|
Wanafunzi hao wanalazimika kupanga kwenye hosteli na nyumba zilizo nje ya chuo hicho kikongwe kutokana na tatizo kubwa la upungufu wa malazi. Hata wale wanaolala chuoni hapo, hulazimika kujazana wengi kwenye chumba kimoja tofauti na zamani wakati chumba kimoja kilikuwa kikitumiwa na wanafunzi wawili tu. Kutokana na upungufu huo, wanafunzi hutumia muda mwingi kwenye safari za kati ya chuoni na maeneo wanayoishi. Hali hiyo ndio iliwasukumu waamue kumfikishia ujumbe mtendaji huyo mkuu wa serikali jana kwenye Ukumbi wa Nkurumah wakati Pinda alipokuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa maadhimisho ya miaka 50 ya UDSM ambayo yamepangwa kufanyika Oktoba mwakani. Iwapo Pinda atamaliza miaka mitano ya uongozi akiwa Waziri Mkuu atakuwa amechangia jumla ya Sh50 milioni katika jitihada za kukiwezesha chuo hicho kikongwe nchini kutatua tatizo la malazi kwa wanafunzi. Katika tukio hilo la kwanza la aina yake kumkuta Pinda tangu alipoteuliwa tena kuwa waziri mkuu na kuapishwa wiki iliyopita, wanafunzi waliokuwa wameketi kwa utulivu sehemu ya juu ya Ukumbi wa Nkrumah walibandika bango hilo lililokuwa na maandishi hayo makubwa. Pinda pamoja na baadhi viongozi waliokuwa meza kuu, walionekana kulisoma bango hilo lililoonyesha kilio cha wanafunzi hao kukosa maeneo ya kulala eneo la chuo na kulazimika kuishi nje ya chuo ambapo gharama za maisha ni kubwa. Alipoanza kutoa hotuba yake, Pinda alianza kwa kulizungumzia bango hilo huku akieleza kuwa ujumbe walioukusudia wanafunzi hao umefika. “Nilipokuwa nimeketi (Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard) Membe aliniandikia ujumbe kwenye karatasi akaniambia 'umeona massage (ujumbe) yako?', nikamwambia 'niliiona toka zamani,'” alisema. “(Makamu mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Profesa Rwekaza) Mukandala naye akaniambia akihoji: 'Hawa wanafunzi sijui walipenya vipi na hili bango'. "Nikamwambia 'itakuwa wametumia kaujanja kadogo tu kwa kulikunja likawa kama madaftari, kwa hiyo mtu akabeba kama kitabu anachoenda kujisomea', lakini pamoja na mwandiko na bango lao baya baya, nasema massage imefika.” Kutoka na hali hiyo, Pinda alitoa ahadi ya kuchangia Sh10 milioni kila mwaka mpaka pale muda wa uongozi wake utakapomalizika. Hata hivyo, baada ya kutoa ahadi hiyo Pinda alimtaka Membe naye kutoa ahadi yake na waziri huyo wa mambo ya nje akaahidi kutoa Sh5 milioni kila mwaka mpaka pale muda wa uongozi wa Pinda utakapomalizika. “Natumaini utanikubalia ili na mimi niende nikawabane mawaziri, manaibu, makatibu wakuu na mabalozi wote waliosoma hapa ili nao watoe michango yao na ikiwezekana kiwango kiwe ni hiki hiki (Sh5 milioni kila mwaka),” alisema Membe. Baada ya kauli hiyo ya Membe, Waziri Mkuu Pinda aliahidi kuwabana mawaziri na manaibu wote ili kuweza kuchangia chuo hicho. “Desemba saba nitakutana nao, nitawabana mpaka watoe michango yao... nyie wakuu wa wilaya na mikoa zamu yenu inakuja,” alisema Pinda. Hata hivyo, alimtaka Profesa Mukandala kuweka mpango madhubuti wa kutafuta watu mbalimbali waliosoma kwenye chuo hicho ili watoe michango ya kumaliza matatizo yanayokikabili chuo hicho. chanzo - mwananchi |
Ni globu ya kijamii inayojihusisha na mambo yote ya kijamii,natumaini jamii yangu ya kitanzania itafaidika sana pindi ichukuapo fursa ya kuperuzi kwenye globu hii,dhamira yangu ni kufikisha ujumbe pamoja na kuiburudisha jamii yangu na furaha yangu ni kuona natimiza dhamira yangu kwako.natumaini kuwa wewe utaniunga mkono kwa kile ambacho nataka kukifanya kwa ajili ya jamii yangu ya kitanzania.NASHUKURU KWA KUNIELEWA.
Nov 26, 2010
Pinda apokewa kwa bango UDSM
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
ME MYSELF & I
THE DON HIMSELF
Karibuni sana kwenye blog hii ya kijamii iliyosheheni makila kitu kuanzia siasa uchumi afya na burudani kwa ujumla wake.uingiapo kwenye blog hii ni mengi ambayo utapata nafasi ya kukutana nayo,kumbuka mawazo yako ndo hasa yanayojenga na kunifanya niwe na ufanisi zaidi.kariiiiiiibuuuuuuuuuuuu saaaaaaaaaaaaaaanaaaaaaaaaa.(THE DJ HIMSELF-JIWE)
No comments:
Post a Comment