Jul 13, 2010

ZIFF YA 13 YAZIDI KUSONGA ZENJI


Profesa Martin Muhando kulia akitafsiri maelezo ya filmmaker Christa Graf alipokuwa akiongea na waandishi wa habari kuhusu filamu yake Memory Books kwenye ukumbi wa habari ulioko katika hotel ya Al, sayyeda

Mwanamuziki Ambwene Yesaya (AY) akiongea na waandishi wa habari kuhusu makamuzi yake ya usiku wa jana katika chumba cha habari ndani ya hotel ya Al sayeed kushoto na Afisa habari wa ZIFF Asma Makau.

Kikundi cha sarakasi capoeira kikionysha mambo yake katika tamasha la 13 la ZIFF Zazibar jana.

74 killed in the twin bomb blasts in Uganda Kampala!!



An al-Qaeda-linked Somali militant group called Al Shabaab has confirmed on Monday that it carried out two bomb blasts that killed at least 74 people in Uganda's capital Kampala and threatened more attacks if the country kept its peacekeeping troops in Somalia. The attack hit an Ethiopian restaurant in Kampala, normally frequented by western expatriates. The crowds were watching the FIFA's Final World Cup match.

MZINDAKAYA BADO ANAKIU YA KUENDELEA KUKAMUA NONDO AISEE!!!!!!


Mbunge Mbunge wa Jimbo la Kwela Christant Mzindakaya akiwashukuru wabunge wa Bunge la Jamhuri ya muungano wa Tanzania jana mjini Dodoma mara baada ya kutununikiwa Shahada ya Uzamifu ya Heshima katika Filosofia ya Uongozi wa Biashara( Honorary Doctorate Degree of Philosophy in Business Administration) na Chuo Kikuu cha California State Christian cha nchini Marekani. Sherehe fupi za kumpongeza zilifanyika katika ukumbi wa Pius Msekwa mjini dodoma. Picha na tiganya vincent-Dodoma

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samwel Sitta akimpongeza Mbunge wa Jimbo la Kwela Christant Mzindakaya jana mjini Dodoma mara baada ya kutununikiwa Shahada ya Uzamifu ya Heshima katika Filosofia ya Uongozi wa Biashara( Honorary Doctorate Degree of Philosophy in Business Administration) na Chuo Kikuu cha California State Christian cha nchini Marekani. Sherehe fupi za kumpongeza zilifanyika katika ukumbi wa Pius Msekwa mjini dodoma.

JK AMWAGA SUMU NA KUWATAMBULISHA RASMI WAKALI WAKE ATAKAOONGOZANA NAO KUITETEA CCM


Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimtambulisha mgombea mwenza Dr.Mohamed Gharib Bilal kwa wananchi wa mji wa Dodoma leo jioni katika hafla fupi iliyofanyika katika uwanja wa michezo wa Jamhuri.

Mwenyekiti wa CCM Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwahutubia wananchi katika uwanja wa michezo wa Jamhuri mjini Dodoma leo jioni wakati wa kuwatambulisha mgombea mwenza na mgombea Urais wa Zanzibar leo jioni.

Mwenyekiti wa CCM Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mkewe Mama Salma Kikwete wakiingia katika uwanja wa michezo wa Jamhur mjini Dodoma leo jion


miss temeke top 5 wafanya ziara vodacom


Muandaaji wa Miss Temeke Ben Kisaka wapili toka kulia akimkabidhi Mkurugenzi wa masoko wa Vodacom Tanzania Ephraim Mafuru Tuzo ya shukrani kwa udhamini wao katika shindano la kumtafuta mlimbwende wa Temeke,kulia Miss Temeke Genevivu Emmanuel,Mkuu wa Udhamini wa Vodacom George Rwehumbiza(kushoto)Mshindi wa pili miss Temeke Anna Daud.

Afisa ustawi wa wafanyakazi wa Vodacom Tanzania Ndihagati Biduga akiwafafanulia jambo warembo walioingia tano bora katika kinyang’anyiro cha kumtafuta Miss Temeke mara baada ya kutembelea makao makuu ya kampuni hiyo,anaeangalia kulia ni msambazaji wa barua wa kampuni hiyo Rashid Mbonde.

