
Madai ya msanii nguli wa filamu nchini, Charles Tobias Magali kuwa, mwanamuziki wa Bongo Fleva, Sista Fay ni binti yake wa damu, bado yanawekewa alama nyekundu na baadhi ya wasanii.
Wengi ‘walipokohoa’ chini kwa chini na Jiwe the dj kunyaka nyeti zao wameshauri mzee huyo kwenda kwa Mkemia Mkuu kupima vinasaba vyake na mtoto huyo ili kupata uhakika.
Wameshauri kuwa, itamsaidia mzee huyo kuwa na uhakika kwani dunia ya sasa imechafuka kama si kuharibika.
Hata hivyo, fungu lingine la wasanii wamesema hakuna haja ya kutumika kwa DNA wakati Magali mwenyewe kama mzazi hana wasiwasi wa kubambikwa binti huyo.

No comments:
Post a Comment