Nov 2, 2010

SADC YASEMA UCHAGUZI MKUU WA TANZANIA ULIKUWA HURU NA WA HAKI.

Waziri wa Mambo ya nje wa Zambia Kabinga J. Pande ambaye pia ndiye kiongozi wa timu ya Waangalizi kutoka SADC akiongea na waangalizi mbalimbali kutoka jumuiya hiyo wakati alipotoa ripoti ya awali ya Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani wa Jamhuri ya Muunganjo ya Tanzania uliofanyika jumapili iliyopita nchini Kote. Bw Kabinga amesema uchaguzi huo pamoja na mambo mengine uchaguzi huo ulikuwa huru na haki na amepongeza wadau wote waliohusika na uchaguzi huo kwa ujumala mwake.
Baadhi ya Mabalozi na viongozi mbalimbali kutoka SDC waliohudhuria katika utoaji wa ripoti hiyo ya awali ya uchaguzi mkuu.
Wanasheria na maafisa kutoka Ofisi ya Msajili wa vyama vya siasa nao wamekuwepo katika mkutano huo uliofanyika kwenye hoteli ya Kilimanjaro Kempinski jijini Dar es salaam.
Waanagalizi wa SADC katika uchaguzi mkuu wa Tanzania wakiwa katika Hoteli ya Kilimanjaro Kempinski wakimsikiliza Kiongozi wa Waangalizi hao wakati alipotoa ripoti yao ya awali juu ya uchaguzi huo.

huyu ndiye mwanamuziki anayeingia mjengoni Dodoma!

Mr SUGU Joseph Mbilinyi Mbunge Mteule Mbeya mjini. Majimbo yaliyochukuliwa na wapinzania wa CCM
1.Musoma mjini - Vincent Nyerere- CHADEMA 2.Iringa mjini - Mch. Peter Msigwa- CHADEMA 3.Lindi mjini - Salum Halfani Barwani- CUF 4.Arusha mjini- Godbless Lema - CHADEMA 5.Mwanza Nyamagana- Hezekiah Wenje - CHADEMA 6.Moshi Mjini- Philemon Ndesamburo - CHADEMA 7.Maswa Magharibi- John Shibuda- CHADEMA 8.Maswa Mashariki- Silverster Kasulumbayi- CHADEMA 9.Ukerewe - Salvatory Naluyege- CHADEMA 10.Biharamulo - Dr. Mbasa - CHADEMA 11.Ilemela - Haines Samson- CHADEMA 12.Meatu- Meshack Opulukwa- CHADEMA 13.Kigoma Kaskazini- Zitto Kabwe- CHADEMA 14.Mbeya mjini - Joseph Mbilinyi - CHADEMA 15.Hai Kilimanjaro- Freeman Mbowe - CHADEMA 16.Vunjo - Augustino Lyatonga - TLP
17. Kasulu vijijini - Zaituni Buyogera - NCCR Mageuzi
18. Kasulu Mjini - Michael John - NCCR Mageuzi http://www.mwananchi.co.tz/

MRISHO MPOTO-WASANII WA TANZANIA WANA ULIMBUKENI WA KUIGA KILA KITU

Msanii mahiri wa mashairi nchini,Mrisho Mpoto ameeleza kile anachoamini kwamba,tasnia ya sanaa na wasanii wa Bongo hawawezi kamwe kupata mafanikio katika ngazi ya kimataifa kutokana na ulimbukeni wa kuiga sanaa za watu wengine, kudharau asili yao na kujipachika usupastaa wa kubumba.

Mpoto aliyasema hayo wakati akiwasilisha mada yake iliyohusu Muziki wa Asili na Mashairi kwenye Jukwaa la Sanaa Jumatatu hii ambapo alisisitiza kwamba,wasanii wa bongo wamekuwa ni wa kulalama na kulia njaa kutokana na kazi wanazozalisha kushindwa kabisa kupata mvuto wa kimataifa na kushindana kwani zimekuwa kwa asilimia kubwa zikifanana na tamaduni za nje hivyo kukosa jipya.

