Sep 13, 2010

wadau walihudhuria kwenye inshu nzima na pia zawadi zilimwagwa kwa washiriki wa miss tz

MKurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Utalii Nchini TTB Dr. Aloyce Nzuki akimkabidhi taji balozi wa Utalii nchini Salma Mwakalukwa mara baada ya kutangazwa kwenye shindano la Vodacom Miss Tanzania lililofanyika kwenye ukumbi wa Mlimani City usiku wa kuamkia leo numa ni Mmoja wa Maafisa wa Wizara ya Maliasili na Utalii Bw. Ernest Mwamwaja. Mrembo huyu atafanya kazi kubwa ya kuutangaza utalii wa ndani na kuhamasisha jamii kujua na kupenda au kuwa na utamaduni wa kutembelea vivutio vilivyopo nchini akiacha watalii wanaotoka nje ya nchi ambao ndiyo wamekuwa wakitembelea kwa wingi vivutio hivyo.
Makamanda kutoka vyomnbo mbalimbali wakiwa kazini hebu wacheki wanavyowajibika mdau.
Mkurugenzi Mtendaji wa Shiriki la Nyumba NHC Nehemia Kyando Mchechu kushoto na Mkurugenzi wa Masoko wa Vodacom Tanzania Ephraim Mafuru wakifuatilia kwa makini shindano hilo.
Wadau kutoka vyombo mbalimbali vya habari walikuwepo ili kujua kilichojiri katika shindano hilo na kuipasha habari jamii.
Mdau Lusako Owen kulia akiwa na Mkurugenzi wa Masoko wa benki ya CRDB Tuli Mwambapa kulia.
Mkurugenzi wa Sahara Media Group Samwel Nyalla kulia akiongea na Mkurugenzi wa CM. Co. Limited Charles Mtawali.
Mkurugenzi wa kampuni ya Prime Time Juhayna Kusaga kushoto na Mdogo wake Garina hawakutaka kusimuliwa juu ya shindano hilo.
Katibu Mhutasi wa kampuni ya Prime Time Godliver kushoto na rafiki yake nao walipita kwenye Red Carpert.
Mboni Masimba kushoto Mwanamama Shamimu Mwasha ambaye ni Blogger wa www.8020fashion.blogspot.com akiwa kulia pamoja na rafiki yao. nao hawakukosa kushuhudia shindano hilo.
Mwanamuziki AY wa pili kutoka kushoto akiwa na mwanamuziki E.Sniper kushoto, Castro na promota kutoka Uganda ambaye ni Mkurugenzi wa kampuni ya House Of Talent ya Uganda Bw. Eddie DouglasOkila kulia mwisho.
Vijana wa TMK Family Chege kushoto na Mh Temba wakihojiwa na mtangazaji wa kituo cha Televisheni cha Mlimani TV.
Mkurugenzi wa Masoko wa Vodacom Ephraim Mafuru akiongea na Mkurugenzi wa Kamati ya Miss Tanzania kabla ya kuanza kwa shindano hilo Vodacom ndiyo wadhamini wakuu wa shindano la Vodacom Miss Tanzania.
Wadau kutoka MUZASHA TUORS wakiwajibika vilivyo katika shindano hilo.
Ilikuwa si Mchezo kwenye Red Carpet mdau
Mkurugenzi wa Masoko Vodacom Tanzania Ephraim Mafuru wa pili kutoka kulia George Rwehumbiza Mkuu wa Udhamini Vodacom Tanzania wa kwanza kulia Elihuruma Ngowi Afisa Bidhaa wa kwanza kulia na Matina Nkurlu Afisa Habari wakipozi kwa picha mara baada ya kuhakikisha kila kitu kiko sawa katika shindano hilo.
Wadau kutoka Star TV kutoka kushoto ni Saida Mwilima, James Range, Neema na Christina Mbezi nao walikuwepo.
Vodacom Miss Tanzania Geneviva Emmanuel akipokea mfano wa cheki yenye thamani ya shilingi milioni 10 kutoka kwa Mkurugenzi wa Masoko wa Vodacom Tanzania Ephraim Mafuru katika hafla ya kukabidhi zawadi iliyofanyika jana jioni kwenye hoteli ya Giraffe Ocean View Kunduchi Geneviva Emmanuel aliibuka mshindi na kuwapiku wenzake 29 katika shindano lililofanyika jumamosi mwishoni mwa wiki kwenye ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es salaam na anatarajiwa kuwakilisha nchi kwenye shindano la dunia (Miss World 2010) litakalofanyika mwishoni mwa mwaka huu.
Mkurugenzi wa Masoko wa Vodacom Tanzania Ephraim Mafuru katikati akiwa katika picha ya pamoja na warembo kushoto wa kwanza ni Consolata Lukosi, Groly Mwanga na kulia wa kwanza ni Beatrice Premsingh, na Vodacom Miss Tanzania Geneviva Emmanuel.
Mkurugenzi wa masoko wa Vodacom Tanzania Ephraim Mafuru kushoto akikabidhi cheti cha Ushiriki wa shindano la Vodacom Miss Tanzania mrembo Groly Mwanga ambaye ni mshindi wa pili katika shindano hilo
Meneja Uhusiano wa Scangroup Tawi la Tanzania Bw. Barnabas Lugwisha kulia akipokea cheti kwa niaba ya kampuni hiyo ikiwa ni kutambua mchango wa kampuni hiyo katika kufanikisha shindano la Vodacom Miss Tanzania.
Warembo pamoja na waalikwa mbalimbali wakijimwaga ukumbini kwa burudani ya muziki.
Burudani pia hazikkukosa jana katika hafla ya kukabidhi zawadi kwa warembo wa Vodacom Miss Tanzania iliyofanyika kwenye Hoteli ya Giraffe Ocean View Kunduchi.
Mkurugenzi wa Masoko wa Vodacom Tanzania Ephraim Mafuru katikati akiwa pamoja na Mkuu wa Udhamini wa kampuni hiyo Geprge Rwehumbiza kulia pamoja na Ayubu Ryoba aliyekuwa mmoja wa majaji wa shindano hilo.
Wadau wakijadiliana jambo na mmoja wa warembo walioshiriki katika shindano la Vodacom Miss Tanzania lililomalizika hivi karibuni.
Hashim Lundenga Mkurugenzi wa Kamati ya Miss Tanzania katikati akiwa na Mshauri wa Kamati ya Miss Tanzania wa pili kutoka kulia na wadau wengine wakiwa katika hafla hiyo.
Kutoka kushoto ni Loveness, Benny Kisaka, Jeseline na rafiki yake kushoto.

