Jul 30, 2012

WANAKIJIJI WENZANGU NA MCHAKATO WA KATIBA MPYA


Mwenyekiti wa Mtaa wa Mjini, Kata ya Kishapu Mjini, Wilaya ya Kishapu, Bw. Tido Nuhu akiwakaribisha wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba katika mkutano wa kukusanya maoni ya wananchi kuhusu katiba mpya uliofanyika Kijijini hapo.

Bi Faida Faki Kombowa Shehia ya Makombeni, Wilaya ya Makombeni, Wilaya ya Mkoani, Mkoa wa Kusini Pemba akitoa maoni yake kuhusu Katiba Mpya.


Bi Siwema Shaaban Mbato, mkazi wa Kijiji cha Bwilingu, Tarafa ya Msoga, Wilayani Bagamoyo, Mkoa wa Pwani akifunguka juu ya Katiba mpya.
Akina mama wakazi wa Kijiji cha Bwilingu tarafa ya Msoga Wilayani Bagamoyo mkoa wa Pwani wakijisomea vitabu vinavyohusu Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania vilivyogawiwa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba.

Bi Aziza Juma, Mkazi wa Wilaya ya Kishapu, Mkoani Shinyanga naye akifunguka juu ya Katiba.

Bi. Dada naye hakubaki nyuma kufunguka juu ya Katiba Mpya

JK AFUTURISHA VIONGOZI WA DINI IKULU DSM.

 Mheshimiwa Kikwete akisalimiana na mmoja wa masista waliofika Ikulu Jijini Dar es salaam jana kwa ajili ya kufuturu.

CCM,CHADEMA WAWATANGAZIA KIAMA MAFISADI




 
                                                                                        Kizitto Noya, Dodoma na Leon Bahati, Dar
VYAMA vya CCM na Chadema vimetoa onyo kali kwa wabunge wanaotuhumiwa kwa kashfa ya kuhongwa na baadhi ya kampuni za mafuta na kulihujumu Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), vikisema havitasita kuwawajibisha pindi tuhuma hizo zitakapothibitika.
Kauli ya vyama hivyo imekuja siku moja baada ya wabunge watano, watatu wa CCM na wawili wa upinzani kudaiwa kuhusika na vitendo hivyo vya rushwa, ambavyo vimesababisha Spika wa Bunge, Anne Makinda kuivunja Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini na kuagiza uchunguzi wa kina ufanyike ili majina ya wahusika yawekwe hadharani.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti jana, viongozi wa juu wa vyama hivyo walisema wanasubiri kwa hamu taarifa rasmi kutoka bungeni.
CCM: Rushwa adui wa haki
Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara, Pius Msekwa alisema chama hicho kimewaapiza wanachama wake wote kutotoa wala kupokea rushwa.
Alisema rushwa ni kosa la jinai hivyo anaamini vyombo husika vya dola vitachukua hatua zinazofaa kwa mujibu wa sheria za nchi.
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye alikazia kauli hiyo akisema rushwa inaelezwa katika katiba ya chama hicho kwamba ni, ‘adui wa haki’ na wanachama wote waliapishwa kuwa hawatapokea wala kutoa rushwa.
Alisema yeyote anayekwenda kinyume na kanuni za CCM, anajiweka katika kundi la wasaliti wa chama.
Alisema wabunge ni kundi maalumu nchini ambalo linalipwa vizuri ili lisimamie vyema misingi ya maendeleo ya nchi pasipo tamaa wala vishawishi hivyo wanapotajwa miongoni mwa kundi la wala rushwa, CCM kinalaani vikali tukio hilo.
Kuhusu tuhuma hizo kutajwa kuwahusisha wabunge watatu wa chama hicho, Nape aligoma akisema habari hizo siyo rasmi, hivyo hawezi kuzizungumzia.
Hata hivyo, alisema CCM kinasubiri uchunguzi ufanyike ambao  ndiyo utakaoweka bayana wahusika wa tuhuma... “Tusubiri uchunguzi ukamilike.  Idadi inawezekana ikawa hiyo au ikapungua au kuongezeka.”