Afisa habari wa Vodacom Tanzania Kilasa Mtambalike aliyesimama(kulia)akiwa kwenye picha ya pamoja na warembo walioingia tano bora katika kinyang’anyiro cha kumtafuta Miss Temeke mara baada ya kutembelea makao makuu ya Vodacom Tanzania ambao ni wadhamini wakuu wa mashindano hayo. Watatu toka kulia waliokaa ni Afisa wa Vodacom Foundation Grace Lyon.


Jul 12, 2010

HATIMAYE NI DR.GHARIB

hongera mzee mwenzangu,tuungane sasa kuimaliza kazi ambayo tuliianza miaka mitano iliyopita.


Mwenyekiti wa CCM, JK akiwa na Makamu wake Amani wakitoka ukumbini kwajili ya kikao kifupi kabla ya klumtangaza Bilal kuwa Mgombea mwenza.

Pamoja na kupanick baada ya kutoswa lakini alikuwa shwari kuliko washabiki zake, kweli subira huvuta kheri.

Wajumbe wakibanjuka kwa furaha baada ya kutangazwa na JK

Dr Ghalib Bilal mgombea mwenza wa JK ambaye kutangazwa kwake kumeua mzizi wa fitna kwa wanaCCM waliodai kupigia kura upinzani baada ya kumwagwa kwake kugombea ZNZ.


BAADA ya kuangushwa mara tatu katika mbio za kuwania urais wa Zanzibar, nyota na nguvu za kisiasa za Dk Mohamed Gharib Bilal zilizidi kujidhirisha baada ya kuteuliwa kuwa mgombea mwenza wa mwenyekiti wa CCM, Jakaya Kikwete kwenye mbio za urais wa Muungano katika uchaguzi mkuu uliopangwa kufanyika Oktoba 31.

Uteuzi huo wa Dk Bilal, ambao ulitangazwa kwenye mkutano mkuu wa CCM uliofanyika Kizota mjini Dodoma, umefanywa katika kipindi ambacho joto la kisiasa ndani ya CCM lilikuwa limepanda baada ya halmashauri kuu ya chama hicho kumtupa msomi huo kwa mara ya tatu kwenye mbio za urais.

"La mwisho kabla ya mwisho," alisema Kikwete na kuacha muda kidogo akisikiliza majibu yan wanachama ambao walipiga kelele kutaka kutangaziwa jina la mgombea mwenza atangazwe baada ya kusubiri kwa muda mrefu.
"La mwisho kabla ya mwisho, nimemteua Dk Bilal kuwa mgombea mwenza."

Mara baada ya tamko hilo ukumbi mzima ulilipuka kelele za nderemo na vifijo, miruzi na maturumbeta mithili ya mavuvuzela huku Bilal akikumbatiwa na watu tofauti wakati akianza kuelekea kwenye meza kuu.

Wakati Bilal akipongezwa, kikundi cha muziki cha CCM, ToT Plus kilianza kutumbuiza huku Rais Kikwete akicheza muziki na uso wake ukiwa umepambwa kwa tabasamu kuonyesha kufurahishwa na kelele za wajumbe ambazo zilionyesha kukubali uteuzi huo.

Bilal alikwenda moja kwa moja kwenye meza kuu na kuwashika mikono viongozi wote, akimkumbatia Rais Kikwete na baadaye kwenda kwenye jukwaa lililokuwa likitumiwa kutoa hotuba kwa ajili ya kutoa shukrani. Hata hivyo, wajumbe waliendelea kujimwaga ukumbini kushangilia wakicheza muziki wa ToT.

Lakini wakati Dk Bilal akiendelea kusubiri wajumbe watulie ili azungumze, afisa mmoja alimwendea na kumnongeza jambo na ndipo waziri kiongozi huyo wa zamani wa Zanzibar alipoondoka na kurudi kwenye kiti chake.