Akijitolea mfano yeye mwenyewe Mpoto alisema kwamba, ameweza kukaa chini na kubuni sanaa ya asili ya Tanzania ambapo amekuwa akighani mashairi na kuyaweka kwenye mdundo wa muziki na hivyo kupendwa na idadi kubwa ya watanzania na kupenya kimataifa hivyo kumfanya kupata mialiko na fursa nyingi za fedha ambazo zimekuwa zikimpatia mafanikio makubwa.

Kwake yeye Mpoto anaamini kwamba, Sanaa ya Tanzania na wasanii wake hawaonekani kugundua siri ya kufanya kazi za sanaa zenye asili yao na badala yake wamekuwa makasuku wa kujifananisha na kuishi maisha kama ya Ulaya na Marekani huku kazi zao zikifanana kila kitu na hizo za nje hali ambayo imeifanya sanaa kupwaya na wasanii wenyewe kuishi maisha ya njaa.

Aliongeza kwamba, ni ngumu kupata msanii wa bongo anayefanya sanaa peke yake kwani mara nyingi lazima wachanganye na shughuli zingine ili kupata kipato kutokana na kazi zao kutowalipa.Katika hili Mpoto anaamini kwa kiasi kikubwa limesababishwa na wasanii wenyewe kukosa ubunifu, kuiga kila kitu kutoka nje, kulewa sifa za mapema, kukumbatia sanaa zisizo za asili yao na kujipachika usupastaa wa kubumba.

“Nimekuwa nikipata mialiko mingi nje ya nchi,siku chache zijazo nitaenda Denmark,Finland,Ufaransa, na Uholanzi.Si kwa kuwa napendwa sana bali ni aina ya sanaa ninayofanya ina asili yangu ya Tanzania na inanitambulisha kila ninakokwenda.Waache wasanii wengine wavae nguo chini ya makalio yao au hata watembee uchi mimi nitabaki na magunia yangu.Hili ndilo naamini litaweza kunipa mafanikio na ninayapata” alisisitiza Mpoto.

Mpoto ambaye kwa sasa ni msanii pekee aliyepata mafanikio makubwa kutokana na kupata mikataba mingi ya matangazo, mauzo ya kazi zake na mialiko ya kimataifa kutokana na kukumbatia sanaa ya asili aliwashauri wasanii wa bongo kuacha kunakiri (kukopi) sanaa za nje na badala yake wakune vichwa katika kubeba sanaa ya asili ambayo hapana shaka itawatambulisha kimataifa na kuwapa mikataba minono ya ndani na ya nje.

Mpoto aliyekuwa ameambatana na muimbaji wake wa Mjomba Band,Ismail alisema kwamba, inatia aibu na kinyaa unapoangalia sanaa za bongo kwani zinaonekana kuandaliwa na watu wenye njaa, wanaosaka fedha za fastafasta kuliko kujali nini wanapeleka sokoni hali ambayo imekuwa ikiwafanya wasanii wa Tanzania waonekane ni wa hovyohovyo, wa kudharaulika na wasio na mkakati wa kufikia mafanikio ya kisanaa.

“Kuna watu wamefanya sanaa miaka nenda miaka rudi lakini hawapigi hatua.Wamekuwa ni watu wa kulalamika bila kuzingatia ni kwa kiwango gani sanaa zao zina ubunifu na kubeba asili na utambulisho wao.Ndugu zangu tusipozingatia haya mafaniko tutayasikia tu na tutakuwa watu wa kuganga njaa na kupiga mizinga ya vocha” alimalizia Mpoto.

TASWIRA LA TAIFA KATIKA PICHA

Wafanyabiashara hapakukalika hivyo walilazimika kusitisha huduma kwa muda.Hivi ndivyo hali ilivyokuwa katika kitongoji cha Tandika mara baada ya kuchelewa kutangazwa kwa matokeo ya uchaguzi mkuu.Hali hiyo ambayo ililete mtafaruku mkubwa sana katika eneo hilo mpaka kupelekea jeshi la Polisi kufika katika eneo hilo na kuanza kutuliza ghasia zilizokuwa zikiendelea katika eneo hilo,ambapo maduka yalifungwa na wamiliki wake kulazimika kuondoka kabisa katika eneo hilo.

