Profesa Jay |
Neno mkongwe lina maana kubwa sana na kila mwenye kuitwa
jina hilo anabeba uzito Fulani, iwe katika nyanja ya kisiasa,uchumi & sanaa
na hata michezo. Mtu huyo hutegemewa kufanya kitu kizuri katika eneo lake
husika ili liwe mfano kwa vijana wanaotamani kuwa kama yeye. Mathalani mchezaji
wa mpira wa miguu wa timu ya taifa ya Italia aitwaye Andrew Pirlo, tumeona
jinsi alivyotumia kipaji chake na hasa kuonyesha ukongwe wake katika timu
wakati wa michuano Euro iliyomalizika hivi karibuni katika nchi za Poland &
Ukrane ambazo ndizo zilikuwa wenyeji wa michuano hiyo,kiasi kwamba kila mmoja
wetu amekuwa akilitaja jina lake. Utasikia mtu wa mpira akisema “ Pirlo bwana yule
mzee fundi sana” hapa utaona jina mzee limetumika kama mkongwe!
Lady Jaydee |
Njoo katika tasnia ya muziki ambako ndiko nilikokusudia
kuyaandika haya utakayoyasoma. Hakika nchi yetu imejaliwa sana katika tasnia ya
muziki kuanzia ule wa dansi mpaka wa muziki wa kizazi kipya na tunajivunia kuwa
na wakongwe katika kila idara. Lakini je, ukongwe wa watu hawa unaleta tija?
Unatoa mwangaza kwa vijana chipukizi? Unaonyesha kweli ukomavu wao? Je wanaweza
kweli kuwanyooshea vijana hao chipukizi vidole kuwa eneo fulani wanakosea
ilhali wao wenyewe wanakosea? Hawawezi kufanya hivyo kwa sababu wao wenyewe
hawaonyeshi ukongwe wao. Hatuoni ukomavu wao ambao tunatarajia tuuone!
Unapotaja wakongwe ambao wapo katika tasnia ya muziki
wetu wa kizazi kipya hautakosa kuwataja watu kama Mr II,Lady JD,Prof Jay nk
hawa ni watu ambao wamehangaika na muziki huu kuufikisha hapa ulipofikia hakuna
ambaye hajui juhudi zao.Hakuna ambaye havijui vipaji vyao. Sote tunakubali
kwamba hawa ni majabari ya muziki wa kizazi kipya. Kwangu mimi hilo sina tatizo
nalo japo lipo tatizo ambalo mimi
ninaliona na ndilo lilonisukuma kuandika makala hii. Makosa yanayofanywa
na wasanii wetu wakongwe! Licha ya ukongwe wao lakini yapo makosa ambayo
yanawarudisha nyuma, makosa hayo huwapa chipukizi nafasi za kutokea!
Juma Nature |
Mathalani mkongwe Profesa Jay zamani kama Niggar Jay,
kwa siku za karibuni naona jamaa kama anatoka nje ya mstari, kwa nini?
Nitakwambia na kama nikikosea niambie! Hakuna ambaye hajui uwezo wa huyu jamaa
katika kuandika mashairi makali ya hip hop. Ni mmoja kati ya ma legendary wa
muziki wetu wa kizazi kipya lakini jamaa anaangushwa sana na kazi zake za video
nitakupa mfano, unamfahamu Ryan Leslie? Kama haumfahamu ngoja nikufahamishe
machache kuhusu yeye, jamaa ni mwandishi wa nyimbo,mtayarishaji wa nyimbo “
producer” na pia ni mwimbaji, je umekwisha wahi kuangalia baadhi ya nyimbo
zake? Unaufahamu wimbo wake unaitwa BEAUTIFUL LIE? Je umekwisha angalia video
yake? Kama bado tafuta na uangalie!
Wapo wasanii wakongwe Marekani mmoja wao ni Dr Dre,
jamaa kwa ukongwe wake kila anachokifanya
unaona kabisa ukongwe wake unaleta somo kwa vijana chipukizi wa
kimarekani. Mbona wakongwe wetu hatuoni ukongwe wenu? Umewahi kusikiliza toleo jipya la wimbo wa Profesa Jay unaitwa
Kamili Gado kamshirikisha produza Marco
Chali? ( ni toleo lake jipya kwa kuwa hana wimbo mpya tofauti na huo) Je umewahi
kuangalia video yake? Je inaendana na ukongwe wa jamaa? Ki ukweli HAPANA! Na
hapo ndipo makosa wanayofanya wakongwe wetu yanapoonekana.Kwa nini wasanii
chipukizi wasiwapige bao?
Afande Sele |
Kama wewe ni mkongwe ambaye tunakutegemea kwanini
uuchezee ukongwe wako? Kitu gani ambacho Jay anaweza kukisifia katika video
hiyo? Rangi sawa,wale wasichana sawa, uchanganyaji wa picha nao sawa? Vipi
kuhusu story board yake mbona ni wimbo ambao unauona kabisa mwenekano wake?
Kama mnaona ni ngumu kutengeneza “kichupa bora” ni bora
msiwe mnatoa video ambazo zitashusha thamani ya ukongwe wenu.
Ninyi ni watu
tunaowatagemea vijana wajifunze kufanya kilicho bora kutoka kwenu ama sivyo
vijana hao watakuwa wanawapiga bao nanyi mnabaki kulia kuwa media zinawabania
wakongwe, si kweli, ni ubora wa kazi zenu ndiyo utakaowaokoa iwe audio au video
zenu. Kama hazitakuwa bora hakuna atakayewabeba!
Gangwe Mob |
Kwa sasa vipindi
vya redio au runinga hakuna anayetaka viwe vibaya ni lazima viwe vizuri kwa maana ya kujipatia wasikilizaji au
watazamaji, kazi nzuri haiitaji kujua ni mkongwe au chipukizi kafanya, kazi
nzuri ni nzuri tu! Badilikeni wakongwe wetu. Fanyeni kazi zenye kiwango kikubwa
kulinda ukongwe wenu utakaowafanya muendelee kupendwa daima. Watanzania wana
hulka ya kupenda kilicho bora pasipo kujali aliyefanya hivyo ni mkongwe ama la!
Onyesheni ukongwe wenu, teteeni nafasi zenu ili
tujivunie ninyi na tuweze kuwanyooshea vidole vijana chipukizi kwa kutoa mifano
yenu na wao naamini watakubaliana na sisi na muziki wetu uzidi kuvuka boda hadi
boda mkiamua mnaweza sana na nafasi mnayo……………………..kazi kwenu!
No comments:
Post a Comment