Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akiwashukuru jana jijini Dar es salaam, wanachama wa CCM waliojitokeza kumpongeza kwa hatua ya kurejesha fomu katika Ofisi za Tume ya Uchaguzi na pia kukubaliwa kama Mgombea halali wa CCM katika uchaguzi ujao. Picha na Tiganya Vincent-Dar es salaam
Mgombea Mwenza wa Rais Jakaya Mrisho Kikwete Dkt Mohamed Gharib Bilal akiwashukuru wanachama wa CCM na wapenzi waliofika jana katika viwanja vya Ofisi Ndogo ya CCM jijini Dar es salaam kwa ajili ya kuwapongeza kwa kukubaliwa bila na Tume ya Uchaguzi ya Tanzania kuwa wagombea kwa tiketi ya CCM katika uchaguzi ujao.
Katibu Mkuu wa CCM Yusuph Makamba (kushoto) akiteta na Mwenyekiti wa CCM Dkt Jakaya Kikwete jana nje ya Ofisi Ndogo za CCM jijini Dar es salaam mara baada kurejea kutoka Tume ya Uchaguzi alipokuwa amerudisha Fomu ya kuwania Urais wa Tanzania katika uchaguzi Mkuu ujao.
Msaani Ummy Wenceslaus (Dokii) akitumbuiza jana jijini Dar es salaam baadhi ya wanachama waliofika katika Ofisi Ndogo za CCM kuwalaki wagombea wao mara baada ya Rais Kikwete na Mgombea Mweza Dkt Bilal kurejea kutoka Tume ya Uchaguzi ambapo alikuwa amerudisha fomu kuwania Urais wa Tanzania katika uchaguzi Mkuu ujao.
Wanachama wa Chama Cha Mapinduzi wakiwasikiliza wagombea wao wakati walipokuwa wakihutubia maelfu wa wanachama wao katika ofisi ndogo ya chama CCM Lumumba.
Wagombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha CHADEMA Dr. Wilbroad Slaa kushoto na Mgombea Mwenza Khamis Hamad Khamis mara baada ya kurejesha fomu zao katika ofisi za tume hiyo leo jijini Dar es salaam. Tume ya Taifa ya Uchaguzi ilipanga kuwa Wagombea wote wanatakiwa kuwa wamerudisha fomu leo Agost 19 na kesho Agosti 20 ndiyo kampeni zinaanza rasmi kwa vyama vyote ambapo uchaguzi mkuu unatarajiwa kufanyika Oktoba 31 mwaka huu.
Wanachama wa Chama CHADEMA wakishangilia nje ya ofisi za Tume ya Uchaguzi ya Taifa wakati walipomsindikiza wagombea wa urais kupitia chama hicho wakati waliporejesha fomu katika Tume hiyo leo jijini Dar es salaam.
Mwenyekiti wa NCCR Mageuzi James Mbatia akiwa katika msafara nawanachama wa chama hicho katika maeneo ya Moroco Konondoni jijini Dar es salaam mara baada ya kurejesha fomu ya kugombea ubunge jimbo la Kawe leo.
Wanachama wa chama cha NCCR Mageuzi wakiwa katika msafara katika maeneo ya Moroco Kinondoni mara baada ya mgombea wao wa ubunge jimbo la kawe kurejesha fomu za kugombea ubunge kawe leo.
Wagombea Urais kupitia Chama Cha Wananchi CUF Prof. Ibrahim Lipumba kushoto na Mgombea mwenza Duni Haji Duni wakipunga mikono yao mara baada ya kurejesha fomu zao katika Ofisi za Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jijini Dar es salaam leo ambapo wagombea kutoka vyama vyote vyote wanatarajia kuanza kampeni kesho nchini kote.
No comments:
Post a Comment