Aug 14, 2012

FRANCIS CHEKA AZIDI KUNG'AA - AINGIA AKATIKA ORODHA YA MABONDIA DUNIANI


BINGWA wa ngumi za kulipwa, Francis ‘SMG’ Cheka ameingia katika orodha ya mabondia bora 15 duniani wanaotambuliwa na Chama cha Masumbwi cha IBF.

Cheka bingwa wa taji hilo Afrika ameingia kwenye orodha hiyo kufuatia viwango vya ubora vya dunia vya IBF vilivyotolewa hivi karibuni.

Kwa viwango hivyo, bingwa huyo wa Afrika wa uzani wa super middle ana nafasi ya kuwania Ubingwa wa Dunia wa IBF dhidi ya mabingwa kutoka nchi mbalimbali ulimwenguni.

Kwa mujibu wa Rais wa Chama cha Ndondi cha PST, Emmanuel Mlundwa, Cheka anaweza kuwania taji hilo dhidi ya Benjamin Simon na  Henry Weberwa wa Ujerumani.

"Mabondia wengine wanaoweza kucheza na Cheka kuwania ubingwa huo ni Maxim Vlasov  wa Russia, Marco Periban wa Mexico na Ezequiel Maderna wa Argentina," alitaja Mlundwa.

Wengine ni Paul Smith wa United Kingdom, Junior Talipeau na Serge Yannick  (Australia), Nikola Sjekloca na Alexander Johnson (United States),  Roman Shkarupa (United Kingdom), Luis Garcia  (Ireland), Rudy Markussen (Denmark) na Fulgencio Zuniga  wa Colombia. 


souce:mwananchi

No comments:

THE DON HIMSELF

Karibuni sana kwenye blog hii ya kijamii iliyosheheni makila kitu kuanzia siasa uchumi afya na burudani kwa ujumla wake.uingiapo kwenye blog hii ni mengi ambayo utapata nafasi ya kukutana nayo,kumbuka mawazo yako ndo hasa yanayojenga na kunifanya niwe na ufanisi zaidi.kariiiiiiibuuuuuuuuuuuu saaaaaaaaaaaaaaanaaaaaaaaaa.(THE DJ HIMSELF-JIWE)

Followers

BLOG ZA MARAFIKI

Search This Blog

ZILIZOPITA

DUNIA MUZIMA