Oct 3, 2010

usiku wa shear charity ball @ double tree hilton wafana sana usiku huu



Mkurugenzi wa Shear Illutions, Shekha Nasser akisoma hotuba yake mbele ya wageni waalikwa mbalimbali katika harambee ya kuchangia juhudi za CCBRT katika kusaidia watoto wenye matatizo.
Mkurugenzi wa Shear Illutions Shekha Nasser akizindua rasmi jarida la Shear kwa kutimiza mwaka mmoja,hafla hiyo ilikwenda sambamba na tukio la Shear Charity ball usiku huu ndani ya hotel ya Double Tree Hilton,Masaki jijini Dar.
Mgeni rasmi katika harambee ya kuchangia Juhudi za CCBRT katika kusaidia watoto wenye matatizo,Bw. Januari Makamba akizungumza mbele ya wageni waalikwa katika harambee hiyo iliyofanyika kwenye Hoteli ya Double Tree Hilton,Masaki jijini Dar usiku huu.Bw. Januari Makamba amewataka watanzania kusaidia watoto wenye matatizo ili nao waweze kupata mahitaji muhimu kama watoto wengine na kuwapunguzia matatizo waliyonayo.
Baadhi warembo wakiwa katika picha ya pamoja pindi waliposhiriki katika tukio la Shear Charity Ball usiku huu,ndani ya hotel ya Double Tree Hilton,Masaki jijini Dar.
Raqey akiwa na mkewe pamoja na Mdau mwingine wote kutoka I-View Photography
Mgeni rasmi katika harambee ya kuchangia Juhudi za CCBRT katika kusaidia watoto wenye matatizo, Januari Makamba wa pili kushoto akiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi wa Mawasiliano Vodacom Tanzania,Mwamvita Makamba kulia na kushoto ni Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala,Jerry Silaa na katikati ni Lissa Jensen aliyewahi kuwa mshiriki wa Miss Tanzania.
Wageni waalikwa mbalimbali wakifuatilia tukio la Shear Charity Ball usiku huu.
Ma Mc wa shughuli hii maalumu iliofanyika usiku huu ndani ya moja ya ukumbi wa mikutano wa hoteli ya Double Tree Hilton,shoto ni Taji Liundi pamoja na Penny.
Wageni waalikwa mbalimbali walioshiriki katika harambee ya Shear Charity Ball iliyokuwa maalum kwa ajili ya kuchangia harakati za CCBRT katika kusaidia watoto wenye matatizo.
Mkurugenzi wa Mawasiliano Vodacom Tanzania,Mwavita Makamba kushoto akiwa katika picha ya pamoja na Naibu Meya wa Wilaya ya Ilala, Jerry Silaa kulia na katikati ni mrembo Lissa Jensen.
Wageni waalikwa mbalimbali wakiwasili katika kushiriki harambee ya Shear Charity Ball iliyokuwa maalum kwa ajili ya kuchangia harakati za taasisi ya CCBRT katika kusaidia watoto wenye matatizo mbalimbali.Picha na Full Shangwe na Jiachie Blogs.

Oct 2, 2010

DK. BILAL MGENI RASMI MAADHIMISHO YA WIKI YA UMOJA WA WANAWAKE (UWT) DAR LEO!

