Aug 8, 2012

MAGAZETI YA LEO TRH 8/8/12


.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.

PICHA ZA AJALI YA NAIBU WAZIRI WA AFRIKA MASHARIKI


.
.
.
(Picha zimepigwa na francisgodwin.blogspot.com)
Naibu waziri wa Afrika Mashariki Abdullah Juma Saddallah amepata ajali ya gari alilokua akisafiria kwenye eneo la Kongowe Kibaha Pwani akitokea Dodoma kuja Dar es salaam.
Hiyo ajali imetokea leo jioni ambapo Naibu waziri amesema hali yake sio mbaya sana ila dereva ndio ameumia kiasi, bado wanapata matibabu kwenye hospitali ya Tumbi Kibaha Pwani,  chanzo cha ajali amesema ni baada ya dereva wake kukwepa lori lakini hakufanikiwa na gari ikatoka nje ya barabara.

PICHA 6 ZA MAPOKEZI YA PREZZO KENYA AKITOKEA BBA, HUYU NDIO MAMA MZAZI!



CMB PREZZO ambae ni mshindi wa pili wa Big Brother Afrika 2012 akihojiwa na waandishi wa habari baada ya kutua kwenye uwanja wa ndege wa Jomo Kenyatta
.
.
.
Mama na mwana.
(Picha zote ni kutoka bigbrotherafrica.com )

KAGAME CUP YAMTANGAZA BOCCO KIMATAIFA -AITWA KWENYE MAJARIBIO SOUTH AFRICA


Wiki kadhaa baada ya kufanya vizuri kwenye michuano ya Kagame Cup ambayo aliibuka miongoni mwa wafungaji bora wa michuano hiyo, mchezaji wa kimataifa wa Azam na timu ya taifa ya Tanzania John Bocco amepata nafasi ya kwenda kufanya majaribio ya kwenda kufanya majaribio nje ya nchi.

Kwa mujibu wa taarifa rasmi iliyotolewa na Azam FC, ni kwamba Bocco amepata nafasi ya kwenda South Africa kwa ajili ya kufanya majaribio ya wiki moja.
Taarifa hiyo ilisomeka:
"Azam FC imepokea barua ya mwaliko wa majaribio toka klabu ya Super Sport ya Afrika Kusini kwa mchezaji John Bocco ambapo atapaswa kusafiri Jumamosi tarehe 11/08/2012 kwenda Johannesburg Afrika ya Kusini. 
John Bocco atatumia muda wa wiki moja nchini Afrika ya Kusini. Uongozi wa Azam FC unampongeza John Bocco kwa mafanikio haya na unamtakia kila la heri kwenye majaribio yake."

SIMBA YARUDISHA KWA JAMII - WATEMBELEA WAGONJWA NA KUGAWA VYANDARUA - MTOTO AZALIWA APEWA JINA LA KASEJA


Sisi ni watu wa kujali jamii bwana... Makamu Mwenyekiti wa Simba, Geoffrey Nyange 'Kaburu' (katikati) akiwa pamoja na nahodha wa timu hiyo, Juma Kaseja (kulia) na beki Juma Nyosso (kushoto) wakibeba vyandarua na zawadi nyingine kwa ajili ya kugawa kwa wagonjwa wakati walipotembelea hospitali ya Mwananyamala jijini Dar es Salaam leo. Picha: Sanula Athanas
Nahodha wa Simba, Juma Kaseja akiwa katika eneo la hospitali ya Mwananyamala. Picha: Sanula Athanas

Chu chu chuuuuu.... tototoooooooo
Mchezaji mpya wa Simba aliyesajiliwa katika kipindi hiki cha usajili, Salim Kinje pia alikuwepo Mwananyamala Hospital.
Lengo letu ni kusaidia jamii hivi kila mara... Kaburu (kulia) akitoa mawili matatu wakati Simba ilipotembelea wagonjwa na kutoa zawadi leo.
Mnaonaje hali ya hapa hospitali?
Juma K. Juma akitoa chandarua kwa mgonjwa
Kaburu akiongoza msafara
Hii ndio Coaster yetu lakini basi kubwa la kisasa linakuja Agosti 15
Ezekiel Kamwaga akijiandaa kumwaga vyandarua hospitalini Mwananyamala leo

