Siku mbili baada ya kifo cha
mwandishi mwenzao wa habari (Daudi Mwangosi) aliefariki kutokana na
kulipukiwa na bomu akiwa mikononi mwa polisi waliokuwa wanatawanya
wafuasi wa Chadema huko Iringa, mwandishi wa habari Francis Godwin ambae
alikua rafiki wa marehemu amejisalimisha polisi kufata masharti ya
taarifa iliyotolewa kwa yeye na wenzake wawili kusakwa na polisi.
Exclusive na millardayo.com
namkariri Godwin akisema “kutokana na hali halisi ya kushuhudia tukio la
mauaji ya Mwangosi, nilifukuziwa kwa nyuma na gari lisilokua na namba
pia nilipofika nyumbani niliambiwa kuna watu walikuja kuniulizia lakini
hawafahamiki, na taarifa zikatoka kwamba tunasakwa”
Kuhusu kujisalimisha, Godwin
amesema aliamua kufanya huo uamuzi baada ya kusikia taarifa za kusakwa
kwake pamoja na waandishi wengine wawili, jana (september 5) aliamua
kujisalimisha mwenyewe Polisi akiwa amesindikizwa na waandishi wa habari
kama hamsini ambapo baada ya kufika pale walikutana na kamishna wa
makosa ya jinai Tanzania Robert Manumba ambae ilibidi ahoji polisi
Iringa kama ni kweli wanamtafuta Godwin na wenzake.
Namkariri Godwin akisema “baada
ya kumuuliza mmoja kati ya maofisa wake kama ni kweli wanamtafuta
Godwin ofisa huyo alijiumauma na baadae akasema hatumtafuti, baada ya
hapo waandishi wa habari tulisimama tukaondoka kwa sababu ya
kutokubaliana na kilichotaka kuendelea kuhusu taarifa ya uchunguzi ya
Manumba”
Kingine kilichoendelea baada ya
hapo ni Club ya waandishi wa habari Iringa kuziomba redio mbalimbali za
iringa ambazo zimekua zikirusha matangazo ya polisi jamii kusimamisha
matangazo hayo ambapo wamiliki wa vyombo hivyo wamekubali ombi.
Francis Godwin ambae alikua
karibu na marehemu Daudi Mwangosi muda mfupi kabla ya kuuwawa kwa bomu
amesema “Nilijua kwamba mimi ni miongoni mwa waandishi watatu
wanaotafutwa kwa sababu marehemu kabla ya kifo akiwa amekamatwa nilitaka
kwenda kumuokoa pale lakini nilipokua namsogelea Daudi akaniambia
Godwin mdogo wangu kimbia… wakati nakimbia kama hatua 20 mbele nyuma
nageuka nasikia mlipuko mkubwa, kuangalia ni Wangosi amekufa na
nilibahatika kupiga baadhi ya picha ambapo askari waliokuwepo walipoona
narudi kwenye eneo hilo walinionyeshea bunduki ikabidi ninyooshe mikono
juu kwamba jamani mimi nakuja kwa heri wakaniambia potea”
Godwin amesema baada ya kugeuka
na kuanza kukimbia walianza kumfukuzia ila bahati nzuri gari yake
ilikua mbali, baada ya kutishwa na polisi walipokwenda hospitali
ulipopelekwa mwili wa marehemu ilibidi waanze kutoa mabango ya
wanahabari yaliyobandikwa kwenye gari yao pamoja na kutoa namba za gari,
alianza safari ya kuondoka lakini kuna gari zilikua zinamfukuzia kwa
nyuma mpaka alipofika nje kidogo ya mji wa Iringa na kuingia mitaani
ndio akafanikiwa kukimbia.
Kwenye sentensi ya mwisho
Godwin anasema ameibiwa siri na askari mmoja ambae alimwambia kuhusu
kutafutwa kwake yeye na waandishi wa habari awengine mbapo alimuonya
kwamba msimamo na kauli aliokua ameutoa pamoja na ushahidi wa tukio la
mauaji ndio vimefanya atafutwe.
Ni globu ya kijamii inayojihusisha na mambo yote ya kijamii,natumaini jamii yangu ya kitanzania itafaidika sana pindi ichukuapo fursa ya kuperuzi kwenye globu hii,dhamira yangu ni kufikisha ujumbe pamoja na kuiburudisha jamii yangu na furaha yangu ni kuona natimiza dhamira yangu kwako.natumaini kuwa wewe utaniunga mkono kwa kile ambacho nataka kukifanya kwa ajili ya jamii yangu ya kitanzania.NASHUKURU KWA KUNIELEWA.