Mgombea Mwenza wa Urais wa CCM, Dk. Mohamed Gharib Bilal, akiwahutubia mamia ya wanawake, wanachama wa UWT na wanachi waliohudhuria Sherehe za Maadhimisho ya Wiki ya Wanawake Tanzania Kitaifa zilizofanyika kwenye Uwanja wa CCM Mwinjuma Wilaya ya Kinondoni Jijini Dar es salaam leo Okt 2. (Picha zote na Muhidin Sufiani)
Mgombea Mwenza wa Urais wa CCM, Dk. Mohamed Gharib Bilal, akipokea Kadi ya Leila Seif, aliyekuwa Mjumbe wa Baraza la Wanawake wa Chama cha CUF, aliyejiunga na CCM na kukabidhi kadi ya CUF wakati wa Maadhimisho ya Sherehe za Wiki ya Wanawake Tanzania iliyofanyika Kitaifa kwenye Uwanja wa CCM Mwinjuma leo Okt 2.
Wasanii wanaounda kundi la Lady Eyes kutoka (kushoto) Luiza Mbutu, Vicky Kamata, Mwacity Almas, Nyota Waziri na Stara Thoma, wakiimba kwa pamoja kibao maalum kutoa burudani wakati wa Maadhimisho ya Sherehe hizo zilizofanyika kwenye Uwanja wa CCM Mwinjuma Kinondoni Jijini Dar es Salaam.
Wanamuziki wa Bendi ya African Stars ‘Twanga Pepeta’ wakishambulia jukwaa kutua burudani wakati wa Maadhimisho ya Wiki ya Wanawake Tanzania UWT Kitaifa iliyofanyika leo Okt 2 kwenye Uwanja wa CCM Mwinjuma Wilaya ya Kinondoni Jijini Dar es Salaam.
Kikundi cha wanawake wa Kinondoni kikiingia na bango leny e ujumbe wakati wa maadhimisho hayo.
Mgombea Mwenza wa Urais wa CCM, Dk. Mohamed Gharib Bilal, akisalimiana na Mama Maria Nyerere na Mama City Mwinyi, baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa CCM Mwinjuma leo Okt 2 kuhudhulia Sherehe za Maadhimisho ya Wiki ya Wanawake Tanzania Kitaifa, iliyofanyika leo kwenye Uwanja wa CCM Mwinjuma Mwananyamala Wilaya ya Kinondoni Mkoa wa Dar es Salaam.
Mgombea Mwenza wa urais wa CCM, Dk. Mohamed Gharib Bilal, akisalimiana na wanachama wa CCM na Wanachama wa Umoja wa Wanawake Tanzania, baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa CCM Mwinjuma Mwananyamala A jijini Dar es Salaam, katika Sherehe za Maadhimisho ya Siku ya Wiki ya Wanawake Tanzania Kitaifa leo.
Mgombea Mwenz a wa urais wa CCM, Dk. Mohamed Gharib Bilal na mkewe Bi Zakia Bilal, wakiingia kwenye Uwanja wa CCM Mwinjuma Mwananyamala Wilaya ya Kinondoni Jijini Dar es Salaam leo Okt 2, wakati alipokuwa mgeni rasmi katika Sherehe za Maadhimisho ya Siku ya Wiki ya Wanawake Tanzania (UWT) na Mkutano wa kampeni .

USIKU WA KHANGA WAFANA DIAMOND JUBILEE VIP!!

Mwanamitindo Machachari Fiderin Iranga akipita na vazi la Khanga jukwaani katika onesho la Usiku wa Khanga onesho lililoandaliwa na mbunifu wa mavazi Asia Idarous kutoka kampuni ya Faback Fashion, onesho hilo linafanyika kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee VIP usiku huu jijini Dar es salaam. Hivi sasa nahamia upande wa pili katika ukumbi huu huu wa Diambond Jubilee ambako kuna onesha la kukata na shoka la mwanamuziki kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Ferre Golla (Shetani) ambaye anafanya onesho pamoja na bendi ya Mashujaa ya jijini Dar es salaam usiku huu.
Mbunifu wa mavazi kutoka kampuni ya Kapwani Grace Sinamtwa akiwa katika picha ya pamoja na Mathew aliyevaa shati lililobuniwa na mbunifu huyo.
Mwanamuziki Baby Madaha akiimba katika onesho hilo.
Mkurugenzi wa Casablanca Pub ya Kinondoni Mamaa Salma akiwa katika pozi.
Mbunifu wa Mavazi Grace Sinamtwa wa pili kutoka kushoto akiwa katika picha ya pamoja na Jokate Mwegelo ambaye pia ameshiriki katika kuonesha mavazi ya Usiku wa Khanga kulia ni Brighter Fredy na kushoto ni Mathew Mkurugenzi wa Kapwani.
Wapenzi mbalimbali wa mitindo wakifuatilia onesho hilo.
Hebu licheki hili mdau
Vazi la jioni la kutokea lililobuniwa kwa khanga.
Vazi la ajabu lililobuniwa kwa makuti na Khanga.

MAMA SALMA KIKWETE AWASILI MKOANI KAGERA TAYARI KWA ZIARA!!