Dk Slaa: Hatufumbii macho ufisadi
Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa alisema: “Nalaani kitendo cha wabunge kuhusishwa na ufisadi hasa ikizingatiwa kwamba Chadema tumekuwa tukiupinga vikali. Tumekuwa tukipinga rushwa kwa sababu ndiyo inayoielekeza nchi pabaya… Chadema hatufumbii macho rushwa.”
Alisema tangu kuanza Bunge la 10, Chadema kimekuwa kikiona baadhi ya mambo yanayoendelea katika mhimili huo muhimu wa dola yamejaa walakini... “Ndiyo maana sisi Chadema tumekuwa tukisema Bunge limepoteza mwelekeo.”
Alisema akiwa mtendaji mkuu wa chama, anasubiri taarifa kamili kutoka katika kikao cha wabunge wa chama hicho ili kuweka wazi majina ya wahusika na kisha kufuatiwa na kikao cha Kamati Kuu (CC) ambacho kitakaa na kuchukua hatua kali.
“Tunahitaji tupate maelezo ya kina... chama chetu hakikurupuki… Nasubiri taarifa ya kokasi ya chama. Katiba ya Chadema inatambua uwapo wa kikao cha wabunge wetu na kwa bahati nzuri, kiongozi wake mkuu ni Mwenyekiti wa Chadema (Freeman Mbowe) na katibu (David) Silinde ni mbunge wetu. Tunasubiri taarifa yao.”
Alisema Chadema kina kanuni ya kudhibiti rushwa hivyo, mbunge wake akitajwa miongoni mwa wanaohusishwa na rushwa, atawajibishwa kupitia kikao cha CC ya chama hicho.
NCCR-Mageuzi  yakoleza moto

Katika hatua nyingine, Chama cha NCCR- Mageuzi jana kilikoleza moto baada ya kumtaka Spika Anne Makinda awataje wabunge hao bungeni ili wafukuzwe na kufungwa kama Sheria ya Haki, Kinga na Madaraka ya Bunge inavyotaka.
Chama hicho kimetoa wiki moja kwa Spika Makinda kufanya hivyo, kikionya kuwa vinginevyo, chenyewe kitawasilisha hoja mahususi kutaka Bunge lichukue hatua hiyo.
Mwenyekiti wa chama hicho, James Mbatia alitoa tamko hilo mjini Dodoma, akisema  Sheria Namba 3 ya Haki, Kinga na Madaraka ya Bunge ya mwaka 1988, inataka wabunge wanaothibitika kujihusisha na rushwa wafukuzwe na kufungiwa kwa kipindi cha miaka mitano.
“Ni aibu kwa Bunge, taasisi inayoitwa tukufu kuwa na mafisadi. Kitendo cha Spika kukubali kuivunja Kamati ya Nishati na Madini na kuahidi kuzivunja nyingine, maana yake anakubali kuna mafisadi. Sisi tunamtaka atutajie wabunge hao bungeni ndani ya juma moja,” alisema Mbatia.
Mbatia aliyeongozana kwenye mkutano huo na wabunge Moses Machali wa Kasulu Mjini na Agripina Buyogela (Kasulu Vijijini), alisema pamoja na Bunge kuendeshwa kwa kanuni zake, kwa Tanzania kuwa mwanachama wa Jumuiya ya Madola inaweza pia kuiga yaliyofanywa katika nchi nyingine za jumuiya hiyo, zikiwamo India na  Uingereza.
Kwa mujibu wa Sheria zinazotumika katika nchi hizo, mbunge yeyote anayethibitika kutumwa na mtu nje ya Bunge, kuongea au kuandika bungeni kwa masilahi ya mtu huyo, anapaswa kufukuzwa ubunge na kufungwa.
“Kati ya mwaka 1924 na 1956, Uingereza ilifukuza wabunge 59 na kati ya mwaka 2005 hadi sasa, Bunge la India liliwafukuza wabunge 11 baada ya kuthibitika walihongwa na wafanyabiashara kuuliza maswali binafsi,” alisema.
Mbatia aliendelea kueleza kuwa katika Bunge la Nane nchini, wabunge wanne walikamatwa na kushtakiwa, kisha chama chao CUF, kiliwazuia kujihusisha tena na siasa baada ya kubainika kuwa walifunga ndoa batili na Wasomali ili wapate hati ya kuishi nchini.
“Sasa suala hili, wabunge wote wanaohisi wamo kwenye orodha hii ya ufisadi waachie ngazi. Mbunge yeyote na wa chama chochote anayeona ameshiriki uchafu huu, kwa utashi wake aachie ngazi,” alisema na kuongeza:
“Kwa vile vyama viadilifu, waige mfano wa CUF. Bunge lichukue nafasi yake kabla hatujafunga Bunge Agosti 18 tuwe tumefanya uamuzi wa kuwafukuza.”
Mbatia alisema ili Bunge lilirudi kwenye heshima yake, Spika Makinda pia anapaswa kuzitaja kamati nyingine alizosema zinachunguzwa na ikiwezekana nazo zivunjwe ili haki itendeke.
“Sisi (NCCR-Mageuzi) tunataka pia Spika azitaje kamati hizo, ziko sita na tuseme pia kwamba hatuna imani na Kamati ya Haki, Kinga na Madaraka ya Bunge. Tunataka nayo ijisafishe kwanza kwa kuwa nako kuna watuhumiwa.”
“Katika hili niombe kiti cha Spika kitende haki, hata kama kuna mbunge wa NCCR-Mageuzi anahisi alishiriki ufisadi huu, awahi mapema kuondoka, hii isiwe kwa vyama vingine tu,” alisema.
Mbatia alisema suala la Tanesco ni tone tu, akisema ufisadi kwa wabunge ulianza siku nyingi na kuongeza... “Mheshimiwa Kafulila (David) aliwataja wajumbe wa Kamati ya LAAC lakini, mpaka leo hakuna kinachoendelea.”
Alisema tatizo la ufisadi kuhusisha wabunge lilianza Juni 23, 2006 siku ambayo nchi iliingia mkataba na Kampuni ya Richmond... “Kuanzia hapo kumeendelea kuwa na sintofahamu katika Wizara ya Nishati na Madini. Dawa yake ni kuweka mikakati ya Bunge kujitakasa.”

