Jul 2, 2010

SABA SABA SPECIAL








































Jun 24, 2010

AJIRA KWA WATOTO NI TATIZO KWA UKANDA WA KUSINI MWA AFRIKA


Na Anna Nkinda - Nairobi

Idadi ya watoto wanaofanya kazi za kuajiriwa imeongezeka katika nchi zilizopo kusini mwa jangwa la Sahara kutoka milioni 49 kwa mwaka 2004 hadi kufikia milioni 58 kwa mwaka 2008.

Aidha ajira za watoto wenye umri wa kati ya miaka 5 hadi 14 imeongezeka kwani mwaka 2000 ilikuwa milioni 48 sawa na asilimia 28.8, mwaka 2004 milioni 49 sawa na asilimia 26.4 na mwaka 2008 milioni 58 sawa na asilimia 28.4.

Hayo yamesemwa jana na Wangui Inimu ambaye ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Taifa kutoka Shirika la kazi Duniani (ILO) nchini Kenya wakati akitoa ripoti ya kimataifa kuhusu hali ya ajira za watoto ilivyo kwa sasa kwa wadau mbalimbali wanaofanya kazi na watoto katika hoteli ya Pan Africa jijini Nairobi.

Akifafanua takwimu za watoto wote wanaofanya kazi hapa Dunia alisema kuwa hivi sasa wako milioni 215 na kati ya hao watoto milioni 115 wanafanya kazi ambazi siyo salama kwa maisha yao .

Watoto wenye umri wa kati ya miaka mitano hadi 14 katika nchi za Asia na Pacific kwa mwaka 2000 waliokuwa wameajiriwa ni milioni 127 sawa na asilimia 19.1, mwaka 2004 ni milioni 122 sawa na asilimia 18.8 na mwaka 2008 ni milioni 96 sawa na asilimia 14.8. Nchi za Latini Amerika na Visiwa vya Caribbean mwaka 2000 walikuwa watoto milioni 17 sawa na asilimia 16.1, mwaka 2004 milioni 11 sawa na asilimia 10 na mwaka 2008 milioni 10 sawa na asilimia 9.

Inimu alisema, “Katika takwimu za kimataifa watoto kati ya umri wa miaka mitano hadi 17 kwa mwaka 2000 waliokuwa wanafanya kazi za kuajiriwa ni 245,500,000 sawa na asilimia 16, mwaka 2004 ni 222,290,000 sawa na asilimia 14.2 na mwaka 2008 ni milioni 215,270,000 sawa na asilimia 13.6”.

Aliongeza kuwa idadi ya watoto ambao walikuwa wanaofanya kazi ambazo si salama kwa maisha yao wenye umri wa kati ya miaka mitano hadi 17 kwa mwaka 2000 ni 170,500,000 sawa na asilimia 11.1, mwaka 2004 walikuwa 128,380,000 sawa na asilimia 8.2 na mwaka 2008 ni 115, 310,000 sawa na asilimia 7.3.
Aliendelea kusema kuwa watoto waliokuwa wameajiariwa kati ya umri wa miaka mitano hadi 14 kwa mwaka 2000 walikuwa 186,300,000, mwaka 2004 walikuwa 170,380,000 na mwaka 2008 walikuwa 152,850,000.

“Kwa mwaka 2000 watoto wa kike waliokuwa wanafanya kazi za kuajiriwa walikuwa asilimia 15.2 na wa kiume asilimia 16.8, mwaka 2004 watoto wa kike walikuwa asilimia 13.5 wa kiume 14.9 na mwaka 2008 watoto wa kike walikuwa asilimia 11.4 na wa kiume asilimia 15.6” .
“Hivi ajira kwa watoto wa kike imepungua kwa asilimia 15 hii ni kutokana na asasi mbalimbali za serikali na zisizo za kiserikali kuwaangalia kwa ukaribu zaidi na kuwasahau watoto wa kiume”, alisema.