Mke wa Rais Mama Salma Kikwete 1-10-2010 amewasili kwenye uwanja wa ndege wa Bukoba ambapo katika ziara yake atazungumza na wanachama wa Umoja wa WanawakeTanzania(UWT) ili kuwahamasisha kujitokeza kwa wingi kupiga kura kwenye Uchaguzi Mkuu ifikapo 31 Oktoba 2010.Picha zote na Mwanakombo Jumaa. hapa anaonekana akivishwa skafu na chipukizi alipowasili katika uwanja wa ndege wa Bukoba mkoani Kagera (Picha na Mwanamkombo Jumaa wa Maelezo)
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akisalimiana na wanawake mara alipowasili ktk uwanja wa ndege wa Bukoba
Wanachama wa UWT Bukoba wakimlaki Mke wa Rais Mama Salma Kikwete alipowasili katika uwanja wa ndege
Viongozi wa chama na UWT Mkoa Kagera wakimsubiri kumpokea Mke wa Rais Mama Salma Kikwete alipowasili

FERRE GOLLA AKAMUA VILIVYO DIAMOND JUBILEE USIKU HUU!!

Mwanamuziki Ferre Golla kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo akicheza jukwaani wakati alipofanya onesho la kukata na shoka kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee usiku wa kuamkia leo jijini Dar es salaam ambapo alikonga nyoyo za mashabiki kwa kupiga nyimbo zake mbalimbali huku akishangiliwa na mashabiki. Onesho la mwanamuziki huyo lilisindikizwa na bendi ya muziki ya Mashujaa yenye makao yake kwenye ukumbi wa Mashujaa Vingunguti jijini Dar es salaam.
Huyu shabiki ni kama vile anatoka baruti jukwaani! lakini hii ilikuwa ni staili ya uchezaji tu,
Mmoja wa wanenguaji wa mwanamuzki huyo akicheza huku Ferre Golla akiimba.
Mwanamuziki Fere Gola akifanya vitu vyake na mmoja wa waimbaji wake.
Hapa Mecklicius akitafuta taswira ya Ferre Golla hayupo pichani wakati alipokuwa akiimba jukwaani.
Ferre Golla katikati akitambulishwa watangazaji wa TBC1 Benny Kinyaiya kushoto pamoja naye mtangazaji wa Clouds FM Sofia Kessy wakati alipopanda jukwaani ili kuonyesha uwezo wake katika muziki.
Mashabiki wa mwanamuziki Feree Golla wakidimbwilika na muziki wa mkali huyo wakati alipokuwa akifanya vitu vyake.
DJ wa siku nyingi kutoka Clouds FM Charles Mhimiji wa pili kutoka kulia nyuma aliyekaa naye alikuwepo ili kushuhudia burudani hiyo.
Mashabiki mbalimbali wakimshuhudia Ferre Golla mkali wa muziki kutoka nchini Congo wakati walipokuwa wakitumbuiza usiku wa kuamkia leo kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es salaam.

Mwanamuziki na Kiongozi wa bendi ya Mashujaa Jado Field Force akiongoza kundi hilo kwenye onesho lao katika ukumbi wa Diamond Jubilee ambapo bendi hiyo inamsindikiza mwanamuziki Ferre Golla kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo anayetarajiwa kupanda jukwaani na kundi lake dakika chache kutoka sasa ili kuonyesha uwezo wake kwamba yeye kweli ni Shetani katika muziki, haya wadau kaeni mkao wa kula ili kuapata matukio ya mwanamuziki huyo baada ya muda.
Mamaa Frola Bamboocha kama kawa akikamua kwa sana.
Rapa Maarufu wa bendi hiyo Mirinda Nyeusi akikamua jukwaani huku wanenguaji wa bendi hiyo wakimpa tafu.
Mamaa Frola Bamboocha Mnenguaji wa Mashujaa Band akikamua jukwaani kwa kushirikiana na wanenguaji wenzake.
Wanenguaji wa bendi ya Mashujaa wakifanya vitu vyao jukwaani kabla ya Ferre Gola na kundi lake kukamua.
Mgeni Rasmi Naibu Waziri wa Kazi Mh. Makongoro Mahanga kulia ankiwa na Mkurugenzi wa Mashujaa Group Limited Mamaa Sakina tayari kwa kushuhudia burudani.
Mamaa Amina Single aka Mwasi Kitoko wa pekee, First Lady wa Afro Vibes Times Fm na Mecklicius Times Fm, First Lady wa the Cut nao wapo ili kumuona Ferre Golla Live kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee usiku huu.
Dada Christina Malasusa kulia na Rafiki yake ambaye pia ni bosi wake Zahra Kuyugwa nao pia wapo wakishuhudia burudani hii.
Hapa Raymond Kigosi Ray anasinzia, mwenzake Steven Kanumba anasikitika sijui walikuwa wakifikiria nini, Hata hivyo burudani kutoka kwa bendi ya Mashujaa ilikuwa ikiendelea wakati wakionyesha hali hii. labda ulikuwa ni umakini wa kufuatilia onesho lenyewe hebu tuwaachie wenyewe.
Mashabiki mbalimbali waliojitokeza kwenye onyesho la mwanamuziki Ferre Golla na Mashujaa Band wakiwa wakifuatilia onesho hilo kwa makini kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es salaam usiku huu.