Leo sio mwisho, tutakuja tena na tena... Kaburu akizungumza na akina mama hospitalini Mwananyamala


VIONGOZI, wachezaji na wazee mbalimbali wa mabingwa Ligi Kuu ya Tanzania Bara, Simba wamefanya tukio la kihistoria leo baada ya kutembelea wagonjwa kwenye Hospitali ya Mwanaymala jijini Dar es Salaam na kugawa misaada mbalimbali.

Tukio hilo nadra kuonekana likifanywa na klabu za soka nchini limeelezewa na uongozi wa Simba kuwa ni sehemu ya wiki ya maadhimisho ya siku maalum ya kila mwaka ya klabu hiyo ya 'Simba Day'.

Makamu Mwenyekiti wa klabu hiyo, Geofrey Nyange 'Kaburu' ndiye aliyeongoza msafara huo huku kwa upande wa wachezaji, kipa na nahodha Juma Kaseja ni miongoni mwa nyota walioshiriki kukabidhi misaada hiyo, akiambatana na nyota wenzake kadhaa wakiwamo Juma Said Nyosso, Kigi Makassy na kiungo aliyesajiliwa msimu huu kutoka Kenya, Salim Kinje.

Akizungumza hospitalini hapo, Kaburu alisema kuwa wamewatembelea wagonjwa na kuwapa misaada kwa vile klabu yao ni sehemu ya jamii na hivyo wanapaswa kurejesha kidogo wanachokipata kwa kuwajali watu wenye mahitaji maalum.

Akaongeza kuwa mbali na kutembelea wagonjwa, pia watatembelea baadhi ya vituo vya watoto yatima na kuwapelekea misaada mbalimbali.

Baadaye, msafara huo wa Simba uliowatembelea wagonjwa waliolazwa katika wodi ya akina mama wajawazito na pia ya watoto waligawa vitu mbalimbali kama vyandarua, maji na sabuni.

Mganga Mfawidhi wa hospitali hiyo, Dk. Sophinias Ngonyani, aliwashukuru viongozi na wachezaji wa Simba kwa hatua yao ya kuwatembelea na kugawa misaada kwa wagonjwa; huku pia akiziasa klabu za soka na wanamichezo wengine kuiga moyo huo.
 

MTOTO APEWA JINA 'JUMA KASEJA'  

Katika tukio mojawapo la kusisimua hospitalini hapo, mama mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Rose Joseph alisema kuwa amefurahi sana  kuwaona 'live' wachezaji wa timu anayoishabikia ya Simba an kwamba, ameamua kumpa jina la 'Juma Kaseja' mtoto wake aliyemzaa leo asubuhi kwa vile alipata bahati ya kubebwa na kipa huyo nyota wa 'Wekundu wa Msimbazi' na timu ya taifa, Taifa Stars.

“Nimefurahi sana kumuona Kaseja akimbeba mwanangu,” alisema Rose.
Source:http://straikamkali.blogspot.com/

Aug 7, 2012

EXCLUSIVE: HIZI NDIO PICHA 11 ZA UTENGENEZAJI WA VIDEO MPYA YA DOGO JANJA, YA KWANZA TOKA ATOKE TIP TOP.


Location ni Sayansi Kijitonyama.
.
.
.
.
.
.
.
.
Video ya single mpya ya Dogo Janja ‘Yamoyoni’ ilikua ifanywe na Ogopa Dj’s Kenya lakini baada ya ishu flani kutokea ikabidi ifanywe na kampuni ya hapahapa Tanzania, imegharimu shilingi milioni 1.5 chini ya kundi la Watanashati linalomsimamia Dogo Janja.(kwa hisani ya millard ayo web)

