Ile safari ya mwisho ya kila binadamu katika duniani hii kwa Perfect kasiga 'P. Diddy' imehitimishwa jioni ya leo katika makaburi ya Kinondoni jijini Dar es salaam huku warembo kibao wakipoteza fahamu wakati wa kuaga mwili wake. Ibada ya kumuombea marehemu, ambaye alikuwa mchumba wa mtangazaji wa TBC1, Maimartha Jesse, ilifanyika nyumbani kwake Kinondoni kwa Mwanamboka. P. Diddy, alifariki dunia ghafla barabarani mtaa wa Lumumba jana jijini Dar es salaam na kifo chake kushitua wadau wengi wa burudani jijini Dar es salaam.
Mtangazaji wa wa kipindi cha B&M, Ben Kinyaiya, ambaye anafanyakazi pamoja na Maimartha, mchumba wa marehemu, akitoa salamu zake za mwisho mbele ya jeneza huku akilia.
..hakika ni wakati wa majonzi na kilio kwa Ben Kimyaiya.
...warembo waliofanyakazi pamoja na marehemu katika masuala ya burudani walishindwa kujizuia kulia kwa uchungu
'Kimwana wa Manywele' (kati) ambaye anashikilia taji hilo lililoandaliwa na marehemu enzi za uhai wake, alikuwa miongoni mwa warembo waliopoteza fahamu (pichani chini) baada ya kumuaga marehemu.
Judith Mosha akisaidiwa kutembea baada ya kumuaga marehemu. Judith ndiye Mkurugenzi wa bendi ya Diamond Musica ambayo marehemu alikuwa mkurugenzi msaidizi wake ambaye alipanga bendi yake ifanye shoo kabambe wakati wa sikukuu ya Idd leo.
baadhi ya wanamuziki wa bendi waliohudhuria maziko....akiwemo Ali Choki (shoto), Kalala junior (wa pili kulia)
Maimartha Jesse akibebwa kuingia makaburini baada ya kushindwa kutembea.
MUNGU ALITOA NA MUNGU AMETWAA MJA WAKE, AILAZE ROHO YA MAREHEMU PEPONI-AMEEN!
(msaada toka global publisher)