nyumba ya BSS yafunguliwa jijini dar


Meneja wa bia ya Kilimanjaro ambao ni wadhamini wakuu wa mashindano ya Bongo Star Search,George Kavishe akizungumza machache katika hafla ua ufunguzi wa nyumba ya BSS uliohanyika usiku wa jana jijini dar.nyumba hiyo ambayo ipo maeneo ya Mikocheni ndio itakayotumiwa na washiriki wa shindano la Bongo Star Search (BSS) wakati wote wa mchakato wa kumsaka BSS 2010.nyuma ni baadhi ya washiriki hao
Mmoja wa washiriki wa BSS awamu iliyopita,Rogas Lucas akitumbuiza katika hafla hiyo.
Mmoja wa washiriki wa BSS 2010,akionyesha makeke yake katika steji wakati wa ufunguzi wa nyumba ya BSS usiku wa jana.
Washiriki wa Bongo Star Search 2010 wakiwa katika picha ya pamoja katika hafla fupi ya ufunguzi wa nyumba watakayoitumia kwa kipindi chote cha mchakato wa kumtafuta BSS 2010.

Oct 1, 2010

yombo vya ulinzi na usalama vyasema visihusishwe na siasa , vimejindaa kupambana na watakaovunja amani

VYOMBO vya Ulinzi na Usalama vimesema kwamba vina wajibu wa kuhakikisha amani, usalama na utulivu wa nchi kwa wakati wowote, hivyo havifungamani na chama chochote cha cha siasa, bali vinatii viongozi na Serikali iliyoko madarakani.

Aidha vyombo hivyo, vimejiandaa kikamilifu kupambana na mtu, watu kikundi chama au taasisi yoyote itakayokwenda kiunyume na sheria, kuchochea au kufanya fujo, kuvunja amani kwa mujibu wa sheria, ikiwemo kuchochea kuyakataa matokeo ya Uchaguzi Mkuu unaotarajia kufanyika Oktoba 31, Mwaka huu.

Hayo yalisemwa (leo) na Mnadhimu Mkuu wa Jeshi ,nchini, Luteni Jenerali Abdulrahman Shimbo wakati akitoa tamko la vyombo hivyo, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa mikutano wa Makao Makao Makuu ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi Tanzania(JWTZ) jijini Dar es Salaam.

“Maofisa na askari wa vyombo vya ulinzi na usalama kwa mujibu wa sheria na kanuni za utendaji kazi hawana chama cha siasa. Wajibu wao ni kwa wananchi na Serikali iliyoko madarakani.,” alisema Shimbo huku akisema wasihusishwe na vyama vya siasa .

Shimbo alisema dalili zimeanza kuonekana za kutaka kuvunja sheria katika kampeni, kuchochea fujo na uvunjifu wa amani.

Dalili hizo siyo nzuri na zinaweza kuharibu utulivu na amani iliyopo kwa miaka mingi . Aidha baadhi ya taasisi na mashirika yameanza kujiingiza katika kampeni kwa lengo la kuwaelimisha wananchi kuhusu upigaji kura au kutoa matamko yanayolenga, kushabikia vyama vya vya siasa na wagombea.

Hivyo alizitaka taasisi na mashirika hayo kufanya kazi hizo kwa amani na kuelekeza nchi katika amani na utulivu, ikiwemo kufuata sheria.

