Ni globu ya kijamii inayojihusisha na mambo yote ya kijamii,natumaini jamii yangu ya kitanzania itafaidika sana pindi ichukuapo fursa ya kuperuzi kwenye globu hii,dhamira yangu ni kufikisha ujumbe pamoja na kuiburudisha jamii yangu na furaha yangu ni kuona natimiza dhamira yangu kwako.natumaini kuwa wewe utaniunga mkono kwa kile ambacho nataka kukifanya kwa ajili ya jamii yangu ya kitanzania.NASHUKURU KWA KUNIELEWA.
Aug 5, 2010
HYUNDAI YAKABIDHI RASMI MAGARI YA "SHINDA MKOKO" KWA VODACOM TANZANIA
SIJAKATA TAMAA KISIASA ASEMA SHAMSI VUAI NAHODHA!!
Na Juma Mohammed, Maelezo Zanzibar.
Waziri Kiongozi, Shamsi Vuai Nahodha amesema hajakata tama kisiasa kwani ikitokea fursa yengine yoyote ya kuwania Urais wa Zanzibar hatosita kugombea kwa kuwa anaamini anazo sifa zinazotakiwa na Chama cha Mapinduzi(CCM).
Nahodha ambaye ni Mwakilishi wa Jimbo la Mwanakwerekwe alisema jana katika upandishaji bendera Tawi la CCM Mwanakwerekwe Mjini Unguja, alisema akiwa kijana anaamini nanaweza kutimiza matakwa ya CCM na wananchi wote kwa ujumla. “Napenda kuwaeleza kuwa mimi sijakata taamaa, bado nina matumaini na ikiwa itatokea fursa hiyo nitagombea tena, lakini kwa sasa ninayo kazi moja tu nayo ni kukisaidia Chama changu mgombea wetu Dk. Shein ashinde katika Uchaguzi Mkuu” Alisema Nahodha.
Waziri Kiongozi alisema kuwa kama walivyo wazee vijana nao wana uwezo mkubwa katika nafazi za uongozi na wanaosema vingine wamefilisika kisiasa. “Hata wazee wasiokuwa makini wapo kama ilivyo kwa baadhi ya vijana, lakini si sahihi vijana wakanyimwa nafasi ya uongozi eti tu sababu ya ujana wao” Alisema Nahodha ambaye kwa sasa ana umri wa miaka 48.
Nahodha alitumia fursa hiyo kuwataka radhi waliokereka katika Jimbo lake juu ya hatua ya kuwania tena Uwakilishi akisema alifanya hivyo kwa faida ya Chama na Serikali na kuahidi ataweka uzito mkubwa kiutendaji katika Jimbo iwapo atawaa tena nafasi hiyo.
Akizungumzia umuhimu wa ujenzi wa majengo bora ya matawi ya CCM, Nahodha ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu na Halmashauri Kuu, alisema majengo ya Chama hicho lazima yaendane na hadhi ya CCM.
Hata hivyo, alionya kwamba uhai na uimara wa CCM hautokani na majengo mazuri pekee, bali namna wanachama wake watakavyokienzi ndani ya nyoyo zao na viongozi kuwajibika. Nahodha alichangia ujenzi wa jengo hilo shilingi milioni 2 taslimu na kuahidi kutoa shilingi milioni tatu kabla ya Uchaguzi Mkuu ili kutoa msukumo kwa Tawi hilo liweze kutumika mapema.
Mkutano wa wanasheria wa Africa na Asia (AALCO) wafunguliwa jijini Dar es salaam!!
(Picha na Aron Msigwa – MAELEZO).
Mkurugenzi wa Taasisi ya kupambana na Rushwa TAKUKURU Dk. Edward Hosea kushoto Mwanasheria Mkuu wa Serikali Jaji Friderick Werema kulia na Naibu Mwanasheria mkuu George Masaju pamoja na washiriki wengine wa mkutano huo wakifuatilia kwa makini wakati ulipokuwa ukiendelea leo mara baada ya kufunguliwa rasmi.