Kabla ya kumtangaza Dk Bilal, Kikwete aliomba mkutano uende mapumziko kwa dakika 15 ili akutane na wajumbe wa kamati kuu, lakini kikao hicho kilichukua takriban nusu saa na aliporejea alianza na hotuba ndefu ya kueleza mafanikio na matatizo ambayo serikali ya awamu ya nne ilikutana nayo tangu mwaka 2006.

Awali majina mbalimbali yalikuwa yakihusishwa na nafasi hiyo, ikiwa ni pamoja na Waziri Kiongozi Shamsi Vuai Nahodha, waziri wa zamani wa fedha, Zakia Meghji, na Waziri wa Nchi, Mohamad Seif Khatibu ambaye ni Waziri wa Ofisi ya Makamu wa Rais -Muungano kabla ya kitendawili hicho kuteguliwa saa 3:30 usiku.

Jul 11, 2010

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI




ZIFF KUANZA LEO (TAREHE 11 July 2010)

“KIINGILIO BURE”

Tamasha la 13 la filamu limepangwa kuanza leo tarehe 10 Julai 2010 katika uwanja wa Ngome Kongwe ulioko mji mkongwe mjini Zanzibar.

Tamasha hili lenye msisimko linatazamiwa kuhudhuriwa na zaidi ya wageni 200,000 likishirikisha zaidi ya nchi 43, hivyo kuwa tamasha kubwa lenye msisimko wa aina yake.

WAGENI WATAKO UPAMBA UFUNGUZI WA TAMASHA HILI NI:
STEVEN KANUMBA
EVONNY CHERRY YAKUB (MONA LISA)
VICENT KIGOSI


Zaidi ya Filamu100 zitakazoonyeshwa mwaka huu katika tamasha linalotazamiwa kukoma tarehe 18 July 2010.

Filamu ya ufunguzi
Filamu itakayo fungua pazia la tamasha hilo Mwaka huu ni

Youssou N’Dour: I Bring What I Love
Iliyoongozwa na: Elizabeth Chai Vasarhelyi
Filamu itaonyeshwa 10th July, Old Fort, Kuanzia saa 3:00 usiku baada ya ufunguzi rasmi.


Filamu hiyo ya ufunguzi, ni filamu yenye tunzo nyingi. Filamu hiyo inayo muhusu mwanamziki maarufu Youssou N’Dour, I Bring What I love (Naleta nachokipenda), inayozungumzia imani na amani. (addresses the themes of religious tolerance, harmony and peace.) ina lengo la kuhamasisha, inaonysha safari ya kimziki, yenye ushuhuda wa nguvu ya sauti ya mtu mmoja kuhamasisha mamilioni.

“I Bring What I Love” imedhaminiwa na SIGNIS.

FILAMU NYINGINE KUBWA ZITAKAZO ONYESHWA MWAKA HUU NI:

Nipe Jibu: Kuonyeshwa kwa mara ya kwanza . Filamu ya kwanza ya kuchanganya Muziki na kuigiza Muongozaji Nadine Louise Fasera. Nipe Jibu ni filamu nzuri ya Kiswahili yenye kuchanganya muziki iliyotengenezwa kwa mtazamo wa kisasa na kitamaduni kwa simulizi iliyochangamka juu ya binti yatima anayeishi kwenye maisha ya ndoto.

My Policy: Kuonyeshwa kwa mara ya kwanza. Kijana mdogo mfanya biashara anapigwa risasi kwenye siku yake ya kuzaliwa akiwa anarejea nyumbani kwake akitokea kwenye tafrija yake kusherehekea siku hii muhimu akiwa na mchumba wake, Victoria. Wiki chache baadae, Yule aliyempiga risasi amjia na kumchoma kisu hadi kufa. Kwa kupagawa na pigo hili, Victoria aamua kuhama Montreal na kuanza maisha mapya, Lakini muuaji amjia nay eye pia.... Muongozaji: Phad Mutumba

Motherland: African premiere - Kuonyeshwa kwa mara ya kwanza Afrika

Ana’s Playground: - kuonyeshwa kwa mara ya kwanza Afrika

Lamu’s Maulid: Kuonyeshwa kwa mara ya kwanza kidunia: world premiere

Inside Life: : Kuonyeshwa kwa mara ya kwanza kidunia: world premiere
Pumzi: East Africa’s first ever science fiction film
A sneak preview of Twiga Stars