“Vyombo vy usalama vinawahakikishia wananchi usalama, amani na utulivu wakati wa kampeni, upigaji kura, uapishaji na baada ya hapo. Tunataka kuwahakikishia wananchi hakuna damu itakayomwagika na hatutarajii hali hiyo itokee. Tungependa uchaguzi ulivyoanza vizuri uishe vizuri,” alisisitiza

.

Alivitaka vyama vya siasa vifanye kampeni kwa ustaarabu na kufuata sheria na kanuni za uchaguzi, hivyo visitukane vyombo vya dola wala kuvichokoza , kwa vile havihusiki na kampeni za siasa za uchaguzi zaidi ya kulinda amani.

Mnadhimu huyo pia aliwaomba ushirikiano kutoka kwa wananchi katika kutunza amani na usalama, kukataa kuhusishwa na uvunjaji wa sheria, au kukataa matokeo ya uchaguzi kwa fanya fujo kwa vile kufanya hivyo kunaweza kuingiza nchi kwenye machafuko yasiyo ya maana. Pia alivitaka vyama vya saisa na wananchi wote kuwa tayari kupokea matokeo ya uchaguzi huo kwa amani.

Akizungumzia kuhusu vyombo vya habari ,Shimbo alisema taarifa zinazotolewa hazichunjwi ipasavyo kuangalia athari zake kwa amani na utulivu wa nchi wa sasa na hapo baadae. Hivyo alivitaka kuandika habari zisizochea fujo au vurugu.

Wakati huohuo akizungumzia kuhusu uharamia alisema mtuhumiwa suala hilo, ambaye ni raia wa kisomali alikamatwa Septemba 26, mwaka huu kwenye eneo la utafiti wa mafuta block 7 kuwa anahojiwa na anendelea kuhojiwa hivyo atashitakiwa na kufikishwa mahakamani kuwa kuwa sheria za nchi zinaruhusu kumshitaki.

DK, GHALIB BILAL AFURAHIA NGOMA YA WAFIPA SUMBAWANGA!!

Mgombea Mwenza wa urais wa CCM, Dk. Mohamed Gharib Bilal, akimnadi mgombea ubunge wa Jimbo la Sumbawanga mjiji, Aesh Khalfan, wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika jana Spet 30 kwenye Kijiji cha Mtimbwa Kata ya Kasense Wilaya ya Kasense. (Picha na Muhidin Sufiani)
Mgombea Mwenza wa Urais wa CCM, Dk. Mohamed Gharib Bilal, akifurahia ngoma ya utamaduni yaKizuite ya kabila la Wafipa, wakati wa mapokezi yake alipowasili kwenye uwanja wa Kijiji cha Mtimbwa Kata ya Kasense Wilaya ya Sumbawanga Mkoa wa Rukwa, kufanya mkutano wa kempeni jana Sept 30.
Wasanii wa Kikundi cha Ngoma ya Utamaduni cha Kanondo, wakionyesha umahiri wao wa kecheza ngoma hiyo mbele ya Mgombea Mwenza wa urais wa CCM, Dk. Mohamed Gharib Bilal, baada ya kuwasili Kijiji cha Mtimbwa Kata ya Kasense Wilaya ya Sumbawanga Mkoa wa Rukwa kufanya mkutano wa kampeni jana Sept 30.
Wananchi wa Kijiji cha Mtimbwa Kata ya Sense Wilaya ya Sumbawanga Mkoa wa Rukwa, wakishangilia kwa pamoja wakati mgombea Mwenza wa urais wa CCM, Dk. Mohamed Gharib Bilal, alipokuwa akiwahutubia katika mkutano wa kampeni leo Sept 30.

THE DON HIMSELF

Karibuni sana kwenye blog hii ya kijamii iliyosheheni makila kitu kuanzia siasa uchumi afya na burudani kwa ujumla wake.uingiapo kwenye blog hii ni mengi ambayo utapata nafasi ya kukutana nayo,kumbuka mawazo yako ndo hasa yanayojenga na kunifanya niwe na ufanisi zaidi.kariiiiiiibuuuuuuuuuuuu saaaaaaaaaaaaaaanaaaaaaaaaa.(THE DJ HIMSELF-JIWE)

Followers

BLOG ZA MARAFIKI

Search This Blog

ZILIZOPITA

DUNIA MUZIMA