Mwanasheria mkuu wa Malaysia na Rais wa mkutano wa mwaka wa 48 wa Umoja wa Mashauriano ya sheria kwa nchi za Asia na Afrika(AALCO) Bw. Abdul Gani Patail akiongea na washiriki wa mkutano huo leo jijini Dar es salaam.
Waziri wa Nchi , Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge) Philip Marmo kushoto na viongozi wa Mkutano wa 49 wa Umoja wa Mashauriano ya sheria kwa nchi za Asia na Afrika wakifuatilia matukio mbalimbali wakati wa mkutano huo leo jijini Dar es salaam.
MAONESHO YA NANENANE YAENDELEA MKOANI - DODOMA!!
Waziri wa Nchi ,ofisi ya Waziri Mkuu (TAMISEMI) Mhe. Celina Kom bani (kushoto)na wa pili kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Bahi ndugu Betty Mkwasa wakimsikiliza Ofisa mwandamizi wa Karadha ya Fedha ,Benki ya Rasilimali Tanzania ni ndugu Betty Massanja kwenye Maonyesho ya Nanenane Mkoani Dodoma, Maonesho hayo yanatarajiwa kumalizika tarehe 8 Agosti mwaka huu.
Waziri wa nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (TAMISEMI) Mhe. Celina Kombani wa pili kulia akimsikiliza kwa makini Ofisa wa Kilimo (Kilimo na Lishe) ndugu Stella Kimambo jinsi mashine iliyopo mbele yao ijulikanayo kama (Cassava Grater)inayosaga Mhogo mbichi na kupata machicha ambayo unaanika nakusaga tayari kwa unga au unaukamua tayari kuwa wanga na ukautmia kama dawa ,na pia ukatumika kwa kutengenezea chapati ,kwenye maonyesho ya nanenane Mkoani Dodoma. (Picha zote na Anna Itenda- Maelezo).
Mwenyekiti wa kikundi cha Tupendane kilichoko katika kijiji cha Nala Wilayani Dodoma Bwana Peter Lenjole akimpa maelezo jinsi wanavyotumia Trekta ndogo za kulimia (Power Tiller) Waziri wa nchi ,Ofisi ya Waziri Mkuu (TAMISEMI)Mhe.Celina Kombani (wanne kushoto) kwenye Maonyesho ya Nanenane Mkoani Dodoma M-Net's Big Brother ALL STARS: Images from day 16 (Tuesday August 3, 2010)
It’s day 16 on M-Net’s Big Brother All Stars --- and Hannington and Sammi are getting used to life in the Barn! Meanwhile in the main All Stars house, the housemates are having a ‘clucking’ time in their latest task that sees them dressed as chickens!Stay tuned to M-Net’s BIG BROTHER ALL STARS with 24/7 coverage on DStv channel 198 plus daily edited shows on M-Net and AfricaMagic. For more information on the series, log on to www.mnetafrica.com/bigbrother. Pictured here: Yacob
Aug 4, 2010
WAKALI WA JALA MAN RECORDS NDANI YA STUDIO ZA RADIO MLIMANI
super duper producer toka jala man recordz (jalamani) akiwa na vijana wake akijibu moja ya mswali aliyoulizwa katika interview na DJ JIWE4EVER.
DOUBLE H & CHIAA wakiwa ndani ya studio za radio mlimani.
show lav to ya all niggaz''double h''
kama ndo tuko mapumziko tukisikiza ngoma ya NIACHENI NIONGEE toka kwa jalamani akimshirikisha NAY - WAMITEGO na BEKA.
Tayari kwa interview kaka unasay aje JIWE?''jalamani''
JIWE mi nisha choka bana nataka embassy kama vipi mi nasepa mana full baridi na huko nje kuna kimvua aisee.''jalamani''Aug 3, 2010
Wizaraya Viwanda Biashara na Masoko katika Maonesho ya Nane Nane Dodoma
Maonesho ya 88 mwaka 2010 yameanza kwa kishindo mjini Dodoma. Wizara ya Viwanda, Biashara na Masoko(WVBM) imejipanga kikamilifu kutoa huduma bora kwa muda wote wa maonesho. Tafadhali, usikubali kuhadithiwa, fika mwenyewe katika banda lao, ujionee..