Sakata lenyewe

Wabunge hao watano (majina tunayahifadhi kwa sasa) wanatuhumiwa kutumia nafasi zao za uwakilishi bungeni au ujumbe ndani ya kamati husika, kufanya biashara na Tanesco na kutetea mafisadi wanaolihujumu shirika hilo kutoka ndani na nje.
Hata hivyo, baadhi ya wabunge waliochangia hoja hiyo bungeni walisema wanawafahamu wabunge hao kwa majina, lakini wasingependa kuwataja kwa kuwa siyo wakati mwafaka.
Moto wa kutaka kutajwa kwa majina ya wabunge hao ulikolezwa na Mbunge wa Namtumbo (CCM),
Vita Kawawa  ambaye aliomba Spika avunje Kamati ya Nishati na kutaka pia Bunge lijadili kashfa hiyo.
“Waheshimiwa wabunge wamejadili suala hili kwenye wizara, lakini kwa mujibu wa Kifungu cha 55 (3) f, Mbunge au Waziri anaweza kutoa hoja ili jambo fulani lijadiliwe.
Sasa mimi naomba kutoa hoja ya kujadili suala hilo.”Baada ya hoja hiyo kuungwa mkono na idadi kubwa ya wabunge , ndipo Spika Makinda aliposimama na kukubali hoja hiyo ya Mbunge Vita Kawawa na kutangaza kuivunja kamati hiyo.
Spika Makinda alisema tayari pia, ameagiza Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge kutengeneza kanuni za kuwadhibiti wabunge wenye tabia hiyo ya kupokea rushwa kutoka kwa watu mbalimbali ili kutimiza matakwa yao binafsi.
“Nasema kwa dhati kabisa kitendo hiki hakikubaliki ndani ya Bunge. Wabunge mkae vizuri, kama kuna baadhi yetu wanakwenda huku na huku kujitafutia masilahi binafsi mnawezaje kuisimamia Serikali?”

Aliyekuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Nishati na Madini, Seleman Zedi alisema ameshtushwa na uamuzi huo wa Spika na kwamba anasubiri uamuzi wa Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge.
Akihitimisha hoja ya wizara yake bungeni, Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo alisema baadhi ya wabunge ambao wanashiriki kwenye vikao vya uamuzi vya Tanesco kama wajumbe wamekuwa wakilihujumu shirika hilo kwa njia mbalimbali ikiwamo kufanya nalo biashara.
“Shirika liliwahi kulipa Paundi 50,000 za Uingereza kwa ajili ya ununuzi wa vipuri, lakini kilicholetwa nchini ni masanduku ya misumari. Nguzo hizo za umeme kuna biashara inaendelea. Tunajua kwamba nguzo hizo zinazalishwa Iringa na kupelekwa Mombasa kisha kurudishwa nchini kwa maelezo kwamba zimetoka Afrika Kusini,” alisema Profesa Muhongo.(Chanzo mwananchi newspaper)

ALICHOSEMA MH.MNYIKA BAADA YA SPIKA KUVUNJA KAMATI YA BUNGE YA KUDUMU YA NISHATI NA MADINI


Kufuatia uamuzi wa Spika wa Bunge jana jumamosi tarehe 28 Julai 2012 kukubali kuvunja Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini nimetakiwa kutoa maoni yangu kuhusu uamuzi husika kwa nafasi yangu ya Waziri Kivuli wa Nishati na Madini na mbunge: 

Kwa maoni yangu uamuzi huo ni sahihi lakini umechelewa na pekee hauwezi kurejesha heshima ya bunge kwa ukamilifu wala hautaweza kushughulikia uzembe na udhaifu ulioko kwenye bunge na kwenye serikali ikiwa hautaambana na hatua nyingine za ziada na za haraka.Kwa upande mwingine, uamuzi huo umedhihirisha nilichokisema kwa nyakati mbalimbali kuhusu uzembe wa
kibunge pamoja na udhaifu wa serikali.

Ukiondoa tuhuma za wabunge wanaodaiwa kupokea rushwa ama kuwa na maslahi ya kifedha kwenye wizara, taasisi au mashirika wanayoyasimamia kwenye kamati mbalimbali, heshima ya bunge imeathiriwa vile vile na maamuzi mathalani uamuzi wa kuchaguliwa kwa mtuhumiwa wa ufisadi wa Rada Mbunge Andrew Chenge kuwa mwenyekiti wa Kamati ya Fedha na Uchumi.

Hivyo hatua zaidi zichukuliwe ikiwa ni pamoja na kuvunja na kamati zenye wajumbe waliotuhumiwa na pia kufanya mabadiliko makubwa kwenye wajumbe wa kamati mbalimbali za kudumu za bunge ili kupunguza maslahi ya kifedha ama tuhuma za rushwa miongoni mwa wajumbe wa kamati. Aidha Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge imalize kazi yake kwa dharura ili majina ya wahusika yatajwe ndani ya bunge na bunge lijadili kupitisha maazimio ya hatua za ziada za kuchukuliwa na vyombo huru vya kiuchunguzi na hatimaye watakaothibitika kuvunja sheria wafikishwe mahakamani. Pamoja na hatua hizo, Kamati za Vyama nazo zichukue hatua kwa wabunge wake watakaotajwa ili kudumisha misingi ya uadilifu na uwajibikaji kwa maslahi ya umma.
Hata baada ya hatua hizo, izingatiwe kuwa Bunge litaweza kujinasua kwenye uzembe ikiwa litatimiza kikamilifu wajibu wake wa kuisimamia serikali kwa mujibu wa ibara ya 63 kuondoa udhaifu wa serikali kwenye sekta ya nishati na sekta nyingine muhimu za taifa kwa kuhakikisha maazimio yote ya bunge yanatekelezwa kwa ukamilifu na kwa haraka kama nilivyoeleza kwenye maoni ya kambi rasmi ya upinzani bungeni tarehe 15 Julai 2011 na tarehe 27 Julai 2012.