hivi ndivyo ilivyokuwa miss tz bongo

Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom,Dietlof Mare (kushoto) akikabidhi funguo ya gari aina ya Hyundai i10 kwa mrembo wa Vodacom Miss Tanzania 2010,Genevieve Emmanuel mara baada ya kunyakua taji la urembo huo usiku wa kuamkia leo katika ukumbi wa Mlimani City,jijini Dar.
Vodacom Miss Tanzania 2010,Genevieve Emmanuel (kati) akiwa na mshindi wa pili Glory Mwanga (kushoto) na Consolata Lukosi.
AY stejini.
THT.
Vodacom Miss Tanzania aliemaliza muda wake,Miriam Gerald (shoto) akimvisha taji Vodacom Miss Tanzania 2010,Genevieve Emmanuel mara baada ya kutangazwa mshindi wa taji hilo usiku wa kuamkia leo katika ukumbi wa Mlimani City.
Mwakilishi wa Bodi ya Utalii,Dr. Aloyce Nzuki akikabidhi taji kwa mshindi wa Utalii,Salma Mwakalukwa.
shamra shamra wakati wa kutangazwa kwa mshindi wa Vodacom Miss Tanzania 2010.
Meneja wa Bia ya Redd's,Kabula Nshimo (shoto) akiwa na Balozi wa Redd's,Consolata Lukosi mara baada kumtangaza.
Mwenyekiti wa Kamati ya Miss Tanzania, Prashant Patel akitangaza wa Mrembo wa Vodacom Miss Tanzania 2010,katika ukumbi wa Mlimani City usiku wa kuamkia leo.
Majaji wakipitia majina ya warembo kabla ya kuyatangaza.
tano bora.
kumi bora.
MC Taji Liundi akiwa amezunguwa na warembo wa Vodacom Miss Tanzania 2010,wakati akimkaribisha Mratibu wa Majaji,Dr.Ramesh Shah aje kutangaza kumi bora ya warembo hao.
baadi ya warembo wakipita kujionyesha kwa wadau wa urembo waliofika katika ukumbi wa Mlimani City usiku wa kuamkia leo.
Warembo wakipita na vazi la Beach.
Msanii wa Bongo Freva,Mwasiti akiwa na vijana wa THT wakifanya vitu vyao.