Vitu Vya Kutazamia Mwaka Huu:
Kutokana na kufahamu umuhimu wa mashindano ya Mpira Kombe la dunia
Tamasha la ZIFF 2010 litaonyesha Fainali ya Kombe la dunia! KWENYE SCREEN KUBWA.
Fainali hizo zitashuhudiwa katika uwanja wa wazi wa kome kongwe kwenye uzinduzi wa tamasha hili la mwaka huu 2010. Kwa wapenzi wa soka kazi kwenu
KAULI MBIU YA ZIFF MWAKA HUU: ina angaza matakwa ya watu wa kisiwa cha Zanzibar ya amani na muafaka kufuatia kipindi cha uchaguzi.

Muziki
ZIFF 2010 Itakua ikisakata kwenye burudani ya muziki na Dully Sykes – AKA Mr Misifa ama Mr Chicks, Msanii anayetambulika sana kwa miondoko ya dancehall Tanzania. AY, Msanii anayengara ndani ya Africa Mashariki akiwakilisha vyema Tanznia na balozi wa burudani Tanzania, Kidumu , Ndiye mwanamuziki maarufu Africa Mashariki toka Burundi anayeshikilia Tunzo nyingi ikiwemo tunzo ya Muziki bora wa Afrika Mashariki kwa Tunzo za Tanzania Music Awards, Body Mind Soul Bendi ya watu 6 kutoka Kaskazini mwa Malawi wanaopiga mziki wa kiafrika wenye vionjo vya Jazz, Windhund featuring Sekembuke & Siga bendi kutoka Austria inayotumia vionjo vya kizungu na kiafrika, ushairi na sanaa ya simulizi ili kuleto vionjo vipya na vya aina yake kwenye ulimwengu wa muziki.

Filamu za Watoto!
Kwa kushirikiana na taasisi ya filamu ya Kidanish, Maonyesho ya filamu za Watoto zitaonyeshwa makundi makubwa ya Watoto, zikiwa zimetafsiriwa kwa Kiswahili kwajili ya Watoto na vijana wa Mji mkongwe.

Art exhibtions
"Hopes in Harmony" (Matumaini yenye Kuafikiana) – Onyesho la picha yanayoletwa na mpiga picha toka Italy, Carlo Deste"Colour Bash" – Uchoraji wa vitenge kutoka pande mbalimbali za Afrika, na Mahelia de Randamie Artwork kutoka wakina mama wa Iranian, Hii inaletwa na Ubalozi wa Iranian embassykwa kushirikiana na Soko Filam, ambapo watengeneza filamu na wachongaji toka Zanzibar wanakuja kuonyesha na kuuza bidhaa zao..

Tasnia
ZIFF ni tukio muimu kwenye jumuiya ya Cinema duniani. Festival Forum na Festival of Festival program inatoa nafasi kwa wasambazaji, mapromota, waongozaji wa filamu na waandaji kukutana ili kukomaza mizizi kwenye tasnia ya filamu kwenye nchi zinazoendelea. Mwaka huu wawakilishi toka Trinidad na Tobago, Uganda, Holland, Iran, Mexico and Italy watashiriki ZIFF kujadili nafasi ya matamasha ya filamu kwenye nchi zinazoendelea.

Warsha
ZIFF itaendesha warsha tatu wakitoa upendeleo kwa ushiriki wa waandaji filamu toka ukanda huu wa Afrika mashariki kwa waandaji wenye kuonyesha hari na vipaji vyenye mlengo wa kuibuka kwenye tasnia hii.

WARSHA ZA NAMNA YA KUOMBA MISAADA YA KIFEDHA KUANDAA FILAMU NA WARSHA – warsha itaongozwa na wakufunzi toka Sweden and Uganda

UANDAAJI WA MAKALA: CONNIE FIELD – Warsha hii ya siku nzima italeta mtazamo mzima wa namna ya kuandaa makala chini ya usimamizi wa mshikiliaji wa tunzo ya uandaaji wa makala(producer / director), Connie Field.