Aug 6, 2012

URAIS 2015 WAVURUGA UCHAGUZI CCM




NI UCHAGUZI WA UVCCM, UWT, KILA KAMBI INAJIPANGA KUHAKIKISHA INAWEKA MTU WAKE, SHIGELLA ANASEMA WANAJUA MPANGO HUO
Raymond Kaminyoge
MBIO za kuwania nafasi za uongozi wa juu wa Jumuiya za Chama cha Mapinduzi (CCM), imeshika kasi huku taarifa zikionyesha kwamba kambi zinazowania urais wa 2015 ndani ya chama hicho, kila moja inajipanga kuhakikisha inaweka watu wake.
Wakati katika Umoja wa Wanawake (UWT) hadi jana mchuano ulikuwa ukionyesha kuwa mkali kati ya Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Sophia Simba na Mbunge wa Same Mashariki, Anne Kilango Malecela hali ni tofauti kwa Umoja wa Vijana wa chama hicho (UVCCM).
Hadi jana katika mbio za kuwania nafasi ndani ya UVCCM, vijana wanne walikuwa wamechukua fomu kuwania nafasi ya uenyekiti na wengine 16 wakiomba nafasi ya makamu mwenyekiti wa jumuiya hiyo ngazi ya taifa huku Katibu Mkuu wa Umoja huo, Martine Shigella akisema wanafahamu mikakati hiyo ya kambi za urais.
Kwa upande wa UWT, Kilango anaonekana kusimama kundi la makada wa CCM wanaojipambanua kupambana na ufisadi, huku Simba akiwa na kundi jingine tofauti na hilo lakini, pia lenye malengo ya urais wa 2015.
Baadhi ya vyanzo vya habari kutoka ndani ya CCM, vilisema mbali ya nafasi hiyo ya juu ya UWT, kinyang’anyiro hicho pia kipo katika nafasi za wenyeviti wa mikoa.
Tayari vita hiyo ya kambi za urais iko pia katika mikoa ambako kila kambi inajipanga kuweka mtu wake, huku katika Mkoa wa Tabora vita ikitarajiwa kuwa kali zaidi kati ya Margareth Sitta na mgombea wa kambi ya watuhumiwa wa ufisadi.