Nov 1, 2010

HATIMAYE DK ALI MOHAMED SHEIN ASHINDA URAIS ZANZIBAR!

Dk Ally Mohamed Shein ameshinda Urais wa Zanzibar na amewapongeza wananchi wa Wazanzibar wote huku akimuomba mungu ampe hekima na busara ili kuiongoza vizuri Zanzibar na wananchi wake. Dk. Shein amemshukuru mpinzani wake Maalim Seif Sharif Hamad kwa kukubali matokeo hayo ya uchaguzi lakini pia amemshukuru kwa kutoka hotuba nzuri na yenye mwelekeo na uungwana kwa Wazanzibar wote huku akimsifu na kusema nuitashauriana vyema na kufanya kazi na maalim Seif Hamad kama Makamu wa Kwanza wa Rais Kwa moyo mmoja. Amesema uamuzi wa Asilimia 66 ya Wazanzibar ni uamuzi mzito kwani Zanzibar ni yetu wazanzibar wote na na tunatakiwa kuitumikia kwa pamoja ili kuendeleza nchi yetu nzuri ya Zanziba na lazima tuitumikie vizuri na kuienzi kama Wazanzibar wamoja. Dk Shein pia ameishukuru Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar kwa kuandaa na kusimamia uchaguzi vizuri na kwa amani na kuhakikisha umefikia tamati kwa amani kabisa ambapo kwa sasa Serikali ya Mapinduzi Zanziba inakwenda kuundwa kuwa Serikali ya Umoja wa Kitaifa ikishirikisha vyama mbalimbali visiwani humo..

Mawaziri wa Kikwete watupwa nje

Matokeo ya awali katika uchaguzi wa wabunge nchini Tanzania yanaonyesha kuwa mawaziri wasiopungua watatu waliokuwa katika serikali iliyomaliza muda wake tayari wameshapoteza viti vyao vya ubunge.

Aliyekuwa Waziri wan chi katika ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia mazingira, Dr Batilda Buriani wa CCM ameangushwa na Godbless Lema wa CHADEMA katika jimbo la Arusha mjini.

Lawrence Masha, aliyekuwa Waziri wa mambo ya ndani, amepigwa mwereka katika jimbo la Nyamagana na mgombea Ezekiah Wenje pia wa chama cha CHADEMA.

Ingawa CCM imeonyesha uimara wake katika maeneo mengi ya nchi, imeonekana kupoteza viti ambavyo awali vilikuwa ni ngome ya CCM.

"Kigogo" mwingine aliyepigwa mwereka ni Getrude Mongella wa CCM katika jimbo la Ukerewe, aliyewahi kuwa spika wa Bunge la Afrika.

Vincent Nyerere ambaye ni ndugu wa damu wa rais wa kwanza wa Tanzania, Julius Nyerere, ameshinda jimbo la Musoma mjini.

CHADEMA imeendelea kuipokonya viti CCM, ambapo katika jimbo la Iringa mjini Peter Msigwa amemshinda Monica Mbega.

Wengine wa CHADEMA ni John Shibuda, Maswa Magharibi.

Sylvester Kasurumbai - Maswa Mashariki

Pia chama cha wananchi CUF (Civic United Front) kimetwaa jimbo la Lindi mjini ambako Salum Baruan.

Hata hivyo CCM imeshinda kwa idadi kubwa ya kura katika ngome zake kama vile Peramiho, Jenista Mhagama amepata zaidi ya asilimia 90 ya kura.

Mohammed Dewji - Singida Mjini.

Mtutula Abdallah Mtutula – CCM - Tunduru Kusini.

Matale Ramo – CCM - Tunduru Kaskazini.

