RAIS AONANA NA RAIS MPYA WA GHANA, ATEMBELEA MASHAMBA YA MANANASI
|
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiagana na Rais
John Dramani Mahama wa Ghana nyumbani kwake jijini Accra leo Agosti 11,
2012 baada ya kumtembelea na kumpa pole ya msiba wa aliyekuwa Rais wa
nchi hiyo Marehemu John Evans Atta Mills aliyezikwa jana.
|
|
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika mazungumzo na Rais John Dramani Mahama wa Ghana nyumbani
kwake jijini Accra leo Agosti 11, 2012 wakati alipomtembelea kiongozi
huyo mpya wa Ghana na kumpa pole ya msiba wa aliyekuwa Rais wa nchi
hiyo Marehemu John Evans Atta Mills
|
|
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akitazama manasi yakitayarishwa kwa
ajili ya kusafirishwa na kuuzwa nje ya nchi katika kiwanda cha Bomarts
Farms Ltd. katika kitongoji cha Dobro nje kidogo ya jiji la Accra leo
Agosti 11, 2012
|
|
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akitazama ukulima wa kisasa wa manasi
yanayolimwa kwa ajili ya kuuzwa nje ya nchi katika shmaba la Bomarts
Farms Ltd. katika kijiji cha Dobrokatika eneo la Nsawam nje kidogo ya
jiji la Accra leo Agosti 11, 2012. Kulia kwake ni Mtendaji Mkuu wa
shamba hilo Bw. Anthony Botchway na mwenye suti ya buluu ni Waziri wa
Chakula na Kilimo Mhe Kwesi Ahwol
|
|
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiangalia upandaji wa miche ya
mananasi katika shamba la Koranco kijiji cha Obotweri nje kidogo ya
jiji la Accra. Kulia kwake ni Mkurugenzi Mkuu wa Koranco Farms Ltd. Bw
Emmanuel B. Koranteng ambaye amekuwa akilima shamba la matunda kwa miaka
27. Mwalimu Nyerere aliwahi kumtembelea shambani hapo katikati ya miaka
ya 1980 kujionea ukulima huo wa matunda.
PICHA NA IKULU
|
THE DON HIMSELF
Karibuni sana kwenye blog hii ya kijamii iliyosheheni makila kitu kuanzia siasa uchumi afya na burudani kwa ujumla wake.uingiapo kwenye blog hii ni mengi ambayo utapata nafasi ya kukutana nayo,kumbuka mawazo yako ndo hasa yanayojenga na kunifanya niwe na ufanisi zaidi.kariiiiiiibuuuuuuuuuuuu saaaaaaaaaaaaaaanaaaaaaaaaa.(THE DJ HIMSELF-JIWE)
No comments:
Post a Comment