Nov 3, 2010

Balozi wa Marekani apongeza ushindi wa Dr. Shein, Zanzibar


Balozi wa Marekani nchini Tanzania,Alfonso E. Lenhardt

Marekani inampongeza Dk. Ali Mohamed Shein kwa kuchaguliwa kwake kuwa Rais wa Zanzibar. Uchaguzi huu wa kihistoria na ambao umeripotiwa kuwa uchaguzi wa amani na uliosimamiwa vyema zaidi katika historia ya Zanzibar, utawezesha kuundwa kwa serikali ya kwanza ya umoja wa kitaifa visiwani humo.

Watu wa Zanzibar walijitokeza kwa wingi kutekeleza wajibu wao wa kupiga kura, wakitambua kuwa serikali yao mpya itawawakilisha Wazanzibari wote.

Viongozi wote wawili, Dk. Shein na Maalim Seif Sharif Hamad, ambao hivi sasa wanageuka kutoka kuwa wapinzani wakuu na kuwa wabia katika kuiongoza nchi yao, wanastahili pongezi kwa kuendesha kampeni za kuwaandaa wanachama na wafuasi wao kwa aina mpya ya serikali.

Ni imani kwamba Dk. Shein and Maalim Seif wataweza kufanyakazi pamoja kama wabia na kuweka malengo ya pamoja kwa maslahi ya Wazanzibari wote.

Watu wameshatoa kauli yao, hivi sasa ni wakati wa kujenga imani katika taasisi za serikali na kujenga Zanzibar mpya yenye msingi imara kwa ustawi na maendeleo ya kijamii. Kwa kujenga utamaduni mpya wa kisiasa, viongozi wa Zanzibar wataweza kuchochea ubunifu wa watu wa Zanzibar.

Serikali mpya itawajengea wapiga kura imani kwa kuhakikisha kuwa manufaa ya fursa za maendeleo ya kijamii na kiuchumi yanafika katika mikoa yote ya Zanzibar.

Urafiki kati ya Marekani na Zanzibar ni wa kina na wa kihistoria. Ninapenda kuwahakikishia Wazanzibari kwamba Marekani itaendelea kuwa rafiki wa kweli wa Zanzibar.

Tutadumisha kiwango cha juu cha misaada yetu katika maeneo muhimu na yanayowagusa watu wote, ambayo ni pamoja na elimu, afya, nishati na miundombinu. Mradi wa umeme wa Megawati 100 kwenda Unguja unaendelea.

Mradi wa ujenzi wa barabara huko Pemba unaendelea. Jitihada zetu katika kuzuia na kutokomeza maradhi nazo zitaendelea.

Tukishirikiana na wadau wengine duniani katika nyanja ya teknolojia, tunaongeza jitihada zetu za kupeleka kompyuta katika kila shule ya msingi visiwani Zanzibar. Ni matarajio yangu kuwa nitashirikiana na uongozi mpya wa Zanzibar katika kutekeleza mambo yote haya muhimu.

Ni vyema tuwe wakweli kuhusu changamoto zilizo mbele yetu. Serikali ya umoja wa kitaifa itakuwa na masuala mengi magumu ya kutatua. Pamoja na hayo, ni matumaini yangu ya dhati kwamba uchaguzi huu ni hatua muhimu sana katika safari ya kuelekeza Zama Mpya na Bora za Zanzibar.

No comments:

THE DON HIMSELF

Karibuni sana kwenye blog hii ya kijamii iliyosheheni makila kitu kuanzia siasa uchumi afya na burudani kwa ujumla wake.uingiapo kwenye blog hii ni mengi ambayo utapata nafasi ya kukutana nayo,kumbuka mawazo yako ndo hasa yanayojenga na kunifanya niwe na ufanisi zaidi.kariiiiiiibuuuuuuuuuuuu saaaaaaaaaaaaaaanaaaaaaaaaa.(THE DJ HIMSELF-JIWE)

Followers

BLOG ZA MARAFIKI

Search This Blog

ZILIZOPITA

DUNIA MUZIMA