Siku mbili baada ya kifo cha
mwandishi mwenzao wa habari (Daudi Mwangosi) aliefariki kutokana na
kulipukiwa na bomu akiwa mikononi mwa polisi waliokuwa wanatawanya
wafuasi wa Chadema huko Iringa, mwandishi wa habari Francis Godwin ambae
alikua rafiki wa marehemu amejisalimisha polisi kufata masharti ya
taarifa iliyotolewa kwa yeye na wenzake wawili kusakwa na polisi.
Exclusive na millardayo.com
namkariri Godwin akisema “kutokana na hali halisi ya kushuhudia tukio la
mauaji ya Mwangosi, nilifukuziwa kwa nyuma na gari lisilokua na namba
pia nilipofika nyumbani niliambiwa kuna watu walikuja kuniulizia lakini
hawafahamiki, na taarifa zikatoka kwamba tunasakwa”
Kuhusu kujisalimisha, Godwin
amesema aliamua kufanya huo uamuzi baada ya kusikia taarifa za kusakwa
kwake pamoja na waandishi wengine wawili, jana (september 5) aliamua
kujisalimisha mwenyewe Polisi akiwa amesindikizwa na waandishi wa habari
kama hamsini ambapo baada ya kufika pale walikutana na kamishna wa
makosa ya jinai Tanzania Robert Manumba ambae ilibidi ahoji polisi
Iringa kama ni kweli wanamtafuta Godwin na wenzake.
Namkariri Godwin akisema “baada
ya kumuuliza mmoja kati ya maofisa wake kama ni kweli wanamtafuta
Godwin ofisa huyo alijiumauma na baadae akasema hatumtafuti, baada ya
hapo waandishi wa habari tulisimama tukaondoka kwa sababu ya
kutokubaliana na kilichotaka kuendelea kuhusu taarifa ya uchunguzi ya
Manumba”
Kingine kilichoendelea baada ya
hapo ni Club ya waandishi wa habari Iringa kuziomba redio mbalimbali za
iringa ambazo zimekua zikirusha matangazo ya polisi jamii kusimamisha
matangazo hayo ambapo wamiliki wa vyombo hivyo wamekubali ombi.
Francis Godwin ambae alikua
karibu na marehemu Daudi Mwangosi muda mfupi kabla ya kuuwawa kwa bomu
amesema “Nilijua kwamba mimi ni miongoni mwa waandishi watatu
wanaotafutwa kwa sababu marehemu kabla ya kifo akiwa amekamatwa nilitaka
kwenda kumuokoa pale lakini nilipokua namsogelea Daudi akaniambia
Godwin mdogo wangu kimbia… wakati nakimbia kama hatua 20 mbele nyuma
nageuka nasikia mlipuko mkubwa, kuangalia ni Wangosi amekufa na
nilibahatika kupiga baadhi ya picha ambapo askari waliokuwepo walipoona
narudi kwenye eneo hilo walinionyeshea bunduki ikabidi ninyooshe mikono
juu kwamba jamani mimi nakuja kwa heri wakaniambia potea”
Godwin amesema baada ya kugeuka
na kuanza kukimbia walianza kumfukuzia ila bahati nzuri gari yake
ilikua mbali, baada ya kutishwa na polisi walipokwenda hospitali
ulipopelekwa mwili wa marehemu ilibidi waanze kutoa mabango ya
wanahabari yaliyobandikwa kwenye gari yao pamoja na kutoa namba za gari,
alianza safari ya kuondoka lakini kuna gari zilikua zinamfukuzia kwa
nyuma mpaka alipofika nje kidogo ya mji wa Iringa na kuingia mitaani
ndio akafanikiwa kukimbia.
Kwenye sentensi ya mwisho
Godwin anasema ameibiwa siri na askari mmoja ambae alimwambia kuhusu
kutafutwa kwake yeye na waandishi wa habari awengine mbapo alimuonya
kwamba msimamo na kauli aliokua ameutoa pamoja na ushahidi wa tukio la
mauaji ndio vimefanya atafutwe.
Ni globu ya kijamii inayojihusisha na mambo yote ya kijamii,natumaini jamii yangu ya kitanzania itafaidika sana pindi ichukuapo fursa ya kuperuzi kwenye globu hii,dhamira yangu ni kufikisha ujumbe pamoja na kuiburudisha jamii yangu na furaha yangu ni kuona natimiza dhamira yangu kwako.natumaini kuwa wewe utaniunga mkono kwa kile ambacho nataka kukifanya kwa ajili ya jamii yangu ya kitanzania.NASHUKURU KWA KUNIELEWA.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
ME MYSELF & I
THE DON HIMSELF
Karibuni sana kwenye blog hii ya kijamii iliyosheheni makila kitu kuanzia siasa uchumi afya na burudani kwa ujumla wake.uingiapo kwenye blog hii ni mengi ambayo utapata nafasi ya kukutana nayo,kumbuka mawazo yako ndo hasa yanayojenga na kunifanya niwe na ufanisi zaidi.kariiiiiiibuuuuuuuuuuuu saaaaaaaaaaaaaaanaaaaaaaaaa.(THE DJ HIMSELF-JIWE)
No comments:
Post a Comment