Naibu Waziri wa Miundo mbinu Mh Hezekia Chibulunje na Mkuu wa Mkoa wa Singida Parseko Kone wakitembelea banda la WVBM.
Mgeni rasmi katika ufunguzi Mh Parseko Kone akipata maelezo kuhusu trekta jipya la kisasa lilitengenzwa na taasisi ya Camartec.
Dk. Asha-Rose Migiro Azindua Mradi wa Maktaba Mtandao LRCT
HAWA NDIYO WACHEZAJI WALIOITWA KWENYE TIMU YA TAIFA AKIWEMO JUMA KASEJA BAADA YA KUSOTA MUDA MREFU!!
Wachezaji 27, watakaoingia kambini kwa ajili ya kujiandaa na mchezo kati ya timu ya taifa ya Misri na timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars ambao wanatarajiwa kuingia kambini siku ya jumatano. Golikipa wiki hii na majina yao chini ya kocha Jan Paulsen.
Jackson Chove (Azam FC), Shaaban Kado (Mtibwa), Juma Kaseja (Simba) Fullbacks Shadrack Nsajigwa (Yanga) Salum Kanoni (Simb Stephano Mwasika Juma Jabu (Simba) Idrissa Rajab (Sofapaka Kenya) Center Backs Nadir Haroub 'Cannavaro' (Yanga) Kelvin Yondani (Simba) Erasto Nyoni (Azam FC) Aggrey Morris (Azam FC) Midfielders Nurdin Bakari (Yanga) Abdulhalim Humoud (Simba) Henry Joseph (Kongsvinger- Norway), Uhuru Seleman (Simba) Abdi Kassim (Yanga) Jabir Aziz (Azam FC) Kigi Makasi (Yanga) Seleman Kassim 'Selembe' Nizar Khalfan (Vancouver Whitecaps-USA) Forwards Mrisho Ngassa (Azam FC) John Bocco (Azam FC) Jerson Tegete (Yanga) Mussa Hassan 'Mgosi' (Simba). Danny Mrwanda (DT Long An- Vietnam).
LADY JAY DEE AMSHUKURU MUNGU, WAZAZI NA MUME WAKE GADNER G. HABASH!!
KWANZA NATOA SHUKRANI KWA MWENYEZI MUNGU KWA KUNIPA NGUVU NA KIPAJIWAZAZI BABA (MAREHEMU) NA MAMA KWA KUNILEA KATIKA MAADILI MAZURIWADAU NA MASHABIKI WA MUZIKI WANGU, VYOMBO VYOTE VYA HABARI KWA SUPPORTGARDNER G HABASH KWA KUNIPA MUONGOZO MZURI KATIKA KAZI YANGU:
KUHUSU MIAKA 10 YA LADY JAYDEE:Ni hatua kubwa kwangu binafsi kufikisha miaka 10 kwani kuna wengi nilioanzanao wameshindwa na kuishia njiani, hii ni changamoto kubwa sana kwangu yakunifanya niogope kuhusu kesho...Nimeamua kufanya sherehe za kuadhimisha kudumu kwangu katika kiwanda cha muzikikwa miaka 10.
Ambapo show itafanyika tar 6 August 2010. Kaitka ukumbi wa MZALENDO PUBMillenium TowersKiingilio kitakuwa 20,000/= kwa watakao book table (reserved)Na sh. 10,000/= kwa wengine wote watakaolipia mlangoni siku hiyo ya onyesho.
Siku hiyo kutakuwa na uzinduzi wa Albuma ya kwanza ya Band yangu ya MACHOZIinayoitwa COMBINATIONGazeti la Shear Illusions litauzwa kwa sh.5,000/= ambapo ndani ya gazeti hilokuna free copy ya CD mpya ya MACHOZI BAND.