Inimu alisema kuwa tatizo kubwa lililopo hivi sasa ni kuongezeka kwa ajira za watoto wa kiume ambapo zimeongezeka kwa asilimia 20 kwa watoto wa kati ya umri wa miaka 15 na 17 ambao wanaajiriwa kwa wingi na wanafanya kazi ambazo ni hatari kwa maisha yao. Aliongeza kuwa ajira za watoto hao kwa mwaka 2000 zilikuwa asilimia 17.8, mwaka 2004 asilimia 14.4 na mwaka 2008 asilimia 16.9.

Asilimia 60 ya watoto walioajiriwa wanafanya kazi za mashambani, asilimia 25.6 kazi za kutoa huduma, asilimia 7 kazi za viwandani na 7.5 wanafanya kazi zisizoeleweka .
Afisa huyo alizitaja sababu za kuongezeka kwa ajira za watoto kuwa ni umaskini unaozikabili familia nyingi jambo ambalo linawafanya wazazi wengi kuwatumia watoto wao kama mtaji wa kujipatia fedha za kukidhi mahitaji yao ya kila siku.

VODACOM KUMLETA TENA KIDUMU NDANI YA BONGO


Maracas kwa kushirikiana na Sophie Entertainment wanakuletea LIVE show ya Kidumu siku ya Ijumaa 25/06/2010 itakayofanyika pale Movenpick Royal Palm Hotel DSM kuanzia saa 2 usiku na kuendelea. Tiketi ni Tsh 15,000 tu.

Show hii kali ya LAST FRIDAY ya mwezi huu wa sita inaletwa kwenu kwa udhamini mkubwa wa Isham Mobile Phones na Vodacom Tanzania.

MAISHA CLUB KAMA KAWA MZAZI



UKUMBI maarufu wa starehe wa Club Maisha unatarajiwa kufunguliwa upya Juni 24 mwaka huu, baada ya kufanyiwa ujenzi mkubwa kutokana na kuungua moto mwaka jana.

Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Entertainment Masters inayomiliki klabu hiyo, Francis Anthony Ciza (Majey), alisema klabu hiyo imefanyiwa ubunifu mkubwa ili kukonga nyoyo kwa kutoa burudani murua na ya uhakika kwa wateja wake.

“Club Maisha inakuja katika mtazamo mpya kwa kutoa burudani za usiku Dar es Salaam iliyopambwa vizuri, sauti ya kutosha na inaipeleka Tanzania mbele katika kutoa burudani za usiku.

“Baada ya miezi kadhaa wateja wetu kukosa burudani, klabu yao sasa inarudi ikiwa ni ya kisasa zaidi yenye televisheni 32 zitakazokuwa zikionesha fainali za Kombe la Dunia na video za muziki, sehemu mbili za kuchezea, vyumba viwili maalumu vya VIP, hii yote ni katika kuuweka kuwa ya kisasa,” alisema Majey.

Vitu vingine vilivyopo katika Club Maisha ni pamoja na sehemu za kuvutia sigara, varanda ya juu, sehemu saba (7) za baa, jiko na TV kubwa inayoonesha fainali za Kombe la Dunia na michezo mingine kwa nje.

Mkurugenzi Mtendaji huyo alisema siku itakayofunguliwa Club Maisha itakolezwa na kusisimuliwa na baadhi ya wachezeshaji muziki (ma-DJ) kutoka Afrika Mashariki na Marekani ambao watapiga nyimbo kali zinazotesa kwa sasa duniani.

“Klabu tayari imekaguliwa na mainjinia kutoka Idara ya Zimamoto pamoja na Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) ili kuhakikisha hakuna ajali ya moto inayoweza kutokea tena, na milango ya dharura imeongezwa ili kuhakikisha usalama mkubwa unakuwepo,” alisema Majey.

