katika safari ya kuelekeza Zama Mpya na Bora za Zanzibar.

Mathias Chikawe ahutubia mkutano wa AALCO, New York Marekani

Waziri wa Katiba na sheria na Rais wa Jumuiya ya Mashauriano ya Kisheria kati ya Nchi za Afrika na Asia (AALCO), Bw. Mathias Chikawe alihutubia mkutano wa Jumuiya hiyo uliofanyika kando ya vikao vya 65 vya Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa vinavyoendelea mjini New York, Marekani tarehe 02 Novemba 2010.

Kwenye hotuba iliyosomwa kwa niaba yake na Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania kwenye Umoja wa Mataifa, Balozi Ombeni Sefue, Bw. Chikawe aliwaeleza wajumbe wa mkutano huo baadhi ya masuala muhimu yaliyojadiliwa wakati wa mkutano wa 49 wa mwaka wa AALCO uliofanyika Dar es Salaam kuanzia Tarehe 05 hadi 08 Agosti, 2010.

Baadhi ya masuala hayo ni pamoja na urejeshwaji wa Wapalestina katika maeneo yao na vitendo vya Israel vya kuyakalia kwa nguvu maeneo ya Wapelestina pamoja na changamoto za kupambana na ufisadi.

Kuhusu suala la Palestina, Waziri Chikawe alieleza kuwa nchi wanachama zililaani vikwazo vilivyowekwa na Israel dhidi ya Ukanda wa Gaza kwa kusema kuwa vikwazo hivyo ni ukiukwaji wa sheria za kimataifa, ikiwa ni pamoja na Mkataba wa nne wa Geneva wa mwaka 1949.

Kuhusu suala la ufisadi, Waziri Chikawe alibainisha kuwa nchi zote wanachama zilikubaliana kuwa, Azimio la Umoja wa Mataifa la kupambana na ufisadi (UNCAC) ni silaha pekee ya kukabiliana na tatizo hilo. Nchi zilishauriwa kutunga sheria na vyombo husika kwa ajili ya utekelezaji wa Azimio hilo.

Aidha, Waziri Chikawe alieleza mikakati AALCO inayokusudia kuchukua kuongeza ushiriki wake kwenye Tume ya Kimataifa ya Sheria (ILC). Alieleza kuwa, katika mkutano wa Dar es Salaam nchi wanachama zilikubaliana kuwa AALCO iendelea kuzitupia jicho mada ambazo ILC inazipa kipaumbele.

Jambo lingine ambalo Waziri Chikawe alilizungumzia na pia lilijadiliwa kwenye mkutano wa Dar es Salaam ni suala la Mahakama ya Kimataifa ya Makosa ya Jinai (ICC). Alieleza kuwa, AALCO inafuatilia kwa karibu masuala yanayogusa Mahakama hiyo. Alisema kuwa, mkutano wa Dar es Salaam uliangalia masuala yaliyojadiliwa kwenye mkutano wa kwanza wa kupitia Mkataba wa Rome uliofanyika Kampala, Uganda kuanzia tarehe 31 Mei hadi tarehe 11 Juni 2010.

Alieleza kuwa, mkutano huo ulitoa ufafanuzi wa masuala kadhaa ikiwa ni pamoja na tafsiri ya kosa la uchokozi (crime of aggression). Maelezo yaliyotolewa na wataalamu kuhusu kosa hilo ni mazuri na yanajitosheleza. Aidha, nchi nyingi wanachama wa AALCO zilionesha wasiwasi kuhusu uhuru wa Mahakama hiyo na kwamba waliweka msisitizo kuwa mahakama hiyo lazima iwe huru na isiyumbishwe na msukumo wowote wa kisiasa.

Mwisho, Waziri Chikawe aligusia suala la mazingira na maendeleo endelevu. Suala hili lilijadiliwa pia katika mkutano wa Dar es Salaam kama maandalizi kwa ajili ya mkutano wa mabadiliko ya tabianchi unaotarajiwa kufanyika Cancun, Mexico mwishoni mwa mwaka 2010. Mkutano ulisisitiza umuhimu wa nchi wanachama kuwa na utashi wa kisiasa katika kukabiliana na tatizo la mabadiliko ya tabianchi kwa kufuata kanuni za rasimu ya Mkataba wa Umoja wa Mataifa kuhusu mabadiliko ya Tabianchi (UNFCCC).

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ilijiunga na AALCO mwaka 1973 na tangu wakati huo inajihusisha na shughuli za jumuiya hiyo kikamilifu. Vile vile, Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ilishakuwa mwenyeji wa mikutano miwili ya mwaka ya AALCO. Mkutano wa 25 wa mwaka uliofanyika Arusha mwaka 1986 na mkutano wa 49 wa mwaka uliofanyika Dar es Salaam Agosti 2010.