Nitapiga nyimbo zote kuanzia album ya kwanza ya 1.MACHOZI, 2.BINTI, 3.MOTO4.SHUKRANI na nyimbo zingine za band zilizotamba kama Mtarimbo na Nilizama(Brotherman)
ALBUM YA COMBINATIONMajina ya nyimbo zilizomo kwenye album ya Combination ni:1. Raha2. Siku ya Kufurahi3. Teja 4. Mtarimbo dORO5. Elimu Shule6. Nilivyo7. Tunakuja8. Uko Juu9. Inuka Simama10. Nilizama (Brother)11. Natamani Kuwa Malaika12. Teja (Afro - Pop) Majina ya waimbaji wa mbele wa Machozi Band ni, Jonico Flower, Mao Santiago,Mwinyi Goha na Sam Machozi.
KURA ZA MAONI CCM HADI SASA!!
Na www.michuzi-matukio.blogspot.com
Miongoni mwa wanasiasa mahiri na wakongwe walioangushwa ni Mbunge wa Mtera, John Malecela, ambaye ameliongoza jimbo hilo kwa miaka zaidi ya 25, ambapo amekwaa kisiki kutoka kwa Katibu wa UVCCM wilaya ya Tarime, Livingstone Lusinde.
Mzee Malecela alipata kura 3,326 katika kata 13 kati ya 19 wakati mpinzani wake Lusinde amepata kura 3,375.Hata hivyo, Lusinde alifika katika ofisi za katibu huyo na kudai amekamilisha matokeo ya kata zote na ameshinda kwa kupata kura 5,810 wakati Malecela ana kura 5,379 .Barongo alisema katika jimbo la Mpwapwa, mbunge wa zamani George Lubeleje alipata kura 4,830 huku mpinzani wake Gregory Teu akipata kura 7,777.Jimbo la Kibakwe, George Simbachawene, aliibuka kidedea katika kata 13 kati 16 baada ya kupata kura 8,824 huku mpinzani wake Aggrey Galawika akiwa na kura 2,537.Miongoni mwa wanasiasa mahiri na wakongwe walioangushwa ni Mbunge wa Mtera, John Malecela, ambaye ameliongoza jimbo hilo kwa miaka zaidi ya 25, ambapo amekwaa kisiki kutoka kwa Katibu wa UVCCM wilaya ya Tarime, Livingstone Lusinde.
KATIKA KUSHEREKEA MIAKA KUMI JAY DEE KUSOMESHA YATIMA WAWILI!!
Mwanamuziki huyo amesema katika kusherehekea miaka yake hiyo kumi katika muziki PIA atawachagua watoto wawili ambao ni yatima kutoka katika vitua kadhaa hapa nchini na kuwasomesha kwa kulipia gharama zote kuanzia kidato cha kwanza mpaka kidato cha Nne katika kusaidia watoto wenye matatizo mbalimbali ya kibinadamu.
Jay Dee amesema kwamba anafurahia mafanikio yake katika muziki na amesema kitu kikubwa ni kuwa na nidhamu unapofanya kitu chochote kinachoweza kukuletea mafanikio katika maisha yako ya kila siku hivyo muziki anauheshimu na kuupenda kwa kuwa ndiyo kazi yake.
MGOMBEA URAIS WA NCCRA MAGEUZI ACHUKUA FOMU TUME YA UCHAGUZI!