UVCCM
Kwa upande wa umoja huo wa vijana, kambi hizo zimekuwa zikiumana kuhakikisha kila moja inaweka mtu wake katika nafasi ya uenyekiti, makamu na ujumbe wa Baraza Kuu.
Hadi jana waliokuwa wakiwania nafasi za uenyekiti wa UVCCM Taifa ambao tayari walikuwa wamerejesha fomu ni Thabit Jecha Kombo, Sadifa Juma Khamis na Rashid Simai Msaraka.
Katika nafasi ya Makamu Mwenyekiti ni Paul Makonda, Ally Salum Hapi na Agustino Matefu. Makonda alirejesha jana na kuzungumza na waandishi akiahidi kupambana na mafisadi.
Wanaowania nafasi za Ujumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (Nec), kupitia UVCCM ni Theresia Mtewele, Halima Bulembo, Olivia Sanare, Ahmed Nyangani, Santo Tena, Vaileth Sambilwa, Faidha Salim na Augustino Samwiya.
Katika nafasi za Ujumbe wa Baraza Kuu la Taifa ni, David Mwakiposa, Mteweke Bulembo na Ester Mambali.
UVCCM ni ngome muhimu kimkakati kutokana na kuwa na vijana wengi wanaoweza kufanikisha ajenda mbalimbali ndani na nje ya vikao vya chama na jumuiya.
Uchaguzi huo wa UVCCM unafanyika wakati, kiti cha mwenyekiti kikiwa wazi tangu mwaka 2010 baada ya aliyekuwa mwenyekiti wake, Yusuf Hamad Masauni kuong’olewa akituhumiwa kudanganya umri na tangu wakati huo nafasi yake ilikuwa ikishikiliwa na Makamu wake, Beno Malisa.
Taarifa ya Sekretarieti ya chama hicho iliyowasilishwa katika kikao cha NEC mjini Dodoma mapema mwaka huu ilieleza kuwa makundi ya urais 2015 ndiyo yanayosababisha mpasuko ndani ya chama hicho.
Shigella: Tunajua
Akizungumzia mikakati hiyo ya vigogo wanaotaka urais kumwaga fedha ili kujiweka mazingira mazuri ya kuwa na watu wao ndani ya UVCCM, Shigella alisema wanajua mipango hiyo na kuonya kwamba kama kuna mgombea ambaye ametumwa na genge la watu wanaotarajia kuwania urais 2015, ajue anapoteza muda kwa sababu hatapitishwa.
Alisema jumuiya hiyo haijawahi kuwa na kiongozi aliyepandikizwa na mtu yoyote.
Alisema watatumia njia mbalimbali kuwabaini watu wa aina hiyo, hasa kwa kuitumia Kamati ya Usalama na Maadili ya jumuiya hiyo na kuwafanyia usaili wagombea na kuangalia historia zao.
“Kwa hiyo, kama kuna wanaowania nafasi za urais mwaka 2015 ambao wametuma vijana kutafuta nafasi UVCCM wafahamu kuwa hawatafanikiwa kwa kuwa tumejiandaa kukabiliana nao,” alisema Shigela.
Makonda na ufisadi
Kwa upande wake Makonda ambaye jana alikuwa wa mwisho kurejesha fomu kwa wiki iliyoisha jana, aliwaambia waandishi wa habari kuwa tatizo la rushwa na ufisadi kwa baadhi ya watu ndani ya UVCCM ndilo lililomsukuma kuwania nafasi hiyo.
Alisema historia ya UVCCM kutoka Tanu Youth League imejengeka katika misingi ya uadilifu na uzalendo, lakini katika siku za karibuni kumekuwa na baadhi ya watuhumiwa wa ufisadi ambao wamekuwa wakibomoa misingi hiyo na kujenga ya kwao ya kifisadi.
“Hii ndiyo changamoto ambayo imenifanya nijitose katika  kinyanganyiro hiki, si vizuri kuhama chama kikiwa na matatizo. Njia sahihi ni kutafuta uongozi ili kukabiliana nayo. Tukiwa na viongozi bora tutakuwa na uchungu wa namna ya kutatua matatizo ya vijana, kama uchumi na hata mikakati ya ajira,” alisema.
Alisema wakati rushwa ilitajwa kama adui wa haki katika moja ya ahadi 10 za Mwana-TANU, sasa hivi imekuwa ikitumika kama haki ya kupata uongozi hivyo vijana wanyonge wasiokuwa na fedha za kutoa rushwa kukosa nafasi za kuongoza.
Nape: Tumejipanga
Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa, Itikadi na Uenezi, Nape Nauye alisema hafahamu kama kuna vijana wanaowania nafasi mbalimbali kwa lengo la kuwasaidia vigogo kwenye mbio za urais mwaka 2015.
“Ndiyo kwanza unaniambia, sina habari hizo. Katika CCM tunachoangalia ni kwamba wanaowania nafasi hizo ni kutojihusisha na rushwa vinginevyo hawatakuwa na sifa za kuchaguliwa,” alisema Nape.(source mwananchi)

Twite: Simba mtanipenda tu


Asema maumivu ya Yondani yamemalizika
Kalunde Jamal
BEKI wa timu ya APR ya Rwanda aliyeingia mkataba wa miaka miwili na Simba, Mbuyu Twite amesema kuwa anakuja Simba kuleta raha na anaamini atakuwa kipenzi cha mashabiki kutokana na soka yake.

Mbuyu aliyeng'ara na APR katika michuano ya Kombe la Kagame, kwa mara ya kwanza alihojiwa na Spoti Mikiki wakati wa michuano hiyo akielezea kumalizika kwa mkataba wake na nia yake ya kutaka kuichezea Simba.

Akizungumza na Mwananchi Jumapili kwa njia ya mtandao wa facebook, Twite alisema: "Nimekubali kwa ridhaa yangu, nitakuja kuichezea Simba na kuonyesha kiwango...lakini zaidi kuleta ushindani kwenye Ligi Kuu ya Tanzania."