Sep 6, 2012
ALICHOSEMA PRODUCER MANECK BAADA YA KUONA DOGO JANJA ANATAKA KUMGOMBANISHA NA MARCO CHALI.
Producer Maneck ambae ni
mshindi wa tuzo kwenye KTMA 2012 ameamua kuzungumza ya moyoni kwa
kuijibu kauli Dogo Janja aliyoitoa kwamba Producer huyo kauponda uwezo
wa Marco Chali.
Ishu ilianza wakiwa club Maisha Dar es salaam jumapili iliyopita ambapo Dogo Janja anadai alikwenda sehemu ya V.I.P na kumsalimia Maneck ambae hakujibu salamu ila aliporomosha matusi mazito kwa Dogo Janja pamoja na kumpiga biti kwamba asimsogelee.
Baada ya hapo Dogo Janja akashuka chini kwenda kumwita meneja wake wa WATANASHATI ambae ni Ustaz Juma ambapo kwa maelezo ya Dogo Janja, Maneck alianza kuiponda single mpya ya Dogo Janja na PNC waliyoirekodi kwa Marco Chali ambayo mwanzoni ilikua irekodiwe kwa Maneck alieiponda kwa kusema ni ya kawaida sana kwa sababu imefanywa na Marco Chali.
Jibu alilolitoa Maneck baada ya kusikia kwamba Dogo Janja amenukuliwa kwa hayo maneno, namkariri akisema “ndio ninavyokwambia sitakagi watu masnich kama huyo, Marco Chali ni mtu ambae namfil sana anafanya kazi nzuri, siwezi kuongea kitu kibaya kwa Marco kwa sababu leo na kesho nitamfata nitamuomba msaada wa kitu chochote kile hata material sasa nitawezaji kusema hivyo kwa mfano sasa, Dogo Janja ni mtu ambae anataka tu kufanyaga vitu watu wapishane kauli mambo ya kijinga ni utoto akikua nadhani ataacha hizo tabia zake, na ndio maana nikamwambia kaa mbali sitaki uongee na mimi that’s all”(kwa hisani ya www.millardayo.com)
Ishu ilianza wakiwa club Maisha Dar es salaam jumapili iliyopita ambapo Dogo Janja anadai alikwenda sehemu ya V.I.P na kumsalimia Maneck ambae hakujibu salamu ila aliporomosha matusi mazito kwa Dogo Janja pamoja na kumpiga biti kwamba asimsogelee.
Baada ya hapo Dogo Janja akashuka chini kwenda kumwita meneja wake wa WATANASHATI ambae ni Ustaz Juma ambapo kwa maelezo ya Dogo Janja, Maneck alianza kuiponda single mpya ya Dogo Janja na PNC waliyoirekodi kwa Marco Chali ambayo mwanzoni ilikua irekodiwe kwa Maneck alieiponda kwa kusema ni ya kawaida sana kwa sababu imefanywa na Marco Chali.
Jibu alilolitoa Maneck baada ya kusikia kwamba Dogo Janja amenukuliwa kwa hayo maneno, namkariri akisema “ndio ninavyokwambia sitakagi watu masnich kama huyo, Marco Chali ni mtu ambae namfil sana anafanya kazi nzuri, siwezi kuongea kitu kibaya kwa Marco kwa sababu leo na kesho nitamfata nitamuomba msaada wa kitu chochote kile hata material sasa nitawezaji kusema hivyo kwa mfano sasa, Dogo Janja ni mtu ambae anataka tu kufanyaga vitu watu wapishane kauli mambo ya kijinga ni utoto akikua nadhani ataacha hizo tabia zake, na ndio maana nikamwambia kaa mbali sitaki uongee na mimi that’s all”(kwa hisani ya www.millardayo.com)
MBWANA SAMATTA - THE KING IN THE MAKING
Hili ni moja ya bango la kumsifia Mbwana Samatta lilochorwa na washabiki wa Mazembe |
Huyu ni shabiki wa Mazembe akiwa na jezi yenye jina la Samatta |
Kama Spain -vile ni vigari maalum kubebea wachezaji wanaoumia uwanjani katika uwanja wa TP Mazembe |
Mbwana Samatta mwenye jezi namba 15 akiwa anapigwa konga na beki wa Al Ahly |
Huyu ndio mshabiki aliyevaa jezi yenye jina la Samatta |
Mfalme wa Mazembe Tresor Mputu akiwafanyia balaa waarabu |
Kidiyaba ndani ya uzi wake wa golikipa |
MATUMIZI MABAYA YA FEDHA YANAVYOTISHIA KUMFILISI MWANASOKA NEYMAR
Hakuna ubishi juu ya kipaji alichonacho mwanasoka wa kibrazil Neymar .
