Hivi ndivyo ilivyokuwa baada ya Dr. Ulimboka kuwasili uwanja wa ndege wa Mwl Nyerere Dar es salaam leo mchana.
Hivi leo majira ya saa nane mchana Dr. Ulimboka aliyekuwa nchini Afrika Kusini
kwa ajili ya matibabu baada ya kutekwa, kupigwa na kuumizwa sana. Hali hiyo ilimkuta baada ya kutekwa na watu
wasiojulikana na kumpiga na kumtesa kisha kumtelekeza kwenye msitu wa Magwe Pande.
Baada ya kurejea Dr. Ulimboka alipokelewa kwa shangwe kubwa sana na watanzania wenye mapenzi mema na wanaharakati mbalimbali.
Dr. Ulimboka alipewa nafasi ya kuzungumza machache kwa watanzania na
kitu cha kwanza alichokiongea ni kutoa shukrani kwa ndugu, jamaa na
marafiki pamoja na watanzania wote kwa kuwa pamoja nae kwa kila jambo na
hasa katika kipindi chote cha matibabu kwake.
Pia Dr. Ulimboka alitoa shukrani zake za zati kwa Mwenyezi Mungu kwani ndiye
aliyemnusuri na kifo na hatimae kuifikia siku hii ya leo na kuwa anafuraha kubwa kwa hatua
yake ya kiafya aliyofikia kwani alisema anawahakikishia watanzania kuwa
amepona na yuko fiti kabisa kwa kufanya lolote lile.
Na bila kusahau alitoa shukrani zake kwa madaktari wenzake kwa kuwa wamekuwa pamoja nae katika kila jambo.
Dr. Ullimboka kabla ya kutekwa alipokuwa kwenye moja ya vikao vya chama cha madaktari nchini Tanzania.
Dr. Ulimboka wakati alipookotwa baada ya kutekwa na watu wasiojulikana.
Dr. Ulimboka wakati akiwa hospital ya MOI jijini Dar es salaam .
DR. ULIMBOKA AMERUDI,
JE NI NINI HATIMA YA ALIYEFANYA MAASI HAYO?
JE NINI TAMKO LA MAHAKAMA KUHUSIANA NA SUALA LA UTEKAJI WA DR. ULIMBOKA?
JE NI NINI HATIMA YA ALIYEFANYA MAASI HAYO?
JE NINI TAMKO LA MAHAKAMA KUHUSIANA NA SUALA LA UTEKAJI WA DR. ULIMBOKA?
No comments:
Post a Comment