WAANGALIZI WA UCHAGUZI KUTOKA EU NA AU WASEMA UCHAGUZI ULIKUWA HURU NA WA AMANI

NA MAGRETH KINABO – MAELEZO

WAANGALIZI wa Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu uliofanyika Oktoba 31,kutoka Jumuiya ya Ulaya ( EU EOM) na Umoja wa Afrika wamesema kuwa uchaguzi huo ulikuwa wa huru na haki, utulivu na amani.

Waangalizi hao walitoa kauli hizo kwa nyakati tofauti wakati walipofanya mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana(leo) kuhusu taarifa ya awali ya uchaguzi huo.

Akizungumza na waandishi wa habari Mwangalizi Mkuu wa EU EOM, David Martin alisema uchaguzi huo ambao ni wa nne kufanyika nchini tangu mfumo wa vyama vingi kuanzishwa Tanzania, hadi sasa kwa ujumla umefanyika kwa amani na mpangilio mzuri.

“ Siku ya Uchaguzi Mkuu ilijitokeza kwa utulivu mkubwa na kwa ujuml a waangalizi wa uchaguzi wa Ujumbe Maaalumu wa Jumuiya ya Ulaya(EU EOM) ulikadria mchakato mzima wa uchaguzi huo kuwa ama ulikuwa ‘mzuri’ au ‘ kuridhisha’ katika asilimia 95 ya vituo vyote vya kupigia kura walivyovitembelea upande wa Tanzania Bara na upande wa Zanzibar,” alisema Martin.

Aliongeza kuwa kwa ujumla taratibu muhimu katika vituo vya kupigia kura zilitumwa kwa ulinganifu kwa kila kituo cha kupigia kura nchini kote, licha kuwepo mapungufu machache.

Martin alisema Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) na Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC) zilisimamia chaguzi kwa namna ya kitaalamu, hivyo kwa sehemu kubwa ziliwapatia watu watu wote haki ya kupiga kura.

Aliongeza kuwa ujumbe huo utabakia nchini kuzidi kufuatilia kwa karibu zaidi zoezi la kuhesabu matokeo ya uchaguzi, utangazaji wa matokeo na matukio yoyote yatakayojitokeza baada ya uchaguzi.

“Taarifa hii ni ya awali .Taarifa ya kina ya mwisho itatolewa baina ya miezi miwili na miezi mitatu baada ya mchakato mzima wa uchaguzi kukamilika,” alisema.

Kwa upande wake Kiongozi wa waangalizi hao, kutoka AU, Rais wa zamani wa Jamhuri ya Sierra Leone, Dk. Ahmad Tejan Kabbah alisema uchaguzi huo umefanyika wa amani na umefanyika kwa mujibu wa sheria za uchaguzi wa Tanzania .

Aliongeza kuwa umefanyika kwa kuzingatia Azimia la Durban Demorasia katika Chaguzi za Afrika la Julai mwaka 2002.

“ Waangalizi wa Umoja wa Afrika wamesema uchaguzi umefanyika kwa huru, haki , uwazi na uadilifu(Credible) .

Waangalizi hao ,waliwapongeza wananchi wa Tanzania, Vyama vya Siasa, wagombea , NEC, ZEC na vyombo vya usalama kwa kuwezesha uchaguzi huo ufanyike kwa amani na kuwashauri wagombea kukubali matokeo yanayotangazwa na NEC.

MPIGIE KURA LEAH MUDY ASITOKE TUSKER PROJECT FAME.








Wafuatao ni washiriki wa TUSKER PROJECT FAME 2010 4 na anayetakiwa kipigiwa kura nyingi ni Leah mwenye namba 3 hivyo watanzania tunaomba mumpigie kura nyingi Leah Mud na kumpa kwa kuandika Tusker 3 kwenda 15522 mara nyingi zaidi kadiri iwezekanzavyo jitahidini kupiga kura kwa mtanzania mwenzetu ili asitoke kwenye nyumba ya Project Fame. wiki hii.

Tusker 1 – Atete Gaelle

Tusker 2 – Thomas

Tusker 3 – Leah

Tusker 4 – Amileena

Tusker 5 – Davis

Tusker 6 – Kuonck Deng

Tusker 7 – Rachel

Tusker 8 – Elizabeth Gaga

Tusker 9 – Msechu

Tusker 10 – Steve

Tusker 12 – Aneth

Tusker 13 – Paleki

Tusker 14 – Prudence

Tusker 15 – Gabiro

THE DON HIMSELF

Karibuni sana kwenye blog hii ya kijamii iliyosheheni makila kitu kuanzia siasa uchumi afya na burudani kwa ujumla wake.uingiapo kwenye blog hii ni mengi ambayo utapata nafasi ya kukutana nayo,kumbuka mawazo yako ndo hasa yanayojenga na kunifanya niwe na ufanisi zaidi.kariiiiiiibuuuuuuuuuuuu saaaaaaaaaaaaaaanaaaaaaaaaa.(THE DJ HIMSELF-JIWE)

Followers

BLOG ZA MARAFIKI

Search This Blog

ZILIZOPITA

DUNIA MUZIMA