Abdulkarim Shah wa CCM ameibuka kidedea katika jimbo la Mafia.

www.bbcswahili.com

Oct 31, 2010

HAYA NI MATUKIO YA ASUBUHI KATIKA VITUO VYA KUPIGIA KURA WILAYANI TEMEKE, KINONDONI NA ILALA

Askari akiwatawanya wananchi waliokuwa wamejikusanya katika kituo cha shule ya msingi ya Madenge kata ya 14 Wilayani Temeke jijini Dar es salaam, watu hao walitii amri na kuondoka katika eneo hilo, haya ni matukio mbalimbali yaliyojiri katika baadhi ya vituo vya kupigia kura katika wilaya za Kinondoni, Ilala na Temeke tutaendelea kukuletea matukio kadiri hali itakavyokuwa
Hapa ni Shule ya Msingi Kijitonyama watu wakiwa wamejipanga tayari kwa kupiga kura mara baada ya kuona majina yao ubaoni.
Watu wakiangalia majina yao kwenye ubao ili kupiga kura katika kitu cha kupigia kura Shule ya Msingi Kijitonyama Wilayani Kinondoni hali ni tulivu kabisa.
Hapa ni Buguruni katika wilya ya Ilala ambapo waangalizi wa kimataifa wameonekana wakifuatilia mwenendo wa uchaguzi huo kwa kurekodi mambo mbalimbali yanayoendelea katika kituo hicho watu walikuwa ni wengi wakiendelea na zoezi la kupiga kura.
Hapa ni kitu cha Temeke kata ya 14 katika Shule ya msingi Madenge ambapo askari walionekana wakitawanya kikundi kidogo cha watu waliokuwa wamesimama karibu na kituo hicho.
Hiki ni kituo cha Temeke kata ya 14 jijini Dar es salaam na watu wako katika foleini kwa ajili ya kupiga kura hali ni shwari kabisa.
Hiki ni kituo cha Temeke Mwisho kilikuwa ni kitupu Kwani idadi ya wapiga kura ilikuwa ni kidogo lakini wasimamizi wa kituo hicho wamesema watu wanakuja kidogokidogo.
Wapiga kura wakiangalia majina yao kabla ya kupiga kura Mtoni Sifa.
Askari Polisi kutoka kituoa cha Kirwa Road wakipanga mikakati ya kuweka usalama wakati wote wa zoezi la kupiga kura katika kituo cha Mtoni Sifa asubuhi leo.
Wananchi wakiwa wamejipanga katika mstari kwa ajili ya kupiga kura katika kituo cha Mtoni Sifa Wilayani Temeke jijini Dar es salaam hali ni tulivu kabisa.
(kwa msaada wa blog jirani-fullshangwe)

CCM yahitimisha Kampeni zake


Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya CCM,Dr. Jakaya Kikwete akisalimiana na wananchi wakati alipowasili kwenye viwanja vya Jangwani leo kwa ajili ya kufunga mikutano ya kampeni kwa CCM.
Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Dk. Mohamed Gharib Bilal akiwahutubia wanachama na wapenzi wa Chama Cha Mapinduzi waliofurika katika viwanja vya Jangwani,jijini Dar leo wakati wa hafla ya kufunga mikutano ya kampeni za chama hicho.
Mgombea Urais kwa tiketi ya CCM, Dr. Jakaya Kikwete akisalimiana na mgombea mwenza wake Dk. Mohamed Gharib Bilal wakati akishuka jukwaani baada ya kumaliza kutoa salamu kwa wanaCCM kwenye hafla ya kufunga mikutano ya kampeni kwa CCM, iliyofanyika kwenye viwanja wa Jangwani jioni hii.
Dk. Mohamed Gharib Bilal akisalimiana na Rais Mstaaafu wa awamu ya tatu,Mh. Benjamin Mkapa na rais Mstaafu wa awamu ya pili,Mh. Ali Hassan Mwinyi wakati alipomaliza kutoa salamu zake kwa wapenzi na wanachama wa CCM waliofurika leo katika viweanja vya Jangwani jijini Dar wakati wa hafla ya kufunga mikutano ya kampeni.
Dr. Jakaya Kikwete akisalimiana na Mjumbe wa Halmashauri kuu kwa Mkoa wa Dar es Salaam, Asha Baraka, wakati akiingia kwenye viwanja vya Jangwani leo.
Sehemu ya wanachama na wapenzi wa CCM wakiwa wamefurika katika viwanja Jangwani kuhudhulia hafla hiyo ya kufunga mikutano ya kampeni kwa CCM iliyofanyika jioni hii.