“Tumewekeza vya kutosha ili kuirejesha Club Maisha katika nafasi yake ya ubora kwa klabu za usiku Tanzani, tumeweka staili za kisasa kwa lengo la kutoa burudani iliyotakata kwa wapenda burudani za usiku,” alisema.

Viingilio vitabaki kuwa vya kawaida ambavyo ni sh. 10,000 sehemu ya kawaida na sh. 20,000 kwa VIP.Ukumbi wa Club Maisha ulifungwa mwaka jana baada ya kuungua moto.

MWANAHARAKATI SHIGONGO NDANI YA NEW YORK KWENYE KONGAMANO MWEZI UJAO




Mkurugenzi Mtendaji wa Global Publishers & General Enterprises Ltd na mjasiriamali, Bw. Eric Shigongo(pichani), anatarajiwa kuhutubia nchini Marekani katika Mkutano maalum ulioandaliwa na Watanzania waishio nchini humo (Diaspora Council of Tanzanians in America – DICOTA).

Katika mkutano huo unaotarajiwa kufanyika kwa muda wa siku nne kuanzia Julai 1, mwaka huu katika jiji la Minneapolis, Marriott Hotel, Minnesota, Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Mh. Aman Abeid Karume, amealikwa kuwa mgeni rasmi. Viongozi wengine watakaohudhuria mkutano huo ni pamoja na maofisa waandamizi na wafanyabishara wakubwa kutoka Serikali ya Tanzania na Marekani.

Aidha, Mwenyekiti Mtendaji wa makampuni ya IPP, Bw. Reginald Abraham Mengi, naye ni miongoni mwa wageni waalikwa wa mkutano huo ambao unafanyika kwa mara ya pili nchini humo ukiwakutanisha Watanzania waishio ughaibuni. Mada mbalimbali zitatolewa na Watanzania waishio ndani na nje ya Marekani.

Katika mkutano huo, Bw. Shigongo anatarajiwa kutoa mada itakayoelezea jinsi ya kufanikiwa kiuchumi katika mazingira ya Tanzania na anatarajiwa kuwahamasisha Watanzania waishio ughaibuni kuwekeza nyumbani Tanzania.

Katika siku za hivi karibuni, Bw. Shigongo amejipatia umaarufu kwa kutoa elimu, ushauri kwa vijana na wanafunzi wa shule za msingi, sekondari na vyuo vikuu nchini kupitia mikutano na hafla mbalimbali anazoandaa au kualikwa kwa lengo la kutoa elimu ya ujasiriamali kwa vijana wa kitanzania.

Kwa taarifa zaidi juu ya mkutano huo tafadhali tembelea ukurasa wa Diaspora Council of Tanzanians in America-DICOTA)

KYELA KWAANZA KUWAKA MOTO AISEE



Mratibu wa Kitaifa wa Shirika la Kazi Duniani(ILO) Bi. Rhoda Mwamunyange (katikati) akitangaza jana jijini Dar es salaam nia yake ya kugombea Ubunge katika Jimbo la Kyela kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM).

Jimbo la Kyela,mkoani Mbeya, hivi sasa liko chini ya Mheshimiwa Dkt Harrison Mwakyembe. Wengine kushoto ni Mpambe wa Rhoda na kulia ni Ofisa Habari Mwandamizi wa Idara ya Habari Mwirabi Sise.

Jun 22, 2010

SIKIO LA KUFA HALISIKII DAWA SOUTH AFRICA NAO NJE!!!!!!!!