CINEPHILMS:UTENGENEZAJI WA FILAMU KUTUMIA SIMU YA MKONONI – Hii warsha ya aina yake itaongozwa na Jonathan Dockney wa chuo kikuu cha Natal South Africa. Utengenezaji wa filamu kwa kutumia simu za mkononi ni teknolojia inayo ibuka kwa kasi sana. Njo ujifunze jinsi ya kutengeneza filamu kwa simu!

Tafadhali bonyeza hapa kwa maelezo zaidi: http://www.ziff.or.tz/ ama www.ziff.or.tz/press

KWA ZIADA WASILIANA NA:
Asmah Makau
Afisa Habari (Swahili Press)
asmahmakau@yahoo.co.in Tel no: 0713711413 / 0767711413
Laura Martin-Robinson (English language Press)
press@ziff.or.tz
Tel: +255 782689845 begin_of_the_skype_highlighting +255 782689845 end_of_the_skype_highlighting


RATIBA YA SIKU YA UFUNGUZI

TIME

WHO/ WHAT
7:00-8:00
Background music, Trailers

ZIFF team
8:00-8:02
Opening presentation

MC Hassan and Linda
8:02-8:07
Video ZIFF Biography

ZIFF technical team
8:07-8:08
MC presentation music act

MCs
8:08-8:13
MUSIC

KJETIL HAUGBRO
8:14-
MC presenting Chairperson

MCs
8:15-8:18
Speech by the Chairperson

Mr Mitawi
8:18-
CHAIRPERSON presenting CEO

Martin Mhando
8:18-8:21
Mr. Mhando launches ZIFF 2010

DHOW sail and fires
8:25-
MC presentation Zanzibar Poetry

MCs
8:26-8:31
ZANZIBAR POETRY

Amina
8:32
MC presenting GUEST of HONOR

MCs
8:32-8:37
Guest of HONOR SPEECH


8:37-
MC presenting dance act

MCs
8:38-8:45
DANCE group Zanzibar

D six group
8:45-
MC calls SIGNIS representative on stage

MCs
8:46-8:51
SIGNIS present the opening film

SIGNIS JURY
8:51-10:20
Launch of the opening film
Greetings by MCs Happy Tamash
a !!!

NI SHAIN ZANZIBAR




MBIO za urais wa Zanzibar ndani ya CCM zilifikia ukingoni jana wakati Makamu wa Rais, Dk Ali Mohamed Shein alipopoibuka na ushindi wa kishindo, akimbwaga mpinzani aliyeonekana kuwa wa karibu, Dk Mohamed Gharib Bilal. Dk Shein, ambaye amekuwa makamu wa rais tangu mwaka 2001 baada ya Dk Omar Juma kufariki, alikusanya kura 117 za wajumbe wa halmashauri kuu ya CCM iliyokutana mjini hapa jana na kumuacha mbali Dk Bilal ambaye alipata kura 54, ambazo ni takriban nusu ya kura alizopata mshindi.

Waziri Kiongozi Shamsi Vuai Nahodha alishika mkia katika majina matatu yaliyopelekwa na kamati kuu ya CCM iliyokutana jana asubuhi na kumaliza kikao chake mchana. Nahodha, ambaye alikuwa na umri mdogo kulinganisha na wagombea wenzake wawili, aliambulia kura 33 tu.

Dk Bilal na Nahodha walikubaliana na matokeo hayo na kutangaza kumuunga mkono Dk Shein, ambaye sasa anatakiwa kujiandaa kwa mpambano mkali dhidi ya chama kikuu cha upinzani visiwani Zanzibar, CUF, ambacho kimeshamteua mwanasiasa mkongwe, Seif Sharrif Hamad kuwania kiti hicho kwa mara ya nne baada ya kuangushwa na Dk Salmin Amour mwaka 1995 na baadaye Rais Amani Abeid Karume mwaka 2000 na 2005.