Oct 30, 2010

FRIENDS OF JAKAYA KIKWETE WAWATAKA WATANZANIA KUMPA KURA JAKAYA KIKWETE!

Mwenyekiti wa Friends Of Jakaya Kikwete kutoka nchi za nje Haruna Mbeyu kutoka London Uingerea na Katibu wa Taasisi hiyo Zainab Janguo kutoka Marekani wakionyesha tuzo maalum waliyoitoa kwa Dk. Jakaya Kikwete kutokana na utendaji kazi wake wakati walipofanya mkutano na waandishi wa habari leo kwenye ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo jijini Dar es salaam. Friends Of Jakaya Kikwete wamewataka watanzania kumpigia kura Dk.Jakaya Kikwete ili aendelee kuijenga Tanzania katika miaka mitano ijayo.
Haruna Mbey Kulia na Zainab Janguo wakionyesha pia cheti cha kumtambua Dk. Jakaya Kikwete kwa uttendaji wake.
Mmoja wa wajumbe wa taasisi hiyo Baraka akiongea katika mkutano huo.
Bw. Mickey John Amos akiongea na waandishi wa habari katika mkutano huo.
Waandishi wa habari mbalimbali wakiendelea na kazi yao katika mkutano huo uliofanyika leo kwenye ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo jijini Dar es salaam.

SUPER COACH SYLLESAID MZIRAY HE IS NO MORE

HABARI ZIMEINGIA ASUBUHI HII ZINASEMA SUPER COACH SYLLESAID MZIRAY AMEFARIKI DUNIA ALFAJIRI YA LEO KATIKA HOSPITALI YA AGA KHAN JIJINI DAR ALIKOKUWA AMELAZWA AKISUMBULIWA N MALARIA. HABARI ZA MIPANGO YA MAZISHI ZITAFUATA MARA TU BAADA YA KUPATIKANA.
COACH MZIRAY , ALIYEKUWA MWAJIRIWA WA CHUO KIKUUU HURIA KAMA MHADHIRI, ATAKUMBUKWA KWA UMAHIRI KATIKA UFUNDISHAJI SOKA KATIKA VILABU MBALIMBALI HADI TIMU YA TAIFA ILIYOSHINDA UBINGWA WA NCHI ZA AFRIKA MASHARIKI. ALIFUNDISHA PIA PILSNER, SIMBA, YANGA, PAN AFRICAN NA KABLA YA MAUTI KUMKUTA ALIKUWA MWALIMU WA VIUNGO NA SAIKOLOJIA WA KLABU YA SIMBA. TUNAUNGANA NA WATANZANIA WOTE KUOMBOLEZA MSIBA HUU MZITO AMBAO NI PIGO KWA TASNIA YA MICHEZO NCHINI UKIZINGATIA KUWA TUNA MAKOCHA WACHACHE WALIOSOMEA FANI HIYO NA KUBOBEA.
MOLA AIWEKE ROHO YA MAREHEMU
MAHALA PEMA PEPONI
- AMIN

THE DON HIMSELF

Karibuni sana kwenye blog hii ya kijamii iliyosheheni makila kitu kuanzia siasa uchumi afya na burudani kwa ujumla wake.uingiapo kwenye blog hii ni mengi ambayo utapata nafasi ya kukutana nayo,kumbuka mawazo yako ndo hasa yanayojenga na kunifanya niwe na ufanisi zaidi.kariiiiiiibuuuuuuuuuuuu saaaaaaaaaaaaaaanaaaaaaaaaa.(THE DJ HIMSELF-JIWE)

Followers

BLOG ZA MARAFIKI

Search This Blog

ZILIZOPITA

DUNIA MUZIMA