Nikama walikuwa wakikamilisha ratiba baada ya kufangashwa virago rasmi hii leo pamoja na kushinda kwa goli mbila kwa moja dhidi ya ufaransa bado magoli hayo hayakuisaidia bafana bafana kusonga mbele kutokana na kuwa na magoli mengi ya kufungwa tofauti na mexico ambao nao walikubali kichapo cha goli moja kwa bila toka kwa uruguay.

south africa haijatoka kapa kwenye michuano hii ya fifa ya dunia kwani imeambulia kuweka rekodi ya kuwa timu ya kwanza kuandaa mashindano hayo na kutolewa mapema pasipo kugusa round ya pili ya kumi na sita bora.pole sana south africa na waafrica kwa ujumla kwa matokeo hayo na kufanya sa kuwa timu ya tatu kuyaaga mashindano hayo baasa ya cameroon kuwa timu ya kwanza na ivory coast ilisukumwa nje ya michuano hiyo baada ya ureno kutoa kichapo cha mbwa mwizi kwa kuikandamiza dpr korea kwa magoli saba kwa buyu huku south africa ikisukumwa nje ya michuano hiyo baada ya kuwa na uwiano mbaya wa magoli ya kufungwa.

ZANZIBAR NAKO KUMEKUCHA AISEE





WAGOMBEA wanane kutoka chama cha mapinduzi CCM leo wamechukua fomu za kuwania nafasi ya urais wa Zanzibar baada ya rais aliyepo madarakani Amani Abeid Karume kumaliza vipindi vyake viwili vya uongozi kwa mujibu wa katiba.
Takriban wagombea wote wanane wanaotaka kuwania kinyanganyiro hicho wamezungumzia suala la kudumisha amani na kuendeleza maridhiano yaliofikiwa na Rais wa Zanzibar Amani Karume na katibu mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad. iwapo watapata ridhaa ya wananchi ya kuiongoza Zanzibar.
Wagombea waliochukua fomu leo ni Waziri Kiongozi, Shamsi Vuai Nahodha ambaye alichukua fomu saa 3: 00 asubuhi na kuzungumza na waandishi katika Hoteli ya Bwawani. Ali Karume alichukua fomu saa nne asubuhi, Alli Juma Shamhuna alichukua fomu saa tano, Bakari Mshindo saa sita mchana, Dk Billal akachukua saa nane, Dk Shein saa tisa na Mohammed Aboud saa 10 jioni.
Akizungumza katika mkutano wake na waandishi wa habari muda mfupi baada ya kuchukua fomu, Naibu Waziri wa Afrika Mashariki, Mohammed Aboud alisema Zanzibar hivi sasa iko kwenye mazingira mazuri zaidi kuliko nyakati nyingine zozote katika historia yake.
Makamu wa Rais Dk Ali Mohamed Shein aliahidi kuwa atahakikisha Wanzanzibari wanaishi kwa amani na kuendeleza utamaduni wao wa kuvumiliana na kusaidiana.
Akizungumza katika hilo Balozi wa Italia Ali Karume alisema pamoja na kuwa anaunga mkono maridhiano, lakini suala la kura ya kuundwa kwa serikali ya umoja wa kitaifa ya ndio au hapana hawezi kutaja msimamo wake kwa kuwa kura ya maoni itategemea wakati husika.
Waziri Kiongozi Mstaafu Dk Mohammed Gharib Bilal alisema endapo Wazanzibari watampa ridhaa ya kuongoza ataendesha nchi kwa misingi ya utawala wa sheria huku akisisitiza suala la nidhamu katika utawala wake.
Kamishna wa Elimu na Utamaduni, Hamad Bakari Mshindo alisema kwamba Zanzibar inahitaji mabadiliko makubwa katika sekta mbalimbali kwa ajili ya kuleta maendeleo ikiwemo elimu. Habari ya Salma Said na Picha za Martin Kabemba wa Zanzibar

MAMIA WAJITOKEZA KUMDHAMINI JK


Jamani napenda kuwapa updates ya kinachoendelea hivi sasa mjini Dodoma. Mambo ni motomoto sasa hivi, na kwa kweli wana CCM wana kila sababu ya kumdhamini Mh. Jakaya Kikwete.

