BAADA ya kuingia kwenye skendo ya kutoa picha za binti mwenzake mitandaoni msanii Sintah, huwenda akapoteza nafasi yake aliyopewa hivi karibuni kuwa Balozi wa UNAMID – United Nations Mission In Darfur.
Msanii huyo alipata kazi hiyo baada ya kuonekana ni mmoja kati ya wasanii wanajituma na kutafuta maendeleo, pia hayupo kwenye maskendo ya kumchafulia jina, lakini baada ya hii ya kutoa picha za utupu za Agnes Gerald (Agnes Masogange) kwenye mitandao inaweza kumfanya akatolewa kwenye nafasi yake.
Baadhi ya wasanii ambao wameshtushwa na ishu hiyo, bila kutaja majina yao, walidai kuwa nafasi aliyokuwa nayo Sintah ni kubwa na mambo anayoyafanya yanatia aibu kitu ambacho kitamfanya apoteze heshima yake.
Kwa upande wake Ray ambaye ndiye rafiki yake wa karibu kwa sasa, alidai kuwa haoni kama Sintah anaweza kupoteza nafasi hiyo, uwezo wake ni mkubwa na ishu hiyo ilitokea kwake na Agnes si ya kuweza kuchukuliwa kama sababu.
Kwa upande wake muhusika mkuu wa ishu hii Sintah, alidai kuwa hafikirii kama kuna uwezekano wa kupoteza nafasi hiyo kwani tatizo si lake ni la mtu mwingine zaidi ya yote yeye amewekwa ili kufuta ushahidi wa aliyeonekana naye humo katika uchafu wa Agnes.
“Uchafu uliofanywa na mtu mwingine hauwezi kunifanya mimi nishindwe kuishi mjini vizuri naamini alichokifanya hadi alikuwa anataka kunifanya mimi niwepo kwenye ishu yake, pia suala alilosema kuwa anataka kuweka picha zangu chafu mitandaoni najua hawezi,” alidai Sintah.
Ni globu ya kijamii inayojihusisha na mambo yote ya kijamii,natumaini jamii yangu ya kitanzania itafaidika sana pindi ichukuapo fursa ya kuperuzi kwenye globu hii,dhamira yangu ni kufikisha ujumbe pamoja na kuiburudisha jamii yangu na furaha yangu ni kuona natimiza dhamira yangu kwako.natumaini kuwa wewe utaniunga mkono kwa kile ambacho nataka kukifanya kwa ajili ya jamii yangu ya kitanzania.NASHUKURU KWA KUNIELEWA.
Aug 13, 2012
SAKATA LA PICHA ZA UTUPU HUENDA LIKAMFANYA SINTAH APOTEZE SHAVU LA ‘UNAMID-UNITED NATIONS MISSION IN DARFUR’...!
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
ME MYSELF & I
THE DON HIMSELF
Karibuni sana kwenye blog hii ya kijamii iliyosheheni makila kitu kuanzia siasa uchumi afya na burudani kwa ujumla wake.uingiapo kwenye blog hii ni mengi ambayo utapata nafasi ya kukutana nayo,kumbuka mawazo yako ndo hasa yanayojenga na kunifanya niwe na ufanisi zaidi.kariiiiiiibuuuuuuuuuuuu saaaaaaaaaaaaaaanaaaaaaaaaa.(THE DJ HIMSELF-JIWE)
No comments:
Post a Comment