Nilisema bungeni kwamba “Naamini iwapo maazimio ya Bunge juu ya Mkataba baina ya TANESCO na Kampuni ya Richmond Development Company LLC yangetekelezwa yote na kwa wakati toka mwaka 2008, maazimio ya bunge juu ya uendeshaji wa sekta ndogo ya gesi asili ya mwaka 2011 yangezingatiwa yote na kwa haraka, maazimio kuhusu uhalali wa utaratibu wa Wizara ya Nishati na Madini kuchangisha fedha kwa ajili ya kupitisha bajeti bungeni ya mwaka 2011 yangechukuliwa kwa uzito unaostahili; taifa lingeepushwa kurudia mijadala ile ile kuhusu Wizara hii hii mara kwa mara”.

Mathalani, Waziri wa Nishati na Madini ameeleza bungeni tarehe 28 Julai 2012 kuwa wapo wabunge wanaotuhumiwa kufanya biashara zenye kulihujumu Shirika la Umeme (TANESCO) na Spika wa Bunge akahitimisha kuwa Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge itachunguza tuhuma husika na pia kwamba inakusudiwa kutungwa kwa Kanuni za Maadili (Code of Conduct) ili kudhibiti hali hiyo.

Hata hivyo, Serikali na Uongozi wa Bunge kwa pamoja wamesahau kuwa mwaka 2008 baada ya Kashfa ya Richmond iliazimiwa katika Azimio Na. 11, kwamba “Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma ya Mwaka 1995 (The Public Leadership Code of Ethics Act), ifanyiwe marekebisho makubwa ili kudhibiti utaratibu unaoonekana wa kawaida sasa wa Viongozi Waandamizi wenye dhamana ya kisiasa kuendelea na biashara zao binafsi wakiwa madarakani, jambo ambalo lina mgongano wa kimaslahi. Serikali ianze rasmi maandalizi ya majadiliano ya kina kuhusu suala hili ndani na nje ya Bunge kwa kuwashirikisha wadau mbalimbali.”

Bunge lilitaarifiwa Februari 2010 kuhusu utekelezaji wa Serikali kwamba kikundi kazi (Task Force) kiliundwa ambacho kiliandaa waraka wenye mapendekezo ya kurekebisha Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma, (Sura 398) ambao ulikuwa katika ngazi ya kujadiliwa na Kamati ya Makatibu Wakuu (IMTC). Aidha, Bunge lilielezwa kuwa serikali ilitarajia kuwasilisha muswada husika katika mkutano wa kumi na tisa wa Bunge la tisa. Muswada huo haukupitishwa katika Bunge la tisa kama ilivyoshauriwa na kamati na mpaka kutokana na uzembe na udhaifu azimio hilo halijatekelezwa na tuhuma nyingine zimeendelea kuibuka.

Aidha, kumetolewa madai ya baadhi ya wabunge kupokea ama kudai rushwa suala ambalo nalo Spika wa Bunge ametoa uamuzi kuwa litashughulikiwa na Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge. Lakini Serikali na Uongozi wa Bunge kwa pamoja wamesahau kwamba hii si mara ya kwanza kwa tuhuma za namna hiyo kutolewa juu ya baadhi ya wabunge wa kamati mbalimbali za bunge.

Hata hivyo, kwa sababu ya kutochukua hatua kwa haraka na kwa ukamilifu tuhuma kama hizo zitaendelea kujirudia hata baada ya kuvunjwa kwa kamati ya bunge ya nishati na madini. Izingatiwe kwamba madai ya rushwa kutolewa kwa wabunge yaliwahi kujitokeza kuhusu Kamati ya Nishati na Madini na binafsi nilitoa ushuhuda kwa Ofisi ya Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) mwaka 2011, na nikatoa ushuhuda tena kwa Kamati Teule ya Bunge iliyochunguza uhalali wa utaratibu wa Wizara ya Nishati na Madini kuchangisha fedha kwa ajili ya kupitisha bajeti bungeni mwaka 2011 kuwa yamekuwepo matukio ya kushawishi wabunge kwa rushwa hata hivyo hatua hazikuchukuliwa ama kuvunja kamati zilizotajwa au kuwachukulia hatua wahusika.