Warembo wa Vodacom Miss Tanzania wakionyesha shoo yao ambayo ilipendeza na kuvutia sana.
Wasanii wa Bongo Freva toka TMK,Mh. Temba (shoto) na Chege walipagawisha vilivyo ndani ya ukumbi wa Mlimani City usiku wa kuamkia leo.
Msanii Wahuu toka Kenya nae hakuwa nyuma katika kutoa burudani kwa wadau wa urembo waliofika Mlimani City usiku wa kuamkia leo.
Mzee wa Kiduku,Mataluma nae hakuwa nyuma katika burudani.
TMK wanaumeeeee.........
Ma MC wa shughuli hiyo,kulia ni Taji Liundi na Jokate Mwegelo.
Mie nikiwa na wadau toka shoto ni Mrembo alieshiriki Miss Tanzania 2009,Sylvia Sharry,Martin pamoja na Mwanamitindo Maarufu nchini,Mustafa Hassanali.
Waheshimiwa,kulia ni Waziri wa Nishati na Madini,Mh. William Ngeleja akiwa na mkewe,Pia Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam,Mh. William Lukuvi na mkewe wakifuatilia kwa makini mashindano hayo.
Wadau wa TBL
wageni mbali mbali walihudhulia katika mashindano hayo ya urembo.

Sep 11, 2010

GENEVIVA MPANGALA NDIYE VODACOM MISS TANZANIA 2010!!

Vodacom Miss Tanzania Geneviva Mpangala akiwa na washindi wenzie mara baada ya kutangazwa mshindi kwenye shindano hilo lililofanyika kwenye ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es salaam usiku huu kulia ni mshindi wa tatu Consolata Msofe na kulia ni mshindi wa pili Groly Mwanga, Geneviva ataiwakilisha nchi katika shindano kubwa la Dunia Miss World litakalofanyika mwishoni mwa mwaka huu. Katika shindano hilo wanamuziki mbalimbali wa muziki wa kizazi kipya wamefanya vitu vyao wakiwemo Temba na Chege kutoka TMK Family, Ambwene Yessaya (AY) Mataluma, Mwasiti na kundi la THT kutoka jijini Dar es salaam na wengine wengi.
Hii ni Tano Bora ya Vodacom Miss Tanzania mara baada ya kutangazwa ambapo waliulizwa maswali na kuyajibu kabla ya kutangaza mshindi wa shindano hilo kwa mwaka huu wa 2010.
Hii ndiyo kumi bora ya Vodacom Miss Tanzania mara baada ya kutangazwa kwenye ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es salaam usiku huu.
Washiriki wa shindano la Vodacom Miss Tanzania wakipita jukwaani na vazi la ufukweni ilikuwa si mchezo.
Utambulisho
Utambulisho
Warembo wakipita na kujitambulisha kwa wageni waalikwa na mashabiki wa urembo.
Wakuu wa Kampuni ya MUZASHA TOURS wakishuhudia shindano hilo kulia ni Benedictor Mulokozi Mkurugenzi wa CM Co. Limited Charles Mtawali Mkurugenzi wa MUZASHA TOURS Muzamir Katunzi pamoja na Pamela ambaye ni maiwaifu wa Charles Mtawali.
Warembo wanaoshiriki kwenye shindano la Vodacom Miss Tanzania wakiingia kwa shoo ya utambulisho.
Kulia ni Waziri wa Nishati na Madini William Ngeleja akiongea na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam William Lukuvi aliyekaa chini pamoja na Mkurugenzi wa Kamati ya Miss Tanzania Hashim Lundenga.
Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii Dk Ladslaus Komba akiingia na ujumbe wake kutoka Bodi ya Utalii na Mamlaka ya hifadhi za Ngorongoro kabla ya kuanza kwa shindano hilo huku akisindikizwa na Mkurugenzi wa Kamti ya Miss Tanzania Hashim Lundenga.
Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania Dietlof Mare akihojiwa na mtangazaji wa Star Tv kabla ya kuanza kwa shindano hilo.
Warembo wakiingia kwenye ukumbi wa Mlimani City tayari kwa kupanda jukwaani.

THE DON HIMSELF

Karibuni sana kwenye blog hii ya kijamii iliyosheheni makila kitu kuanzia siasa uchumi afya na burudani kwa ujumla wake.uingiapo kwenye blog hii ni mengi ambayo utapata nafasi ya kukutana nayo,kumbuka mawazo yako ndo hasa yanayojenga na kunifanya niwe na ufanisi zaidi.kariiiiiiibuuuuuuuuuuuu saaaaaaaaaaaaaaanaaaaaaaaaa.(THE DJ HIMSELF-JIWE)

Followers

BLOG ZA MARAFIKI

Search This Blog

ZILIZOPITA

DUNIA MUZIMA