Kauli hiyo ya Twite imekuja muda mfupi baada ya kusaini mkataba wa miaka miwili na timu hiyo ya Mtaa wa Msimbazi.

Twite aliyedakwa na Ismail Aden Rage aliyempatia Dola30,000 kwa mujibu wa gazeti dada la Mwanaspoti toleo la jana, anatarajia kujiunga na Simba wakati wowote baada ya kutoka DR Congo alikokwenda kuaga familia yake.

Akizungumza katika mtandao huo, Twite alisema alipokuwa kwenye michuano ya  Kagame iliyomalizika wiki mbili zilizopita alisikia sifa za timu mbili pinzani, Simba na Yanga ambazo zote zilikuwa zikimwania.

Alisema kuwa aliziona timu zote kuwa zina wachezaji wazuri na wanaoleta upinzani na zaidi ni kutoka nje hivyo kulingana na uwezo alionao anaamini anakuja kuleta mabadiliko kwenye ligi hiyo.

Mbuyu aliyewahi kuzichezea FC Lupopo ya DR Congo, alikiri kusema kuwa kabla ya kuingia mkataba na timu hiyo kuna kiongozi mmoja wa Yanga alikuwa amemwambia wataonana siku hiyo kwa ajili ya kumsajili lakini tayari alikuwa amemalizana na Simba.

"Nilichagua Simba kwa mapenzi yangu...ni kweli kulikuwa na kiongozi wa Yanga alikuwa Kigali kwa ajili ya kunisajili lakini nikaamua nibaki na hii kwa kuwa tayari Simba iko na faranga (fedha) mingi," aliandika Twite kwa maneno ya Kikongo.

Aliongeza kusema kuwa akiwa Tanzania aliiona Simba na anaifahamu vizuri soka yao hivyo ana uhakika wa kuja kuibadilisha na kuleta upinzani kwenye timu ambazo Simba itakuwa ikikutana nazo.

"...nimekubali kuja Simba, lakini pia viongozi inabidi wafanye mabadiliko kwa baadhi ya sehemu ikiwemo safu ya ushambuliaji ili tuweze kwenda sawa na kutwaa kila kikombe kinachokuja," alisema Twite ambaye amemaliza mkataba na timu ya APR mwezi huu.

Alifafanua kuwa kulingana na alivyoona uchezaji wa timu za Tanzania zilizoshiriki kwenye michuano ya Kagame na kwa mujibu wa michuano hiyo ndizo timu zilizofanya vizuri kwenye ligi  na bado ana nafasi ya kuonyesha uwezo kutokana na wachezaji wengi kuwa na uwezo wa kawaida na siyo wa kutisha.

Mwenyekiti wa klabu ya Simba Aden Rage alikwenda Kigali, Rwanda kwa ajili ya kumsajili mchezaji huyo na alifanya zoezi hilo Juzi na kumsainisha mkataba wa miaka  miwili wenye thamani ya Dola 30,000 .

Kwa mujibu wa Mwanaspoti, wakati Rage akiwa amemalizana na mchezaji huyo wakiwa wanakunywa chai, Binkleb alifanikiwa kumpata Mbuyu kwenye simu na alipomwambia anataka waonane kwa ajili ya kusaini Yanga, Mbuyu alijibu kwa Kiswahili cha lafudhi ya ki-Congo akisema: "Nipo na bamutu ba Simba, tumekwisha malizana."

Kusajiliwa kwa Mbuyu, sasa kunaifanya Simba kuimarisha ngome yake baada ya kumtema Lino Masombo wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo aliyeshindwa kuwika katika Kombe la Kagame.

Ilikuwa inaaminika kuwa Mbuyu na pacha wake, Kabange Twite, hawawezi kwenda popote bila kuachana na huko nyuma walikuwa pamoja katika timu ya Lupopo.(source mwananchi.com)

MANJI ATIMBA NA YANGA BUNGENI, AFUNGUA TAWI JIPYA - WAPONGEZWA





Mabingwa wa kombe la klabu Bingwa Afrika Mshariki na kati kombe la Kagame, timu ya Young Africans Sports Club leo imepongezwa na Wabunge wa Bunge la Jamhuri wa Muungano Tanzania kwa kufanikiwa kutwaa Ubingwa huo.