WAKATI WA KUCHUKUA FOMU OFISI ZA TUME YA UCHAGUZI LEO
Mgombea Urais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya CCM Dkt Jakaya Kikwete(katikati) akiwahutubia wanachama mbalimbali wa CCM waliojitokeza kumsindikiza wakati akienda kuchukua fomu katika ofisi za Tume ya Uchaguzi ya Taifa jijini Dar es salaam leo . (Picha Aron Msigwa - MAELEZO na Freddy maro)
Msafara wa magari ukielekea katika ofisi za Tume ya Uchaguzi wakati Mgombea Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi Rais Jakaya Kikwete alipokuwa akisindikizwa na wana CCM kwenda kuchukua fomu leo
Mgombea Urais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya CCM Dkt. Jakaya Kikwete kuchukua fomu Tume ya Taifa ya Uchaguzi akiteta jambo na Katibu mkuu wa CCM Yusuph Makamba(kulia) leo katika viwanja vya ofisi ndogo ya CCM ya Makao makuu Dar es salaam wakati wa kumsindikiza Mgombea Urais kwa tiketi ya CCM Jakaya Kikwete kuchukua fomu ya Urais Tume ya Taifa ya Uchaguzi.Kushoto ni mgombea mwenza Dkt Mohammed Gharib Bilal.
Mama Salma Kikwete akiwa na Mama Maria Nyerere leo katika viwanja vya ofisi ndogo ya CCM ya Makao makuu Dar es salaam tayari kumsindikiza Mgombea Urais kwa tiketi ya CCM Dkt. Jakaya Kikwete kuchukua fomu ya kugombea Urais Tume ya Taifa ya Uchaguzi
Makundi ya watu wenye ulemavu yakijitokeza kuunga mkono juhudi za Mgombea Urais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya CCM Dkt. Jakaya Kikwete kuchukua fomu leo jijini Dar es salaam.
Msafara wa magari ukielekea katika ofisi za Tume ya Uchaguzi wakati Mgombea Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi Rais Jakaya Kikwete alipokuwa akisindikizwa na wana CCM kwenda kuchukua fomu leo
Mgombea Urais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya CCM Dkt. Jakaya Kikwete kuchukua fomu Tume ya Taifa ya Uchaguzi akiteta jambo na Katibu mkuu wa CCM Yusuph Makamba(kulia) leo katika viwanja vya ofisi ndogo ya CCM ya Makao makuu Dar es salaam wakati wa kumsindikiza Mgombea Urais kwa tiketi ya CCM Jakaya Kikwete kuchukua fomu ya Urais Tume ya Taifa ya Uchaguzi.Kushoto ni mgombea mwenza Dkt Mohammed Gharib Bilal.
Mama Salma Kikwete akiwa na Mama Maria Nyerere leo katika viwanja vya ofisi ndogo ya CCM ya Makao makuu Dar es salaam tayari kumsindikiza Mgombea Urais kwa tiketi ya CCM Dkt. Jakaya Kikwete kuchukua fomu ya kugombea Urais Tume ya Taifa ya Uchaguzi RAIS JAKAYA NA MGOMBEA MWENZA WACHUKUA FOMU TUME YA UCHAGUZI LEO!!
Aug 1, 2010
MLIMANI TV LEGEND-SYLIVIAH MWEHOZI
SYLIVIAH MWEHOZI
just chilling
akiwa ndani ya ofisi ya mhariri mkuu wa mlimani radio KHAMIS HASSAN DAMBAYA.
mmoja kati ya waanzilishi wa mlimani tv syliviah mwehozi aka WHITE akiwa nje ya mlango wa kuingia studio za mlimani radio.
Mwandaaji wa kipindi cha asili yetu mlimaini radio EDGER NGELELA,mhariri mkuu msaidizi mlimani radio TUMA PROVIAN DANDI na legend wa mlimani tv syliviah mwehozi wakiwa katika studio za radio mlimani.
Subscribe to:
Comments (Atom)
ME MYSELF & I
THE DON HIMSELF
Karibuni sana kwenye blog hii ya kijamii iliyosheheni makila kitu kuanzia siasa uchumi afya na burudani kwa ujumla wake.uingiapo kwenye blog hii ni mengi ambayo utapata nafasi ya kukutana nayo,kumbuka mawazo yako ndo hasa yanayojenga na kunifanya niwe na ufanisi zaidi.kariiiiiiibuuuuuuuuuuuu saaaaaaaaaaaaaaanaaaaaaaaaa.(THE DJ HIMSELF-JIWE)


