


Ni globu ya kijamii inayojihusisha na mambo yote ya kijamii,natumaini jamii yangu ya kitanzania itafaidika sana pindi ichukuapo fursa ya kuperuzi kwenye globu hii,dhamira yangu ni kufikisha ujumbe pamoja na kuiburudisha jamii yangu na furaha yangu ni kuona natimiza dhamira yangu kwako.natumaini kuwa wewe utaniunga mkono kwa kile ambacho nataka kukifanya kwa ajili ya jamii yangu ya kitanzania.NASHUKURU KWA KUNIELEWA.
Kinamama waliokuwa wakimsubiri kwa hamu JK katika uwanja wa Kambarage mjini shinyanga wakirukaruka kwa furaha mara helikopta ya JK ilipokuwa ikitua nje ya uwanja huo. |
· Ni kwa Face Book na nyinginezo
Dar es Salaam, 26 Septemba, 2010. Kampuni ya Simu za Mkononi ya Vodacom Tanzania, imezindua huduma mpya ya Intaneti ambayo itawawezesha wateja wake kuchati kwa intaneti bure.
Mkurugenzi wa Uhusiano wa Vodacom Tanzania, Bi Mwamvita Makamba alisema jana kwamba wateja wa Vodacom sasa wanaweza kuchati bure kwenye tovuti za Face Book, the Grid na Vodamail.
Alisema Vodacom Tanzania inatoa huduma hiyo kwa lengo la kuwawezesha wateja wake kupata muda wa kuchati zaidi.
Alifafanua kwamba hayo yote yatawezekana kwa kutumia mtandao wa 3G ambao una kasi na nguvu kubwa.
“Tunapenda wateja wetu watumie mtandao wetu kwa kuwasiliana bure na hivyo kukata kiu yao ya mawasiliano”.
Alitoa wito kwa wateja wa Vodacom na Watanzania kwa ujumla kutumia huduma hiyo ya mtandao wa Intaneti.
Aliwaomba Watanzania kujiunga na Vodacom ili kupata huduma hiyo bure na hivyo kuwasiliana zaidi.
Alisema huduma hiyo itapatikana kwa simu za mkononi na pia kwa Laptop zilizounganishwa na USB Moderm.
Tangu kuanzishwa kwake miaka kumi iliyopita Vodacom imekuwa ikizindua huduma mpya kila mara kwa lengo la kurahisha huduma za mawasiliano kwa wateja wake.
Hivi sasa kampuni hiyo inawateja zaidi ya milioni saba ambao wanaunganishwa na huduma mbalimbali zenye lengo la kuboresha maisha yao, baadhi ya huduma hizo ni kama M-Pesa, ambayo ni njia ya haraka na uhakika ya utumaji wa pesa hapa nchini.
Vodacom ndiyo wa kwanza kuanzisha huduma hiyo hapa nchini.
Wanachama Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Lindi mjini wakimsikiliza Mke wa Rais Mama Salma Kikwete wakati alipokuwa akiwahutubia.Picha na Mwanakombo Jumaa |