
Mwanamuziki Ferre Golla kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo akicheza jukwaani wakati alipofanya onesho la kukata na shoka kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee usiku wa kuamkia leo jijini Dar es salaam ambapo alikonga nyoyo za mashabiki kwa kupiga nyimbo zake mbalimbali huku akishangiliwa na mashabiki. Onesho la mwanamuziki huyo lilisindikizwa na bendi ya muziki ya Mashujaa yenye makao yake kwenye ukumbi wa Mashujaa Vingunguti jijini Dar es salaam.

Huyu shabiki ni kama vile anatoka baruti jukwaani! lakini hii ilikuwa ni staili ya uchezaji tu,

Mmoja wa wanenguaji wa mwanamuzki huyo akicheza huku Ferre Golla akiimba.

Mwanamuziki Fere Gola akifanya vitu vyake na mmoja wa waimbaji wake.

Hapa Mecklicius akitafuta taswira ya Ferre Golla hayupo pichani wakati alipokuwa akiimba jukwaani.

Ferre Golla katikati akitambulishwa watangazaji wa TBC1 Benny Kinyaiya kushoto pamoja naye mtangazaji wa Clouds FM Sofia Kessy wakati alipopanda jukwaani ili kuonyesha uwezo wake katika muziki.

Mashabiki wa mwanamuziki Feree Golla wakidimbwilika na muziki wa mkali huyo wakati alipokuwa akifanya vitu vyake.

DJ wa siku nyingi kutoka Clouds FM Charles Mhimiji wa pili kutoka kulia nyuma aliyekaa naye alikuwepo ili kushuhudia burudani hiyo.

Mashabiki mbalimbali wakimshuhudia Ferre Golla mkali wa muziki kutoka nchini Congo wakati walipokuwa wakitumbuiza usiku wa kuamkia leo kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es salaam.

Mwanamuziki na Kiongozi wa bendi ya Mashujaa Jado Field Force akiongoza kundi hilo kwenye onesho lao katika ukumbi wa Diamond Jubilee ambapo bendi hiyo inamsindikiza mwanamuziki Ferre Golla kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo anayetarajiwa kupanda jukwaani na kundi lake dakika chache kutoka sasa ili kuonyesha uwezo wake kwamba yeye kweli ni Shetani katika muziki, haya wadau kaeni mkao wa kula ili kuapata matukio ya mwanamuziki huyo baada ya muda.

Mamaa Frola Bamboocha kama kawa akikamua kwa sana.

Rapa Maarufu wa bendi hiyo Mirinda Nyeusi akikamua jukwaani huku wanenguaji wa bendi hiyo wakimpa tafu.

Mamaa Frola Bamboocha Mnenguaji wa Mashujaa Band akikamua jukwaani kwa kushirikiana na wanenguaji wenzake.

Wanenguaji wa bendi ya Mashujaa wakifanya vitu vyao jukwaani kabla ya Ferre Gola na kundi lake kukamua.

Mgeni Rasmi Naibu Waziri wa Kazi Mh. Makongoro Mahanga kulia ankiwa na Mkurugenzi wa Mashujaa Group Limited Mamaa Sakina tayari kwa kushuhudia burudani.

Mamaa Amina Single aka Mwasi Kitoko wa pekee, First Lady wa Afro Vibes Times Fm na Mecklicius Times Fm, First Lady wa the Cut nao wapo ili kumuona Ferre Golla Live kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee usiku huu.

Dada Christina Malasusa kulia na Rafiki yake ambaye pia ni bosi wake Zahra Kuyugwa nao pia wapo wakishuhudia burudani hii.

Hapa Raymond Kigosi Ray anasinzia, mwenzake Steven Kanumba anasikitika sijui walikuwa wakifikiria nini, Hata hivyo burudani kutoka kwa bendi ya Mashujaa ilikuwa ikiendelea wakati wakionyesha hali hii. labda ulikuwa ni umakini wa kufuatilia onesho lenyewe hebu tuwaachie wenyewe.

Mashabiki mbalimbali waliojitokeza kwenye onyesho la mwanamuziki Ferre Golla na Mashujaa Band wakiwa wakifuatilia onesho hilo kwa makini kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es salaam usiku huu.
No comments:
Post a Comment