Zoezi linaloendelea sasa hivi ni kwamba wana CCM wa Mkoa wa Dodoma wanatia saini (kudhamini) kwenye fomu za mgombea wa urais kupitia CCM Ndugu Jakaya Mrisho Kikwete. Vijana wa UVCCM ndio wanaoendelea na shughuli hii.
Awali mgombea Urais Mh. Jakaya Kikwete alipita kuwasalimu wana CCM wenzake na kuwashukuru kwa kitendo chao cha kumdhamini ili kuendelea na awamu ya pili ya urais.

Kabla ya hapo, Mgombea pia alipokea michango kutoka vikundi mbalimbali vya wana CCM kumsaidia katika shughuli nzima ya kuzunguka mikoa yote ya Tanzania kuomba udhamini wa kuendelea na uongozi wa CCM ngazi ya juu kabisa.


RIDHAWAN AKABIDHIWA MIKOBA YA KUMSAKIA DINGI WADHAMINI




Ridhawan akabidhiwa mikoba ya kusaka wadhamini wa JK

*Kikwete asema sababu za kumpa jukumu ni rahisi kumpata

*Awaomba madereva kutokwenda kasi wakati wa kuomba wadhamini

MTOTO wa Rais Jakaya Kikwete , Ridhiwani Kikwete amekabidhiwa mikoba ya kutembeza fomu za kusaka wadhamini katika mikoa 10 nchini akishirikiana na baadhi ya viongozi wa Jumuiya ya Baraza la Kuu la Vijana wa Chama Cha Mapinduzi(UVCCM) na wanafunzi wachache kutoka Vyuo Vikuu nchini.

Kwa mujibu wa chama hicho ni kwamba Ridhiwani ndio atakuwa mwenyekiti wa kamati hiyo akishikiana na Makamu Mwenyekiti wa UVCCM Beno Malisa ambao watawaongoza vijana wngine 32 kuzunguka katika mikoa hiyo ambayo imegwanywa katika kanda nane ikiwemo Kanda A ya Dar es Salaam ambayo kiongozi wake ni ridhiwani pia.

Tukio la Ridhiwani kukabidhiwa fomu za kuomba wadhamini lilifanyika Mjini Dodoma jana mchana, baada ya rais kukamilisha tukio la kuchukua fomu asubuhi ambalo lilifanyika Makao Makuu ya CCM na kasha kufuatiwa na kukutana na wadhamini 250 wa Mkoa wa Dodoma.

Akizungumza mbele ya Rais Kikwete , Katibu Mkuu wa UVCCM, Maltin Shigela alisema vijana hao ambao viongozi wa jumuiya, makada na wanachama makini watazunguka katika maeneo hayo ambpo kila mkoa wanatakiwa kupata wadhimini 250 na hiyo inatokana na kwamba mgombea wao kutokana na majukumu kuwa mengi hivyo hataweza kutafuta wadhimini yeye mwenyewe.

Alisema katika mgawanyo huo wa kanda kila kila itakuwa na vijana wane ambao watashirikiana kuhakikisha wanalifanikisha suala hilo kwa wakati lakini pia kwa umakini mkubwa.Wakiwa huko maeneo ya mikoani watapata ushirikiano mzuri kutoka kwa wanachama.

“Katika kutafua wadhamini, chama kimeamua kutoa jukumu la kufanya kazi hiyo kwa vijana wetu wachama nkutoka jumuiya yetu lakini pia tunao wasomi kutoka vyuo vikuu vyote nchini ambapo walipatikana kwa utaratibu maalumu.Mwanzoni walikuwa 90 lakini tumeamua hao 32 ndio watafanya kazi hiyo,”alisema Shigela.

Kwa mujibu wa taratibu za chama Rais Kikwete aliamua kukabidhi fomu hizo kwa Ridhani ikiwa ndio ishara ya kuanza safari ya kwenda huko mikoani kwa ajili ya kutafuta wadhamini hao.

Rais Kikwete akizungumzia sababu za kuamua kumpa fomu Ridhiwani ili ashirikiane na vijana wenzake, alisema sababu kubwa inatokana na kwamba akimpa Ridhiwani itakuwa rahisi kuwasiliana naye na atakapomuhitaji itakuwa rahisi kumpata tofauti na mtu mwingine.