Kumalizika kwa mchakato huo kunaifanya CCM sasa itue mzigo ulioonekana mzito na itamalizia shughuli za kujiweka sawa kwa uchaguzi mkuu wakati wa mkutano wake mkuu uliopangwa kufanyika leo na kesho kushughulikia mambo mablimbali, ikiwa ni pamoja na kumbariki Rais Jakaya Kikwete kuwa mgombea urais wa Jamhuri ya Muungano.

Harakati za kumpata mgombea wa CCM zilitawaliwa na kila aina ya kampeni, huku Dk Shein akikumbana na rafu hata kabla ya kuja Dodoma baada ya baadhi ya watu kusambaza vipeperushi vilivyokuwa na maandishi yanayohoji uhalali wake wa kusimamishwa na chama kuwania urais.

Dk Shein alidaiwa kuwa hakujiandikisha kupiga kura Zanzibar na hajaishi visiwani humo kwa miezi 36 mfulululizo na hivyo kupoteza sifa ya kuwa mgombea. Hata kabla ya kutulia kwa tuhuma hizo, habari zilienea mjini hapa kuwa makamu huyo wa rais aliwasilisha barua ya kujiengua kwenye kinyang'anyiro hicho.

Lakini jana, Dk Shein alionekana kuwa mtu anayejiamini na alisalimiana na wajumbe wengi waliokuwa eneo la majengo ya ofisi za makao makuu ya CCM, akionekana kutaka kura za kila mjumbe, wakiwemo wauzaji wa nguo za chama hicho ambao hufanya shughuli za nje ya ofisi hizo.

Aliwasili kwenye viwanja hivyo majira ya saa 4:25 asubuhi akiwa na ulinzi mkali na alilakiwa na baadhi ya mawaziri wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.

Baada ya kusalimiana na baadhi ya wajumbe na viongozi wa CCM, Dk Shein aliyeonekana kujaa tabasamu, alienda moja kwa moja kwa wanachama na wajumbe wa CCM wa mikoa mbalimbali na kuwasalimia kwa kuwapa mkono.
Kitendo hicho cha Dk Shein kilivuta hisia za wanaCCM wengi ambao walianza kumkimbilia, kujipanga na kusubiri mkono wake.

Lakini Dk Bilal, ambaye awali alikuwa akipewa nafasi kubwa ya kuteuliwa kugombea urais kwa tiketi ya chama hicho baada ya kufanya vizuri mwaka 2000, alionekana kutokuwa katika hali ya kawaida na mara baada ya kutua kwenye viwanja hivyo aliingia ndani moja kwa moja na baadaye kutoka nje na kuelekea kwenye gari kabla ya kurudi ndani bila ya kuzungumza na mtu yeyote.

Baada ya kushuka kwenye gari, Dk Bilal Bilal aliinua kofia yake ya CCM na kuishusha kuangalia waliopo eneo hilo kuingia moja kwa moja kwenye ukumbi wa mikutano.

Balozi Ali Karume, ambaye ni mdogo wa rais wa Zanzibar, ndiye aliyekuwa wa kwanza kuingia kwenye viwanja hivyo na alipishana na Dk Shein kwa takriban dakika tatu tu.

Balozi Karume aliwasili viwanjani hapo akisindikizwa na wapambe wake, mkewe na baadhi ya wanafamilia waliovalia sare za CCM. Alisalimiana na baadhi ya wazee wa CCM, akiwamo Dk Shein ambaye alimfuatia.

Waziri Kiongozi wa Zanzibar, Shamsi Vuai Nahodha aliingia baada ya Dk Shein na kupokewa kwa bashasha na vijana wa CCM. Baada ya kusalimiana na baadhi ya wazee, Vuai alienda moja kwa moja kuwapa mkono wanachama waliokusanyika kumsubiri.

Kitendo chake kiliibua shangwe kwa wajumbe na watu wengine ambao walimwimbia nyimbo za kumsifu wakati akisalimiana na watu waliokuwepo kwenye viwanja hivyo.

Naibu Waziri Kiongozi Ali Juma Shemhuna aliwasili saa 5:08 akifuatiwa na Mohammed Raza na baadaye Mohammed Yusuph Mshamba aliyeingia moja kwa moja mkutanoni na kutoka baadaye kuonana na waandishi wa habari akiidokeza Mwananchi kuwa ana matarajio ya kuteuliwa.