Neymar kwa sasa sio tu mwanasoka anayependwa sana kuliko wote nchini Brazil, bali pia ni tumaini kubwa la kuiwezesha nchi hiyo kutwaa kombe la dunia mwaka 2014, ambalo litafanyika katika taifa hilo la bara la Amerika ya kusini.
Ameelezewa na Pele, ambaye anatajwa kama mwanasoka bora kabisa kuwahi kutokea katika historia ya mchezo huo - kuwa na mtaalam wa soka, mwenye miguu ya majaabu, huku akiwa na umri wa miaka 20. Lakini kipaji cha Neymar uwanjani ni tofauti kabisa na akili yake linapokuja suala la matumizi ya fedha. Anatengeneza fedha nyingi sana lakini anatumia karibu na chote anachoingiza.
Gari aina ya Porsche Panamer |
Yatch ya Neymar |
Neymar na mwanae ambaye anamgharimu zaidi ya $15,000 kwa mwezi kumlea. |
"Kiukweli anatumia fedha nyingi sana karibu na kile chote anachoingiza," anasema mtaalam wa mambo ya fedha wa jarida la Forbes bwana Settimi huku akisisitiza lazima klabu yake itakuwa inamsaidia kwa kumpa fedha nyingine nje ya mkataba wake.
"Inawezekana Santos wana mkono wao kwa sababu ukiangalia matumizi yake ndani ya kipindi cha miaka miwili iliyopita unaona kwamba ametumia zaidi ya kile alichoingiza - kuna taarifa zinasema klabu yake inampa fedha nyingi hata nje ya mkataba ili kumridhisha na kumfanya asahau kwenda barani ulaya."
Mhariri mkuu wa jarida la Forbes Kurt Badenhausen anamfananisha Neymar na Mike Tyson: " neymar ndio kwanza anakuwa na anatengeneza fedha nzuri sana. Kama ilivyokuwa kwa Tyson ambaye nae alianza kutengeneza fedha akiwa na miaka 18 na miaka kadhaa baadae alikuwa na utajiri wa $400 million - hivi ndivyo nahisi Neymar akavyokuwa ikiwa itaacha kutumia vibaya fedha zake."
Mike Tyson akiwa kwenye kiwango cha juu, pambano lake moja alikuwa akitia ndani kiasi cha $30 million. Lakini wakati wa kipindi hicho, Tyson alinunua mahekalu, magari ya kifahari, chui wa kufuga. Mwishoni mwa mwaka 2002, aliingia kwenye duka la kuuza vito na kununua cheni ya dhahabu yenye thamani ya $174,000 huku ikiwa imenakishiwa na almasi kiasi. Miezi nane baadae Tyson akatangaza kufulisika huku akiwa na madeni yanayofikia $23 million.
Watu wengine maarufu ni kama vile star wa NBA Antoine Walker, ambaye alitengeneza zaidi ya $110 million wakati akicheza bado, na Evander Holyfield, wote wamefilisika.
Mfano mwingine mzuri haupo mbali na yeye. Nchini Brazil mwanasoka Romario, ambaye alikuwa mchezaji muhimu sana kwa Brazil katika fainali za kombe la dunia 1994, alikamatwa mwaka 2009 kwa kesi ya kushindwa kutoa fedha ya malezi ya mtoto. Huku akiwa na deni linalofikia $5 million.
Neymar anatakiwa kufuata mfano wa gwiji wa soka wa nchi hiyo Ronaldo De Lima ambaye aliwekeza fedha zake vizuri. Ronaldo sasa hivi anamiliki asilimia 45 za kampuni ya 9ine Sports and Entertainment Agency, kampuni inayodili na masuala ya soka, ambapo moja ya wateja wao ni Neymar.
Shukrani kwa 9ine inayofanya vizuri sana kwenye biashara zake, Ronaldo de lima sasa ana thamani ya utajiri unaofikia $250 million. Kwa maana hiyo Neymar itabidi afuate nyayo za huyu jamaa ili aweze kuwa na mafanikio miaka kadhaa ijayo, na sio kufuata nyayo za Romario na akina Tyson.