Alisema kazi ya kuomba wadhamini ni kubwa na inahitaji muda wa kutosha na kwa muda alionao sasa na majukumu yaliyopo mbele yake ndio maana ameamua kuomba vijana hao wasomi kuifanya kazi hiyo ambapo anaamini itafanyikla vizuri kwa sababu vyuo vimefungwa.

JAKAYA AJITOSA RASMI KURUDISHA KITI CHAKE CHA URAISI KUPITIA CCM

Jamani mmeziona?ndivyo alivyo onekana akisema Rais DR. JAKAYA MRISHO KIKWETE muda mfupi baada ya kukabidhiwa fomu za kugombe uraisi kupitia chama chake cha mapinduzi CCM na katibu mkuu wa chama hicho Mh Rashid Makamba huko chimwaga dodoma.
sasa katibu si ufanye fasta kunipa hizo fomu nataka niwahi kuangalia kombe la dunia aisee

Haya sasa mr kashachukua fomu mwendo wa kula bata mwanzo mwisho shosti.

RAIS Jakaya Kikwete jana alianza rasmi mbio za kutetea nafasi yake ya urais na kueleza kuwa vipaumbele vya serikali yake mpya vitasukumwa na misingi kumi, ikiwemo kuongeza kasi ya mapambano ya rushwa na matumizi mabaya ya madaraka.
Akihutubia mamia ya wakazi wa mji wa Dodoma muda mfupi baada ya kuchukua fomu ya kuomba ridhaa ya CCM kugombea urais, Rais Kikwete alisema vita dhidi ya rushwa itaenda sambamba na kuimarisha utawala bora, utawala wa sheria, demokrasia na mapambano ya ubadhirifu wa mali za umma.
“Nitatumia bidii yangu yote kufanya kampeni ya kukipigania chama chetu kipate ushindi mkubwa na mara tutakapofanikiwa, vipaumbele vya serikali ijayo vitasukumwa na misingi kumi ifuatayo,” alisena Rais Kikwete na kuongeza:
“Kuhakikisha kwamba nchi inaendelea kuwa na umoja, amani na usalama, Kujenga msingi wa uchumi wa kisasa wa Taifa linalojitegemea kwa kuchukua hatua madhubuti za kuharakisha zaidi mapinduzi ya kilimo, ufugaji, uvuvi na viwanda”
Alisema vipaumbele vingine ni kuongeza jitihada na mipango zaidi ya kuwawezesha kiuchumi wananchi hasa wa hali ya chini ili wawezze kushiriki na kunufaika na uchumi wwetu unaokua. Lakini vilevile tutaweka mkazo katiak ulitambua na kuliwezesha kwa namba yak kundi la wajasiriamali wa tabaka la kati ili waweze kushiriki katika uwekezaji mkubwa katika nchi yetu.



Jun 20, 2010

YAMETIMIA,IVORYCOAST NAYO YACHEZEA KICHAPO

Huku mamilioni ya waafrika wakiipigia chapuo timu ya taifa ya ivorycoast,hii leo imekubali kichapo cha magoli matatu kwa moja toka kwa miamba wa soka duniani wanao ongoza kwa ubora duniani(brazil),huku wakishuhudia kiungo wake mchezesha timu aliyesaidia kupatikana kwa goli la kwanza(kaka)akisukumizwa nje kwa kadi ya pili ya njano na kumfanya kukosa michezo miwili.
sina shaka matumaini ya waafrika walio wengi yamebakia kwa timu ya taifa ya Ghana ambayo iko kileleni katika kundi lake ambapo itashuka dimbani kukamilisha ratiba na timu ngumu ya ujerumani huku ikihitaji sare ili iweze kusonga mbele kwenye hatua ya 16 bora,kila la kheri ghana.