Haroun Suleiman, ambaye ni Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali, aliwasili eneo hilo lakini muda mfupi baadaye, aliondoka. Hata hivyo, wagombea Mohammed Aboud ambaye ni Naibu Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki na Omar Sheha hawakuonekana katika viwanja hivyo.

Mji wa Dodoma na viunga vyake ulifurika wanachama wa CCM ambao wanatarajiwa kuhudhuria mkutano mkuu utakaompitisha mgombea urais wa chama hicho kesho.

Ujio wa watu hao umefanya nyumba nyingi za kulala wageni kufurika na watu wengi kukosa mahala pa kulala jambo ambalo pia lilisababisha msuguano baina ya wamiliki wa nyumba hizo na wateja ambao awali walikubaliana kwamba wangehama kuwapisha wajumbe hao.

Awali kikao cha kamati kuu ya CCM kilichofanyika jana mjini hapa kilipitisha majina matatu kati ya 11 walioomba kugombea urais wa Zanzibar.

Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, John Chiligati alitangaza majina hayo mbele ya waandishi wa habari baada ya kikao hicho cha kamati kuu

Jul 6, 2010

kama ulikuwa unadhani wachina ni hodari kwa kutengeneza simu pekee umekosea,wachina kwenye maonesho haya ya saba saba huwezi amini wamekuja na bidhaa ambazo kilo yake dukani kwa mangi inauzwa sh miatano,nazungumzia misumari ya bati hata scrub ambazo kwa meku tunanunua sh mia kwa kila scruu moja.


kama huamini hebu cheki meneja masoko wa mlimani tv na raadio akipiga domo na muuzaji wa bidhaa toka china,hapa jamaa anakamuliwa panga kwa buku tano huku jamaa akitaka kupunguziwa walau alipe buku mbili.
muonekeno wa banda la wachina katika picha
hapa jamaa wanaangalia kiwafaacho ili waweze kubeba aisee.
umeiona misumari?





Jul 4, 2010

SABA SABA SPECIAL PART III

''max hakikisha unapiga shot za ukweli mana ni muhimu sana na inawekwa kwenye documentary ya chuo''dir zuhura selemeni akitoa maelekezo
kijana wa kazi akiwa kazini katika kuhakikisha mlimani tv upande wa habari unakuwa na story za kutosha toka katika viwanja hivi vya saba saba
chief injinia wa mlimani tv& radio Stanley Nathan Chungu akiwa kwenye kuhakikisha kuwa hakuna kinachoharibika kwenye banda la mlimani tv&radio.
mpiga picha kiongozi wa mlimani tv maximilian john ngobe akiwa kwenye harakati za kazi kama kawaida yake
tanesco nao walikuwepo katika kuhakikisha kila kitu kuhusu umeme kinakuwa poa,pongezi kwa hilo
na hili ndo vazi rasmi la zain ingawa kiukweli ni miungoni mwa mabanda yaliyokuwa yamepooza sana mana hata maandalizi yao hayakuwa ya uhakika.


karibu na banda la maliasili watu walikuwa wengi sana kushuhudia wanyamapori waliokaushwa na walio hai,kiukweli banda linavutia sana aisee
usishangae sana hilo ndo vazi rasmi la heineken kipindi hiki cha saba saba,dizaini mpaka uwe umefaulu somo la big wowowo!!!!!!!!!!!!!

THE DON HIMSELF

Karibuni sana kwenye blog hii ya kijamii iliyosheheni makila kitu kuanzia siasa uchumi afya na burudani kwa ujumla wake.uingiapo kwenye blog hii ni mengi ambayo utapata nafasi ya kukutana nayo,kumbuka mawazo yako ndo hasa yanayojenga na kunifanya niwe na ufanisi zaidi.kariiiiiiibuuuuuuuuuuuu saaaaaaaaaaaaaaanaaaaaaaaaa.(THE DJ HIMSELF-JIWE)

Followers

BLOG ZA MARAFIKI

Search This Blog

ZILIZOPITA

DUNIA MUZIMA