Akiongea katika Ukumbi wa Bunge, Spika wa Bunge la Jahmuri ya Muungano wa Tanzania mh, Anna Makinda alisema anawapongeza wachezaji na viongozi wake wote, kwa kulilteta Taifa ubingwa huo ambao timu 11 kutoka nchi wanachama zilishiriki.

Mh Makinda alisema anafuraha siku ya leo, kwa kuwa Bunge limetembelewa na wageni wengi, wakiwemo watu mashuhuri na wageni maalumu timu ya Young Africans Sports Club.

Spika alianza kwa kuwatambulisha Bodi ya Wadhamin wa klabu ya Young Africans wakiongozwa na mama mlezi wa klabu hiyo, Mama Karume, Francis Kifukwe kisha akawatambulisha Mwenyekiti mpya wa Young Africans Yusuph Manji na makamu mwenyekiti ndugu Clement Sanga.

Baada ya hapo ilifuata zamu ya wachezaji na viongozi wakiwa na wazee wa klabu hyo, makofi mengi mfululizo zaidi ya dakika moja vilianza kupigwa kwenye meza baada ya Nahodha Nadir Haroub Cannavaro kusimama na kuonyesha Kombe kwa watu wote na wabunge waliokuwepo ndani ya bunge.

Waziri Mkuu Mizengo Pinda pamoja na baadhi ya wabunge na mawaziri baada ya utambulisho wa Young Africans ndani ya bunge, walitoka nje kwa pamoja na kupiga picha na wachezaji na viongozi wa yanga wakiwa na kombe hilo la Kagame.

Baada ya utambulisho, wabunge wa wanachama wa Young Africans waliaaalika wageni wao wote kupata kifungua kinywa katika mgahawa wa bunge.

Wabunge wanachama wa Young Africans waliandaa kikao cha mda mfupi ndani ya ukumbe wa bunge la zaman (Msekwa Hall) ambapo wabunge, viongozi na wachezaji waliweza kufahamiana kwa undani zaidi.

Mwenyekiti Yusph Manji alifungua rasmi tawi jipya katika eneo la Bunge ambapo mwenyekiti wa Yanga tawi la bungeni ni mh. misanga, katibu mkuu wake akiwa ni Mh Godfrey Zambi, mweka hazina mh.Martha Mlata huku Grace Kiwelu, Mwigulu Nchemba, Faki Makame, na wengineo wakitajwa kama wajumbe katika uongozi huo.

Mh Captain George Mkuchika ambaye jana aliteuliwa kuwa mjumbe wa bodi ya wadhamin wa klabu, pia ndio aliyeteuliwa kuwa mlezi wa tawi la Young Africans bungeni.

Dua za kubariki tawi hilo zilisomwa kwa pande zote mbili za dini kisha wabunge na viongozi kupiga picha za pamoja, ambapo pia jioni ya leo wabunge wameaanda futari kwa ajili ya wageni hao.

Timu inatarajiwa kureje jijini Dar kesho kuendelea na maaandalizi ya msimu mpya wa ligi kuu nchini inayotazamiwa kuanza septembe mosi.

Source: http://www.youngafricans.co.tz

THE DON HIMSELF

Karibuni sana kwenye blog hii ya kijamii iliyosheheni makila kitu kuanzia siasa uchumi afya na burudani kwa ujumla wake.uingiapo kwenye blog hii ni mengi ambayo utapata nafasi ya kukutana nayo,kumbuka mawazo yako ndo hasa yanayojenga na kunifanya niwe na ufanisi zaidi.kariiiiiiibuuuuuuuuuuuu saaaaaaaaaaaaaaanaaaaaaaaaa.(THE DJ HIMSELF-JIWE)

Followers

BLOG ZA MARAFIKI

Search This Blog

ZILIZOPITA

DUNIA MUZIMA