Suala hili likatajwa tena na Mbunge wa Kigoma Kaskazini David Kafulila kuhusu Kamati ya Hesabu za Serikali za Mitaa na likatajwa tena na Kiongozi wa Upinzani Freeman Mbowe na Mbunge wa Kyela Dr Harrison Mwakyembe kuhusu uchaguzi wa Afrika Mashariki lakini hatua hazikuchukuliwa kuchunguza wabunge husika na kuchukua hatua. Iwapo maazimio kuhusu uhalali wa utaratibu wa Wizara ya Nishati na Madini kuchangisha fedha kwa ajili ya kupitisha bajeti bungeni ya mwaka 2011 (Maarufu kama Sakata la Jairo), yangetekelezwa na wahusika wangechukuliwa hatua ingejenga nidhamu pia kwa watendaji wa wizara na mashirika ya umma kuhusu rushwa na matumizi mabaya ya fedha za umma yenye kulenga kuwaathiri wabunge kwa rushwa na maslahi mengine ya kifedha.

Katika hali inayoonyeha kwamba Serikali bado haioni uharaka na ulazima wa kuchukua hatua, wakati bunge lilipokaa kama kamati tarehe 28 Julai 2012 kupitisha bajeti ya Wizara ya Nishati na Madini nilitaka ufafanuzi kutoka kwa Waziri wa Nishati na Madini kuhusu utekelezaji wa maazimio hayo ambayo mpaka sasa hakuna taarifa ya utekelezaji iliyowasilishwa bungeni toka yapitishwe mwezi Novemba mwaka 2011; lakini Waziri akajibu tu kwamba hawezi kufanyia kazi taarifa za magazetini, bila kujali kwamba nilichouliza hakihusu taarifa za magazetini bali maazimio ya bunge baada ya kazi iliyofanywa na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali na ikarudiwa tena na Kamati Teule ya Bunge ambayo ilihoji wahusika na kupata pia vielelezo.

Kwa hiyo, ni muhimu Serikali na Uongozi wa Bunge ukarejea kwenye Hotuba niliyowasilisha bungeni na kuchukua hatua kwa usimamizi wa Rais, Waziri Mkuu na Spika wa Bunge juu ya masuala yote niliyoyaeleza. Pamoja na kutaja ushawishi uliokuwa ukifanywa kwa wabunge kuhusu suala la ununuzi wa mafuta ya IPTL, na ufisadi ndani ya TANESCO nilieleza pia masuala mengine makubwa kwenye nishati na madini yenye kuhusu mabilioni ya shilingi kwenye mikataba mikubwa ya umeme, madini, mafuta na gesi asili pamoja na hatua za mabadiliko ya kimfumo zinazopaswa kuchukuliwa.

Nimetoa maoni hayaleo jumapili tarehe 29 Julai 2012:

Ben Pol-Maneno Official Video

Shetta feat. Diamond - Nidanganye

Ali Kiba ft Lady Jay dee - Single boy

"Mawazo"-Diamond(Official Video)

BOB JUNIOR NI CHUM

NI WEWE - AMIN.VOB

Mshindi wa TUSKER PROJECT FAME 2012 ni RUTH kutoka NAIROBI-KENYA


Pichani: Ruth mshindi wa kwanza
 
Age: 26 Years Old
Country: Kenya

I am a 26 year old lady born in the Western part of Kenya.
I love music and I believe that I will die doing music because that is my passion. Aside from being a passion, I know it is a gift I got from God. It keeps me going through life's issues.
Through music, I get to express myself easier and better.

However, I want to use my music as a tool to speak to the voiceless out there. People who cannot speak for themselves yet they have a lot that they would want to share with the rest of the world.

I am currently participating in the Tusker Project fame music competition and I am enjoying every bit of it despite the few surprises that come with it. I love God and I thank Him for the gift.

 Pichani: Doreen mshindi wa pili

Age: 21 Years Old
Country: Kenya

Purple Diva is what they call me. Doreen Naira is the name my parents gave me... I am a lover of art, a student of nature, a poet and a girl that is crazy about the color purple...but above all these, I am a music fanatic. I come from Kenya, the closest place I know to the mythical land of milk and honey.

I am no scientist; in fact, I believe music makes the earth go round. I am a spirited singer (music is bigger than me, than you and its greater than us all) music is not what I do it is who I am, it is through music, I believe, that I can tap into my reservoir, and give to human kind the best of me.
It’s a unifying factor that makes us come together and bring out the best in us... Try as we may, we cannot live without music (at least I can’t)

I want them to remember me, and when I am gone... I don’t want them to say much... Just that I was here," and boy, did she sing her heart out!" I will feel that I lived my life, and lived it well.

