Aug 14, 2012

MWENYEKITI WA KAMATI YA USAJILI SIMBA HANS POPE ATOA YA MOYONI - ASEMA YANGA WALIANZA NA BAHANUZI, KAVUMBAGU, TWITE, NA SASA WANAMUWINDA PASCAL OCHIENG


Said Bhanuzi na Didier Kavumbagu wakitambulishwa na Msemaji wa Yanga Luis Sendo - wachezaji hawa wawili Simba inadai Yanga imefanyia uhuni kama ilivyokuwa Mbuyi Twite.

Usajili wa Mbuyu Twite aliyejiunga Yanga, huku Simba nayo ikiingia naye mkataba, umeendelea kuwa 'kivutio', ambapo sasa Wekundu hao wa Msimbazi wameibuka na madai mapya.
Mwenyekiti wa Kamati ya usajili klabu ya Simba, Zacharia Hans Pope ameilaumu Yanga kwa kuuingiza mchezo wa soka kwenye machafuko.

Pope amesema kitendo cha wenzao kuwazunguka na kumshawishi Twite kurejesha fedha walizompa ili asajili Simba, kinaweza kuleta uhasama usio na ulazima."Tumepata taarifa kuwa baba mzazi wa Mbuyu (Twite) amemkataza mwanaye kuja kuichezea Yanga kwa hofu maisha yake."

"Mzee Twite anataka Simba na Yanga zikutane kufanya mazungumzo kwa lengo la kuweka mambo sawa kisha ndipo amruhusu kuja Tanzania," alisema Pope.

"Unadhani kwa kitendo walichofanya Yanga, mashabiki wa Simba watafurahi? Baba yake mzazi (Twite) amechukizwa na hali hiyo, anahofia usalama wa kijana wake," alisema Pope.
"Vita ya soka haina tofauti na ile ya siasa au dini. Kwa hiyo baba mzazi wa Mbuyu ameomba Yanga na Simba kumaliza suala hili mwanaye aweze kucheza soka kama ilivyo kazi yake."

Katika kusisitiza ukweli wa madai yao, Pope alisema tayari uongozi wa Yanga umeomba kukutana nao ili kuzunguza na kumaliza suala hilo.
"Ukweli ni kamba, hatuna tatizo na Yanga. Nafikiri siyo mara yao ya kwanza wala mwisho kutufanyia mchezo huu mchafu. Ni kawaida yao."

"Wameomba [Yanga] tukutane ili kumaliza utata wa suala hili, vinginevyo Twite hatakuja siyo kujiunga na Yanga au Simba, bali haji kabisa."
Aliongeza: "Tulianza mazungumzo na Bahanuzi (Said)wakatuzunguka na kumsainisha, ikawa hivyo tena kwa Kavumbagu (Didier) na sasa wametuma viongozi Kenya kutaka kumsainisha Pascal Ochien ambaye yupo na timu Arusha."

Pascla Ochieng - mchezaji mpya wa Simba ambaye Hans Pope Yanga wameshaanza kumuwinda.

"Nafikiri Yanga kama wanataka kulipa kisasi cha mabao matano tuliyowafunga, wacheze mpira na siyo kutuzunguka na kusajili wachezaji wetu."
"Hata sisi tunaweza mchezo huo mchafu---ni kweli tunaweza kuwafanyia, lakini hatuoni sababu ya kufanya hivyo," alisema zaidi Pope.


Source: Mwananchi.co.tz

No comments:

THE DON HIMSELF

Karibuni sana kwenye blog hii ya kijamii iliyosheheni makila kitu kuanzia siasa uchumi afya na burudani kwa ujumla wake.uingiapo kwenye blog hii ni mengi ambayo utapata nafasi ya kukutana nayo,kumbuka mawazo yako ndo hasa yanayojenga na kunifanya niwe na ufanisi zaidi.kariiiiiiibuuuuuuuuuuuu saaaaaaaaaaaaaaanaaaaaaaaaa.(THE DJ HIMSELF-JIWE)

Followers

BLOG ZA MARAFIKI

Search This Blog

ZILIZOPITA

DUNIA MUZIMA