Jun 19, 2010

SIKU YANGU YA LEO IKO HIVI

mchana wa leo nakwenda kuendeleza libeneke la kugonga albam yangu pale IBAM RECORDS kwa NAS B maeneo flan ya masaki kama vipi usiku nitakuwa kwenye pindi la campass connect kama kawa kuendeleza libeneke la malovedave aisee.jumapili njema wapendwa.

SIKU ZOTE MCHEZA KWAO HUTUNZWA,MO ATEMBELEA CHUO CHA UHASIBU SINGIDA NA KUGAWA MIZAWADI


Pichani Mh.Mohammed Dewji Mbunge wa Singida mjini akiangalia Picha yenye ramani ya Mjengo wa Chuo Cha Taasisi ya Uhasibu Tanzania Tawi la Singida alipotembelea Chuoni hapo week end iliyopita,anayeshuhudia ni Mkuu wa Chuo cha Uhasibu Bw.Emmanuel Kingu alipomkaribisha MO ofisini kwake.

(Katikati) MO akiwa na Viongozi wa Chuo cha Uhasibu akiongozwa na Mkuu wa Chuo Bw.Emmanuel Kingu(wa pili kulia) wakati wa kukagua Majengo ya Chuo hicho(Kushoto) Rais wa Chuo Bw.Evans Crispin(Kulia) Waziri Mkuu wa Chuo Bw.Mbaraka Ismail.

MO akizindua Viti Maalum kwa ajili ya kukalia wanafunzi wakati wa Kujisomea”VIMBWETA”.

VIMBETA hivi vimejengwa na kuzinduliwa Mh.Mohammed Dewji Mbunge wa Singida Mjini.

MO akiwa na Uongozi wa Chuo hicho pamoja na Wanafunzi wakiwa wanaonekana wamekalia viti hivyo(VIMBWETA).

Pichani ni Baadhi ya Wanafunzi wa Chuo cha Uhasibu TIASO wakimsikiliza Mh.Mohammed Dewji Mbunge wa Singida Mjini(hayupo pichani) alipokuwa akiongea na Wanafunzi wa Chuo hicho kuwahimiza kusoma kwa bidii na pia aliwaahidi wanafunzi hao kuwapa Jezi za Michezo seti 5 pamoja na Mipira 20.

MO pia alifanya zoezi la kukabidhi vyeti vya Uongozi kwa wanafunzi wa Chuo hicho,pichani ni zoezi hilo likitendeka.

MO akimkabidhi cheti Waziri wa Wanawake na Maendeleo ya Jamii(TIASO) Mh.Fatuma Hamisi akipokea cheti cha Uongozi bora.

MO akimkabidhi cheti cha Uongozi Bora Rais wa TIASO,Mh.Evans Crispin

MO akishow love na Wanafunzi wa Chuo cha Uhasibu Tawi la Singida alipofanya ziara Chuoni hapo.

Wanafunzi wakifurahia kupiga picha na Mbunge wao MO katikati

Wanafunzi wa Chuo cha TIASO wakifurahia katika picha na Mh.Mohammed Dewji alipotembelea chuoni kwao.

MO Katika Picha ya Pamoja na Uongozi wa Chuo cha TIASO.
(Picha zote kwa msaada wa mo blog)












MZEE KUNA UKWELI KATIKA HILI?



Madai ya msanii nguli wa filamu nchini, Charles Tobias Magali kuwa, mwanamuziki wa Bongo Fleva, Sista Fay ni binti yake wa damu, bado yanawekewa alama nyekundu na baadhi ya wasanii.

Wengi ‘walipokohoa’ chini kwa chini na Jiwe the dj kunyaka nyeti zao wameshauri mzee huyo kwenda kwa Mkemia Mkuu kupima vinasaba vyake na mtoto huyo ili kupata uhakika.

Wameshauri kuwa, itamsaidia mzee huyo kuwa na uhakika kwani dunia ya sasa imechafuka kama si kuharibika.
Hata hivyo, fungu lingine la wasanii wamesema hakuna haja ya kutumika kwa DNA wakati Magali mwenyewe kama mzazi hana wasiwasi wa kubambikwa binti huyo.