Much love
Doreen xoxox

Pichani: Jackson mshindi wa tatu
Age: 25 Years Old
Country: Rwanda

Hi I am Jackson, I am a performing artist from a beautiful country; they call it the land of a thousand hills. I am the fourth of six children and I love my mother. She always told me that if I loved something, I should do it wholeheartedly.

Since my childhood ,I have loved music....it is my greatest passion. I believe that music has power, it inspires me. To all my fans, my music is like the spirit...it unites the body to the soul. It is good for us to know our fellow men while on earth, since the heart has a lot of secrets it hides....God gave man the ability to compose and perform music...so that we can share what is in our hearts.

Jackson

Pichani: Joe mshindi wa nne
Age: 24 Years Old
Country: Burundi

hellowz
Its Joe Irankunda aka Kiki in the Tusker Project Fame Academy.....

I am from Burundi with the current help of the best East African faculty of Tusker Project Fame I’m on my way too being a singer by career! I have been singing since I was 5 years old and i would like to thank God for giving me this amazing talent that I’m learning to use skillfully every day. I’m enjoying my time here and loving it.

I’m a caring gentleman with a natural trait of a considerate person, I care about people and I’m always compelled to make you feel better by singing to you.

To my homies, my mom, and my beloved brother thank you for believing me. I want to be with you all, but until then, I enjoy singing for you!

Yours always Joe.

KILICHOJIRI KWENYE MAGAZETI YA LEO PIPOOOO

.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.

EPIQ BONGO STAR SEARCH TANGA - WASHIRIKI WALIOKOSA NAFASI MIJI MINGINE WAFURIKA JIJI LA MAHABA


Umati wa washiriki wa Epiq BSS uliojitokeza katika ukumbi la Lacasa Chica kujaribu bahati zao



Watu na Swaumu zao walikuja kufunguka na EBBS

hata mimi nime mmenisoma?

FC BASEL YAIFUNGA KWA PENATI TSC MWANZA KWENYE FAINALI YA KOMBE LA FALLERHOF




FC BASEL MABINGWA WA KOMBE LA FALLERHOF BAADA YA KUIFUNGA KWA PENATI 5-4 TSC MWANZA

Timu ya soka ya TSC Academy ya Mwanza leo baada ya kuifunga timu ya soka ya Freiburg ya Ujerumani ambayo inatoa wachezaji takribani watano kwenye kwenye timu ya taifa ya nchini hiyo chini ya umri miaka 20, ilifanikiwa kuingia kuingia fainali ya kombe la Fallerhof na ikakutana na timu ya FC Basel kutoka Uswis.
TSC Academy wakiwa kwenye pamoja ya pamoja
Katika mchezo huo uliochezwa jioni kwa saa za Ujerumani, timu hizo zilitoka sare mpaka dakika tisini zinaisha na ikabidi mechi iamuliwe kwa mikwaju ya penati ambapo bahati haikuwa upande wa TSC wakapoteza penati moja kati ya tano, huku wapinzani wao FC Basel wakifunga zote na kufanikiwa kutwaa ubingwa wa michuano hiyo.
Mchezaji bora wa mashindano
TSC wakiwa na kikombe chao cha mshindi wa pili
Mabingwa FC BASEL
Mfungaji bora wa mashindano(kwa hisani ya shaffihdauda.com )                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                              

THE DON HIMSELF

Karibuni sana kwenye blog hii ya kijamii iliyosheheni makila kitu kuanzia siasa uchumi afya na burudani kwa ujumla wake.uingiapo kwenye blog hii ni mengi ambayo utapata nafasi ya kukutana nayo,kumbuka mawazo yako ndo hasa yanayojenga na kunifanya niwe na ufanisi zaidi.kariiiiiiibuuuuuuuuuuuu saaaaaaaaaaaaaaanaaaaaaaaaa.(THE DJ HIMSELF-JIWE)

Followers

BLOG ZA MARAFIKI

Search This Blog

ZILIZOPITA

DUNIA MUZIMA