SIMBA NA YANGA WAKABIDHIWA VIFAA VYA MILLIONI 68 NA KILIMANJARO KWA AJILI YA MSIMU MPYA
Ofisa
Habari wa Yanga, Louis Sendeu (kushoto) na Makamu Mwenyekiti wa Simba,
Geofrey Nyange ‘Kaburu’ (kulia), wakionesha baadhi ya vifaa vya michezo
walivyokabidhiwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), ambao ndio wadhamini
wakuu wa klabu hizo. Wa pili kushoto ni Meneja wa Bia ya Kilimanjaro,
George Kavishe na Mkurugenzi wa Mashindano, Saad Kawemba. Hafla hiyo
ilifanyika katika ofisi za Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), jijini Dar
es SalaamMeneja wa Bia ya Kilimanjaro, George Kavishe
Makamu Mwenyekiti wa Simba, Geofrey Nyange ‘Kaburu’ akizungumza katika hafla hiyo.
Meneja wa Bia ya Kilimanjaro, George Kavishe (kushoto) akimkabidhi baadhi ya vifaa vya michezo Makamu Mwenyekiti wa Simba, Geofrey Nyange ‘Kaburu’ na katikati ni Mkurugenzi wa Mashindano wa TFF, Saad Kawemba.
Ofisa
Habari wa Yanga, Louis Sendeu (kushoto) akipokea vifaa vya michezo
kutoka kwa Meneja wa Bia ya Kilimanjaro, George Kavishe.
Meneja wa Bia ya Kilimanjaro, George Kavishe
Na Clezencia Tryphone
KLABU
kongwe nchini za Simba na Yanga, zimekabidhiwa vifaa mbalimbali vyenye
thamani ya sh milioni 34 kila moja kutoka kwa mdhamini wao mkuu, Kampuni
ya Bia Tanzania (TBL), kupitia bia yake ya Kilimanjaro Premium Lager.
Akikabidhi
vifaa hivyo katika Ofisi za Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), jijini
Dar es Salaam, Meneja wa Bia ya Kilimanjaro, George Kavishe, alisema,
kukabidhi vifaa hivyo ni moja ya sehemu katika mkataba baina yao na
klabu hizo.
Kavishe
alisema lengo kubwa la kudhamini timu hizo ni kutokana na historia
kubwa ya klabu hizo, pamoja na kuleta ushindani wenye burudani kwa
Watanzania, ambao ni wadau wakubwa wa kunywa kinywaji hicho.
“Sisi
tunafanya kazi vema na klabu hizi, tunajisikia faraja kubwa kutokana na
timu hizi kuwa na historia kubwa hapa nchini na ushindani mkubwa katika
soka na huu ni udhamini wa nusu msimu peke yake,” alisema Kavishe.
Alivitaja vifaa hivyo walivyotolewa kuwa ni jezi, bukta, soksi, viatu, bips, nguo za kusafiria, vikinga ugoko na mifuko.
Katika
hatua nyingine, Kavishe alisema, kuhusu mabasi ya timu hizo, wako
katika hatua za mwisho kuyakabidhi kwa wahusika, kwani tayari yamewasili
hapa nchini, ambapo kuna mambo kadhaa wanayakamilisha.
Akizungumza
kwa niaba ya klabu ya Simba, Makamu Mwenyekiti, Geofrey Nyange
‘Kaburu’, aliwashukuru wadhamini hao kwa moyo walionao, huku akiwaahidi
kuhakikisha wanafanya vema na kushinda ili kuonesha umuhimu wa vifaa
ambavyo wamewapa.
“Nawashukuru
TBL kwa kutudhamini na kuona umuhimu kwa sisi Simba bila ya kupepesa
macho na ndiyo maana hata sisi tutapigana kufa na kupona ili kuhakikisha
tunavitendea haki vifaa hivi,” alisema Kaburu.
Kwa
upande wa Yanga, Ofisa Habari wake, Louis Sendeu, naye aliishukuru TBL,
huku akiwaomba kutoishia kwa Simba na Yanga, bali waziangalie na timu
nyingine.
“Tunawashukuru sana ila msiishie kwa Yanga na Simba tu, mziangalie na klabu nyingine ambazo zinasuasua,” alisema Sendeu.
Source: http://francisdande.blogspot.com
Subscribe to:
Posts (Atom)
ME MYSELF & I
THE DON HIMSELF
Karibuni sana kwenye blog hii ya kijamii iliyosheheni makila kitu kuanzia siasa uchumi afya na burudani kwa ujumla wake.uingiapo kwenye blog hii ni mengi ambayo utapata nafasi ya kukutana nayo,kumbuka mawazo yako ndo hasa yanayojenga na kunifanya niwe na ufanisi zaidi.kariiiiiiibuuuuuuuuuuuu saaaaaaaaaaaaaaanaaaaaaaaaa.(THE DJ HIMSELF-JIWE)