KWELI SIKIO LA KUFA HALISIKII DAWA AISEE,CAMEROON ''OUT''


Dalili kwamba mashindano ya mwaka huu ya Kombe la Dunia yanayoendelea huko Afrika Kusini yanaweza kuwa machungu kupita yote kwa bara la Afrika yanaweza kuwa yameanza rasmi kuonekana hivi leo baada ya timu ya Taifa ya Cameroon,maarufu kama Indomitable Lions(Simba wasiofugika) kuwa timu ya kwanza kutolewa katika mashindano hayo.

Cameroon,timu ambayo ilikuwa miongoni mwa timu zilizokuwa zikitajwa kama “tumaini la Afrika”,imeyaaga mashindano hayo baada ya kufungwa jumla ya magoli 2-1 na Denmark.

Kwa maana hiyo kutoka kundi E,Uholanzi imejihakikishia kuendelea na mashindano(Best 16) huku Japan ikisubiri kuumana na Denmark katika mchezo ambao utaamua nani aendelee na nani atoke.Kutoka katika kila kundi timu mbili tu ndizo zinazoendelea.

TIP TOP SASA WAACHIA ''BADO TUNAPANDA''

Baada ya kimya cha muda kirefu, hatimaye kundi la Tip Top Connection limeanza maandalizi ya albamu mpya ambayo imepewa jina la “Bado Tunapanda”
Akiongea na jiwe Kiongozi na Meneja wa kundi hilo, Babu Talle alisema kuwa, albamu hiyo itakuwa na nyimbo nane zitakazoimbwa kwa kushirikisha baadhi ya wasanii nyota wa muziki wa kizazi kipya nchini.

Talle alisema karibu nyimbo zote za albamu hiyo zimekamilika na baadhi kuanza kurushwa hewani kwa nia ya kuitambulisha.
“Tumeamua kuachia albamu ya kundi letu la Tip Top Connection iitwayo ‘Bado Tunapanda,’ ni baada ya kuhakikisha karibu kila msanii mwanachama ametoa kazi yake binafsi nje ya kundi” alisema Talle.
Talle aliongeza kuwa, wimbo unaobeba albamu hiyo, tayari umeshaanza kurushwa hewani na unatarajiwa kutambulishwa rasmi kwa wapenzi na mashabiki wao na kuwataka wakae tayari kuupokea ujio wao mpya na albam kali

VIPI MZAZI MUZIKI HAULIPI AMA NDO MULT TALENT MH?


Msimsake saana yule mwanamuziki Mr Blue kwani kwa sasa amegeukia tasnia hii ya filamu inayokuja kwa kasi saana nchini

Mr Blue ameanza kutupa jiwe lake la kwanza kwa kuigiza filamu ya Pretty Teacher ambayo ameshirikiana na waigizaji wakongwe kama Lucy Komba, Mzee Chilo na Idriss

Tasnia hii ya uigizaji kwa sasa inaokoteza macelebrity woote wa tasnia mbali mbali nchini, bila kuangalia kipaji nadhan itaishia kuwa ni kwa wauza sura zaidi.

THE DON HIMSELF

Karibuni sana kwenye blog hii ya kijamii iliyosheheni makila kitu kuanzia siasa uchumi afya na burudani kwa ujumla wake.uingiapo kwenye blog hii ni mengi ambayo utapata nafasi ya kukutana nayo,kumbuka mawazo yako ndo hasa yanayojenga na kunifanya niwe na ufanisi zaidi.kariiiiiiibuuuuuuuuuuuu saaaaaaaaaaaaaaanaaaaaaaaaa.(THE DJ HIMSELF-JIWE)

Followers

BLOG ZA MARAFIKI

Search This Blog

ZILIZOPITA

DUNIA MUZIMA